Tuesday, August 30, 2011
Monday, August 29, 2011
Sir Alex Ferguson amshauri Wenger kufanya usajili makini kabla ya kesho kutwa.
Baada ya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 8-2 dhidi ya Arsenal,meneja wa Man Utd amemshauri kocha wa Arsenal kufanya usajili makini kwa masaa 48 yaliyobaki kabla ya msimu wa usajili kufungwa hapo jumatano.
Naye Wenger amesema sababu ya kipigo hicho ni uchovu wa wachezaji wake ambao jumatano iliyopita walicheza na Udinesse ya Italia kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na hivyo kusababisha majeruhi kwenye kikosi hicho na kufanya wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kutocheza.
Wenger ni kocha pekee aliyeiletea mafanikio timu ya Arsenal na kuifanya kuwa na wapenzi wengi duniani lakini mambo sasa yanataka kumuendea kombo kutokana na kipigo hicho kikubwa ambacho kwa mara ya mwisho timu hiyo ilifungwa mabao 8-0 mwaka 1896,hata hivyo Wenger amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo duniani kote.
Sunday, August 28, 2011
Manchester yaifanyia kufuru Arsenal yawachapa 8-2
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza leo wameifanyia kitu mbaya timu ya Arsenal kwa kuichapa mabao 8-2,kichapo hicho ni kikubwa kwa maisha ya mzee Arsenal Wenger ambaye ana tabia ya kujiamini sana,na sasa amekuwa na wakati mgumu kubaki kwenye timu hiyo ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu na inasemekana ndiye kocha pekee aliyeleta mabadiliko kwenye ligi hiyo ya Uingereza na kufuta ubaguzi wa rangi.
Lakini kutokana na kipigo cha leo kinamuweka kwenye wakati mgumu zaidi hasa baada ya kuwauza wachezaji wake nyota na kushindwa kutafuta mbadala wao,pamoja na bodi ya klabu hiyo kuruhusu fedha zitumike kwenye usajili wa msimu huu lakini alikaidi agizo hili.
Mechi hii imehudhuriwa na watazamaji 73414 kwenye dimba la Old Trafford na Man U kuibuka na ushindi mnono wa bao 8-2.
HII NDIYO KYELA BWANA
Kama kuna wilaya ambayo wanafahamu matumizi na umuhimu wa baiskeli hatuwezi kuacha kuitaja wilaya ya Kyela,kwenye picha ni baadhi ya baiskeli ambazo zimeegeshwa eneo la shule na bado ukipita mitaani wakina utawakuta wakiendesha na mtoto mgongoni,ukiuliza safari ya wapi?unajibiwa anaenda kliniki au kabeba bonge la mzigo
Tuesday, August 23, 2011
MPAKANI MWA TANZANIA NA MALAWI
Hapa ndio mpaka wa Tanzania na Malawi unaojulikana kwa jina la Border ya Kasumulu ambayo inaonekana na utulivu wa hali ya juu tofauti na mipaka mingine.
Huu ndio mto unayozitenganisha nchi hizi mbili |
Baadhi ya magari ya mizigo yakisubiri kupita mpakani | <><>Eneo la Malawi likiwa linafanyiwa ukarabati
Monday, August 22, 2011
Sunday, August 21, 2011
MZIMU WA SIMBA WAENDELEA KUITAFUNA YANGA
Mabingwa wa Tanzania bara leo wameanza ligi ya Vodacom vibaya,baada ya kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu ikiwa ni siku chache baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mahasimu wao Simba cha bao 2-0 kwenye mchezo wa ngao ya hisani,JKT Ruvu walipata bao kwa njia ya penati dakika 22 iliyofungwa na Kesy Mapande kutokana na mlinzi wa Yanga Chacha Marwa kucheza faulo eneo la hatari.
JKT Ruvu walitumia mbinu iliyotumiwa na Simba ya kuchezesha viungo wengi katikati na hivyo kuwafanya viungo wa Yanga Nurdin Bakari na Haruna Niyonzima kushindwa kuonyesha umahiri wao ipasavyo.
Na huko Arusha Simba wameanza ligi vyema baada ya kuwalaza JKT Oljoro mabao 2-0.
Saturday, August 20, 2011
Friday, August 19, 2011
MNYAMA AITAFUNA YANGA USIKU
Timu ya Simba imefanikiwa kuwafunga mahasimu wao Yanga kwa mabao 2-0 na kuchukua ngao ya hisani,Simba wakicheza kwa ushirikiano mkubwa walifanikiwa kupata bao dakika ya 16 kupitia Haruna Moshi Boban na baadaye walipata bao kwa njia ya penati kupitia kwa Sunzu hadi mapumziko Simba walikuwa wakiongoza kwa mabao hayo mawili,kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi na kuwafanya Yanga washindwe kusawazisha kutokana na kuwazidi wapinzani wao kwenye safu ya kiungo na kuwafanya Yanga kucheza bila malengo.
Timu hizi zimekutana mara sita kwenye mechi za usiku na hivyo Simba ikiibuka na ushindi mara tano na Yanga mara moja na mechi hizo zilichezwa uwanja wa Aman Zanzibar,mechi nne zikiwa ni za ubingwa wa Afrika mashariki na kati,moja kombe la muungano na nyingine ndio hii ya ngao ya hisani ambayo imechezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa matokeo hayo inaonyesha Yanga wamekuwa na udhaifu wa mechi za usiku hata za kirafiki,wiki moja tu iliyopita wamechezea kichapo mjini Khartoum Sudan kwa kufungwa mabao 3-1 na El-hilal,na katika mechi ya pili wakapokea kipigo kama hicho hicho
Mvuto zaidi ni kwa makocha wa timu hizo ambao wanatoka nchi moja kwa upande wa Simba ni Moses Basena na Yanga ni Sam Timbe ambao kila mmoja alitaka kuonyesha nani zaidi ya mwenzake kutokana na timu zote kujivunia usajili wa msimu huu.
Tuesday, August 16, 2011
Sunday, August 14, 2011
MASHINDANO YA KUHIFADHI KURAAN TUKUFU YAFANA DAR
Baadhi ya mashekhe na umati wa waislamu uliofurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar-es-salaam,kushuhudia mashindano ya kuhifadhi Kuraan Tukufu yaliyoshirikisha wanafunzi wa madrasa toka bara na visiwani,ambayo mshindi wa kwanza alikuwa Khalid Omar Mbarouk(15) kutoka madrasa ya Madrasat An-nujum ya Temeke na kujishindia pikipiki aina ya Bajaj.
UJENZI WA BARABARA YA SONGEA-MBINGA WAENDELEA KWA KASI.
Ujenzi wa barabara ya Songea-Mbinga kwa kiwango cha lami,unaendelea kwa kasi na kuleta matumaini kwa wakazi mkoa huo kutokana na wilaya ya Mbinga kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
Kukamilika kwa ujenzi kutawanufaisha wakazi wa mkoa wa Ruvuma na maeneo jirani waliokuwa wakitumia muda mrefu kusafiri katika maeneo hayo yenye biashara za mazao na samaki kutoka ziwa Nyasa.
MANCHESTER YAANZA VIZURI
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) leo wameanza michuano hiyo vizuri baada ya kuwafunga timu ya West ham 2-1,Man walikuwa wa kwanza kupata bao dk 14 kupitia kwa Wayne Rooney na baadaye Long aliisawazishia Westham na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi mapumziko,kipindi cha pili Man walifanikiwa kupata bao la ushindi dk 81 kupitia kwa Ashley Young aliyepiga mpira na kuwababatiza mabeki wa Westham na kujaa wavuni
Friday, August 12, 2011
Thursday, August 11, 2011
Wednesday, August 10, 2011
Sunday, August 07, 2011
RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali Davis Mwamunyange.kufuatia kifo cha Luteni Jenerali Silas Peter Mayunga kilichotokea jana katika hospital ya Apollo,mjini New Dhel,India.Mzee Mayunga amefariki akiwa na umri wa miaka 71.
Saturday, August 06, 2011
BIASHARA YA NDIZI TUKUYU.
Wafanyabiashara ya ndizi wakionekana wakisubiri usafiri kwa ajili ya kusafirisha ndizi kupeleka maeneo tofauti,biashara hiyo inaonekana kufanywa na wanawake kuliko wanaume eneo la Tukuyu na hivyo kusababisha soko lake liwe dogo,kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Songwe kutaleta changamoto kwa wanaume nao kujiingiza kwenye biashara hiyo ambayo wamekuwa kama wanahidharau.
Wednesday, August 03, 2011
MAJENGO YA ILIYOKUWA HOSPITAL YA UKOMA MAKETE-KISONDELA YAMETELEKEZWA TOKA 2005
Haya ni majengo ya iliyokuwa hospital ya ukoma Makete Kisondela,Rungwe yakiwa kwenye hali mbaya baada ya hospital hiyo kufungwa rasmi mwaka 2005 na kufanya majengo kubaki yakiwa hayatumiki mpaka leo.
Majengo haya yangeweza kutumika kama shule au kituo cha afya kwenye kata husika lakini yameachwa yakiharibika
Sehemu ya ndani ya majengo hayo ambayo haitumiki kwa sasa
Jengo likiwa limezungukwa na nyasi pande zote |
Monday, August 01, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)