BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Saturday, February 26, 2011


Wakazi wa Gongo la mboto wakishangaa bomu lililokita chini siku chache baada ya milipuko eneo hilo.

Thursday, February 17, 2011

MABOMU GONGO LA MBOTO


Madaktari wa hospitali ya Amana jijini Dar es salaam,wakimuhudumia mmoja wa waathirika wa mabomu hayo ambayo yalilipuka kutoka kwenye ghala la kutunzia silaha la JWTZ.

BREAKING NEWS!!!


Kuna mlipuko mkubwa unaendelea usiku huu eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salaam,inasadikiwa ni kutoka kambi ya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na hivyo kuwafanya wakazi na majirani wa eneo hilo kuyakimbia makazi yao na kuelekea katikati ya jiji na kusababisha msongamano mkubwa kwenye baadhi ya barabara.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kutoka mfuatiliaji wa taarifa hii.

Monday, February 14, 2011

SIMBA YAFUTA AIBU


Mabingwa wa soka Tanzania bara wamefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya kuifunga Elan club de mitsoudje ya Comoro kwa jumla ya magoli 4-2,Elan ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 42 likifungwa na Madaha Mohamed,Simba walisawazisha dak 44 kupitia kwa Mbwana Samata,magoli mengine ya Simba yalifungwa na Patrick Ochan dk 47,Samata dk.56,Amri Kiemba dk.72 na goli la pili la Elan lilifungwa na Abdoulhouda Abdouleafor dk.63,nao mahasimu wao Yanga wameendelea kukumbwa na jinamizi la mechi za kimataifa baada ya kukubali kipigo cha 2-0 kutoka kwa Dedebit mchezo huo ulichezwa jana jijini Adis Ababa-Ethiopia,kwa matokeo hayo Simba itakutana na mabingwa watetezi TP Mazembe ya DRC.

Sunday, February 13, 2011

BOMOA BOMOA


Jengo jipya lililoko Mbeya eneo la Mafiat,likionekana limebomolewa upande kutokana na mmiliki wake kushindwa kuzingatia umbali kati ya barabara na nyumba.

Tuesday, February 08, 2011

Saturday, February 05, 2011

AZAM FC YAZIDI KUTISHA


Timu ya Azam imezidi kujiwekea mazingira mazuri ya kuwania ubingwa wa Tanzania bara baada kuwafunga Toto African mabao 3-0,mabao yao yalipachikwa dakika ya kwanza na 35 na John Boko(Adebayor) na bao la tatu lilifungwa dk ya 56 na Mrisho Ngasa baada ya kupata pasi kutoka kwa Ramadhan Chombo Ridondo,Toto African walipoteana baada ya kufungwa bao la mapema na hivyo kuwafanya Azam kumiliki mchezo huo na kufikisha 29 nyuma ya Yanga yenye pointi 31
na Simba yenye pointi 30 na hivyo kuongeza ushindani wa kuwania ubingwa,ligi hiyo itaendelea tena leo ambapo Yanga watakuwa wageni wa wanalizombe Majimaji huko Songea na AFC Arusha watawakaribisha JKT Ruvu pale Sheikh Amri Abeid mjini Arusha na kesho mabingwa watetezi Simba watashuka uwanja wa Jamhuri Dodoma kukabiliana na Polisi Dodoma.

Wednesday, February 02, 2011

YANGA YAPOKEA KICHAPO CHA KWANZA.


Timu ya Yanga leo imepoteza mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kupoteza toka ligi kuu ya msimu kuanza,kutokana na Yanga kucheza chini ya kiwango ilimulazimu kocha wake Fred Felix Minziro Kataraia(baba Isaya au Majeshi) kusimama muda wote na kuliona benchi chungu baada ya Mtibwa kutawala mchezo huo,mara baada ya mchezo huo kumalizika mashabiki wanaosadikiwa kuwa ni wa Yanga waliwafanyia vurugu wachezaji wa Yanga kwa kutoridishwa na mwenendo wa timu hiyo na kutokuwepo kwa wachezaji kama Shadrack Nsajigwa,Yaw Berko,Athman Idd kunaonekana kuwaathiri Yanga kwenye mechi ya leo bila kumsahau kocha Costadin Papic ambaye ametimkia Africa Kusini kutokana na kutokuelewana na baadhi ya viongozi wa timu hiyo ambayo pia inakabiliwa na mechi ya kombe la shirikisho Africa dhidi Dedebit ya Ethiopia kwenye mchezo wa marudiano.