BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Monday, January 31, 2011

SIMBA KAMA PAKA


Mabingwa wa soka wa Tanzania bara wameshindwa kudhiirisha umwamba wao kwenye mechi za kimataifa baada ya kulazimishwa suluhu na wenyeji wao ELAN CLUB DE MITSOUDJE ya Comoro na hivyo kuwafanya wapinzani wao kuhitaji sare ya magoli ili waweze kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki mbili zijazo jijini Dar,nao mahasimu wao Yanga walishindwa kuutumia vyema uwanja wa taifa baada ya kulazimishwa sare ya mabao 4-4 na Dedebit ya Ethiopia na hivyo kujiweka katika mazingira magumu.

Friday, January 28, 2011

LILONDO


Wakina mama wa eneo la Lilondo wakifanya biashara ya ndizi kwenye mabasi yanayopita eneo hilo,mabasi yanayofanya safari kati ya Songea,Iringa,Mbeya na Dar es salaam.

KITUO CHA MABASI SONGEA.


Wafanyabiashara wa eneo la stendi kuu Songea,wakifanya biashara za vyakula katika eneo lisiloridhisha kwa afya za walaji na usalama kutokana na majiko kuwa jirani na mabasi.

PERAMIHO MISSION


Kanisa kongwe la Roman Catholic la Peramiho.

PERAMIHO HOSPITAL



PERAMIHO SONGEA


Hospital ya Peramiho ni moja ya hospital kubwa zinazotoa huduma bora za kiafya hususan kwa wakazi wa kanda za nyanda za juu kusini na maeneo mengine.

Sunday, January 23, 2011

IHANDA MBOZI


Mabaki ya gari aina ya Coaster,ambayo ilichomwa moto na wananchi wenye hasira baada ya kumgonga mkazi wa kijiji cha Ihanda na kusababisha kifo chake.

Thursday, January 20, 2011



MAMBO YA BAJAJ


Usafiri wa Bajaj umekuwa wa kawaida wa kawaida kwa baadhi ya sehemu hapa nchini,leo imetokea ajali ya Bajaj jijini Mbeya eneo la Meta baada ya Bajaj kuacha njia na kuingia kwenye mtaro kutokana na mwendo wa kasi na hivyo kusababisha dereva kushindwa kuimudu kwenye kona,wanaonekana wananchi wenye huruma wakiitoa bajaj hiyo,dereva na abiria wake walinusurika kwenye ajali hiyo.

AJALI


Daladala inayofanya safari kati ya Mbalizi na Mwanjelwa ikiwa imeigonga gari ndogo eneo la Kadege,kwa bahati nzuri hakuna majeruhi kwenye ajali hii iliyotokea jioni hii.

Wednesday, January 19, 2011

HOLIDAY HILL HOTEL-MBEYA


Moja ya hotel za kisasa jijini Mbeya,Holiday hill hotel iko jirani na kanisa la Efatha,ina huduma za internet,chumba cha mikutana,maegesho ya magari na mambo mengi.

Friday, January 14, 2011

TUCHANGIE DAMU KUWASAIDIA WAGONJWA.


Dr.MATHEO KINEMO wa mpango wa taifa wa damu salama akitoa elimu juu ya kuchangia damu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Meta iliyoko jijini Mbeya,mdau wa globu hii anawapongeza na kuwashukuru wananchi wote wenye moyo wa huruma na kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wenye upungufu wa damu wakiwemo wajawazito,watoto chini ya miaka mitano na waanga wa ajali mbali mbali kama vile ajali za barabarani,moto na kadhalika.

Monday, January 10, 2011


Gari ya zimamoto likiwa eneo la tukio.

WELL DONE ZIMAMOTO


Kikosi cha zimamoto mkoani Mbeya kimefanikiwa kuinusuru hotel ya Calm inn,iliyokuwa imeshika moto,wanaonekana askari wa zimamoto wakiudhibiti moto huo.

Sunday, January 09, 2011

RC PAROKIA YA RUANDA-ILOMBA MBEYA.


Waumini wakijianda kuingia kanisani kwa ajili ya kumuomba na kumshukuru Mwenyezi MUNGU kwa mema mengi aliyotutendea.

ENZI ZA MWALIMU


Gari aina ya LEYLAND ALBION ambazo miaka ya 70 ndio zilikuwa kwenye chati kama ilivyo SCANIA leo,likiwa na mashine za kuchimbia visima vya maji.

Saturday, January 08, 2011

HAUZAN EDWARD


Mfanyakazi wa mamlaka ya maji safi na taka mkoa wa Mbeya akijitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa.

MAZINGIRA


Mfanyakazi anayeshulika na utunzaji wa mazingira kwenye ya sekondari ya Pandahill,akifyeka nyasi kwa kutumia mashine aina ya SHIKUNDAIWA

NELLAS KITUNDU


Mfanyakazi wa mamlaka ya maji Mbeya,akipumzika baada kushiriki zoezi la kuchangia damu.

Friday, January 07, 2011

Tuesday, January 04, 2011

SOKO MATOLA-MBEYA


Wauzaji wa matunda, mboga za majani na viungo wakiwa wamepanga bidhaa zao mbele ya maduka na kuzipanga chini,tunawaomba viongozi wa soko na halmashauri ya jiji kuwawekea mazingira mazuri wajasiliamali hawa kwa kuwaweka eneo zuri kwa afya za walaji na wao pia.

Monday, January 03, 2011

IGURUSI MBEYA


Wakazi wa kijiji cha Igurusi,mkoani Mbeya wakiwa kwenye pilikapilika za kila siku kwa ajili ya kujipatia riziki,kijiji hiki ni maarufu kwa biashara ya mchele.

Saturday, January 01, 2011

HAPPY NEW YEAR 2011


Nights are dark but days are light,wish your life will always be bright.So my dear dont get fear coz,God gift us a "brand new year"
*HAPPY NEW YEAR*