Sunday, December 30, 2012
Sunday, December 23, 2012
TAIFA STARS YAWACHAPA MABINGWA WA AFRIKA
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars imewalaza mabingwa wa soka wa Afrika Zambia(Chipolopolo) goli 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Goli pekee la Taifa Stars lilifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 45 huku Zambia wakiwatumia wachezaji wao makini kama Christopher Katongo,Felix Katongo na Nathan Sinkala lakini hawakuweza kubadili matokeo.
Saturday, December 01, 2012
MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI-MBEYA.
Mamia ya wakazi wa Mbozi Mission wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ambayo yamefanyika kimkoa wilayani Mbozi.
Mh.Kandoro amewaasa wananchi kuepukana na tabia hatarishi na kutowanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi.
Mh.Kandoro aliwaongoza wananchi katika zoezi la kuchangia damu kwa hiari,baada ya kuchangia damu siku ya leo kwenye viwanja vya Mbozi Mission.
Thursday, November 29, 2012
Monday, November 26, 2012
UGANDA YAANZA VYEMA KOMBE LA CHALENJI.
Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuwafunga Harambee Stars 1-0 kwenye uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala.
Goli la Uganda lilifungwa na Geofrey Kizito dakika ya 74 akiunganisha krosi ya Iguma.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo Burundi wameifunga Malawi bila huruma mabao 5-0 na Kilimanjaro Stars(Tanzania) wamewafunga Sudan 2-0
Wednesday, November 21, 2012
SERA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA BADO IPO SANA.
Wananchi wa kata ya Isyonje wilaya ya Mbeya vijijini,wakifyatua tofali kwa ajili ya kuongezea majengo ya shule ya msingi.
Mdau wetu alitembelea kata hiyo na kufurahishwa na ushirikiano huo na yeye kushiriki kama anavyoonekana pichani akiwa anafyatua tofali.
Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu ni maneno ya Baba ya Taifa yaliyojaa hekima na busara.
Saturday, October 13, 2012
MTOTO AZUA BALAA MBAGALA KWA KUKOJOLEA QU-RAAN
Mtoto wa kidato cha kwanza amezua balaa na kusababisha kuvunjika kwa amani kwa muda eneo la Mbagala-Kizuiani, kutokana na kitendo cha kukojolea Qu-raan wakati alipokutana na mtoto mwenzie ambaye alikuwa na kitabu hicho na kuanza ubishi uliopelekea mtoto kufanya kitendo hicho ambacho kimetokana na utoto na kusababisha watu wazima kupandwa na jazba na kuanzisha maandamano yaliyopelekea uharibifu wa vitu mbalimbali yakiwemo makanisa na magari.
Wednesday, September 19, 2012
MTIBWA YAICHAKAZA YANGA 3-0
Timu ya Mtibwa Sugar FC leo wamewafunga Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga kwa bao 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
Yanga ikiwa imesheheni wachezaji wake nyota,walishindwa kuwadhibiti Mtibwa ambao safu ya kiungo ilionekana kucheza vizuri chini ya Shabaan Kisiga na Shaban Nditi.
Matokeo mengine ni kama ifuatavyo:-
Toto African 2-Azam 2
Prison 1-Coastal 1
African Lyon 2-Polisi 1
JKT Oljoro 0-Kagera 0
Simba 2-JKT Ruvu 0
Ruvu Shooting 1-Mgambo 0
Tuesday, September 04, 2012
DAUD MWANGOSI AZIKWA LEO TUKUYU MBEYA.
Katibu mkuu wa taifa wa CHADEMA akiweka shada la maua kwenye kaburi la Daud Mwangosi ambaye alikuwa mwandishi wa kituo cha televisheni Chanel Ten,ambaye aliuawa juzi katika vurugu kati ya polisi na wananchi wanaosadikiwa na wanachama wa Chadema huko Nyololo wilayani Mufindi.
Marehemu Daud Mwangosi amezikwa kijijini kwao Busoka,Tukuyu,watu wengi wamehudhunishwa na kifo hicho na kulitupia lawama jeshi la polisi.
DAUD MWANGOSI AZIKWA LEO TUKUYU MBEYA.
Katibu mkuu wa taifa wa CHADEMA akiweka shada la maua kwenye kaburi la Daud Mwangosi ambaye alikuwa mwandishi wa kituo cha televisheni Chanel Ten,ambaye aliuawa juzi katika vurugu kati ya polisi na wananchi wanaosadikiwa na wanachama wa Chadema huko Nyololo wilayani Mufindi.
Marehemu Daud Mwangosi amezikwa kijijini kwao Busoka,Tukuyu,watu wengi wamehudhunishwa na kifo hicho na kulitupia lawama jeshi la polisi.
Sunday, September 02, 2012
MJASILIAMALI WA KATAVI
Pamoja na kuwepo kwa ushindani wa soko za bidhaa zetu kwenye masoko ya nje,bado Tanzania tuna nafasi ya kuibua vipaji vilivyo vijijini na kuviendeleza,kamera yetu ilimkuta fundi huyu wa vinu(pichani) akitengeneza vinu vidogo kwa kutumia nyenzo duni.
Bidhaa kama hizi zimekuwa zikitumika majumbani na baadhi ya watalii wakinunua kama mapambo au ukumbusho wao kutembelea Afrika,inatakiwa mipango mizuri ya kuwawekea wabunifu wetu misingi mizuri ili kuwafanya wasonge mbele
YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1
Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga ya Dar es salaam jana wameweza kuwafunga Coastal union ya Tanga 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa taifa.
Coastal walipata goli lao dakika ya 16 likifungwa na Razak Khalfan goli hilo lilidumu hadi dakika ya 84 pale beki wa Coastal Phil Kaira alipojifunga,bao la pili lilifungwa na Said Bahanuzi dakika ya 86.
Yanga iliwachezesha wachezaji wake wapya akiwemo Twite.
MBUYU TWITE APATA MAPOKEZI MAKUBWA.
Mchezaji wa Yanga raia wa DRC ameingia Nchini kwa mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo,ambao walikuwa wakimsubiri kwa muda mrefu.
Mashabiki hao walimpatia jezi namba 4 yenye jina la Rage ambaye ni mwenyekiti wa Simba kama kumdhihaki Rage ambaye alimsajili mchezaji huyo na baadaye mchezaji huyo kurudisha fedha na kusajili Yanga kwa kitita kikubwa zaidi.
Pamoja na mapokezi makubwa aliyopata mchezaji huyo,wadau wa soka wamemtaka kufanya kile kilichomleta mashabiki huwa hawachelewi kubadilika katika mchezo wa soka na kumuona si chochote.
Sunday, August 26, 2012
SENSA YAENDELEA NCHINI KWA UTULIVU MKUBWA
Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na familia yake wakishiriki zoezi la kuhesabiwa na kujibu maswali ya makarani wa sensa kwa utulivu mkubwa.
Wewe mwananchi ambaye bado hujafikiwa na makarani wa Sensa fuatilia kwa Mwenyekiti wako wa mtaa ili uhakikishe unahesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu,kuhesabiwa kwako ndio kunalifanya taifa lielewe idadi ya watu na kupanga maendeleo na huduma za kijamii kwa eneo husika-JITOKEZE KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU YA BAADAYE.
Friday, August 24, 2012
YANGA NDANI YA IKULU YA RUANDA
Rais Paul Kagame akiongea na wachezaji na viongozi wa timu ya Yanga ambao ni mabingwa wa Afrika mashariki na kati walipomtembelea Ikulu ya Ruanda,jijini Kigali jana.
Pia timu hiy6 imetembelea makaburi ya watu waliouawa mwaka 1994 kwenye mauaji ya Kimbari nchini humo,mbali na hayo timu hiyo imekuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa soka wa nchini humo.
Tuesday, August 21, 2012
WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA MELES ZENAWI AMERIKI.
Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki dunia jana usiku nchini Belgium alikokuwa akipatiwa matibabu.
Bwana Zenawi aliingia madarakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Mengistu Hailemariam na kusababisha nchi hiyo kuingia kwenye mapigano ya kikabila na majirani zao Eriteria na baadaye akaweza kuleta amani nchini humo mpaka kifo chake hofu imetanda imetanda miongoni mwa wananchi kuwa huenda machafuko ya kikabila yakazuka tena baada ya kifo chake.
Makamu waziri mkuu wa nchi hiyo bw.Hailemariam Deselagan ndio ataongoza nchi hiyo mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2015.
Sunday, August 19, 2012
SIMBA B YANYAKUA UBINGWA WA ABC SUPER 8 KWA KUWACHAPA MTIBWA 4-3.
Timu ya Simba B leo imetwaa ubingwa wa Super 8 cup baada ya kuwafunga Mtibwa goli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa,Dar es salaam.
Timu ya Simba B ambayo inaonyesha kandanda safi iliingia fainali kwa kuwatoa Azam FC kwa goli 2-1 na Mtibwa waliwatoa Jamhuri kwa 5-1,kivutio cha mchezo wa leo alikuwa Christopher Edward ambaye alifunga magoli matatu (hat trick) na kuweza kuchangia ushindi huo wa Simba B.
Nao wapenzi wa soka wamefurahishwa na kikosi cha Simba B na kuomba timu nyingine kuiga mfano huo,wengine wamedai kikosi hicho ni zaidi ya timu yao ya wakubwa na kama wakipambanishwa wanaweza kuwatia aibu kaka zao wa Msimbazi.
SIMBA B YANYAKUA UBINGWA WA ABC SUPER 8 KWA KUWACHAPA MTIBWA 4-3.
Timu ya Simba B leo imetwaa ubingwa wa Super 8 cup baada ya kuwafunga Mtibwa goli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa,Dar es salaam.
Timu ya Simba B ambayo inaonyesha kandanda safi iliingia fainali kwa kuwatoa Azam FC kwa goli 2-1 na Mtibwa waliwatoa Jamhuri kwa 5-1,kivutio cha mchezo wa leo alikuwa Christopher Edward ambaye alifunga magoli matatu (hat trick) na kuweza kuchangia ushindi huo wa Simba B.
Nao wapenzi wa soka wamefurahishwa na kikosi cha Simba B na kuomba timu nyingine kuiga mfano huo,wengine wamedai kikosi hicho ni zaidi ya timu yao ya wakubwa na kama wakipambanishwa wanaweza kuwatia aibu kaka zao wa Msimbazi.
Wednesday, August 15, 2012
PATRICE MUAMBA AJIUZULU SOKA
Mchezaji wa Bolton ya Uingereza ametangaza kujiuzulu soka kutokana na ushauri wa madaktari waliomfanyia upasuaji mdogo wa moyo nchini Belgium.
Muamba ametangaza uamuzi huo leo hii na kusema kwa sasa anaangalia afya yake na pia amewashukuru madaktari wote waliohangaikia uhai wake kwa muda ambao ulikuwa ni mgumu kwake baada ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu.
SIMBA B YAILAZA AZAM FC NA KUTINGA FAINALI YA SUPER8 ABC.
Timu ya Simba B imeweza kuwaduwaza Azam leo kwa kuwafunga bao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliofanyika uwanja wa Taifa.
Azam wakiwa na baadhi ya wachezaji wakongwe walishindwa kulimudu gwaride la watoto hao na kuambulia vumbi,magoli ya Simba yamefungwa na Rashid Idrisa na Christopher Edward wakati la Azam likifungwa na Zahor Pazi
Mechi nyingine ya nusu fainali ilipigwa saa nane mchana kati ya Mtibwa Sugar na Jamhuri ya Zanzibar,Mtibwa wamepata ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Jamhuri,kwa maana hiyo Mtibwa watacheza na Simba fainali Jumamosi.
Tuesday, August 14, 2012
Monday, August 13, 2012
Sunday, August 05, 2012
ANDY MURRAY AMSHINDA ROGER FEDERAR NA KUTWAA DHAHABU
Mcheza tenisi wa Uingereza Andy Murray amefanikiwa kutwaa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olmpiki inayoendelea nchini Uingereza baada ya kumchapa mchezaji maarufu duniani Roger Federar kwa seti 6-1,6-0,6-4 kwenye uwanja wa Wimbledon.
Naye Serena Williams amemfunga Maria Sharapova kwa seti 6-0,6-2 na kujinyakulia medali ya Dhahabu,michezo ya leo imewakutanisha magwiji wa Tenisi duniani,furaha zaidi ni Andy Murray ambaye amekuwa na kiu ya kumufunga Federar kwa muda mrefu na hatimaye amefanikiwa
Monday, July 30, 2012
Sunday, July 29, 2012
Saturday, July 28, 2012
YANGA BINGWA TENA KOMBE LA KAGAME 2012
Wachezaji wa Yanga wakiwa na kombe la Kagame mara baada ya kukabidhiwa kwa kuwafunga Azam FC ya Dar es salaam kwenye mchezo wa fainali kwa goli 2-0,uwanja wa taifa.
Azam walianza mchezo huo kwa kasi na kuwatia hofu wapenzi wa Yanga,lakini Yanga walitulia na kuweza kupata bao dakika ya 44 kupitia kwa Hamis Kiiza na kuwafanya Azam kupoteana kipindi cha pili,Yanga walipata bao la pili dakika za mwisho kupitia kwa Said Bahanuzi.
Yanga wamechukua kwa mara ya pili mfululizo huku ikiwa na kocha mpya kutoka Belgium,Tom Saintfiet
Thursday, July 26, 2012
YANGA NA AZAM FC KUCHEZA FAINALI KOMBE LA KAGAME
Timu ya Yanga na Azam FC zimefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Kagame baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali leo iliyochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Azam wamefanikiwa kuingia fainali baada ya kuwachapa Vita Club ya DRC goli 2-1,kupitia kwa John Bocco na Mrisho Ngasa kwenye mechi iliyochezwa mchana,kwenye mchezo wa pili Yanga ililazimika kucheza kwa dk.120 na hatimaye kupata bao pekee dk.99 kupitia kwa Hamis Kiiza aliyezifumania nyavu za wapinzani wao.
Kwa matokeo hayo timu hizo zitakutana kwenye fainali.
Wednesday, July 25, 2012
AZAM FC YAICHAKAZA SIMBA 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI
Simba imechezea kichapo cha aibu kutoka kwa Azam FC cha mabao 3-1,kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Kagame.
Azam FC walipata goli la kwanza dk.17 likifungwa na John Boko ambaye alikuwa mwiba kwenye ngome ya Simba kwa kupachika mabao yote,dk ya 46 aliipatia bao la pili na Simba walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Shomari Kapombe dk.53 kwa juhudi zake binafsi,kama vile haitoshi John Boko alitupia tena kimiani bao la 3 na kuwafanya Simba wachanganyikiwe zaidi.
Mchezo mwingine uliochezwa mchana timu ya Vita Club ya DRC iliichapa Atletco ya Burundi 2-1,sasa Azam itakutana Vita Club huku Yanga wakicheza na APR ya Rwanda nusu fainali tarehe 26.
Tuesday, July 24, 2012
YANGA YAINGIA NUSU FAINALI KAGAME CUP.
Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Kagame Yanga ya Dar es salaam,wamefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuwatoa timu ngumu ya Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-3.
Hadi dakika 90 zikimalizika matokeo yalikuwa 1-1,Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 likifungwa na Othman Mmanga kwa njia ya kichwa na Yanga walisawazisha bao dakika ya 47 kupitia kwa Said Bahanuzi.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali APR ya Rwanda iliwachapa URA ya Uganda bao 2-1,michezo mingine ya nusu fainali itachezwa kati ya Azam na Simba,Atletco ya Burundi na Vita SC ya DRC.
Sunday, July 08, 2012
TENKI LA MAJI LAMWAGA MAJI MENGI SIMIKE MBEYA.
Hii inasikitisha sana kuona mamlaka husika ikiwa imekaa kimya kwa muda mrefu,kutokana na upotevu wa maelfu ya lita za maji kupotea bila kutumika huku maji hayo yakitiririka na kuingia mto Mabatini kutoka tenki la maji la mtaa wa Simike,jijini Mbeya na kusababisha baadhi ya wakazi wa eneo kukosa maji kwa muda kutokana na tatizo hilo.
Mamlaka husika inaombwa kushughulikia tatizo hili ambalo limekuwa kero kwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo kutokana na maji hayo yanayovuja kwa wingi kupita milangoni mwao.
WEWA SEPETU NA JAQUILINE WOLPER HAKUNA MBABE.
Lile pambano la ndondi la wasanii wa filamu nchini,lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki,limemalizika matokeo yakiwa sare.
Mpambano uliojulikana kama usiku wa matumaini ulionekana kama mchezo wa kuigiza kutokana na wahusika kutokuwa na fani ya mchezo huo wa ndondi,japo Wolper akionekana kumzidi ujanja mpinzani wake.
WEWA SEPETU NA JAQUILINE WOLPER HAKUNA MBABE.
Lile pambano la ndondi la wasanii wa filamu nchini,lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki,limemalizika matokeo yakiwa sare.
Mpambano uliojulikana kama usiku wa matumaini ulionekana kama mchezo wa kuigiza kutokana na wahusika kutokuwa na fani ya mchezo huo wa ndondi,japo Wolper akionekana kumzidi ujanja mpinzani wake.
Monday, July 02, 2012
HISPANIA BINGWA ULAYA 2012
Timu ya taifa ya Hispania imechukua kwa mara nyingine ubingwa wa Ulaya baada ya kuwafunga Italia bao 4-0 jijini Kiev,Ukraine.
Hispania walipata bao la kwanza kupitia kwa David Silva dakika ya 14,goli la pili dak.41 likifungwa na Jordi Alba,goli la tatu likifungwa na Fernando Torres dk.84 na la nne likifungwa na Juan Matta dk.88,Hispania sasa inakuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hilo mfululizo toka michuano hiyo ilipoanzishwa.
Mashabiki hawakutegemea matokeo hayo ya Italia kufungwa goli nyingi kutokana na timu hiyo kuwa na ukuta imara,Hispania wenye uwezo wa kuuchezea mpira walimiliki wapinzani vilivyo na kuwafanya washindwe kufurukuta akiwemo mtukutu Mario Balotteli.
Wednesday, June 27, 2012
WAHAMIAJI HARAMU 42 WAFARIKI.
Zaidi ya watu 40 wamefariki kwa kukosa hewa wakiwa ndani ya lori lililokuwa likiwasafirisha,marehemu hao inasemekana ni raia wa Ethiopia waliokuwa wakielekea Malawi kinyume na taratibu za uhamiaji,marehemu hao wamegundulika mkoanI Dodoma baada ya kutelekezwa porini na wafanyakazi wa gari husika ambalo mpaka sasa halijajulikana.
Naibu waziri mambo ya ndani mh.Pereira Silima amethibitisha na kusema wengine waliopona tayari wanashikiliwa na jeshi la Polisi nchini.
Thursday, June 14, 2012
SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI
Hawa nia baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu siku ya leo ambayo ni siku ya wachangia damu duniani. Nilibahatika kuongea na mmoja kati ya wachangiaji hao na kuniambia kuwa amekuwa akitoa mara kwa mara hata anapokuwa nje ya nchi.
Pia bi. Jaqueline Cypirian na Jamal Abdallah walisema wanafurahia kuchangia damu na kuwataka wananchi wengine kuwa na moyo wa huruma dhidi ya wahitaji wa damu.
Tuesday, June 05, 2012
POSTA YAKABIDHI T-SHIRT KWA AJILI YA WACHANGIA DAMU.
Meneja wa tawi la Posta Mbeya,Bw.Humphrey Julius(kushoto) akimkabidhi moja ya T-shirt kiongozi wa mpango wa Taifa wa Damu salama Ndg.Kundaeli Sariah,hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za mpango wa Taifa wa Damu Salama nyanda za juu kusini,jijini Mbeya na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya posta na damu salama.
Ndg.Sariah ameishukuru Benki ya Posta na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu na kuzitaka taasisi nyingine kujitolea vitu mbalimbali kwa ajili ya wachangia damu.
Sherehe za siku ya wachangiaji damu kitaifa itafanyika mjini Moshi na kanda ya nyanda za juu kusini itafanyika mjini Songea tar.14/06/2012,
KILA MCHANGIAJI DAMU NI SHUJAA
Sunday, May 20, 2012
TIMU YA STENDI KUU MBEYA YAICHAPA ITIJI RANGERS
Mashabiki wa timu ya stendi kuu Mbeya wakishangilia ushindi waliopata dhidi ya Itiji Rangers wa mabao 2-0,kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya msingi Mbata jijini Mbeya,mabao ya stendi kuu yamefungwa na Aliko Sanga na Dominick Meshack,hata hivyo mchezo uliingia dosari na mwamuzi aliamua kuvunja mchezo kutokana na Itiji kugomea mchezo.
Michuano hiyo inadhamiwa na gazeti la Raha Tele
Monday, May 14, 2012
SIMBA YATOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA PENATI
Mabingwa wa Tanzania bara,Simba ya Dar es salaam wametolewa kwenye ya kombe la shirikisho Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao ya 3-0 na timu ya Al-ahly shandy ya Sudan.
Al-ahly Shandy walipata mabao yao dakika ya 46,50 na 60 mpaka mpira unaisha Simba walikuwa nyuma kwa mabao 3-0,kwa matokeo hayo mshindi wa jumla ilibidi hapatikane kwa njia ya penati kutokana na Simba kushinda kwa idadi hiyo hiyo ya magoli kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam.
Zilipigwa penati tisa tisa huku Al-ahly wakipoteza penati ya 3 iliyokolewa na mlinda mlango Juma Kaseja.Simba walipoteza penati ya 4 iliyopigwa na Patrick Mafisango.
Simba walipoteza penati ya mwisho iliyopigwa na Juma Kaseja.
Sunday, May 13, 2012
Monday, May 07, 2012
SIMBA YAWAHARIBIA YANGA HISTORIA
Timu ya Simba jana imewafunga mahasimu wao Yanga kwa magoli 5-0 ambayo ni idadi kubwa ya magoli kwa zaidi ya miaka 37,ambapo mwaka 1976 Simba walipata ushindi wa goli 6 na kusababisha Yanga kusambaratika.
Simba walipata bao la mapema kupitia kwa Emanuel Okwi dakika ya kwanza,bao la pili dk.54 lilifungwa na Felix Sunzu kwa penati,bao la tatu dk.61 na Okwi,goli la nne 67 Kaseja kwa penati na la tano dk.72 Patrick Mafisango dk.72 kwa penati.
Baada ya mchezo huo mwalimu msaidizi wa timu hiyo ya Yanga Fred Felix Minziro Kataraiya alisema "timu ni nzuri tatizo ni migogoro iliyoko ndani ya klabu hiyo"
Nao wapenzi wa klabu hiyo wameutupia lawama uongozi wa timu hiyo kwa kushindwa kuongoza timu hiyo na kusababisha timu kuwa katika kipindi kigumu kwa msimu huu.
CHELSEA FC BINGWA WA FA CUP
Timu ya Chelsea FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa FA jana usiku kwa kuwafunga Liverpool 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Wembly jijini London.
Chelsea walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Lamires dk.ya 10,la pili kwa Drogba dk.59 na Liverpool likifungwa na Andy Carrol aliyeingia kipindi cha pili.
Subscribe to:
Posts (Atom)