08.05.2015 09:02
Hali ya wasi wasi inawakumba sehemu kubwa ya wakazi wa Dar es
Salaam kutokana na mfuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua
zinazoendelea kunyesha.
Kutokana na hali hiyo serikali imewashauri wakazi wa jiji hilo kuu la biashara Tanzania, kuelekea maeneo ya nyanda za juu na kutoka maeneo ya mabondeni.
Maafisa wanasema wanafanya kila wawezalo kuwasaidia wanohitaji msaada baada ya kukoseshwa makazi, lakini hawajaweza kuthibitisha idadi ya watu waloathiriwa na walofariki. vyombo vya habari vinatoa idadi zinazotofautiana kati ya mtu moja kufariki hadi wanne.
Wakazi wa Dar Es Salaam wakizungumza na Sauti ya Amerika wanaulaumu uzembe wa serikali kwa mafuriko hayo, huku wengine wakidai ni ukosefu wa miundo mbinu madhubuti kuweza kuruhusu maji kupita katika mitaro bila ya tatizo.
Chanzo VOA.

No comments:
Post a Comment