BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Saturday, July 30, 2011

SUPER FEO YAPATA AJALI MBEYA

Basi la kampuni ya Super Feo limepata ajali la eneo Chimala Mbeya jana mchana na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa,nilizungumza na mmoja wa majeruhi bw.Jackson Ndaskoy aliyekuwa akitokea Songea,alisema sababu ya ajali ni dereva kutokuwa makini bw.Ndaskoy ameruhusiwa kutoka hospilini mchana huu wa leo

Friday, July 29, 2011

KIONGOZI WA WAASI LIBYA AUAWA

Kiongozi wa waasi wa serikali ya Muamar Gadaffi bwana ABDEL fattah younes,ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Tripoli,

TBL YAKABIDHI VIFAA YANGA NA SIMBA


Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini(TFF) Angetile Osiah akiongea wakati wa hafla hiyo


 
Viongozi wa Yanga na Simba wakionyesha vifaa walivyokabidhiwa na TBL

TUNDU LISSU,PETER MSIGWA NA GODBLESS LEMA WAFUKUZWA BUNGENI

Askari polisi wa bunge wakihakikisha gari lililowabeba wabunge wa CHADEMA Tundu Lissu ,Peter Msigwa na Godbless Lema linaondoka nje ya viwanja vya bunge mara baada ya naibu spika wa bunge Job Ndugai kuwaamuru watoke ndani ya bunge kutkana na kukiuka kanuni za bunge

Wednesday, July 27, 2011

MIKOA YENYE CHAKULA WATUMIE KWA UHANGALIFU

Hapa ni eneo la Kiwira Tukuyu Mbeya,ni eneo maarufu kwa uhuzaji wa ndizi,mananasi,magimbi nk.wanunuzi  wakubwa ni wasafiri waendao nchi jirani,nje ya mkoa na hata wilaya jirani,kutokana na tamaa ya fedha baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza mpaka ndizi ambazo muda wake bado,pia tunawashauri kuwa waangalifu na uhuzaji holela wa vyakula kutokana na upungufu uliojitokeza kwenye baadhi ya mikoa na nchi jirani

MAPOROMOKO YA MAJI IBUNGILA TUKUYU YATUMIKA VIZURI


Maporomoko ya maji eneo la Ibungila Tukuyu yametumiwa vizuri na kuweza kuzalisha umeme kwenye shule ya sekondari Ibungila na maeneo jirani.



Mdau wetu alipotembelea eneo la maporomoko hayo

Hii ndio mashine ya kufua umeme Ibungila

Monday, July 25, 2011

SIKU YA MASHUJAA KITAIFA


Askari wa jeshi la wananchi wakitoa heshima kuwakumbuka mashujaa katika siku ya mashujaa.

Sunday, July 24, 2011

MAZISHI YA MZEE GILBERT MWAKIFULEFULE YAFANYIKA LEO IPINDA KYELA


Mazishi ya mzee Gilbert Mwakifulefule yamefanyika leo kijijini Ngolela,Ipinda-Kyela,askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la Moravian amewataka waumini na waombolezaji kutengeneza maisha yao ya baadaye na upendo-

Wakina mama wakiwa kwenye majonzi

Saturday, July 23, 2011

BABU LOLIONDO ABADILI FANI


Kama kuna mtu ambaye ana ushawishi mkubwa kwa Afrika Mashariki huwezi kuacha kumtaja Mch.Mstaafu A.Mwaisapile,baada ya kupungua wagonjwa waliokuwa wakifika kwake sasa anaendelea kujenga nyumba yake yeye mwenyewe.

Thursday, July 21, 2011

NGASSA AOSHA NYOTA YAKE

Mshambuliaji wa Taifa stars anayechezea timu ya Seattle Sounders ya USA,akijaribu kumtoka mlinzi Fabio(kulia) wa Manchester United kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa nchini Marekani















WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA AJALI YA BASI

Haya ndio mabaki ya basi la Hood lililopata ajali jana  na hatimaye kuungua baada ya kugongana na lori lililokuwa limepakia mafuta ya kula
Lori la mafuta likiteketea kwa moto eneo la Mikumi baada ya kugongana na Hood

MKUU WA MKOA WA MBEYA AKUTANA NA MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. John Mwakipesile akifafanua jambo kuhusu kuongezeka siku za kukagua na kusimamia magari kwenye mizani iliyoko Mpemba-Tunduma-Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu

Kamanda wa polisi wilaya ya Mbozi,afande Ernest Dudu nae alizungumzia utaratibu wa askari wa usalama barabarani kukagua magari hayo eneo la mizani

Wednesday, July 20, 2011

BREAKING NEEEEEWSSSS.


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa mwandishi wetu aliyeko Morogoro ni kuwa basi lililokuwa likisafiri kati ya Mbeya na Arusha limeshika moto eneo la Mikumi na abiria kushindwa kuendelea na safari,basi hilo ni mali ya Hood transport ya Morogoro
Basi likiendelea kuwaka moto

MRISHO NGASA AKIWA MAZOEZINI MAREKANI


Mshambuliaji maarufu wa Taifa stars na Azam fc,akiwa kwenye mazoezi na wenzake kwa ajili ya kuwakabili mabingwa EPL timu ya Manchester United ya Uingereza,Ngassa aliyeonyesha uwezo mkubwa akiwa na Yanga SC misimu iliyopita na hivyo kuwavutia Azam na kumchukua kwa dau kubwa,kwa sasa anafanya majaribio kwenye klabu ya Seattle Sounders ya Marekani na anaendelea vizuri.

Tuesday, July 19, 2011

TERRY-MODRIC 'DISRESPECTFUL'


John Terry believes Luka Modric has been disrespectful to Spurs for trying to engineer a move to Stamford Bridge.

Monday, July 18, 2011

VODACOM NA MRADI WA UTUNZAJI WA MBWA MWITU SERENGETI

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania bw.Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa mwitu mkurugenzi wa shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA,Allan Kijazzi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wautunzaji mbwa mwitu katika hifadhi ya tafa Serengeti(Vodacom foundation's Serengeti wild dogs conservation project)
Mkurugenzi mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akiteta jambo na waziri wa mawasiliano na uchukuzi mh.Mahige

Sunday, July 17, 2011

MBEYA


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ndg.Advocate Nyombi akionyesha silaha iliyotumika kwenye uporaji wa fedha NMB-tawi la Kyela mkoani Mbeya.

Tuesday, July 12, 2011

LADY JAY DEE NA YANGA KESHO NYUMBANI LOUNGE.


Mwanamuziki maarufu ukanda huu wa afrika mashariki na kati,Judith Wambura (lady jay dee) amewaandalia chakula mabingwa wa Kombe la Kagame Castle Cup,timu ya Yanga chakula cha mchana kwenye mgahawa wake maarufu wa NYUMBANI LOUNGE kwa ajili ya kuwapongeza kwa kutwaa ubingwa,inasemekana mwanamuziki ni mnazi wa wanajangwani hao

DIEGO MARADONA APATA AJALI YA GARI


Diego Amando Maradona amepata ajali ya gari akiwa na rafiki yake wa muda mrefu Veronica,ajali hiyo ilitokea kilomita chache alipokuwa akitokea nyumbani kwake kwenda uwanjani kutazama mechi za Coper America zinazoendelea nchini Argentina ambako michuano hiyo inafanyika,mara baada ya ajali alipelekwa hospital na hali yake inaendelea vizuri.

AIRTEL YAWA KAMPUNI YA KWANZA KUWAFIKIA WANANCHI WA MGAZINI-RUVUMA


Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imezindua mnara wake eneo la Mgazini mkoani Ruvuma,na hivyo kuwaondolea adha ya mawasiliano wakazi wa eneo hilo na maeneo ya Mhepai na vijiji jirani,kiongozi wa Airtel bwana Cheikh Sarr amesema ndani ya mwezi huu wanatarajia kuzindua minara 50 hapa nchini,nilifanikiwa kuongea na mmoja wa wananchi wa eneo la Mhepai bw.Morris Mapunda alionyesha kufurahia huduma hiyo na kudai walikuwa na simu kama mapambo kutokana na kutokuwepo mtandao wowote na ameishukuru sana Airtel kwa kuwaletea huduma hiyo.

Monday, July 11, 2011

YANGA BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Hili ndilo kombe la Kagame ambalo Yanga wamelinyakua
Wachezaji wa Yanga wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa kombe hilo

Mshambuliaji wa Yanga Khamis Kiiza akijaribu kumtoka mlinzi wa Simba Said Nassor (Cholo) kwenye uwanja wa Taifa Yanga walishinda 1-0
Makocha wa Yanga na Simba wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza Sam Timbe na Moses Basena (kulia) wa Simba

Sunday, July 10, 2011

TWIGA STARS YASHIKA NAFASI YA TATU COSAFA


Timu ya taifa ya wanawake imefanikiwa kushika nafasi ya michuano ya Cosafa kwa nchi za kusini mwa Afrika licha na maandalizi mabovu,wamewalaza wenzao wa Malawi mabao 3-1

Saturday, July 09, 2011

YANGA YACHAFUA HALI YA HEWA MSIMBAZI

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga jana walifanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kagame Cup baada kuwatoa St.George ya Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4 na hivyo kukutana na Simba kwenye fainali kesho kwenye uwanja wa taifa,Simba ambayo ilionekana kucheza kandanda safi toka ilipoanza michuano hii tofauti na watani wao,watalazimika kucheza kivingine zaidi kutokana na timu kukamiana kila zinapokutana na kuharibu ladha ya mchezo

Mashabiki wa Yanga wakishangilia mara baada ya mpira kumalizika wengine hawakuamini kilichotokea baada ya penati ya mwisho ya St.George kugonga mwamba na kurudi chini jirani na mstari wa goli

MHESHIMIWA SUGU ASHIKILIWA NA POLISI MBEYA

Mh.mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbillinyi jana alishikiliwa kwa muda na jeshi la polisi kwa kufanya mkutano eneo la Nzovwe bila kibali cha jeshi hilo,Mbillinyi ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chadema.
Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya bw. Advocate Nyombi akisisitiza juu ya umuhimu wa amani na watu kufuata sheria

Friday, July 08, 2011

MIUNDO MBINU MBEYA KUBORESHWA


Wafanyakazi wa kampuni ya Sogea Sotum wakitengeneza bomba eneo la Iyunga Mbeya,kampuni hiyo ndio inatengeneza mfumo wa maji taka na safi mkoani Mbeya.

SIMBA YAINGIA FAINALI KAGAME CUP

Timu ya Simba jana imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Kagame baada ya kuiondoa timu ya El-mereikh ya Sudan kwa mikwaju ya penati 5-4,hadi dakika 90 matokeo yalikuwa 1-1 na kuongezwa dakika 30 na matokeo kuwa hivyohivyo na mshindi kupatikana kwa njia ya penati,nusu fainali nyingine itakuwa leo jioni kati ya Yanga na St.George na mshindi wa leo ataungana na Simba kwenye mchezo wa fainali jumapili.

Tuesday, July 05, 2011

DEREVA JOHN GWAU AFANYIWA UNYAMA NA SHEMEJI YAKE SINGIDA MJINI


John Gwau akiwa wodi No.4 kwenye hospital ya mkoa Singida,baada ya kupigwa na chupa ya bia na shemeji yake Celestin Mgoo kwa tuhuma za kufuliwa nguo na dada yake aitwaye Ruth ambaye ametengana na Celestin,dada huyo ni mwalimu wa shule ya msingi Mughanga iliyoko mjini Singida,bwana Celestin aliingia chumbani kwa shemeji na kumpiga na chupa kichwani,baada ya kuzirai kama vile haitoshi alitumia vipande vya chupa kumchanja chanja usoni,mtuhumiwa leo amefikishwa mahakamani.

Monday, July 04, 2011

NOVAK DJOKOVIC ASHINDA WIMBLEDON


DAVID HAYE ALAMBA SAKAFU UJERUMANI

Bondia David Haye wa Uingereza jana alipokea kichapo kutoka kwa Vladimir Klitschko wa Ukraine kwenye pambano la kuwania wa WBC ambao ulikuwa ukishikiliwa na Haye,pambano hilo la raundi 12 liliamuliwa kwa pointi,lakini muda mwingi wa pambano Haye alionekana kuzidiwa na kuanguka mara kadhaa na kuendelea na pambano mpaka mwisho
Vladimir Klitschko akipongezwa na kaka yake Vital klitschko mara baada kupata ushindi dhidi ya David Haye na sasa anashikilia mataji matatu ya WBC,WBA na WBO