Monday, October 24, 2011
Thursday, October 20, 2011
GADAFFI AFA KISHUJAA
Aliyekuwa rais wa Libya Muamar Gadaffi leo ameuawa na jeshi la waasi lililom
muondoa madarakani baada ya kumshika na kumjeruhi kwenye mji wake alikozaliwa na kupelekea kifo chake.
Gadaffi tofauti na marais wengine yeye aliendelea kubakia nchini kwake pamoja na sehemu ya nchi kushikiliwa na waasi,aliendelea na kuishi kwenye mji wa Sirte ambako ndiko alikozaliwa.
muondoa madarakani baada ya kumshika na kumjeruhi kwenye mji wake alikozaliwa na kupelekea kifo chake.
Gadaffi tofauti na marais wengine yeye aliendelea kubakia nchini kwake pamoja na sehemu ya nchi kushikiliwa na waasi,aliendelea na kuishi kwenye mji wa Sirte ambako ndiko alikozaliwa.
Tuesday, October 18, 2011
Sunday, October 16, 2011
LIVERPOOL YAWATOA ULIMI NJE MANCHESTER UNITED
Timu ya Liverpool ikicheza kwa maelewano jana iliweza kutoka sare na Manchester Utd kwa kufungana bao 1-1 kwenye uwanja Anfield,Liverpool walipata bao dakika ya 67 kupitia kwa Steven Gerrald na Manchester walisawazisha dak.80 kupitia kwa Chicharito.
Liverpool walitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kuwafanya walinzi wa Man kuwa na wakati mgumu.
Saturday, October 15, 2011
Tuesday, October 11, 2011
Tuesday, September 27, 2011
Saturday, September 17, 2011
Mh.MBOWE AFUNGUA OFISI YA CHADEMA KATA YA NZOVWE MBEYA.
Mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo mh.Freeman Mbowe leo jioni amefungua ofisi chama hicho katika kata ya Nzovwe jijini Mbeya na ufunguzi huo kuhudhuriwa na watu wengi.
Pia alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wakazi wa jiji la Mbeya baada ya moto kuteketeza soko la Mwanjelwa jana asubuhi.
Friday, September 16, 2011
BREAKING NEWS!! SOKO LA MWANJELWA MBEYA LINAENDELEA KUUNGUA MUDA HUU
Moto unaendelea kuteketeza mabanda yaliyoko ndani ya soko la Mwanjelwa Mbeya,mpaka sasa jitihada za kuuzima moto zinaonekana kuzidiwa nguvu na moto huo.
Moto ukiendelea kuteketeza soko hilo |
Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto |
Baadhi ya wafanyabiashara wakijaribu kuokoa bidhaa zao |
Wednesday, September 14, 2011
MARY MWANJELWA AKABIDHI MAGODORO 90 HOSPITALI YA WAZAZI NA KITUO CHA AFYA MBEYA
Mbunge wa viti maalum CCM,Mhe.Mary Mwanjelwa akikabidhi magodoro 7o kwa Dr.Peter Msafiri wa hospitali ya wazazi meta mjini Mbeya mchana,huku akiwa ameongozana na wakina mama wakereketwa wa chama cha mapinduzi jijini Mbeya,Mh.Mary Mwanjelwa pia atakabidhi magodoro mengine 20 kwenye kituo cha afya Ruanda mchana huu.
Dr.Peter Msafiri akimkaribisha mheshimiwa mbunge Mary Mwanjelwa.
Mama Sichela akiwaongoza wenzake kufurahia msaada huo |
Monday, September 12, 2011
BOMBA LA MAFUTA LALIPUKA NA KUPASUKA NAIROBI NA KUSABABISHA WATU ZAIDI YA 100 KUFARIKI
Bomba la mafuta limelipuka na kupasuka jijini Nairobi Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100,bomba hilo linalomilikiwa na serikali ya Kenya limekatiza katikati ya jiji na mlipuko huo umeanzia eneo la Lungalunga jijini Nairobi,askari wa zimamoto wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mmoja wa majeruhi wa moto akipakiwa kwenye gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali
Mmoja wa majeruhi wa moto akipakiwa kwenye gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali
AFRIKA KUSINI YALETA WAOKOAJI ZANZIBAR
Baadhi ya wananchi wakipita kutambua miili ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali ya meli huko Nungwi Zanzibar.
Saturday, September 10, 2011
MV.SPICE ISLANDER YAZAMA KASKAZINI UNGUJA NA KUSABABISHA MSIBA MKUBWA
Askari wa vikosi mbalimbali wanashiriki katika uokoaji wa abiria na hapa wanaonekana wakiwa wamembeba bi.Mariam Mohamed Murad kutoka Tanga aliyenusurika kwenye ajali hiyo ya meli |
Thursday, September 08, 2011
VODACOM YAKUBALI YAISHE KWA YANGA
Mabingwa wa Tanzania Bara jana walivaa jezi zenye nembo ya wadhamini wa ligi hiyo ya Vodacom premier league kwa mara ya kwanza,Yanga walikuwa wakigoma kuvaa jezi zenye nembo ya Vodacom kutokana na kuwa na rangi nyekundu na nyeupe ambayo inatumiwa na mahasimu wao na hivyo kuwapa wakati mgumu wadhamini hao na kulazimika kuweka nembo nyeusi au ya kijani kwenye jezi za wanajangwani hao
TWIGA STARS YAWAONYESHA KIWANGO BANYANA BANYANA LEO
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (TWIGA STARS) leo imeweza kutoka sare ya magoli 2-2 na wanawake wenzao wa Afrika kusini katika mchezo mkali na kuvutia uliochezwa mchana huu jijini Maputo,mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya hadi zinakwenda zikiwa nguvu sawa. Kipindi kilianza kwa Afrika ya kusini kujipatia goli lililofungwa na Samatha Skity dakika ya 48 kwa krosi iliyojaa moja kwa moja kimiani,kufuatia bao hilo Tanzania waliongeza mashambulizi na kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Sharua Omar aliyewazidi ujanja mabeki wa Banyana Banyana.
Twiga Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ester Chabruma baada ya kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Zena Rashid na dakika ya 72 ilimwingiza Fridian ambaye alikosa goli baada kupiga kichwa kilichotoka sentimita chache.
Banyana Banyana walipata bao la pili kupitia kwa Chantelle Essau dakika ya 74 baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa Twiga Stars na dakika moja baadaye Twiga walisawazisha kupitia kwa Zena Rashid kwa njia ya kichwa kutokana na krosi safi toka upande wa kushoto na hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo
Twiga Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ester Chabruma baada ya kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Zena Rashid na dakika ya 72 ilimwingiza Fridian ambaye alikosa goli baada kupiga kichwa kilichotoka sentimita chache.
Banyana Banyana walipata bao la pili kupitia kwa Chantelle Essau dakika ya 74 baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa Twiga Stars na dakika moja baadaye Twiga walisawazisha kupitia kwa Zena Rashid kwa njia ya kichwa kutokana na krosi safi toka upande wa kushoto na hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo
Wednesday, September 07, 2011
Saturday, September 03, 2011
TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI
Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani huko Equatarial Guinea na Gabon,kwa matokeo haya ya leo yamezidi kupoteza matumaini ya kushiriki michuano hiyo kwa timu ya Taifa ambayo kwa mara ya mwisho ilishiriki michuano hiyo mwaka 1980
Taifa stars walipata bao dakika ya 24 kupitia kwa Mbwana Samata baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Nizar Khalfan,lakini kisicho riziki hakiliki Algeria walisawazisha goli hilo na kuonyesha kandanda safi kipindi cha pili kama vile walikuwa wakisoma mchezo kipindi cha kwanza.
Taifa Stars wakiwatumia wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi waliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia tatizo likiwa ni umaliziaji na makosa kadhaa ya walinzi wetu,mchezo huu umechezwa leo kwenye uwanja Taifa Dar es salaam.
Wachezaji wa Taifa stars Amir Maftah,Mbwana Samata na Dan Mruanda wakishangilia mara baada ya kujipatia bao la kuongoza dhidi ya Algeria |
Tuesday, August 30, 2011
Monday, August 29, 2011
Sir Alex Ferguson amshauri Wenger kufanya usajili makini kabla ya kesho kutwa.
Baada ya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 8-2 dhidi ya Arsenal,meneja wa Man Utd amemshauri kocha wa Arsenal kufanya usajili makini kwa masaa 48 yaliyobaki kabla ya msimu wa usajili kufungwa hapo jumatano.
Naye Wenger amesema sababu ya kipigo hicho ni uchovu wa wachezaji wake ambao jumatano iliyopita walicheza na Udinesse ya Italia kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na hivyo kusababisha majeruhi kwenye kikosi hicho na kufanya wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kutocheza.
Wenger ni kocha pekee aliyeiletea mafanikio timu ya Arsenal na kuifanya kuwa na wapenzi wengi duniani lakini mambo sasa yanataka kumuendea kombo kutokana na kipigo hicho kikubwa ambacho kwa mara ya mwisho timu hiyo ilifungwa mabao 8-0 mwaka 1896,hata hivyo Wenger amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo duniani kote.
Sunday, August 28, 2011
Manchester yaifanyia kufuru Arsenal yawachapa 8-2
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza leo wameifanyia kitu mbaya timu ya Arsenal kwa kuichapa mabao 8-2,kichapo hicho ni kikubwa kwa maisha ya mzee Arsenal Wenger ambaye ana tabia ya kujiamini sana,na sasa amekuwa na wakati mgumu kubaki kwenye timu hiyo ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu na inasemekana ndiye kocha pekee aliyeleta mabadiliko kwenye ligi hiyo ya Uingereza na kufuta ubaguzi wa rangi.
Lakini kutokana na kipigo cha leo kinamuweka kwenye wakati mgumu zaidi hasa baada ya kuwauza wachezaji wake nyota na kushindwa kutafuta mbadala wao,pamoja na bodi ya klabu hiyo kuruhusu fedha zitumike kwenye usajili wa msimu huu lakini alikaidi agizo hili.
Mechi hii imehudhuriwa na watazamaji 73414 kwenye dimba la Old Trafford na Man U kuibuka na ushindi mnono wa bao 8-2.
HII NDIYO KYELA BWANA
Kama kuna wilaya ambayo wanafahamu matumizi na umuhimu wa baiskeli hatuwezi kuacha kuitaja wilaya ya Kyela,kwenye picha ni baadhi ya baiskeli ambazo zimeegeshwa eneo la shule na bado ukipita mitaani wakina utawakuta wakiendesha na mtoto mgongoni,ukiuliza safari ya wapi?unajibiwa anaenda kliniki au kabeba bonge la mzigo
Tuesday, August 23, 2011
MPAKANI MWA TANZANIA NA MALAWI
Hapa ndio mpaka wa Tanzania na Malawi unaojulikana kwa jina la Border ya Kasumulu ambayo inaonekana na utulivu wa hali ya juu tofauti na mipaka mingine.
Huu ndio mto unayozitenganisha nchi hizi mbili |
Baadhi ya magari ya mizigo yakisubiri kupita mpakani | <><>Eneo la Malawi likiwa linafanyiwa ukarabati
Monday, August 22, 2011
Sunday, August 21, 2011
MZIMU WA SIMBA WAENDELEA KUITAFUNA YANGA
Mabingwa wa Tanzania bara leo wameanza ligi ya Vodacom vibaya,baada ya kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu ikiwa ni siku chache baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mahasimu wao Simba cha bao 2-0 kwenye mchezo wa ngao ya hisani,JKT Ruvu walipata bao kwa njia ya penati dakika 22 iliyofungwa na Kesy Mapande kutokana na mlinzi wa Yanga Chacha Marwa kucheza faulo eneo la hatari.
JKT Ruvu walitumia mbinu iliyotumiwa na Simba ya kuchezesha viungo wengi katikati na hivyo kuwafanya viungo wa Yanga Nurdin Bakari na Haruna Niyonzima kushindwa kuonyesha umahiri wao ipasavyo.
Na huko Arusha Simba wameanza ligi vyema baada ya kuwalaza JKT Oljoro mabao 2-0.
Saturday, August 20, 2011
Friday, August 19, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)