Basi la kampuni ya Super Feo limepata ajali la eneo Chimala Mbeya jana mchana na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa,nilizungumza na mmoja wa majeruhi bw.Jackson Ndaskoy aliyekuwa akitokea Songea,alisema sababu ya ajali ni dereva kutokuwa makini bw.Ndaskoy ameruhusiwa kutoka hospilini mchana huu wa leo
Saturday, July 30, 2011
Friday, July 29, 2011
Wednesday, July 27, 2011
MIKOA YENYE CHAKULA WATUMIE KWA UHANGALIFU
Hapa ni eneo la Kiwira Tukuyu Mbeya,ni eneo maarufu kwa uhuzaji wa ndizi,mananasi,magimbi nk.wanunuzi wakubwa ni wasafiri waendao nchi jirani,nje ya mkoa na hata wilaya jirani,kutokana na tamaa ya fedha baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiuza mpaka ndizi ambazo muda wake bado,pia tunawashauri kuwa waangalifu na uhuzaji holela wa vyakula kutokana na upungufu uliojitokeza kwenye baadhi ya mikoa na nchi jirani
Monday, July 25, 2011
Sunday, July 24, 2011
Saturday, July 23, 2011
Thursday, July 21, 2011
MKUU WA MKOA WA MBEYA AKUTANA NA MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA
Mkuu wa mkoa wa Mbeya mh. John Mwakipesile akifafanua jambo kuhusu kuongezeka siku za kukagua na kusimamia magari kwenye mizani iliyoko Mpemba-Tunduma-Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu
Kamanda wa polisi wilaya ya Mbozi,afande Ernest Dudu nae alizungumzia utaratibu wa askari wa usalama barabarani kukagua magari hayo eneo la mizani
Wednesday, July 20, 2011
MRISHO NGASA AKIWA MAZOEZINI MAREKANI
Mshambuliaji maarufu wa Taifa stars na Azam fc,akiwa kwenye mazoezi na wenzake kwa ajili ya kuwakabili mabingwa EPL timu ya Manchester United ya Uingereza,Ngassa aliyeonyesha uwezo mkubwa akiwa na Yanga SC misimu iliyopita na hivyo kuwavutia Azam na kumchukua kwa dau kubwa,kwa sasa anafanya majaribio kwenye klabu ya Seattle Sounders ya Marekani na anaendelea vizuri.
Tuesday, July 19, 2011
Monday, July 18, 2011
VODACOM NA MRADI WA UTUNZAJI WA MBWA MWITU SERENGETI
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania bw.Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa mwitu mkurugenzi wa shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA,Allan Kijazzi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wautunzaji mbwa mwitu katika hifadhi ya tafa Serengeti(Vodacom foundation's Serengeti wild dogs conservation project)
Sunday, July 17, 2011
Tuesday, July 12, 2011
LADY JAY DEE NA YANGA KESHO NYUMBANI LOUNGE.
Mwanamuziki maarufu ukanda huu wa afrika mashariki na kati,Judith Wambura (lady jay dee) amewaandalia chakula mabingwa wa Kombe la Kagame Castle Cup,timu ya Yanga chakula cha mchana kwenye mgahawa wake maarufu wa NYUMBANI LOUNGE kwa ajili ya kuwapongeza kwa kutwaa ubingwa,inasemekana mwanamuziki ni mnazi wa wanajangwani hao
DIEGO MARADONA APATA AJALI YA GARI
Diego Amando Maradona amepata ajali ya gari akiwa na rafiki yake wa muda mrefu Veronica,ajali hiyo ilitokea kilomita chache alipokuwa akitokea nyumbani kwake kwenda uwanjani kutazama mechi za Coper America zinazoendelea nchini Argentina ambako michuano hiyo inafanyika,mara baada ya ajali alipelekwa hospital na hali yake inaendelea vizuri.
AIRTEL YAWA KAMPUNI YA KWANZA KUWAFIKIA WANANCHI WA MGAZINI-RUVUMA
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imezindua mnara wake eneo la Mgazini mkoani Ruvuma,na hivyo kuwaondolea adha ya mawasiliano wakazi wa eneo hilo na maeneo ya Mhepai na vijiji jirani,kiongozi wa Airtel bwana Cheikh Sarr amesema ndani ya mwezi huu wanatarajia kuzindua minara 50 hapa nchini,nilifanikiwa kuongea na mmoja wa wananchi wa eneo la Mhepai bw.Morris Mapunda alionyesha kufurahia huduma hiyo na kudai walikuwa na simu kama mapambo kutokana na kutokuwepo mtandao wowote na ameishukuru sana Airtel kwa kuwaletea huduma hiyo.
Monday, July 11, 2011
YANGA BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Hili ndilo kombe la Kagame ambalo Yanga wamelinyakua
Wachezaji wa Yanga wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa kombe hiloMshambuliaji wa Yanga Khamis Kiiza akijaribu kumtoka mlinzi wa Simba Said Nassor (Cholo) kwenye uwanja wa Taifa Yanga walishinda 1-0
Makocha wa Yanga na Simba wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza Sam Timbe na Moses Basena (kulia) wa Simba
Sunday, July 10, 2011
Saturday, July 09, 2011
YANGA YACHAFUA HALI YA HEWA MSIMBAZI
Mabingwa wa Tanzania bara Yanga jana walifanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kagame Cup baada kuwatoa St.George ya Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4 na hivyo kukutana na Simba kwenye fainali kesho kwenye uwanja wa taifa,Simba ambayo ilionekana kucheza kandanda safi toka ilipoanza michuano hii tofauti na watani wao,watalazimika kucheza kivingine zaidi kutokana na timu kukamiana kila zinapokutana na kuharibu ladha ya mchezo
Mashabiki wa Yanga wakishangilia mara baada ya mpira kumalizika wengine hawakuamini kilichotokea baada ya penati ya mwisho ya St.George kugonga mwamba na kurudi chini jirani na mstari wa goli
MHESHIMIWA SUGU ASHIKILIWA NA POLISI MBEYA
Mh.mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbillinyi jana alishikiliwa kwa muda na jeshi la polisi kwa kufanya mkutano eneo la Nzovwe bila kibali cha jeshi hilo,Mbillinyi ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chadema.
Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya bw. Advocate Nyombi akisisitiza juu ya umuhimu wa amani na watu kufuata sheria
Friday, July 08, 2011
SIMBA YAINGIA FAINALI KAGAME CUP
Timu ya Simba jana imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Kagame baada ya kuiondoa timu ya El-mereikh ya Sudan kwa mikwaju ya penati 5-4,hadi dakika 90 matokeo yalikuwa 1-1 na kuongezwa dakika 30 na matokeo kuwa hivyohivyo na mshindi kupatikana kwa njia ya penati,nusu fainali nyingine itakuwa leo jioni kati ya Yanga na St.George na mshindi wa leo ataungana na Simba kwenye mchezo wa fainali jumapili.
Tuesday, July 05, 2011
DEREVA JOHN GWAU AFANYIWA UNYAMA NA SHEMEJI YAKE SINGIDA MJINI
John Gwau akiwa wodi No.4 kwenye hospital ya mkoa Singida,baada ya kupigwa na chupa ya bia na shemeji yake Celestin Mgoo kwa tuhuma za kufuliwa nguo na dada yake aitwaye Ruth ambaye ametengana na Celestin,dada huyo ni mwalimu wa shule ya msingi Mughanga iliyoko mjini Singida,bwana Celestin aliingia chumbani kwa shemeji na kumpiga na chupa kichwani,baada ya kuzirai kama vile haitoshi alitumia vipande vya chupa kumchanja chanja usoni,mtuhumiwa leo amefikishwa mahakamani.
Monday, July 04, 2011
DAVID HAYE ALAMBA SAKAFU UJERUMANI
Bondia David Haye wa Uingereza jana alipokea kichapo kutoka kwa Vladimir Klitschko wa Ukraine kwenye pambano la kuwania wa WBC ambao ulikuwa ukishikiliwa na Haye,pambano hilo la raundi 12 liliamuliwa kwa pointi,lakini muda mwingi wa pambano Haye alionekana kuzidiwa na kuanguka mara kadhaa na kuendelea na pambano mpaka mwisho
Vladimir Klitschko akipongezwa na kaka yake Vital klitschko mara baada kupata ushindi dhidi ya David Haye na sasa anashikilia mataji matatu ya WBC,WBA na WBO
Vladimir Klitschko akipongezwa na kaka yake Vital klitschko mara baada kupata ushindi dhidi ya David Haye na sasa anashikilia mataji matatu ya WBC,WBA na WBO
Friday, July 01, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)