Zaidi ya watu 30 wamefariki kwenye ajali iliyohusisha magari matatu eneo la Sabasaba mjini Musoma leo,ajali hiyo imetokea leo mchana kwa kuhusisha mabasi mawili ya Mwanza Coach na J4 Express na gari ndogo aina ya Nissan Terrano baada ya J4 Express
kuigonga ubavuni Nissan hiyo kuisukumia mtoni kabla ya kukutana uso kwa
uso na Mwanza Coach nje kidogo ya daraja.
Sababu kubwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo ambayo yalikutana kwenye daraja ambalo ni jembamba na kusababisha maafa kwa abiria na wengine kujeruhiwa.
Haraka za madereva wa mabasi zimekuwa ni vyanzo vya ajali nyingi ambazo zingeweza kuepukika lakini imekuwa ni kawaida kwa madereva kujifanya kama hawajui nini kinaweza kutokea kutokana na mwendokasi wao na hii imekuwa ikichangiwa hata na baadhi ya abiria wanaojifanya wana haraka za kuwahi biashara zao na kuwakejeli madereva wanaokwenda mwendo wa taratibu.

Hii ni sehemu ya mabaki ya basi baada ya ajali |
Baadhi ya wananchi wakiangalia kwa hudhuni moja ya basi lililopata |
No comments:
Post a Comment