Monday, July 30, 2012
Sunday, July 29, 2012
Saturday, July 28, 2012
YANGA BINGWA TENA KOMBE LA KAGAME 2012
Wachezaji wa Yanga wakiwa na kombe la Kagame mara baada ya kukabidhiwa kwa kuwafunga Azam FC ya Dar es salaam kwenye mchezo wa fainali kwa goli 2-0,uwanja wa taifa.
Azam walianza mchezo huo kwa kasi na kuwatia hofu wapenzi wa Yanga,lakini Yanga walitulia na kuweza kupata bao dakika ya 44 kupitia kwa Hamis Kiiza na kuwafanya Azam kupoteana kipindi cha pili,Yanga walipata bao la pili dakika za mwisho kupitia kwa Said Bahanuzi.
Yanga wamechukua kwa mara ya pili mfululizo huku ikiwa na kocha mpya kutoka Belgium,Tom Saintfiet
Thursday, July 26, 2012
YANGA NA AZAM FC KUCHEZA FAINALI KOMBE LA KAGAME
Timu ya Yanga na Azam FC zimefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Kagame baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali leo iliyochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Azam wamefanikiwa kuingia fainali baada ya kuwachapa Vita Club ya DRC goli 2-1,kupitia kwa John Bocco na Mrisho Ngasa kwenye mechi iliyochezwa mchana,kwenye mchezo wa pili Yanga ililazimika kucheza kwa dk.120 na hatimaye kupata bao pekee dk.99 kupitia kwa Hamis Kiiza aliyezifumania nyavu za wapinzani wao.
Kwa matokeo hayo timu hizo zitakutana kwenye fainali.
Wednesday, July 25, 2012
AZAM FC YAICHAKAZA SIMBA 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI
Simba imechezea kichapo cha aibu kutoka kwa Azam FC cha mabao 3-1,kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Kagame.
Azam FC walipata goli la kwanza dk.17 likifungwa na John Boko ambaye alikuwa mwiba kwenye ngome ya Simba kwa kupachika mabao yote,dk ya 46 aliipatia bao la pili na Simba walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Shomari Kapombe dk.53 kwa juhudi zake binafsi,kama vile haitoshi John Boko alitupia tena kimiani bao la 3 na kuwafanya Simba wachanganyikiwe zaidi.
Mchezo mwingine uliochezwa mchana timu ya Vita Club ya DRC iliichapa Atletco ya Burundi 2-1,sasa Azam itakutana Vita Club huku Yanga wakicheza na APR ya Rwanda nusu fainali tarehe 26.
Tuesday, July 24, 2012
YANGA YAINGIA NUSU FAINALI KAGAME CUP.
Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Kagame Yanga ya Dar es salaam,wamefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuwatoa timu ngumu ya Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-3.
Hadi dakika 90 zikimalizika matokeo yalikuwa 1-1,Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 likifungwa na Othman Mmanga kwa njia ya kichwa na Yanga walisawazisha bao dakika ya 47 kupitia kwa Said Bahanuzi.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali APR ya Rwanda iliwachapa URA ya Uganda bao 2-1,michezo mingine ya nusu fainali itachezwa kati ya Azam na Simba,Atletco ya Burundi na Vita SC ya DRC.
Sunday, July 08, 2012
TENKI LA MAJI LAMWAGA MAJI MENGI SIMIKE MBEYA.
Hii inasikitisha sana kuona mamlaka husika ikiwa imekaa kimya kwa muda mrefu,kutokana na upotevu wa maelfu ya lita za maji kupotea bila kutumika huku maji hayo yakitiririka na kuingia mto Mabatini kutoka tenki la maji la mtaa wa Simike,jijini Mbeya na kusababisha baadhi ya wakazi wa eneo kukosa maji kwa muda kutokana na tatizo hilo.
Mamlaka husika inaombwa kushughulikia tatizo hili ambalo limekuwa kero kwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo kutokana na maji hayo yanayovuja kwa wingi kupita milangoni mwao.
WEWA SEPETU NA JAQUILINE WOLPER HAKUNA MBABE.
Lile pambano la ndondi la wasanii wa filamu nchini,lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki,limemalizika matokeo yakiwa sare.
Mpambano uliojulikana kama usiku wa matumaini ulionekana kama mchezo wa kuigiza kutokana na wahusika kutokuwa na fani ya mchezo huo wa ndondi,japo Wolper akionekana kumzidi ujanja mpinzani wake.
WEWA SEPETU NA JAQUILINE WOLPER HAKUNA MBABE.
Lile pambano la ndondi la wasanii wa filamu nchini,lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki,limemalizika matokeo yakiwa sare.
Mpambano uliojulikana kama usiku wa matumaini ulionekana kama mchezo wa kuigiza kutokana na wahusika kutokuwa na fani ya mchezo huo wa ndondi,japo Wolper akionekana kumzidi ujanja mpinzani wake.
Monday, July 02, 2012
HISPANIA BINGWA ULAYA 2012
Timu ya taifa ya Hispania imechukua kwa mara nyingine ubingwa wa Ulaya baada ya kuwafunga Italia bao 4-0 jijini Kiev,Ukraine.
Hispania walipata bao la kwanza kupitia kwa David Silva dakika ya 14,goli la pili dak.41 likifungwa na Jordi Alba,goli la tatu likifungwa na Fernando Torres dk.84 na la nne likifungwa na Juan Matta dk.88,Hispania sasa inakuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hilo mfululizo toka michuano hiyo ilipoanzishwa.
Mashabiki hawakutegemea matokeo hayo ya Italia kufungwa goli nyingi kutokana na timu hiyo kuwa na ukuta imara,Hispania wenye uwezo wa kuuchezea mpira walimiliki wapinzani vilivyo na kuwafanya washindwe kufurukuta akiwemo mtukutu Mario Balotteli.
Subscribe to:
Posts (Atom)