BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Saturday, September 27, 2014

POLISI MORO YAWABANIA SIMBA

  Timu ya Polisi ya Morogoro leo imeilazimisha timu ya Simba ya Dar es salaam sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa pili wa ligi kuu ya Vodacom, mchezo huo umechezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam ambapo Simba walikuwa wenyeji.
  Mchezo huo ulianza kwa simba kutawala kipindi cha kwanza na kuwawezesha kupata goli lililofungwa na Emmanuel Okwi na kuenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja,kipindi cha pili Polisi Morogoro waliingia uwanjani wakiwa wamebadilika na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kusawazisha goli kupitia kwa Dan Mruanda aliyepokea pasi ya Salum Machaku na kumchambua golikipa wa Simba Hussein Sharrif na kuukwamisha mpira wavuni kiufundi.
Polisi walionyesha kandanda safi baada ya kuingia kwa Christopher Edward na Seleman Selembe na kukosa magoli mawili ya wazi ambayo yangeweza kupeleka majonzi mtaa wa Msimbazi.
Matokeo mengine ya ligi kuu ya Vodacom kwa leo:-
 .Azam FC 2-Ruvu Shooting 0
 .Mtibwa 3-Ndanda FC 1
 .Mgambo JKT 0-Stand UTD 1
 .Mbeya City 1-Coastal 0
  Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili ambapo uwanja wa Taifa Dar es salaam Yanga watawakaribisha Tanzania Prisons ya Mbeya na JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Chamazi Complex.
Mpaka sasa Didier Kavumbagu wa Azam anaongoza kwa kupachika magoli akiwa na magoli manne kwa mechi mbili .

Hiki ni kikosi cha polisi Morogoro kabla ya ligi kuu

No comments:

Post a Comment