Monday, May 30, 2011
Sunday, May 29, 2011
BARCELONA BINGWA ULAYA
Timu ya Barcelona imetwaa ubingwa wa ulaya baada kuwachapa Manchester united bao 3-1,goli la kwanza la Barca liliwekwa kimiani na Pedro na Man walisawazisha kupitia Wayne Rooney hadi mapumziko timu hizo zilikuwa nguvu sawa,kipindi cha pili Barcelona walifanikiwa kupata mabao mawili kupitia kwa Leone Messi na David Villa mechi hiyo imechezwa kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Saturday, May 28, 2011
WYDAD CANSABLANCA YAICHAPA SIMBA 3-0.
Timu ya Simba leo imefungwa jumla ya mabao 3-0 na Wydad Cansablanca ya Morroco magoli ya wamorroco hao yamefungwa dakika ya 87 na mengine mawili yakifungwa dakika za majeruhi,mchezo huo umechezwa kwenye uwanja Petrosport jijini Cairo,na hivyo kuzima ndoto za Simba kucheza hatua ya makundi klabu bingwa Africa,sasa wataingia kwenye michuano ya kombe la shirikisho na kucheza na Motema Pembe ya Congo
Wednesday, May 25, 2011
MBEYA YAINGIA FAINALI KOMBE LA TAIFA
Timu ya mkoa wa Mbeya(Mapinduzi stars) imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya kombe la taifa,baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Kagera kwa jumla ya mabao 2-1,mchezo huo umechezwa kwa dakika 120,hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1,Mbeya ndio waliofanikiwa kupata ushindi baada ya beki wa Kagera kujifunga baada ya shambulizi kutokea golini kwao,mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kucheza soka maridadi na golikipa wa Mbeya Ivo Mapunda kuonyesha uwezo mkubwa,Mbeya watakutana na Mwanza Heroes siku ya jumamosi uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha katika fainali.
Thursday, May 19, 2011
SIMBA KUVAANA NA WYDAD CANSABLANCA CAIRO
Timu ya Simba imfanikiwa kurudi kwenye michuano ya klabu bingwa Africa baada ya rufaa yao kukubaliwa na shirikisho la soka Africa(CAF) na kuitupia mbali timu ya TP Mazembe ambao ndio mabingwa wa kombe hilo baada ya kumchezesha mlinzi halali wa timu ya Esperence ya Tunisia,sasa simba watacheza na wydad cansablanca ya Morocco kwenye uwanja huru huko jijini Cairo
Sunday, May 15, 2011
Thursday, May 12, 2011
Sunday, May 08, 2011
KOMBE LA TAIFA
Timu ya mkoa wa Rukwa imeweza kufanya maajabu kwa kuifunga timu ya mkoa wa Temeke kwa jumla ya bao 2-1,Rukwa walikuwa wa kwanza kupata goli kwa njia ya adhabu dakika 12 baadaye nao Temeke walisawazisha nao kwa njia ya adhabu,kipindi cha pili Rukwa walifanikiwa kupata bao la pili.Katika mchezo wa kwanza Mbeya walifanikiwa kuwafunga Iringa 2-1.
Thursday, May 05, 2011
MANCHESTER UTD USO KWA USO NA BARCELONA MEI 28
Wachezaji wa manchester united wakishangilia moja ya mabao waliopata jana kwenye mchezo wa klabu bingwa ulaya kati yake na SCHALKE 04,ambapo manchester walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 na kusonga kwa jumla mabao 6-1,sasa watakutana na Barcelona katika mchezo wa fainali tarehe 28 mei,kwenye uwanja wa Wembley England.
Wednesday, May 04, 2011
BARCELONA YATINGA FAINALI
Timu ya Barcelona jana ilifanikiwa kuingia fainali ya klabu bingwa ulaya baada ya kutoka sare na Real madrid 1-1,ilikuwa ni Barcelona iliyokuwa ya kwanza kujipatia lililofungwa Pedro dakika ya 56 madrid walisawazisha dakika ya 66 kupitia Marcus kwa matokeo hayo Barca wanaingia fainali na moja kati ya itakayoshinda leo kati Man utd v/s Schalke 04
Monday, May 02, 2011
Thursday, April 28, 2011
CHANGIA DAMU OKOA MAISHA
Waelimishaji kutoka kitengo cha taifa cha damu salama kanda ya nyanda za kusini,wakitoa elimu juu ya uchangiaji damu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lwati wilayani Mbozi-Mbeya.Kwa kutumia blog hii nawapongeza wafanyakazi wa kitengo husika na wale wote wenye moyo wa kujitolea kwa ajili ya wahitaji-Amen.
Sunday, April 24, 2011
Sunday, April 17, 2011
Saturday, April 16, 2011
AJALI MBAYA YATOKEA ARUSHA
Poleni ndugu zetu wa Arusha kwa msiba uliowapata kutokana na ajali ya iliyohusisha basi la kampuni ya ngorika na basi dogo aina ya hiace na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.
Thursday, April 14, 2011
SHITAMBALA AISALITI CHADEMA
Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha maendeleo mkoa wa Mbeya ameamua kuhama chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM,uamuzi wake umepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi mkoani Mbeya
Monday, April 11, 2011
YANGA BINGWA
Timu ya Yanga imetwaa ubingwa wa Tanzania bara baada ya kuifunga Toto African kwa jumla ya mabao 3-0,magoli ya Yanga yalifungwa na Nurdin Bakar na Davies Mwape yote kipindi cha pili,hivyo kuifanya Yanga kufikisha pointi 49 sawa na mahasimu wao Simba lakini wanakuwa mabingwa kwa tofauti ya magoli,Simba waliifunga Majimaji ya Songea bao 4-1.
Saturday, April 09, 2011
Wednesday, April 06, 2011
SIMBA ALMANUSRA KWA RUVU JKT
Mabingwa watetezi wa Tanzania bara Simba leo wamenusurika kichapo kutoka kwa maafande wa JKT RUVU baada ya kusawazisha bao kwa njia ya penati iliyofungwa na Emanuel Okwi,ilikuwa ni JKT RUVU iliyokuwa ya kwanza kujipatia bao la kuongoza kipindi cha kwanza lililowekwa kimiani na Hussein Bunu na kudumu hadi mapumziko,Simba ambao leo walionekana kubanwa vilivyo na wapinzani wao,mwamuzi wa mchezo huo alishindwa kuumudu mchezo huo na kuwatoa nje wachezaji wa JKT akiwemo Shabaan Dihile na George Minja,ligi hiyo itaendelea tena kesho kati ya Yanga dhidi ya African Lyon,Yanga wanahitaji ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kunyakua ubingwa.
VODACOM WABADILISHA RANGI YAO.
Linaloonekana ni jengo la Vodashop Mbeya,likiwa linaendelea kupigwa rangi tofauti na ile iliyozoeleka na wengi ya bluu sijui na jina litakuwaje?umekuwepo mchezo wa kubadili majina na rangi kwa baadhi ya makampuni ya simu kama vile mobitel wakaitwa Buzy na sasa tigo na Celtel wakaitwa Zain na sasa Airtel.
Friday, March 11, 2011
Thursday, March 10, 2011
SIMBA YAZIKALIA AZAM NA YANGA
Timu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara jana walifanikiwa kuongoza ligi kwa kuifunga Ruvu shooting ya Pwani kwa bao 1-0 dakika ya 87 likifungwa na mchezaji Ally Ahmed 'Shiboli' aliyeingia dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Mbwana Samata aliyebanwa vilivyo na mabeki wa Ruvu,sasa Simba imefikisha pointi 41 baada kucheza michezo 18,ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 39 huku Azam ikiwa na pointi 37
Tuesday, March 08, 2011
Monday, March 07, 2011
Friday, March 04, 2011
CRDB WAFUNGUA TAWI JIPYA MWANJELWA- MBEYA
Waziri wa maji,Profesa Mark Mwandosya (watatu kushoto) akikata utepe kufungua tawi jipya la benki ya CRDB eneo la Mwanjelwa jijini MBEYA,kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo bw.Martin Mmari,kulia ni mama Mwandosya,kufunguliwa kwa tawi hilo kutawasaidia wakazi wa jiji la Mbeya ambao walikuwa wakipanga foleni kwenye tawi pekee lililokuwa mjini Mbeya.
Subscribe to:
Posts (Atom)