Latifa akiendelea kuchangia damu. |
Hakuna njia mbadala kwa mgonjwa anayehitaji tiba ya damu isipokuwa kwa watu kujitokeza kuchangia damu,ili kuwasaidia wahitaji wa tiba hiyo ambao kundi kubwa ni wakina mama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano,watu wanaopata ajali na makundi mengine mengi.
Jamii inapaswa kuwa na mazoea ya kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara badala ya kusubiri matukio ambayo yanawalazimu kuchangia damu kama vile mtu kuwa na mgonjwa ndio anajitokeza,inabidi wanajamii tujue umuhimu wa kuwa na akiba ya damu kwenye mahospital,ili tunapopata uhitaji wa damu iwe rahisi kwa wagonjwa kupata tiba hiyo.
Damu ni tiba pekee ambayo haitengenezwi viwandani wala mashambani isipokuwa inapatikana kwa binadamu kwa njia ya kujitolea ambako hakuna madhara na ukumbuke Damu hutolewa bure na wala haiuzwi-CHANGIA DAMU OKOA MAISHA.
Zoezi la uchangiaji likiendelea. |
No comments:
Post a Comment