BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Friday, November 11, 2011

Taifa Stars yaichapa Chad 2-1


Timu ya soka ya Tanzania leo imefanikiwa kupata ushindi ugenini kwa kuichapa timu ya taifa ya Chad mabao 2-1,mabao ya Taifa Stars yamefungwa na Mrisho Ngasa na Nurdin Bakar.

VURUGU ZATAWALA MBEYA LEO


Askari wa jeshi la polisi wakijaribu kutuliza ghasia maeneo ya tukio jijini Mbeya

Gari likiwa limebinuliwa na waandamanaji na kufunga barabara kuu ya Dar-Tunduma eneo la Kabwe


Matairi chakavu yakiwa yamechomwa katikati ya barabara  na kuleta taabu kwa wasafiri na moshi mzito kusambaa eneo la Kabwe (Picha kwa hisani ya  Mwaisango)


Thursday, November 10, 2011

WAKULIMA WA MANANASI RUNGWE WANAHITAJI SOKO LA UHAKIKA ILI KUBORESHA KILIMO CHA MATUNDA HAYO



Mfanyabiashara wa mananasi akikusanya mananasi kutoka kwa wakulima wa Ikuti wilayani Rungwe 


Wakazi wa kijiji cha Ikuti hujipumzisha maeneo haya mara baada ya kumaliza shughuli zao za kila siku
 

Wednesday, November 09, 2011

BONDIA JOE FRAZIER AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa nguli wa mchezo wa masumbwi kwenye miaka ya 60 na 70,Frazier amefariki juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa saratani ya ini.
Frazier alikuwa bondia wa kwanza kumpiga bingwa wa kipindi hicho Muhammad Ally katika mpambano uliochezwa DR Congo machi, 1971,amefariki akiwa na umri wa miaka 67,wapenzi wa mchezo huo wataendelea kumkumbuka kutokana na umahiri wake ulingoni na hasa kwa kumchapa bingwa aliyeshindikana Muhammad Ally.

Monday, November 07, 2011

WATOTO WANAPENDA KUPENDWA


Watoto wa shule ya msingi Itenya,kijiji cha Ngonga wilayani Kyela wakiwa na bw Benjamin alipopita maeneo ya kijiji hicho

Thursday, November 03, 2011

IRINGA YAENDELEA KUKUA KWA KASI


Mdau wetu akiwa kwenye kijiji cha Ilambilole wilayani Kilolo

Hapa akiwa mtaa wa Mshindo Iringa mjini

Mdau wetu akiwa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani mjini Iringa

Kati ya vivutio vilivyoko mkoani Iringa ni pamoja na mawe mazuri yaliyo kando ya barabara kuu

Tuesday, November 01, 2011

MASELE NA WENZAKE WAWALEMAZA WASAFIRI KITUO CHA MABASI MBEYA.


Msanii maarufu na wenzake toka jijini Dar es salaam,leo wamewateka wasafiri waliokuwepo kituo kikuu cha mabasi jijini Mbeya,na kuwafanya wabaki wakiwaangalia na kusahau kufanya mipango ya safari kutokana na vituko vyao vya maigizo walivyokuwa wakionyesha na kuwavutia wasafiri wengi na baadhi wafanyabiashara wa eneo hilo.

Saturday, October 29, 2011

YANGA YAICHAPA SIMBA 1-0


Mabingwa watetezi wa Tanzania bara leo wameichapa Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliyofanyika uwanja wa Taifa,Yanga walipata bao hilo dakika ya 72 kupitia kwa mshambuliaji wao wa kimataifa Davies Mwape baada ya walinzi wa Simba kufanya makosa,mchezo huo ulianza kwa kasi na Simba kutawala kipindi cha kwanza,Simba walipoteza nafasi kadhaa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga walijipanga na kubadili mchezo na hivyo kuwafanya waibuke na ushindi huo.
Michezo mingine ya ligi hiyo imechezwa huko Mwanza kati ya Toto African na Coastal Union matokeo ni 0-0,huko Dodoma ilikuwa ni kati ya Polisi na Oljoro matokeo ni 0-0,kwa matokeo haya bado hayabadili msimamo wa ligi bado Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 27,ikifuatiwa na Yanga yenye alama 24,Azam 21.

Monday, October 24, 2011

MANCHESTER CITY YAWAFANYIA VIBAYA MANCHESTER UNITED NDANI YA OLD TRAFFORD


Timu ya Manchester City leo imevunja mwiko wa Manchester United baada ya kuwaadhibu kwa goli 6-1 kwenye uwanja Old Trafford.
Manchester Utd imekuwa na rekodi ya kutofungwa kwenye uwanja wa nyumbani lakini leo imeweza kutokea tena idadi kubwa ya magoli.

Thursday, October 20, 2011

GADAFFI AFA KISHUJAA

Aliyekuwa rais wa Libya Muamar Gadaffi leo ameuawa na jeshi la waasi lililom
muondoa madarakani baada ya kumshika na kumjeruhi kwenye mji wake alikozaliwa na kupelekea kifo chake.
 Gadaffi tofauti na marais wengine yeye aliendelea kubakia nchini kwake pamoja na sehemu ya nchi kushikiliwa na waasi,aliendelea na kuishi kwenye mji wa Sirte ambako ndiko alikozaliwa.

Tuesday, October 18, 2011

HUU NDIO USAFIRI WA MLOWO-KAMSAMBA WILAYANI MBOZI.


Pamoja na ajali nyingi kugharimu maisha ya watu,lakini bado watu wamekuwa wakijisahau na kuvunja sheria za usalama barabarani kama inavyoonekana hapa gari ya mizigo ikiwa imebeba abiria wengi kupita kiasi na wengine kukaa juu ya mabomba.

Sunday, October 16, 2011

LIVERPOOL YAWATOA ULIMI NJE MANCHESTER UNITED


Timu ya Liverpool ikicheza kwa maelewano jana iliweza kutoka sare na Manchester Utd kwa kufungana bao 1-1 kwenye uwanja Anfield,Liverpool walipata bao dakika ya 67 kupitia kwa Steven Gerrald na Manchester walisawazisha dak.80 kupitia kwa Chicharito.
Liverpool walitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kuwafanya walinzi wa Man kuwa na wakati mgumu.

Saturday, October 15, 2011

LIGI DARAJA LA KWANZA,PRISON YAANZA VIBAYA MBEYA


Timu ya Tanzania Prison leo imeanza vibaya baada ya kufungwa bao 1-0 na timu ya Mbeya City Council,bao la Mbeya City limefungwa na Yona Ndabila kwa njia ya penati kipindi cha kwanza,hadi mapumziko Prison walikuwa nyuma kwa bao 1

Tuesday, October 11, 2011

TUWE NA MOYO WA KUJITOLEA DAMU KWA AJILI YA KUWASAIDIA WAGONJWA MAHOSPITALINI

Darling Lyatuu naye akichangia damu siku ya leo chini ya uangalizi wa mtaalamu wa kitengo cha taifa cha damu salama bi.Joyce Yonael Msuya.

Tuesday, September 27, 2011

BASI LAANGUKIA KORONGONI, ABIRIA WANUSURIKA

Basi la kampuni ya Budget leo limeangukia korongoni maeneo ya mlima Kitonga,kwa bahati nzuri hakuna abiria aliyepoteza maisha katika ajali hiyo,isipokuwa kuna majeruhi kadhaa.

Saturday, September 17, 2011

Mh.MBOWE AFUNGUA OFISI YA CHADEMA KATA YA NZOVWE MBEYA.


Mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo mh.Freeman Mbowe leo jioni amefungua ofisi chama hicho katika kata ya Nzovwe jijini Mbeya na ufunguzi huo kuhudhuriwa na watu wengi.
Pia alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa wakazi wa jiji la Mbeya baada ya moto kuteketeza soko la Mwanjelwa jana asubuhi.

Friday, September 16, 2011

BREAKING NEWS!! SOKO LA MWANJELWA MBEYA LINAENDELEA KUUNGUA MUDA HUU

Moto unaendelea kuteketeza mabanda yaliyoko ndani ya soko la Mwanjelwa Mbeya,mpaka sasa jitihada za kuuzima moto zinaonekana kuzidiwa nguvu na moto huo.

Moto ukiendelea kuteketeza soko hilo

Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto

Baadhi  ya wafanyabiashara wakijaribu kuokoa bidhaa zao


Wednesday, September 14, 2011

MARY MWANJELWA AKABIDHI MAGODORO 90 HOSPITALI YA WAZAZI NA KITUO CHA AFYA MBEYA

Mbunge wa viti maalum CCM,Mhe.Mary Mwanjelwa akikabidhi magodoro 7o kwa Dr.Peter Msafiri wa hospitali ya wazazi meta mjini Mbeya mchana,huku akiwa ameongozana na wakina mama wakereketwa wa chama cha mapinduzi jijini Mbeya,Mh.Mary Mwanjelwa pia atakabidhi magodoro mengine 20 kwenye kituo cha afya Ruanda mchana huu.

Dr.Peter Msafiri akimkaribisha mheshimiwa mbunge Mary Mwanjelwa.

Gari likiwa limebeba magodoro yaliyotolewa na mh.Mary Mwanjelwa
Mama Sichela akiwaongoza wenzake kufurahia msaada huo

Monday, September 12, 2011

BOMBA LA MAFUTA LALIPUKA NA KUPASUKA NAIROBI NA KUSABABISHA WATU ZAIDI YA 100 KUFARIKI

Bomba la mafuta limelipuka na kupasuka jijini Nairobi Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100,bomba hilo linalomilikiwa na serikali ya Kenya limekatiza katikati ya jiji na mlipuko huo umeanzia eneo la Lungalunga jijini Nairobi,askari wa zimamoto wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mmoja wa majeruhi wa moto akipakiwa kwenye gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali

AFRIKA KUSINI YALETA WAOKOAJI ZANZIBAR

Baadhi ya wananchi wakipita kutambua miili ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali ya meli huko Nungwi Zanzibar.
 <><>
<>
<><>Baadhi ya watalii wakishiriki kuwahudumia watoto waliokolewa kwenye meli eneo la Nungwi Zanzibar
Mtoto Said Gerald akiwa hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar mara baada ya kuokolewa kwenye ajali ya meli


Saturday, September 10, 2011

MV.SPICE ISLANDER YAZAMA KASKAZINI UNGUJA NA KUSABABISHA MSIBA MKUBWA






Meli ijulikanayo kwa jina la Mv. SPICE ISLANDER inayofanya safari zake kati ya Pemba na Unguja,jana usiku ilipata dhoruba na kupinduka hatimaye kuzama na kusababisha zaidi ya watu 100 kupoteza maisha,japokuwa jitihada kuokoa watu abiria zinaendelea na mpaka sasa wameshaokolewa zaidi ya abiria 150 wakiwa hai na shughuli hiyo inaendelea.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi  Dr. Ally M.Shein  na makamu wa rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad wakiwa na huzuni kubwa walipotembelea eneo la ufukwe wa Nungwi kuangalia ajali hiyo ya meli.


Askari wa vikosi mbalimbali wanashiriki katika uokoaji wa abiria na hapa wanaonekana wakiwa wamembeba bi.Mariam Mohamed Murad kutoka Tanga aliyenusurika kwenye ajali hiyo ya meli


Thursday, September 08, 2011

VODACOM YAKUBALI YAISHE KWA YANGA

Mabingwa wa Tanzania Bara jana walivaa jezi zenye nembo ya wadhamini wa ligi hiyo ya Vodacom premier league kwa mara ya kwanza,Yanga walikuwa wakigoma kuvaa jezi zenye nembo ya Vodacom kutokana na kuwa na rangi nyekundu na nyeupe ambayo inatumiwa na mahasimu wao na hivyo kuwapa wakati mgumu wadhamini hao na kulazimika kuweka nembo nyeusi au ya kijani kwenye jezi za wanajangwani hao

TWIGA STARS YAWAONYESHA KIWANGO BANYANA BANYANA LEO

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (TWIGA STARS) leo imeweza kutoka sare ya magoli 2-2 na wanawake wenzao wa Afrika kusini katika mchezo mkali na kuvutia uliochezwa mchana huu jijini Maputo,mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya hadi zinakwenda zikiwa nguvu sawa.  Kipindi kilianza kwa Afrika ya kusini kujipatia goli lililofungwa na Samatha Skity dakika ya 48 kwa krosi iliyojaa moja kwa moja kimiani,kufuatia bao hilo Tanzania waliongeza mashambulizi na kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Sharua Omar aliyewazidi ujanja mabeki wa Banyana Banyana.
  Twiga Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ester Chabruma baada ya kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Zena Rashid na dakika ya 72 ilimwingiza Fridian ambaye alikosa goli baada kupiga kichwa kilichotoka sentimita chache.
 Banyana Banyana walipata bao la pili kupitia kwa Chantelle Essau dakika ya 74 baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa Twiga Stars na dakika moja baadaye Twiga walisawazisha kupitia kwa Zena Rashid kwa njia ya kichwa kutokana na krosi safi toka upande wa kushoto na hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo

Wednesday, September 07, 2011

JIENDELEZE SACCOS YAWASAIDIA WAKULIMA WA MAHINDI IWINDI MBEYA.


Wakulima wa mahindi kata ya Iwindi Mbeya vijijini wamenufaika na viongozi wao baada ya kuanzisha uwekaji akiba kwa kutumia mazao na ambayo baadaye huuzwa na mkulima kuingiziwa amana kwenye SACCOS na kuwawezesha kupata mikopo midogo dogo.

BIASHARA YA KUKU IWINDI MBEYA


Mfanyabiashara eneo la kata ya Iwindi Mbeya vijijini,akiuza kuku kwa kutumia baiskeli na kuwafunga kuku kama mzigo fulani vile.

Saturday, September 03, 2011

TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani huko Equatarial Guinea na Gabon,kwa matokeo haya ya leo yamezidi kupoteza matumaini ya kushiriki michuano hiyo kwa timu ya Taifa ambayo kwa mara ya mwisho ilishiriki michuano hiyo mwaka 1980
  Taifa stars walipata bao dakika ya 24 kupitia kwa Mbwana Samata baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Nizar Khalfan,lakini kisicho riziki hakiliki Algeria walisawazisha goli hilo na kuonyesha kandanda safi kipindi cha pili kama vile walikuwa wakisoma mchezo kipindi cha kwanza.
 Taifa Stars wakiwatumia wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi waliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia tatizo likiwa ni umaliziaji na makosa kadhaa ya walinzi wetu,mchezo huu umechezwa leo kwenye uwanja Taifa Dar es salaam.


Wachezaji wa Taifa stars Amir Maftah,Mbwana Samata na Dan Mruanda wakishangilia mara baada ya kujipatia bao la kuongoza dhidi ya Algeria