Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Azam FC wanaelekea kupoteza ubingwa wao kutokana na spidi ya timu kongwe hapa nchini Yanga kutokamatika,timu ya Azam leo imeshuka dimbani na kujikusanyia alama 3 dhidi ya Stand United kwa kuifunga magoli 3-0 kwenye uwanja wa Chamazi Complex.
Nao Simba walikuwa kwenye uwanja wa taifa kuminyana na Ndanda FC kutoka Mtwara na matokeo Simba wamechomoza na ushindi wa magoli 3-0 na hivyo kufanya mechi ya Azam na Simba jumamosi ijayo kuwa ngumu kutokana na timu hizo kukaribiana pointi na mshindi wa mechi hiyo anaweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Azam wao wanahitaji ushindi ili mechi yao ya mwisho na Yanga iwe haina madhara kwa matokeo ya aina yeyote huku Simba wakihitaji ushindi na kuomba Yanga awafunge Azam kitu ambacho ni kigumu kwa miaka mingi watani hao wa jadi kuombeana mema.
Huko Mbeya timu ya Mbeya City nayo imeibuka na ushindi mnono wa goli 2-0 dhidi ya wakata miwa wa Kagera Sugar na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutoshuka daraja.
Huu ndio msimamo wa ligi kuu ya Vodacom baada ya mechi za leo:-
Bado hali si shwari kwa timu za Tanzania Prisons,Ndanda FC,Polisi Moro,JKT Ruvu wanaonekana kuchungulia kaburi na kurudi daraja la kwanza msimu ujao kwa yeyote atakayefanya vibaya kwenye yake ya mwisho.

No comments:
Post a Comment