Thursday, December 01, 2011
TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA
Friday, November 25, 2011
Wednesday, November 23, 2011
CHANGIA DAMU OKOA MAISHA
Damu ni tiba inayotokana na binadamu wenyewe kwa maana hiyo sisi ndio wenye jukumu la kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wanaohitaji tiba hiyo na kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji tiba hiyo,kwa wale wale walioko Mbeya unaweza ukafika kwenye kituo cha damu salama kilichoko hospitali ya wazazi Meta,Mwanza damu salama Bugando,kwa wale walioko Dar es salaam na maeneo jirani mtafika kituo cha damu salama kilichoko Mchikichini,Moshi mkabala na hospitali KCMC,Mtwara kituo cha damu salama Mtwara na Tabora fika kwenye kituo cha damu salama Tabora-CHANGIA DAMU MARA KWA MARA ILI UOKOE MAISHA.
PAPA BENEDICT XVI KUTEMBELEA BENIN
Kiongozi wa kanisa la katoliki duniani,Papa Benedict wa 16 anatarajia kutembelea nchi ya Benin wiki hii.
Hii ni ziara ya pili kwa Papa Benedict barani Africa tangu kuteuliwa kwake,na ni mara ya tatu kwa taifa la Benin kutembelewa na uongozi wa juu wa kanisa hilo,mwaka 1982 na 1993 walitembelewa na Papa John Paul II.
Msemaji wa Vatican amesema ziara hiyo ni ya kuleta amani na maridhiano barani Afrika.
TUKUYU NI NEEMA TU
Wakina mama wa eneo la Kiwira wakiuza matunda ya aina mbalimbali kwa wageni na wenyeji wa wanaopita kwenye barabara ya Dar-Malawi. |
Wakina mama wakisubiri wateja wa ndizi eneo la Kiwira |
Eneo hili ndilo linlofanyiwa biashara eneo la Kiwira,licha kukaa kihatarihatari |
Wakina mama wakiuza ndizi,maparachichi,mananasi nk.kwenye basi linalofanya safari kati ya Mbeya na Kyela |
MACHAFUKO MENGINE CAIRO
Mmoja wa majeruhi akipata huduma ya kwanza |
Hili ni eneo la Tahrir jijini Cairo ambalo linaonekana kuwa na vurugu zaidi
Thursday, November 17, 2011
Tuesday, November 15, 2011
LORI LANUSURIKA NA KUZIBA BARABARA.
Lori la mizigo aina ya Scania,jioni hii limenusurika kuanguka baada ya kuacha njia na kuingia kwenye mtaro ulioko kando ya barabara na kurudi tena barabarani na kuziba barabara kwa muda na kusababisha magari makubwa kushindwa kupita,ajali imetokea leo jioni eneo la Ntokela,barabara ya Uyole-Tukuyu,hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Sunday, November 13, 2011
MAREKANI YAOMBA MSAMAHA KWA INDIA
Marekani imeiomba msamaha serikali ya India kutokana na kitendo cha maafisa wake wa uwanja wa ndege wa New York kumpekua rais wa zamani wa India,bwana Abdul Kalam mwezi Septemba.
Serikali ilitoa malalamiko yake kwa Marekani kufuatia kitendo hicho kilichoonekana kama udhalilishaji kwa mheshimiwa huyo,pia mcheza sinema maarufu wa India Shah Rukh Khan aliwahi kulalamikia kitendo kama hicho alichofanyiwa mwaka 2009.
Friday, November 11, 2011
VURUGU ZATAWALA MBEYA LEO
Askari wa jeshi la polisi wakijaribu kutuliza ghasia maeneo ya tukio jijini Mbeya |
Gari likiwa limebinuliwa na waandamanaji na kufunga barabara kuu ya Dar-Tunduma eneo la Kabwe |
Matairi chakavu yakiwa yamechomwa katikati ya barabara na kuleta taabu kwa wasafiri na moshi mzito kusambaa eneo la Kabwe (Picha kwa hisani ya Mwaisango) |
Thursday, November 10, 2011
Wednesday, November 09, 2011
BONDIA JOE FRAZIER AFARIKI DUNIA
Aliyekuwa nguli wa mchezo wa masumbwi kwenye miaka ya 60 na 70,Frazier amefariki juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa saratani ya ini.
Frazier alikuwa bondia wa kwanza kumpiga bingwa wa kipindi hicho Muhammad Ally katika mpambano uliochezwa DR Congo machi, 1971,amefariki akiwa na umri wa miaka 67,wapenzi wa mchezo huo wataendelea kumkumbuka kutokana na umahiri wake ulingoni na hasa kwa kumchapa bingwa aliyeshindikana Muhammad Ally.
Monday, November 07, 2011
Thursday, November 03, 2011
Tuesday, November 01, 2011
MASELE NA WENZAKE WAWALEMAZA WASAFIRI KITUO CHA MABASI MBEYA.
Msanii maarufu na wenzake toka jijini Dar es salaam,leo wamewateka wasafiri waliokuwepo kituo kikuu cha mabasi jijini Mbeya,na kuwafanya wabaki wakiwaangalia na kusahau kufanya mipango ya safari kutokana na vituko vyao vya maigizo walivyokuwa wakionyesha na kuwavutia wasafiri wengi na baadhi wafanyabiashara wa eneo hilo.
Saturday, October 29, 2011
YANGA YAICHAPA SIMBA 1-0
Mabingwa watetezi wa Tanzania bara leo wameichapa Simba bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliyofanyika uwanja wa Taifa,Yanga walipata bao hilo dakika ya 72 kupitia kwa mshambuliaji wao wa kimataifa Davies Mwape baada ya walinzi wa Simba kufanya makosa,mchezo huo ulianza kwa kasi na Simba kutawala kipindi cha kwanza,Simba walipoteza nafasi kadhaa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Yanga walijipanga na kubadili mchezo na hivyo kuwafanya waibuke na ushindi huo.
Michezo mingine ya ligi hiyo imechezwa huko Mwanza kati ya Toto African na Coastal Union matokeo ni 0-0,huko Dodoma ilikuwa ni kati ya Polisi na Oljoro matokeo ni 0-0,kwa matokeo haya bado hayabadili msimamo wa ligi bado Simba inaongoza ligi ikiwa na alama 27,ikifuatiwa na Yanga yenye alama 24,Azam 21.
Monday, October 24, 2011
Thursday, October 20, 2011
GADAFFI AFA KISHUJAA
Aliyekuwa rais wa Libya Muamar Gadaffi leo ameuawa na jeshi la waasi lililom
muondoa madarakani baada ya kumshika na kumjeruhi kwenye mji wake alikozaliwa na kupelekea kifo chake.
Gadaffi tofauti na marais wengine yeye aliendelea kubakia nchini kwake pamoja na sehemu ya nchi kushikiliwa na waasi,aliendelea na kuishi kwenye mji wa Sirte ambako ndiko alikozaliwa.
muondoa madarakani baada ya kumshika na kumjeruhi kwenye mji wake alikozaliwa na kupelekea kifo chake.
Gadaffi tofauti na marais wengine yeye aliendelea kubakia nchini kwake pamoja na sehemu ya nchi kushikiliwa na waasi,aliendelea na kuishi kwenye mji wa Sirte ambako ndiko alikozaliwa.
Tuesday, October 18, 2011
Sunday, October 16, 2011
LIVERPOOL YAWATOA ULIMI NJE MANCHESTER UNITED
Timu ya Liverpool ikicheza kwa maelewano jana iliweza kutoka sare na Manchester Utd kwa kufungana bao 1-1 kwenye uwanja Anfield,Liverpool walipata bao dakika ya 67 kupitia kwa Steven Gerrald na Manchester walisawazisha dak.80 kupitia kwa Chicharito.
Liverpool walitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa na kuwafanya walinzi wa Man kuwa na wakati mgumu.
Saturday, October 15, 2011
Tuesday, October 11, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)