Katika hali isiyo ya kawaida,mashabiki wa soka hapa nchini wakifanya vitu vya tofauti sana ukilinganisha na nchi nyingine.
Haya ni moja ya matatizo ya mashabiki:-
1.Kuzomea timu ya taifa inapocheza.
2.Kuzomea baadhi ya wachezaji Taifa Stars,mfano Mwaikimba na Boko.
3.Kushangilia wageni kwenye michuano mbalimbali sababu ya Usimba na Uyanga.
4.Kutolipa viingilio vilivyopangwa.
5.Hawahudhurii kwenye mechi kama vile Villa Squad v/s Polisi Dom.
6.Kuwarushia chupa na makopo wachezaji na makocha.
7.Kutumia lugha chafu badala ya kushangilia.
8.Wanahitaji ushindi tu sio kushindwa.
9.Wanataka mafanikio ya haraka bila kujiandaa
Hizi ndizo sababu zinazoua soka la Tanzania na kuwapa wakati mgumu makocha na wachezaji wa kigeni.
Timu ya Simba leo imefanikiwa kuwafunga El Satif 2-0, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,mchezo huo ulikuwa ni wa kombe la shirikisho.
Simba walipata mabao hayo kipindi cha pili yakiwekwa wavuni na Moshi Kazimoto na Haruna Moshi,Simba walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kutawala eneo la kiungo na wapinzani wao wakiwa na wakati mgumu wote wa dakika 30 za mwanzo cha kipindi cha pili.
Es Satif wakiongozwa na Yousef Satif walishindwa kuhimili muziki wa Simba kutokana na mikakati ya wachezaji wa Simba.
Mchezaji wa Bolton ya Uingereza Fabrice Muamba sasa anaendelea vizuri baada ya kuweza kupumua mwenyewe bila msaada wa mashine na ameweza pia kuwatambua baadhi ya watu waliomtembelea hospitali leo.
Muamba alianguka ghafla kwenye mchezo wa kombe la FA kwenye uwanja wa White hart lane,wakati timu yake ikicheza na Tottenham Hotspur,mchezo huo ilibidi huahirishwe kutokana na hali ya Muamba kuwa mbaya,huku matokeo yakiwa 1-1 na kukimbizwa hospital ya Heart attack Centre jijini London.
Muamba alijiunga na Bolton 2008 akitokea Birmingham City kwa ada ya paundi (£) milion 5.
Muamba alizaliwa DRC miaka 23 iliyopita,na alipokuwa na umri wa miaka 11 alimufuata baba yake jijini London ambako alikuwa akifanya kazi.
Tukio hili limewakumbusha wanasoka na wapenzi wa soka mchezaji wa zamani wa Cameroun Mark Vivien Foe ambaye naye alianguka uwanjani na kupoteza maisha.
Mdau wetu akiwa nje ya kanisa kuu la katoliki Sumbawanga Mjini.
Kanisa hilo ni moja ya majengo yanayopendezesha mji huo kutokana na usafi wake.
Umati wa waombolezaji wakiwa kijijini Ichesa wilayani Mbozi,wakkwenye mazishi ya diwani wa kata ya Myovizi kwa tiketi ya CCM.
Mh.Shulla alifariki jana asubuhi katika hospitali ya wilaya ya Mbozi na mazishi yake ndio yanafanyika muda huu.
Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaendelea kwa kasi eneo la Kaengesa.
Mdau wetu alipita maeneo na kukuta kazi hiyo ikiendelea licha ya mvua nayo kuendelea kunyesha.
Timu ya netball ya Mazwi Secondary leo imewafunga wenzao wa African Rainbow mabao 46-39.
Nyota wa mchezo wa leo alikuwa Georgina Maheka wa Mazwi licha ya kukabiliana na ukuta mgumu wa African Rainbow ukiongozwa na Tamali Joseph.
Mchezo umechezwa kwenye uwanja wa Mazwi Secondary.
Timu ya Jamaica FC imeifunga timu ya Rukwa united bao 2-1,kwenye ligi ya mkoa huo,magoli ya Jamaica yamefungwa na Steve Mwansite dakika ya 4 na la pili likifungwa na Torres,bao la kufutia machozi la Rukwa united limefungwa kwa njia ya Penati.