BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Monday, February 09, 2015

IVORY COAST BINGWA WA AFRIKA 2015

 Timu ya taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa mataifa ya Afrika 2015 kwa kuwafunga Ghana kwa mikwaju ya Penati 9-8 kwenye uwanja Bata nchini Equitarial Guinea,timu hizo zilicheza dakika 120 na kufanya matokeo kuwa 0-0 hadi dakika 90 na dakika 30 za nyongeza na hivyo kufikia kwenye hatua ya mikwaju ya penati,Ivory Coast walianza kwa kukosa penati iliyopigwa na Wilfred Bon kugonga mwamba na kurudi uwanjani,Ghana walipata penati yao ya kwanza,pili na nne na kupoteza ya tatu na ya tano,huku wenzao wakipoteza tena ya pili huku wakipata ya tatu,nne na tano,baada ya penati tano ikawa ikiongezwa moja moja mpaka kufikia jumla penati 11 kwa kila timu na kumfanya golikipa wa Ivory Coast Boubacary Barry kuibuka shujaa aliweza kucheza penati 2 na kufunga ya mwisho huku golikipa wa Ghana,Razak akipiga penati ambayo iliokolewa na Barry.
Timu ya Ivory Coast wakishangilia ubingwa wa Afrika 2015
Wilfred Bon akiwa amembeba golikipa Boubacary Barry wa Ivory Coast baada ya kuokoa penati na  kuifungia timu yake penati ya mwisho. 

Nahodha wa Ivory Coast Yaya Toure akiwa na wenzake wakishangilia ubingwa wa Afrika.
Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfred Bon akijaribu kumtoka mlinzi wa Ghana

No comments:

Post a Comment