BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Tuesday, May 31, 2011

MSIBA


Mwili wa marehemu magreth Komba ukipakiwa kwenye gari tayari kwa mazishi yatakayofanyika eneo la Uyole Mbeya kabla ya kufanyiwa swala na viongozi wa dini.

Wauguzi na madaktari wa hospitali ya rufaa Mbeya, wakitoa heshima za mwisho kwa mtumishi mwenzao Magreth Komba pamoja na mumewe waliofariki kwa ajali ya basi.

Monday, May 30, 2011

MBEYA (MAPINDUZI STARS) WAPOKELEWA KWA VIFIJO NA NDEREMO.


Golikipa wa mkoa wa Mbeya Ivo Mapunda akimkabidhi kombe la ubingwa wa taifa mkuu wa mkoa wa Mbeya mh.John Mwakipesile leo katika hafla fupi ya kuwapokea mashujaa hao wa mkoa wa Mbeya mara baada ya kurejea kutoka Arusha-picha kwa hisani ya mbeya yetu blogspot.com

Mchezaji bora wa kombe la Taifa kwa mwaka 2011 Juma Mpola akiwa na daktari wa timu ya mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye trela la TBL ambao ni wadhamini wa Kombe la Taifa kwa kupitia bia yao ya kilimanjaro

Sunday, May 29, 2011

BARCELONA BINGWA ULAYA


Timu ya Barcelona imetwaa ubingwa wa ulaya baada kuwachapa Manchester united bao 3-1,goli la kwanza la Barca liliwekwa kimiani na Pedro na Man walisawazisha kupitia Wayne Rooney hadi mapumziko timu hizo zilikuwa nguvu sawa,kipindi cha pili Barcelona walifanikiwa kupata mabao mawili kupitia kwa Leone Messi na David Villa mechi hiyo imechezwa kwenye uwanja wa Wembley jijini London.

Saturday, May 28, 2011

WYDAD CANSABLANCA YAICHAPA SIMBA 3-0.


Timu ya Simba leo imefungwa jumla ya mabao 3-0 na Wydad Cansablanca ya Morroco magoli ya wamorroco hao yamefungwa dakika ya 87 na mengine mawili yakifungwa dakika za majeruhi,mchezo huo umechezwa kwenye uwanja Petrosport jijini Cairo,na hivyo kuzima ndoto za Simba kucheza hatua ya makundi klabu bingwa Africa,sasa wataingia kwenye michuano ya kombe la shirikisho na kucheza na Motema Pembe ya Congo

MBEYA BINGWA KOMBE LA TAIFA


Timu ya mkoa wa Mbeya leo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la taifa baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Mwanza kwa bao 1-0,bao pekee la Mbeya limefungwa dakika ya 87 na mshambuliaji tishio nchini Gaudence Mwaikimba.

BASI LA TAQWA LAANGUKA.


Zaidi ya abiria 50 wamenusirika kifo baada ya basi la taqwa kuanguka eneo la Iyofi mpakani mwa mikoa ya Morogoro na Iringa,basi hilo lilikuwa likielekea jijini Dar es salaam.

SUMRY YAPATA AJALI MBAYA.


Basi la kampuni ya Sumry high class limepata ajali eneo la Igawa na kupoteza maisha ya abiria 13 na wengine kujeruhiwa,basi hilo lilipata ajali kutokana na kupasuka tairi la mbele na kusababisha basi hilo kupinduka,basi hilo lilikuwa likitokea jijini Arusha.

Wednesday, May 25, 2011

OBAMA ASEMA LAZIMA GADAFFI AONDOKE


Rais Barack Obama amesema lazima rais Muamar Gadaffi aondoke madarakani,ameyasema katika yake nchini Uingereza,nchi imekuwa na machafuko ya kisiasa kwa mitatu na zaidi,huku nchi za ulaya zikionekana kuwaunga mkono waasi wa serikali ya Libya.

MBEYA YAINGIA FAINALI KOMBE LA TAIFA


Timu ya mkoa wa Mbeya(Mapinduzi stars) imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya kombe la taifa,baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Kagera kwa jumla ya mabao 2-1,mchezo huo umechezwa kwa dakika 120,hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1,Mbeya ndio waliofanikiwa kupata ushindi baada ya beki wa Kagera kujifunga baada ya shambulizi kutokea golini kwao,mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kucheza soka maridadi na golikipa wa Mbeya Ivo Mapunda kuonyesha uwezo mkubwa,Mbeya watakutana na Mwanza Heroes siku ya jumamosi uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha katika fainali.

Thursday, May 19, 2011

SIMBA KUVAANA NA WYDAD CANSABLANCA CAIRO

Timu ya Simba imfanikiwa kurudi kwenye michuano ya klabu bingwa Africa baada ya rufaa yao kukubaliwa na shirikisho la soka Africa(CAF) na kuitupia mbali timu ya TP Mazembe ambao ndio mabingwa wa kombe hilo baada ya kumchezesha mlinzi halali wa timu ya Esperence ya Tunisia,sasa simba watacheza na wydad cansablanca ya Morocco kwenye uwanja huru huko jijini Cairo

AJALI MBAYA GEITA

Ajali mbaya imetokea Geita baada ya basi la sheraton kugongana na lori na kusababisha watu kumi na sita kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa

Sunday, May 15, 2011

AJALI


Gari kubwa aina ya scania likiwa limeacha njia na kujikita kwenye mitaro iliyopo pembeni ya barabara,eneo la Iwambi Mbeya.

Msongamano huu umesababishwa na lori liliacha njia na kujikita kwenye mtaro wa barabara eneo la Iwambi-Mbeya.

Thursday, May 12, 2011

MAMA NA MWANA

Mama Mchungaji wa kanisa la moravian usharika wa NZOVWE  mama Salome Kalengo,akiwa na watoto wake walipotembelea ofisini kwake

Sunday, May 08, 2011

MANCHESTER UTD YAICHAPA CHELSEA 2-0


Manchester utd imezidi kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa England baada ya kuwachapa Chelsea kwa bao 2-0,na hivyo kuwa mbele kwa pointi 6 na zikiwa zimebakiwa na mechi 2 nao Arsenal wamepokea kichapo cha bao 3-1 kutoka kwa Stoke City.

KOMBE LA TAIFA


Timu ya mkoa wa Rukwa imeweza kufanya maajabu kwa kuifunga timu ya mkoa wa Temeke kwa jumla ya bao 2-1,Rukwa walikuwa wa kwanza kupata goli kwa njia ya adhabu dakika 12 baadaye nao Temeke walisawazisha nao kwa njia ya adhabu,kipindi cha pili Rukwa walifanikiwa kupata bao la pili.Katika mchezo wa kwanza Mbeya walifanikiwa kuwafunga Iringa 2-1.

Thursday, May 05, 2011

WEMBLEY PATACHIMBIKA


Kocha wa manchester akishangilia ushindi dhidi ya Schalke 04 ya Ujerumani

MANCHESTER UTD USO KWA USO NA BARCELONA MEI 28

Wachezaji wa manchester united wakishangilia moja ya mabao waliopata jana kwenye mchezo wa klabu bingwa ulaya kati yake na SCHALKE 04,ambapo manchester walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 na kusonga kwa jumla mabao 6-1,sasa watakutana na Barcelona katika mchezo wa fainali tarehe 28 mei,kwenye uwanja wa Wembley  England.

Wednesday, May 04, 2011

BARCELONA YATINGA FAINALI

Timu ya Barcelona jana ilifanikiwa kuingia fainali ya klabu bingwa ulaya baada ya kutoka sare na Real madrid 1-1,ilikuwa ni Barcelona iliyokuwa ya kwanza kujipatia lililofungwa Pedro dakika ya 56 madrid walisawazisha dakika ya 66 kupitia Marcus kwa matokeo hayo Barca wanaingia fainali na moja kati ya itakayoshinda leo kati Man utd v/s Schalke 04

SEHEMU ALIYOKUWA AKIISHI OSAMA BIN LADEN

Hii ndio nyumba aliyokuwa akiishi Osama bin Laden eneo la obbottabad nje kidogo ya jiji Islamabad Pakistan,ambayo ilishambuliwa na majasusi wa kimarekani na kufanikiwa kumuuwa kiongozi huyo wa kundi la al quaider

Monday, May 02, 2011

OSAMA BIN LADEN AUAWA PAKISTAN

Kiongozi wa kundi la al-queida ameuawa na wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakifanya operesheni maalum nchini Pakistan,Osama bin laden amekuwa akisakwa kwa zaidi ya miaka kumi na moja sasa