Tuesday, June 28, 2011
BEI YA MAFUTA YAATHIRI WENGI
Picha inayoonekana ni mwili wa marehemu ukifungwa kwenye pikipiki tayari kwa safari ya kuelekea kijiji cha Isansa wilayani Mbozi kutoka wilaya Mbeya,inaonekana ni kitu cha ajabu lakini ndio halisi iliyotokea,inakadiriwa kuwa kufika kijijini kwao ni zaidi kilomita 90 kama wangetumia gari ingewagharimu kuliko uwezo wao,hii inaashiria wananchi wanavyoishi kwa taabu na kubuni njia mbadala za kutatua matatizo yao bila kujali athari zinazoweza kutokea.
Monday, June 27, 2011
Sunday, June 26, 2011
YANGA ULIMI NJE KWA EL-MEREIKH
Leo El-mereikh imewalazimisha mabingwa wa Tanzania bara timu ya Yanga sare ya bao 2-2 kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa,El-mereikh waliweza kuwatawala Yanga kipindi cha pili kwa kucheza jinsi wanavyotaka na kufanikiwa kusawazisha bao la pili,Yanga kipindi waliingia cha pili safu ya kiungo ilikuwa imezidiwa na kuwapa nafasi El-mereikh kutawala mpira.
KAGAME CUP YAANZA
Michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika mashariki na kati imeanza kwa mechi za ufunguzi,zimepigwa mechi mbili,katika mechi ya kwanza timu ya Ocean view imeilaza timu ya Eticele ya Ruanda 3-2,huku Simba ikitoka 0-0 na vitalo ya Burundi,mechi hizo zitaendelea tena kwenye viwanja vya Jamhuri Morogoro na uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Friday, June 24, 2011
Thursday, June 23, 2011
Wednesday, June 22, 2011
Tuesday, June 21, 2011
Monday, June 20, 2011
KANISA LA MORAVIAN KUHAMISHIA MAKAO MAKUU MJINI DODOMA
Kanisa la Moravian liko kwenye mipango ya kuhamishia makao makuu ya kanisa hilo mjini Dodoma hayo yameelezwa na Askofu mkuu wa kanisa ndg.Alinikisa Cheyo katika ibada ilyofanyika jana kwenye kanisa la Ruanda Mbeya,alisema tayari wameshapata ekari 225 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi na vitega uchumi mbalimbali pia alielezea kuwa wako kwenye mipango ya kufungua campus ya chuo kikuu kinachomilikiwa na kanisa hilo kwenye mikoa ya Tabora na Dar es salaam na wanategemea kuanza september mwaka huu.
Saturday, June 18, 2011
Friday, June 17, 2011
Tuesday, June 14, 2011
SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI
Leo ni siku ya wachangia damu kwa hiari duniani,maadhimisho haya hufanyika kila june 14,picha inayoonekana ni bw.Paul Haule mkazi wa Nzovwe Mbeya akichangia damu katika siku hii kwenye kitengo cha damu salama akiwa na mtaalamu wa kitengo hicho bi. Salome Magwaza.Kumbuka damu haiuzwi
Sunday, June 05, 2011
TAIFA STARS YACHAPWA TENA,U-23 YAIFUNGA NIGERIA 1-0
Timu ya Taifa ya Tanzania leo imefungwa na timu ya taifa ya Africa ya kati bao 2-1 kwenye uliofanyika uwanja wa Complex Barthelemy Bonganda mjini Bangui huko Africa ya kati,kwenye mchezo mwingine timu ya vijana ya chini ya miaka 23 leo imefanikiwa kuwafunga wenzao wa Nigeria bao 1-0,Tanzania walipata bao dakika ya 84 likiwekwa kimiani na Thomas Ulimwengu kwenye uwanja Taifa jijini Dar es salaam
Thursday, June 02, 2011
AJALI NYINGINE MBEYA
Basi la kampuni ya Abood jana lilianguka eneo la mlima nyoka na kujeruhi abiria 36,kwa bahati nzuri halikusababisha vifo kwa abiria wake,huu ni mfululizo wa ajali kutokea mkoani Mbeya,Ijumaa iliyopita basi la Sumry lilipata ajali na kupoteza maisha ya watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa,Abood ilikuwa ikitokea Dar es salaam kuja Mbeya.
Subscribe to:
Posts (Atom)