BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Thursday, April 30, 2015

FLOYD MAYWEATHER v/s MANNY PACQUIAO


 Wanamasumbwi wenye majina makubwa kwa sasa duniani,Manny Pacquiao na Floyd Mayweather wanategemea kupanda ulingoni tarehe 02/05/2015 usiku wa jumamosi huko marekani kwa saa za Afrika mashariki tayari itakuwa alfajiri ya tarehe 03/05/2015 siku ya jumapili.
 Mpambano huo wa kusisimua utakata mzizi wa fitna kwa kujua ni nani zaidi katika masumbwi kutokana na kutambiana kwa muda mrefu na kuonekana kama walikuwa wakikwepana.
  Pambano hilo litafanyika ukumbi wa MGM Grand Cassino huko Las Vegas,Marekani na kuhudhuriwa na watu wengi zaidi na watu maarufu kutokana na tiketi ambazo zimeshauzwa kwa ajili ya pambano hili.
  Manny Pacquiao akiongea kwa kujiamini amesema "Every thing i have accomplished,God has given me this strength.I used to sleep in the street,hungry,and i cannot imagine that the Lord raised me to this level of life"  

Wednesday, April 29, 2015

YANGA BINGWA TANZANIA KWA MARA YA 25

 Timu ya Yanga ya Dar es salaam imefanikiwa kunyakuwa taji la 25 tangu kuanziswa kwa ligi kuu ya Tanzania mwaka 1965,timu hii imefanikiwa kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa 2014/15 kwa kuwafunga Polisi morogoro 4-1 na huku ikiwa imesaliwa na mechi mbili mkononi kati ya Ndanda FC na Azam FC.
  Yanga kabla ya kumalizia mechi zake mbili zilizobaki itakwenda Tunisia kucheza mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Etoile Du Sahel ambapo kwenye mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1 jijini Dar es salaam,ikumbukwe kuwa Yanga ndio mwakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa baada ya wawakilishi wengine kutolewa mapema.
 Kwa kufanikiwa kuchukua ubingwa wa mwaka huu Yanga itawakilisha tena Taifa mwakani,kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika ambayo mwaka huu mwakilishi alikuwa Azam FC ambaye alitolewa na El-merreikh ya Sudan raundi ya kwanza.
Viongozi,walimu na wachezaji wa timu ya Yanga wakiwa na furaha mara baada ya ushindi.

Saturday, April 25, 2015

AZAM NA SIMBA KUTOANA ROHO KWENYE MECHI YAO INAYOFUATA

 Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Azam FC wanaelekea kupoteza ubingwa wao kutokana na spidi ya timu kongwe hapa nchini Yanga kutokamatika,timu ya Azam leo imeshuka dimbani na kujikusanyia alama 3 dhidi ya Stand United kwa kuifunga magoli 3-0 kwenye uwanja wa Chamazi Complex.
 Nao Simba walikuwa kwenye uwanja wa taifa kuminyana na Ndanda FC kutoka Mtwara na matokeo Simba wamechomoza na ushindi wa magoli 3-0 na hivyo kufanya mechi ya Azam na Simba jumamosi ijayo  kuwa ngumu kutokana na timu hizo kukaribiana pointi na mshindi wa mechi hiyo anaweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
 Azam wao wanahitaji ushindi ili mechi yao ya mwisho na Yanga iwe haina madhara kwa matokeo ya aina yeyote huku Simba wakihitaji ushindi na kuomba Yanga awafunge Azam kitu ambacho ni kigumu kwa miaka mingi watani hao wa jadi kuombeana mema.
 Huko Mbeya timu ya Mbeya City nayo imeibuka na ushindi mnono wa goli 2-0 dhidi ya wakata miwa wa Kagera Sugar na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutoshuka daraja.
 Huu ndio msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya mechi za leo:-
 Bado hali si shwari kwa timu za Tanzania Prisons,Ndanda FC,Polisi Moro,JKT Ruvu wanaonekana kuchungulia kaburi na kurudi daraja la kwanza msimu ujao kwa yeyote atakayefanya vibaya kwenye yake ya mwisho.

Wednesday, April 22, 2015

SIMBA YAMALIZIA HASIRA ZA MBEYA CITY KWA MGAMBO JKT.

  Timu ya Simba SC ya Dar es salaam leo imewaadhibu Mgambo JKT ya Tanga kwa jumla ya magoli 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
 Magoli ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi matatu na Ramadhani Singano Messi akipachika goli moja kwa mpira wa adhabu ambao ulikwenda moja kwa moja wavuni,Simba waliweza kutawala mchezo huo kwa muda wote na kama washambuliaji wake wangekuwa makini zaidi wangeweza kuondoka na kapu la magoli,Simba ambayo siku nne zilizopita ilifungwa goli 2-0 na Mbeya City leo wamerekebisha makosa yao na kucheza mpira wa hali ya juu na kuweza kuwadhibiti wapinzani wao ambao kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Mkwakwani Tanga waliweza kuwafunga Simba goli 2-0.
 Simba sasa inafikisha alama 38,ikiwa imecheza michezo 23 wakiwa nyuma ya Azam fc wenye alama 42 na michezo 22,timu ya Yanga ndio inaongoza ligi ikiwa na alama 49 kwa michezo 22 ni dhahiri kuwa Yanga wamejihakikishia moja kati ya nafasi mbili za juu kutokana na Simba hata kama itashinda michezo yake iliyobaki itaishia alama 47 ambazo zimeshapitwa na Yanga,Simba sasa itabidi amuombee Azam matokeo mabaya ili aweze kupata nafasi ya pili ambayo itampa tiketi ya kuliwakilisha Taifa kwenye michezo ya shirikisho mwakani.
 Huu ndio msimamo wa ligi kuu baada ya mechi ya leo:
 Hali si nzuri kwa timu za Tanzania Prisons,Polisi Morogoro,Ndanda FC na JKT Ruvu zisipofanya marekebisha ya haraka zinaweza zikajikuta miongoni mwao zinashuka daraja msimu huu.

Saturday, April 11, 2015

MLOWO UNITED YAWASHUSHIA KIPIGO SHUKRANI MWALEMBE CHA GOLI 4-1

 Mlowo United timu kongwe wilayani Mbozi imewashushia kipigo cha goli 4-1 timu ya Shukrani Mwalembe FC kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya msingi ya Mlowo.
 Mlowo United waliokuwa wenyeji wa mchezo walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi,Mlowo United walijipatia magoli yao kupitia kwa wachezaji wao mahiri,goli la kwanza likifungwa na Francis Mwigani,la pili likifungwa na mshambuliaji hatari Noah Kaminyoge huku la tatu na la nne likifungwa na nyota wa mchezo huo Derick Walulya.
                                   Wachezaji wa Mlowo United wakipiga dua kabla ya mchezo.
                               Mlowo United wakisubiri kukaguliwa na mwamuzi wa pambano hilo.  
                     Wachezaji wakisalimiana na wapinzani wao pamoja na waamuzi wa mchezo huo.
                                    Wachezaji wa Mlowo United wakichukua picha ya pamoja.
  Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa Mlowo United 4,Shukrani Mwalembe 1 mara baada ya mchezo niliongea na baadhi ya mashabiki wa timu zote mbili lakini waliokuwa na furaha zaidi ni shabiki wa Mlowo United Bwana Moses Lwesya ambaye amewamwagia sifa kibao wachezaji wa Mlowo United,michuano inadhaminiwa na Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki Mh.Godfrey Zambi.