Mabingwa wa Afrika mashariki na kati timu ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 24 tangu ligi ihanzishwe 1965 kwa kuwafunga watani wao wa jadi Simba kwa goli 2-0.
Magoli ya mabingwa hao yalifungwa na Didier Kavumbagu dk ya 5 huku la pili likifungwa na Hamis Kiiza dk ya 63,Yanga walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kushangiliwa kwa muda wote na mashabiki wake.
Simba walikosa penati dk ya 26 iliyopigwa na Mussa Mude lakini kwa umahiri wa kipa Ally Mustapha aliweza kuidaka penati hiyo.Sasa Yanga italikilisha Taifa kwenye michezo ya klabu bingwa Afrika na mshindi wa pili Azam atashiriki kombe la shirikisho Afrika.
Wawakilishi pekee wa Tanzania waliokuwa wamebaki kwenye michuano ya kimataifa,timu ya AZAM FC leo wametolewa na AS FAR RABAAT ya Morocco kwa kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa nchini Morocco.
Azam walipata bao la kuongoza dakika ya 6 likifungwa na John Bocco na Far Rabaat walifanikiwa kusawazisha dakika ya 12 na kupata goli la pili dakika ya 43,dakika za mwisho wa mchezo Azam waliweza kupata penati lakini bahati haikuwa yao baada ya penati yao kugonga mwamba penati ilipigwa na John Bocco.
Mwamuzi alitoa kadi nyekundu tatu,moja kwa Far Rabaat na mbili kwa Azam, wadau wa soka wameisifu Azam kwa kuwa na maandalizi mazuri ya michuano ya kimataifa na kutegemea msimu ujao kufanya vizuri zaidi hii ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano mikubwa kama hii.
Timu ya Barcelona jana imepokea kipigo cha goli 3-0 nyumbani kutoka Bayern Munich na kutolewa kwenye nusu fainali na wajerumani hao
Mchezo wa kwanza uliochezwa Alienz Arena wiki moja iliyopita Barcelona walifungwa goli 4-0.
Bayern Munich sasa watakutana na wajerumani wenzao wa Borussia Dortmund kwenye mchezo wa fainali utaofanyika uwanja wa Wembly nchini Uingereza.