Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo inayotokana na kutumia kinywaji 1- 2 kwa siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swala lenye utata. Shauku zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta ya dawa, wadau wa sekta ya pombe piawamehusika katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na hipependekezwi kwa-ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba za dawa.
Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho na presha.Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo, wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwatahadhari kwa sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza matumizi wastani ya pombe kunaweza kusababisha ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana. Manufaa haya ya matumizi wastani ya pombe yanapitwa na hatari za matumizi ya pombe wastani.
Yaliyomo
- 1 Tafiti za kisayansi
- 2 Vifo vinavyohusiana na Pombe
- 3 Mfumo wa mishipa ya moyo
- 4 Mfumo wa neva
- 5 Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ongezeko la uzani
- 6 Mifumo mingine
- 7 Mfumo wa kinga, bakteria Ukolezi, maambukizi ya virusi na kansa
- 8 Athari za pombe kwa kijusi
- 9 Tazama Pia
- 10 Marejeleo
- 11 Sehemu nyinginezo
Tafiti za kisayansi
Historia
Madhara mabaya ya matumizi ya pombe kwa muda mrefu kupita kiasi ni sawa na yale yanaoonekana katika vitulizi-hipnoti vingine (mbali na sumu kwa viungo ambayo hutatiza zaidi katika pombe). Athari za kujiondoakatika pombe na utegemezi hukaribia sana kufanana.Pombe ya wastani ina athari chanya na hasi kwa afya. Athari hasi ni pamoja na ongezeka la hatari ya magonjwa ya ini, sarataniya orofarinji, kansa ya umio na ugonjwa wa kongosho. Kinyume na hayo, unywaji wastani wa pombe unaweza kuwa na athiri za faida kwa gastriti na kolelithiasi. Matumizi sugu na mabaya ya pombe huwa na athari kubwa kwa afya ya mwili na akili. Unywaji sugu wa pombe kupita kiasi au utegemezi pombe, unaweza kusababisha uharibifu mpana viungo mbalimbali vya nevaza ubongo,mfumo wa neva ama ugonjwa wa mishipa ya moyo, maradhi ya ini, na neoplasmsi isiyopona. Matatizo ya akili ambayo huhusishwa na ulevi ni pamoja na mfadhaiko mkubwa, disthimia, mania, hipomania, tatizo la hofu fobia , tatizo la wasiwasi wa kijumla, tatizo la tabia za mtu, skizofrenia, kujinyonga, upunufu wa mfumo wa utendakazi mwilini (km kazi za kumbukumbu, hisia, kazi za uamuzi, uwezo wa kuona,mwendo na uwiano) na uharibifu wa ubongo. utegemezi wa pombe ni huhusishwa na shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na kiharusi cha iskemi, kansa ya mfumo wa upumuaji, mbali pia na saratani ya mfumo wa mlo, ini, kifua na ovari. Unywaji kupita kiasi huhusishwa na ugonjwa wa ini, kama vile sairosi.Utafiti zimelenga wanaume na wanawake, vikundi vya umri mbalimbali na watu wa makundi mengi ya kijamii. Machapisho kwa sasa yanafikia jumla ya mamia huku tafiti zikiweza kuonyesha uwiano uliopo kati ya matumizi wastani ya pombe na afya ambayo labda yanaweza kuwa yalitokana na athari za manufaa ya maingiliano ya kijamii ambayo mara nyingi huambatana na matumizi ya pombe. Baadhi ya njia mahususi ambapo pombe huweza kuathiri afya ya mishipa ya moyo zimetafitiwa.Mtazamo wa kisasa
Utafiti fulani katika baadhi ya nchi umedai kuwa vifo vinavyosababishwa na sababu zozote zile vinaweza kufikia viwango vya baina ya 16 hadi 28% kwa uchache miongoni mwa wanywaji wa wastani (vinywaji 1-2 kwa siku) ikilinganishwa na ile miongoni mwa wanaojiepusha na unywaji kabisa. Mwandishi wa habari Roni Caryn Rabin wa New York Times anasema kwamba takwimu za utafiti huu zina makosa.Upeo wa kiasi kinachopendekezwa
Habari zaidi: Recommended maximum intake of alcoholic beverages
Nchi mbalimbali hupendekeza kiasi tofauti cha upeo wa kunywewa . Kwa
nchi nyingi kiasi cha upeo kwa wanaume ni 210g-140g kwa wiki. Kwa
wanawake, kiasi ni 84g-140g kwa wiki. Nchi nyingi hupendekeza kutumiwa
kwa pombe kabisa wakati ujauzito ama kunyonyesha.Matumizi ya pombe kupita kiasi ni mojawapo ya sababu zinazoweza kuzuilikaambayo husababisha vifo vingi kote duniani. Utafiti mmoja unahusisha pombe na kila kifo 1 katika 25 kote duniani na kwamba 5% ya miaka wanayoishi watu na ulemavu hutokana na matumizi ya pombe.
Nchi hukusanya takwimu kuhusu wanaofariki kwa ajili ya pombe. Huku baadhi ya takwimu zikihusiana na athari za muda mfupi kama vile ajali, nyingi huhusiana na athari za muda mrefu wa kutumia pombe.
Urusi
"Matumizi ya pombe kupita kiasi nchini Urusi, hasa kmiongoni mwa wanaume, katika miaka ya hivi karibuni imesababisha zaidi ya nusu ya vifo katika umri wa miaka 15-54.Uingereza
Vifo vinavyohusiana na pombe nchini Uingereza ni huainishwa kwa kutumia Uainisho wa Kimataifa wa Magonjwa, Toleo la Kumi (ICD-10).ICD-10 hujumuisha:- Matatizo ya akili na tabia kutokana na matumizi ya pombe - ICD-10 F10
- Kuzorota kwa mfumo wa neva kutokana na pombe - ICD-10 G31.2
- Polineuropathi ya pombe - ICD-10 G62.1
- Kadiomiopathi ya pombe - ICD-10 I42.6
- Gastriti ya Pombe - ICD-10 K29.2
- Ugonjwa wa ini wa pombe - ICD-10 K70
- Hepatitis sugu , isiyoainishwa mahali kwingine kokote - ICD-10 K73
- Fibrosi na sairosi ya ini - ICD-10 K74 (bila kujumuisha K74.5 K74.3-Sairosi ya biliari)
- Ugonjwa sugu wa kongosho kutokana na pombe - ICD-10 K86.0
- Sumu itumikayo kiajali kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10 X45
- Sumu itumikayo na mtu binafsi kimaksudi kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10 X65
- Sumu kutokana matumizi na kukumbana na pombe, bila kusudi wazi - Y15 ICD-10
Nchini Skotlandi, NHS inakisio kwamba katika mwaka 2003 kifi cha kia mtu mmoja katika 20 waliofariki inaweza kuhusishwa na pombe.
Utafiti wa 2009 uligundua kuwa watu 9,000 hufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na pombe kila mwaka, mara tatu ya idadi ya miaka 25 ya hapo awali.
Marekani
Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji Magonjwa kinaripoti kuwa, "Kutoka 2001-2005, kulikuwa na takribani vifo 79,000 kila mwaka zinazotokana na matumizi ya pombe kupita kiasi. Kwa hakika, matumizi ya pombe kupita kiasi ni ya 3 katika sababu zinazoambatana na mitindo ya kimaisha kwa kusababisha vifo kwa watu nchini Marekani kila mwaka". Utafiti mmoja wa 1993 ulikadiria vifo vya waliofariki Marekani kupitia pombe kuwa 100,000.Vifo kwa ujumla
Utafiti uliotazamiwa wa miaka 23 wa madaktari wa kiume 12,000 Waingereza Ufalme wa Muunganowenye umri wa miaka 48-78, waligundua kuwa vifo kwa jumla vilikuwa vya chini sana kwa makundi yaliyokunywa chini ya "vipimo" 2 (Vipimo vya Uingereza = 8 g) kwa siku zaidi ya ilivyokuwa katika makundi ya wasiokunywa pombe. Zaidi ya vipimo 2 kwa siku ilihusishwa na ongezeko la hatari ya vifo. Pombe iliwakilishwa 5% ya vifo katika sampuli ya madaktari.Mfumo wa mishipa ya moyo
Licha ya ushahidi wa kiepidemiolojia, baadhi ya watu wanakosoa wazo la kupendekeza pombe kuwa na faida za kiafya. Daktari katika Shirika la Afya Duniani alisema kuwa kupendekeza matumizi ya pombe wastani kwa faida za kiafya ni "ya ujinga na hatari." Kumekuwa hakuna majaribio yaliyoratibiwa na kudhibitiwa kuonyesha faida za pombe kwa moyo . Kutokana na hatari ya kutumia vibaya, utegemezi, athari mbaya, pombe haifai kamwe kupendekezwa kwa faida za moyo. Badala yake, chakula bora, mazoezi na kama inapohitajika matumizi ya dawa ndizo tiba zinazopendekezwa kwa kutunza moyo. Imesemwa kuwa faida za kiafya za pombe ni swala la kujadiliwa na huenda lilitiliwa chumvi na wadau wa sekta ya pombe. Pombe inafaa kuchukuliwa kama dawa-lewevu ya burudani ambayo ina uwezo wa kuzua athari kali na mbaya kwa afya na haipaswi kutangazwa kwa utunzaji wa moyo.
Ugonjwa wa pembeni wa mishipa (PAD)
"Matumizi wastani ya pombe inaonekana kupunguza hatari ya PAD katika wanaume walio na afya"."Katika utafiti huu mkubwa uliohusu raia, matumizi wastani ya pombe yalionyesha uhusiano wa kupungua kuhusiana na ugonjwa wa pembeni wa mishipa miongoni mwa wanawake, waliplinganishwa na wanaume. Mkolezo wa mabaki kutokana na sigara huenda uliweza kuwa kuathiri matokeo. Miongoni mwa wasiovuta sigara, uhusiano wa kinyume ulionekana kati ya matumizi ya pombe na ugonjwa wa pembeni wa mishipa katika wanaume na wanawake."Uzibifu wa muda (IC)
Utafiti uligundua kwamba matumizi wastani ya pombe yalikuwa na athari ya kinga dhidi ya uzibifu wa muda. Hatari ya chini zidi ilionekana katika wanaume waliotumia na vinywaji 1 hadi 2 kwa siku na kwa wanawake ambao wanaotumia kinywaji nusu hadi 1 kwa siku.Mshtuko wa moyo na kiharusi
Unywaji pombe wa kiasi cha wastani umeonekana kuwasaidia wale ambao wamekumbwa na mshtuko wa moyo kuendelea kuishi. Hata hivyo, matumizi ya pombe kupita kiasi husababisha ongezeko la hatari ya kupata ugonjwa wa moyo. Durusu ya maandishi iligundua kuwa unywaji pombe kwa kiasi nusu ulitoa kiwango bora zidi cha ulinzi kwa moyo. Hata hivyo, walibainisha kuwa kwa sasa hapajakuwa na majaribio yaliyoratibiwa kuthibitisha ushahidi ambao unaonyesha jukumu la vipimo vidogo vya pombe kukinga kwa dhidi ya mshtuko wa moyo.Hata hivyo, matumizi wastani ya pombe huhusishwa na shinikizo la damu. Pana ongezeko la hatari ya kwa hipatrigliseridemia, kadiomiopathi presha,, na kiharusi iwapo vinywaji 3 au zaidi vya pombe vitatumiwa kwa siku.Ikilinganishwa na kuacha pombe, unywaji wa kiasi wastani huhusishwa na ongezeko la hatari ya kiharusi. Unywaji wa kiasi cha chini hauna faida yeyote kwa kuzuia kiharusi.
Kadiomiopathi
Kiasi kikubwa cha pombe kinaweza kusababisha kadiomiopathiya pombe, inayojulikana kama " dalili za moyo wa likizo." Kadiomiopathi ya pombe hujitokeza kwa namna ambayo kimatibabu ya hufanana na kadiomiopathi iliyopanuka idiopathi, inayoshirikisha hipartrofi ya misuli ya moyo ambayo inaweza kusababisha aina fulani ya arithmia ya moyo. Tofauti hizi zisizo za kawaida za umeme, zinazowakilisha katika EKG, mara nyingi hutofautiana kwa hali, lakini huwa kutoka mabadiliko mbalimbali ya vipindi vya muda vya PR, QRS, au QT hadi vipindi na matukio paroxsysmal ya tachycardia ventricular. Pathofisiolojia (sababu za kuugua mwilini) ya kadiomiopathi ya pombe haijatambuliwa kikamilifu, lakini baadhi ya nadharia huelezea kuhusu ongezeko la utoaji wa epinefrini na norepinefrini, ongezeko la utendaji, au ongezeko la kiwango cha asidi huria za mafuta zisizo na plazma ya kama taratibu inayowezekana.Magonjwa ya damu
Walevi wanaweza kuwa na upungufu wa damu kutokana na sababu kadhaa, pia wanaweza kupata thrombositopenia kutokana na athari ya sumu ya megakariositi, au kutokana na hipespleni.Mfumo wa neva
Matumizi ya pombe sugu ya kiasi kikubwa cha pombe huvuruga ukuaji wa ubongo, na kusababisha ubongo kunywea, shida ya akili, utegemezi wa kimwili, kuongezeka kwa matatizo ya neva za akili na matatizo na usumbufu wa utambuzi licha ya kuvuruga kemia ya ubongo. Hata hivyo baadhi ya tafiti zimeonyesha kwamba unywaji pombe cha kiwango wastani unaweza kupunguza hatari ya shida ya akili ikiwa ni pamoja na ugonjwa Alzeima, ingawa pana tafiti ambazo zilipata matokeo kinyume. Kwa sasa kutokana na miundo duni ya mbinu za utafiti, maandishi sio toshelezi kuhusu iwapo unywaji wastani wa pombe huongeza au hupunguza hatari ya shida ya akili. Ushahidi kuhusu athari za kinga ya matumizi wastani ya pombe kwa upungufu wa utambuzi katika misingi inayohusiana na umri imependekezwa na utafiti fulani, hata hivyo, utafiti mwingine haukupata athari za kinga kutokana na matumizi ya pombe kwa wastani. Baadhi ya ushahidi unaonyesha kuwa matumizi ya kiwango cha pombe cha chini hadi wastani unaweza kuharakisha kupunguka kwa kiasi cha ubongo.Kiharusi
Utafiti wa 2003 uliofanywa na Johns Hopkins ulihusisha matumizi wastani ya pombe na kunywea kwa ubongo nao haukuona upungufu wowote wa hatari ya kiharusi miongoni mwa wanywao kwa wastani.Ukuaji wa ubongo
Matumizi ya kiasi kikubwa cha pombe kwa kipindi cha muda unaweza kutatiza ukuaji wa ubongo wa kawaida binadamu. Upungufu katika kukumbuka taarifa za kimazungumzo na zisizozungumzwa na katika utendaji wa kuona zilidhihirika kwa vijana walio na historia ya unywaji katika miaka ya mapema na katikati ya ubaleghe.Wakati wa ubaleghe hatua muhimu za ukuaji wa neva hutokea. Unywaji wa kilevi, ambayo ni kawaida miongoni mwa vijana huhitilatiana na hatua hii muhimu ya ukuaji. Matumizi mazito ya pombe huzuia ukuaji wa seli mpya za ubongo.
Takribani nusu ya walevi sugu wanaweza kuwa na miopathi. Vikundi vya misuli inayokaribiana ndiyo hasa huathirika. Asilimia ishirini na tano ya walevi wanaweza kuwa na neuropathi ya pembeni, ikiwa ni pamoja na zilizo huru
Utambuzi na shida ya akili
Unywaji wa pombe kupita kiasi huhusishwa na mvurugiko wa kumbukumbu unaoweza kuwepo. Uwezo huu wa utambuzi uliovurugika husababisha ongezeko la kushindwa kutimiza kazi inayonuiwa katika siku zijazo, kwa mfano, kusahau kufunga mlango au kutuma barua kwa wakati unaotakikana. Jinsi kiasi cha pombe na muda wa kutumika unavyoongezeka ndivyo ukali wa madhara huongezeka kwa viungo. Kiungo mojawapo kinachohisi sana madhara ya sumu ya matumizi ya pombe kwa muda mrefu ni ubongo. Nchini Ufaransa takribani 20% ya wanaolzwa katika vituo vya afya ya akili huhusiana na kuvurugika kwa utambuzi kutokana na ulevi, hasa shida za akili kuhusiana na pombe. Unywaji pombe sugu kupita kiasi pia huhusishwa na upungufu mkubwa wa utambuzi na matatizo mbalimbali ya neva za akili. Wazee ndio huhisi sana mwathiriko wa sumu ya madhara ya pombe kwenye ubongo.Pana baadhi ya ushahidi usio mkamilifu kuwa kiasi kidogo cha pombe kinachotumiwa katika katika miaka ya mapema ya maisha ya utu uzima huw a na kinga ya ni maisha ya baadaye dhidi ya kupungua kwa utambuzi na shida ya akili. Hata hivyo, utafiti fulani ulihitimisha kuwa, "Matokeo yetu yanaonyesha kwamba, licha ya mapendekezo yaliyopita, matumizi ya kiasi wastani cha pombe hayawezi kuwalinda watu wazee dhidi ya kupungua kwa utambuzi wao".Asetaldehidi hutolewa na ini ini wakati wa kusagwa kwa ethanoli. Watu walio na upungufu wa jeni ambayo hutumika kubadilisha asetaldehidi baadaye kuwa asidi asetiki (hali inayobainika zaidi kwa watu wa asili ya Asia ya Mashariki) wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kupataugonjwa wa Alzeima. "Matokeo haya yanaonyesha kwamba upungufu wa ALDH2 ni kigezo cha hatari kwa LOAD [-kujitokeza kwa ugonjwa Alzeima katika miaka ya baadaye ] .
Dalili za Wernicke-Korsakoff ni dhihirisho la upungufu wathiamini, kwa kawaida kama athari ya kiwango cha pili cha matumizi mabaya ya pombe. Dalili hizi ni dhihirisho la pamoja la matatizo mawili ya mwanzoni , Saikosi ya Korsakoff na uvimbaji ubongo (enselopathia) wa Wernicke, yaliyotajwa kuambatana na majina ya Dkt. Sergei Korsakoff na Dkt. Carl Wernicke. Uvimbe wa ubongo wa Wernicke ni dhihirisho kubwa wa dalili na hubainika kwa hali ya kuchanganyikiwa wakati ambapo dalili kuu za saikosi ya Korsakoff ni amnesia na mvurugiko wa utendaji.
Mitetemo Isiyoepukika
Mitetemo isiyoepukika inaweza kuondolewa kwa muda mfupi kufikia kwa hadi thuluthi mbili ya wagonjwa kwa kunywa kiasi kidogo cha pombe.Usingizi
Matumizi sugu ya pombe katika kuleta usingizi yanaweza kusababisha ukosefu wa usingizi. Kutembea mara kwa mara katika hatua za usingizi, huku kukiwa na kuamkaamka kutokana na maumivu ya kichwa na diaforesi. Kusitisha matumizi mabaya sugu ya pombe pia kunaweza kusababisha usumbufu makubwa wa usingizi kwa ndoto nyingi. Matumizi mabaya sugu ya pombe huhusishwa na NREM hatua ya kulala ya 3 na 4 pamoja na ukandamizaji usingizi wa REM na kugawanyika kwa usingizi wa REM . Wakati wa kujiondoa katika ulevi, usingizi wa REM kwa kawaida hukolezwa kama sehemu ya athari ya kujibia.Athari za afya ya akili
Viwango vya juu ya vya mfadhaiko mkubwa hutokea kwa wanywaji pombe kwa wingi na wale ambao hutumia pombe vibaya. Utata hapo awali umehusu swala la iwapo wale waliotumia pombe vibaya na kupatwa na tatizo la mfadhaiko mkubwa walikuwa wakijitibu kibinafsi(ambayo inaweza kuwa kweli katika baadhi ya matukio), lakini utafiti wa hivi karibuni sasa umehitimisha kuwa unywaji sugu wa pombe kupita kiasi nayo yenyewe huweza moja kwa moja kusababisha ukuaji wa tatizo la mfadhaiko mkubwa katika idadi kubwa ya watumiaji wa pombe vibaya. Matumizi mabaya ya pombe inahuhusishwa na idadi kadhaa ya matatizo ya afya ya akili na viwango vya juu sana vya walevi kujiua. Utafiti wa watu waliolazwa hospitalini kwa ajili ya majaribio ya kujiua uligundua kwamba wale ambao walikuwa walevi walikuwa mara 75 zaidi ya wale ambao wangefanikiwa kujiua kuliko wasiotimia pombe ambao walijaribu kujiua.Katika idadi jumla ya wanywaji pombe, ongezeko la hatari ya kujiua ikilinganishwa na umma yote kijumla ni mara 5-20 zaidi. Karibu asilimia 15 ya walevi hujiua. Matumizi mabaya ya dawa nyingine pia huhusishwa na ongezeko la hatari ya kujiua. Takribani asilimia 33 ya visa vya kujiua kwa walio chini ya miaka 35 ni kutokana na pombe au dutu matumizi mabaya ya vilewevu vingine.Tafiti zimeonyesha kwamba utegemezi wa pombe unahusiana moja kwa moja na tamaa na mwasho. Utafiti mwingine umeonyesha kuwa matumizi ya pombe ni kigezo muhimu cha kumwelekeza mtu katika tabia zisizoambatana na maadili ya jamii kwa watoto. Unyogovu, wasiwasi na hofu ni matatizo ya kawaida yaliyoripotiwa na watu wanaotegemea pombe . Ulevi huhusishwa na upungukaji wa kutenda katika mifanyiko ya ubongo ambayo huwajibikia mchakato wa kihisia (kwa mfano amigdala na hipokampusi). Ushahidi kwamba matatizo ya afya ya akili mara nyingi hutokana na matumizi mabaya ya pombe kuvuruga kemikali za neva za ubongo hudihirika kupitia kuimarika au upotevu wa dalili ambako hutokea baada ya muda mrefu bila kutumia pombe, ingawa matatizo yanaweza kuwa kuzidi katika kipindi cha awali baada ya kujionda katika pombe na kupona. Tatizo la akili (saikosi) ni matokeo ya kiwango cha pili ya hali nyingi zinazohusiana na pombe ikiwa ni pamoja na madhara makali ya sumu na kujitoa baada ya matumizi ya muda mrefu. Matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu yanaweza kusababisha dalili za namna ya tatizo la akili kuibuka, zaidi ya ilivyo na dawa nyingine za matumizi mabaya. Matumizi mabaya ya pombe yameonyeshwa kusababisha ongezeko la 800% ya hatari ya tatizo la akili(saikosi) kwa wanaume, na ongezeko la 300% la hatari ya tatizo la sikosi kwa wanawake,ambazo hazihusiani na matatizo ya akili kabla ya yaliyopo kwa sasa. Hii ni kubwa zaidi kuliko ongezeko la hatari ya ugonjwa wa akili unaonekana kutokana na bangi ambayo hufanya matumizi mabaya ya pombe kuwa chanzo kikubwa sana cha matatizo ya akili.Maono-njozi kwa wingina / au ya udanganyifu wa akili ni kawaida sasa wakati mgonjwa amelewa au kujiondoa kutoka ulevi kwa siku za karibuni.
Ingawa pombe husaidia awali kupunguza dalili za fobia au hofu za kijamii, matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu yanaweza kuzidisha dalili za fobia ya kijamii na kusababisha dalili za fobia ya kijamii hasa wakati wa kujiondoa katika pombe. Athari hii si ya kipekee kwa pombe lakini inaweza pia kutokea kwa matumizi ya muda mrefu wa dawa za kulevya ambazo zina mfumo sawa wa utendaji wa pombe kama vile benzodiazepini ambazo ni wakati mwingine hupendekezwa kama vitulizi kwa watu walio na matatizo ya pombe. Takriban nusu ya wagonjwa wanaohudhuria huduma za afya ya akili kwa hali ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa wasiwasi kama vile tatizo la hofu au fobia ya kijamii ni matokeo ya pombe au utegemezi wa benzodiazepini. Ilibainishwa kwamba kila mtu ana kiwango cha uhisivu wake binafsi kwa matumizi ya pombe au dawa za hipnotiki-tulizi hivyo basi kitu ambacho mtu mmoja anaweza kuvumilia bila ya kuathirika kiafya, mgonjwa mwingine anaweza kutatizika sana kiafya na kwamba hata unywaji wastani unaweza kusababisha dalili za wasiwasi unaojibia na matatizo ya kulala. Mtu ambaye anatatizika na madhara ya sumu ya pombe hawezi kufaidika na aina nyingine za tiba au dawa kwa vile hazizisulihishi dalili za kimsingi.
Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ongezeko la uzani
Tazama pia: Alcohol and weight, Alcoholic liver disease, Alcoholic hepatitis, Fatty liver, na Cirrhosis
Athari za pombe kwa ongezeko la uzani ni swala tata: huku tafiti nyingine zikishindwa kugundua upungufu nyingine zimegundua pombe kuwa na athari kwa ongezeko la uzani.Matumizi ya pombe kwa muda mrefu huongeza hatari ya gastriti sugu (kuvimba tumbo),ni sababu mojawapo ya sairosi, hepatiti, na wa kongosho katika hali zake zote, sugu na kali.
Dalili za Metaboli
Utafiti ulihitimisha kuwa, "Matumizi madogo hadi wastani ya pombe huhusishwa na tatizo la upungufu wa dalili za metaboli , pamoja na athari nzuri kwa mafuta, mzingo wa kiuno, na mfungo wa insulini. Uhusiano huu alibainika zaidi miongoni mwa wazungu na miongoni mwa wanywaji wa bia na mvinyo." "Uwiano usio wa kawaida wa dalili za metaboli na vipengele vyake vilionyesha kuongeza kwa matumizi ya pombe.Athari kwa Kibofu nyongo
Utafiti umegundua kwamba unywaji pombe hupunguza hatari ya kupatwa na vijiwe vya nyongo. Ikilinganishwa na ilivyo kwa watu wanaojiepusha na pombe, hatari jumla kutokana na ugonjwa wa vijiwe vya nyongo, kudhibiti umri, jinsia, elimu sigara, na uwiano wa ukubwa-mwili na uzani , ni 0.83 kwa wanywao mara chache na wanywao mara nyingi kwa kiasi wastani (<25 ml ya ethanoli kwa siku), 0.67 kwa wanywao kiasi cha kati ( 25-50 ml kwa siku), na 0.58 kwa wanywao kwa wingi. Uhusiano huu wa kinyume ulionyesha uthabiti katika safu za umri, jinsia na mwili uwiano wa ukubwa-mwili na uzani."Idadi ya nyakati za unywaji pia inaonekana kuwa sababu inayochangia. "Ongezeka la idadi ya nyakati za matumizi ya pombe pia ilihusishwa na ya upungufu wa hatari. Kwa kuunganisha taarifa za wingi wa kiasi cha pombe na idadi ya nyakati za unywaji pombe, mkondo wa matumizi ya pombe uliodhihirisha unywaji wa mara kwa mara (siku 5-7 kwa wiki) wa kiasi chochote cha pombe ulihusishwa na upungufu wa hatari ya kuugua ikilinganishwa na wasiotumia pombe. Kinyume na hayo, unywaji pombe wa mara kwa mara (siku 1-2 kwa wiki) haukuonyesha uhusiano wowote na hatari ya kuugua."Matumizi ya pombe hayahusiani na ugonjwa wa vijiwe vya nyongo. Hata hivyo utafiti mmoja ulipendekeza kuwa wanywaji pombe ambao huchukua vitamini C (asidi ya askorbi) inaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa vijiwe vya nyongo.
Ugonjwa wa ini
Ugonjwa wa ini kutokana na pombe ni tatizo kubwa kwa afya ya umma. Kwa mfano nchini Marekani hadi kufikia watu milioni mbili wana matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa ini. Matumizi mabaya ya pombe kwa muda mrefu yanaweza kusababisha mafuta ya ini, sirosi na hepatiti ya pombe. Njia za matibabu ni chache na hatua mojawapo muhimu zaidi inayojumuisha ni kusitisha matumizi ya pombe. Katika matukio ya ugonjwa mkali wa ini, njia ya pekee ya matibabu inaweza kuwa kupandikiza ini kwa wagonjwa walioacha pombe. Utafiti kubainisha ufanisi viziua-TNF. Baadhi ya dawa za nyongeza, kwa mfano, mbaruti za maziwa na silimarini, zinaonekana kuwa faida fulani. Pombe ni sababu inayoongoza katika kusababisha kansa ya ini katika nchi za Magharibi, huchangia 32-45% ya saratani ya hepati. Hadi watu nusu milioni nchini Marekani hupata matatizo ya kansa ya ini inayohusiana na pombe Matumizi ya pombe wastani pia huongeza hatari ya ugonjwa wa ini.Ugonjwa wa Kongosho
Matumizi mabaya ya pombe ni sababu inayoongoza ya ugonjwa kali wa kongosho na ugonjwa wa kongosho wa muda mrefu. Unwaji pombe sugu wa kupindukia unaweza kusababisha uharibifu wa kongosho unaopelekea maumivu makali ya muda mrefu ambayo yanaweza kuendeleo na kuwa kansa ya kongosho. Kongosho sugu mara nyingi husababisha matatizo ya ufyonzaji wa chakula tumboni na ugonjwa wa kisukari.Mifumo mingine
Ugonjwa wa mapafu kutokana na pombe
Utumiaji sugu wa pombe hutatiza kazi nyingi muhimu za seli katika mapafu. Hitilafu za seli hizi huzidisha uwezekano wa kuongezeka kwa kupata matatizo makubwa kutokana na ugonjwa wa mapafu. Tafiti za hivi karibuni zinabainisha vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa ini kutokana na pombe zikilinganishwa na vya ugonjwa wa ini kutokana na pombe . Watumiaji pombe wako katika hatari kubwa ya kupatwa na dalili mbaya za dhiki za upumuaji (ARDS) na hupatwa na kiwango cha juu cha vifo kutokana na ARDS ikilinganishwa na wasiokunywa pombe.Vijiwe vya figo
Utafiti unaonyesha kuwa unywaji pombe unahusiana na upungufu wa hatari ya kupatwa na vijiwe vya figo. Utafiti mmoja ulihitimisha kuwa, "Kwa vile bia ilionekana kukinga dhidi ya vijiwe vya figo,athari za kimwili za vilewevu mbali na ethanoli, hasa zile za hopsi, lazima pia kuchunguzwa"."... Matumizi ya kahawa, pombe na virutubisho vya vitamini C vihusiana kwa kinyume na vijiwe". "Baada ya mpatano wa kimwili na matayarisho kwa ajili ya unywaji wa vinywaji vingine, hatari ya ukuaji wa vijiwe ulipungua kwa kiasi kifuatacho kwa kila 240-ml (8-oz) iliyonywewa kwa siku: 10% kwa kahawa yenye kafeni ; 10% kwa kahawa isiyo na kafeni, 14 % kwa chai, 21% kwa bia, na mvinyo, 39% ". "... ukuaji wa vijiwe ulipungua kwa kiasi kifuatazo kwa kila 240-ml (8-oz) iliyotunywewa kila siku: 10% a kahawa yenye kafeni, 9% kwa kahawa isiyo na kafeni, 8% ya chai, na 59% kwa divai." (Cl data iliyotolewa kutoka nukuu mbili za mwisho.).Hitilafi katika Ngono
Unywaji pombe kupindukia wa muda mrefu unaweza kusababisha uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni na kupelekea kupoteza tamaa ya ngono na kutosisimka kwa wanaume.Utofautiano wa Homoni
Unywaji pombe kupita kiasi unaweza kusababisha mchakato wa hiperoestrojeni. Imekisiwa kwamba vinywaji vilivyo pombe vinaweza kudhibiti misombo ya estrojeni. Kwa wanaume, viwango vikubwa vya estrojeni vinaweza kusababisha kushindwa kwa kazi za makende na ukuaji wa hulka ya uke ikiwa ni pamoja na ukuaji wa matiti ya kiume zinazoitwa jainekomastia. Kwa wanawake, viwango juu vya estrojeni kutokana na unywaji pombe kupindukia vimehusishwa na ongezeko la hatari ya kansa ya matiti.Ugonjwa wa kisukari melitusi
Wanywaji pombe wa wastani wanaweza kuwa katika hatari ndogo ya kupata kisukari kuliko wasiokunywa . Kwa upande mwingine, ulevi wa pombe na matumizi ya pombe kwa kiasi cha kikubwa huweza kuzidisha hatari ya aina 2 za ugonjwa wa kisukari kwa wanawake." Matumizi ya pombe huimarisha uhisivu wa insulini.Ugonjwa wa maumivu ya viungo
Matumizi ya kila mara ya pombe huhusishwa na ongezeko la hatari ya maumivu ya viungo kutokana na jongo. Matumizi ya pombe huhusishwa na upungufu wa hatari ya maumivu ya viungo. Tafiti mbili za hivi karibuni zinaripoti kwamba jinsi pombe zaidi inavyotumiwa, ndivyo hatari ya kupatwa na maumivu ya viungo hupungua. Miongoni mwa watu wanaokuunywa mara kwa mara, robo moja ya wanaokunywa zaidi walikuwa na kiwango cha hadi 50% cha chini cha uwezekano wa kupata ugonjwa wakilinganishwa na nusu ambao hunywa kidogo.Watafiti walibainisha kuwa matumizi ya pombe wastani pia hupunguza hatari ya matukio mengine ya kutatiza kama vile ugonjwa mishipa ya moyo. Baadhi ya michakato ya kibayolojia ambapo kwayo ethanoli hupunguza hatari ya maumivu ya viungo na kuzuia uharibifu wa upotevu wa madini ya uzito wa fupa (BMD), ambayo ni sehemu ya mchakato wa maradhi.
Utafiti ulihitimisha kuwa, "Pombe ama hulinda dhidi ya RAmaumivu ya viungo au, watu walio na RA husitisha unywaji wao baada ya kudhihirika kwa RA". Utafiti mwingine uligundua kuwa, "Wanawake waliopitisha miaka ya kuzaa ambao kwa wastani hutumia zaidi ya vinywaji 14 vya pombe kwa wiki walikuwa na upungufu wa hatari ya maumivu ya viungo ..."
Osteoporosi
Matumizi wastani ya pombe huhusishwa na uzito wamadini ya mfupa kwa wanawake waliopitisha umri wa kujifungua. "...Matumizi ya pombe yalipunguza sana ya uwezekano wa [osteoporosis]." "Unywaji wa pombe wastani ulihusishwa na BMD katika wanawake wazee waliopita miaka ya kujifungua". "Unywa wa kijamii huhusishwa na uzito wa juu wa madini ya mfupa katika wanaume na wanawake [juu] 45". Hata hivyo,matumizi mabaya ya pombe ni huhusishwa na upungufu wa mfupa.Ngozi
Matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi ni huhusishwa na matatizo mbalimbali ya ngozi ikiwa ni pamoja naurtikaria, pofiria tarda kutanea, kuhisi joto na kujaa, stigmata ya ngozi ya saiirosi, soriasisi, pruritusi, ugonjwa wa seborei ya ngozi na rosasea.Utafiti wa 2010 ulihitimisha, "unywaji bia usio mwepesi huhusishwa na hatari ya kuongezeka kwa uwezekano wa kupata soriasisi kwa wanawake. Vinywaji vingine vya kulevya havikuongeza hatari ya soriasis katika katika utafiti huu.
Mfumo wa kinga, bakteria Ukolezi, maambukizi ya virusi na kansa
Maambukizi ya bakteria
Kuna athari za kinga ya matumizi ya pombe dhidi ya maambukizi makali ya H pylori Kinyume na hayo, unywaji pombe (unapolinganisha wale ambao hunywa> 30 gm ya pombe kila siku kwa wasiokunywa) haihusiani na hatari kubwa ya vidonda vya duodena. Matumizi ya pombe kupita kiasi ya pombe unaoonekana katika walevi hujulikana kama kigezo hatari cha nyumonia.Homa ya mafua
Utafiti kuhusu homa ya mafua ulipata kuwa "Idadi kubwa ya vinynywaji vya pombe (hadi vitatu au vinne kwa siku) vilihusishwa na upungufu wa hatari ya kupata homa ya mafua kwa sababu ya kunywa kulihusishwa na ulipunguaji wa magonjwa baada ya kuugua. Hata hivyo, faida za kunywa zilitokeza tu miongoni mwa wasiovuta sigara. ... Ingawa matumizi ya pombe hayakuchangia hatari ya ugonjwa ya kimwili kwa wavutaji,matumizi wastani ya pombe yalihusishwa na upunguaji wa hatari kwa wasiovuta sigara."Utafiti mwingine ulihitimisha kuwa, "Matokeo yanaonyesha kwamba unywaji divai, hasa divai nyekundu unaweza kuwa na athari ya kinga dhidi ya hioma ya mafua. Bia, vileo vikali na pombe jumla hazionekani kuathiri matukio ya homa ya mafua.
Kansa
Idara ya Marekani & Huduma za Kibinadamu 'Mpango wa Afya ya Taifa uliotaja pombe kama kasinojeni inajulikana mwaka wa 2000.
Utafiti mmoja uliamua kwamba "3.6% ya matukio yote ya kansa duniani yanahusiana na kunywa pombe ambayo husababisha 3.5% ya vifo vyote vya kansa ".
Ripoti ya jopo la Wakfu wa Utafiti wa Saratani Duniani iitwayo Chakula, Lishe, Shughuli za kimwili na Kuzuia Saratani: Mtazamo wa Kilimwengu wapata ushahidi wa "kushawishi" kwamba kunywa pombe huongeza hatari aina za saratani zifuatazo: kinywa na koo, umio, kolorektamu (wanaume), kifua (kabla na baada ya umri wa kujifungua).
Ukolezi mkubwa wa asetalidehidi, ambayo huzalika wakati mwili unavunja ethanoli, unaweza kuharibu DNA katika seli zilizo na afya. Taasisi ya Taifa ya Matumizi mabaya ya Pombe na Ulevi zimeonyesha kwamba asetalidehidi hushikamana na poliaminesi ambayo ni misombo inayotokea kwa kawaida nayo ni muhimu kwa ukuaji wa seli - kuibusha aina ya msingi wa DNA hatari inayoitwa Cr-Pdg adduct. Hata viwango vya wastani vya matumizi ya pombe huhusishwa na ongezeko la hatari ya aina fulani za kansa.
No comments:
Post a Comment