BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Wednesday, September 14, 2011

MARY MWANJELWA AKABIDHI MAGODORO 90 HOSPITALI YA WAZAZI NA KITUO CHA AFYA MBEYA

Mbunge wa viti maalum CCM,Mhe.Mary Mwanjelwa akikabidhi magodoro 7o kwa Dr.Peter Msafiri wa hospitali ya wazazi meta mjini Mbeya mchana,huku akiwa ameongozana na wakina mama wakereketwa wa chama cha mapinduzi jijini Mbeya,Mh.Mary Mwanjelwa pia atakabidhi magodoro mengine 20 kwenye kituo cha afya Ruanda mchana huu.

Dr.Peter Msafiri akimkaribisha mheshimiwa mbunge Mary Mwanjelwa.

Gari likiwa limebeba magodoro yaliyotolewa na mh.Mary Mwanjelwa
Mama Sichela akiwaongoza wenzake kufurahia msaada huo

Monday, September 12, 2011

BOMBA LA MAFUTA LALIPUKA NA KUPASUKA NAIROBI NA KUSABABISHA WATU ZAIDI YA 100 KUFARIKI

Bomba la mafuta limelipuka na kupasuka jijini Nairobi Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100,bomba hilo linalomilikiwa na serikali ya Kenya limekatiza katikati ya jiji na mlipuko huo umeanzia eneo la Lungalunga jijini Nairobi,askari wa zimamoto wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mmoja wa majeruhi wa moto akipakiwa kwenye gari ya wagonjwa na kupelekwa hospitali

AFRIKA KUSINI YALETA WAOKOAJI ZANZIBAR

Baadhi ya wananchi wakipita kutambua miili ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali ya meli huko Nungwi Zanzibar.
 <><>
<>
<><>Baadhi ya watalii wakishiriki kuwahudumia watoto waliokolewa kwenye meli eneo la Nungwi Zanzibar
Mtoto Said Gerald akiwa hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar mara baada ya kuokolewa kwenye ajali ya meli


Saturday, September 10, 2011

MV.SPICE ISLANDER YAZAMA KASKAZINI UNGUJA NA KUSABABISHA MSIBA MKUBWA






Meli ijulikanayo kwa jina la Mv. SPICE ISLANDER inayofanya safari zake kati ya Pemba na Unguja,jana usiku ilipata dhoruba na kupinduka hatimaye kuzama na kusababisha zaidi ya watu 100 kupoteza maisha,japokuwa jitihada kuokoa watu abiria zinaendelea na mpaka sasa wameshaokolewa zaidi ya abiria 150 wakiwa hai na shughuli hiyo inaendelea.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi  Dr. Ally M.Shein  na makamu wa rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad wakiwa na huzuni kubwa walipotembelea eneo la ufukwe wa Nungwi kuangalia ajali hiyo ya meli.


Askari wa vikosi mbalimbali wanashiriki katika uokoaji wa abiria na hapa wanaonekana wakiwa wamembeba bi.Mariam Mohamed Murad kutoka Tanga aliyenusurika kwenye ajali hiyo ya meli


Thursday, September 08, 2011

VODACOM YAKUBALI YAISHE KWA YANGA

Mabingwa wa Tanzania Bara jana walivaa jezi zenye nembo ya wadhamini wa ligi hiyo ya Vodacom premier league kwa mara ya kwanza,Yanga walikuwa wakigoma kuvaa jezi zenye nembo ya Vodacom kutokana na kuwa na rangi nyekundu na nyeupe ambayo inatumiwa na mahasimu wao na hivyo kuwapa wakati mgumu wadhamini hao na kulazimika kuweka nembo nyeusi au ya kijani kwenye jezi za wanajangwani hao

TWIGA STARS YAWAONYESHA KIWANGO BANYANA BANYANA LEO

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (TWIGA STARS) leo imeweza kutoka sare ya magoli 2-2 na wanawake wenzao wa Afrika kusini katika mchezo mkali na kuvutia uliochezwa mchana huu jijini Maputo,mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya hadi zinakwenda zikiwa nguvu sawa.  Kipindi kilianza kwa Afrika ya kusini kujipatia goli lililofungwa na Samatha Skity dakika ya 48 kwa krosi iliyojaa moja kwa moja kimiani,kufuatia bao hilo Tanzania waliongeza mashambulizi na kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Sharua Omar aliyewazidi ujanja mabeki wa Banyana Banyana.
  Twiga Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ester Chabruma baada ya kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Zena Rashid na dakika ya 72 ilimwingiza Fridian ambaye alikosa goli baada kupiga kichwa kilichotoka sentimita chache.
 Banyana Banyana walipata bao la pili kupitia kwa Chantelle Essau dakika ya 74 baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa Twiga Stars na dakika moja baadaye Twiga walisawazisha kupitia kwa Zena Rashid kwa njia ya kichwa kutokana na krosi safi toka upande wa kushoto na hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo

Wednesday, September 07, 2011

JIENDELEZE SACCOS YAWASAIDIA WAKULIMA WA MAHINDI IWINDI MBEYA.


Wakulima wa mahindi kata ya Iwindi Mbeya vijijini wamenufaika na viongozi wao baada ya kuanzisha uwekaji akiba kwa kutumia mazao na ambayo baadaye huuzwa na mkulima kuingiziwa amana kwenye SACCOS na kuwawezesha kupata mikopo midogo dogo.

BIASHARA YA KUKU IWINDI MBEYA


Mfanyabiashara eneo la kata ya Iwindi Mbeya vijijini,akiuza kuku kwa kutumia baiskeli na kuwafunga kuku kama mzigo fulani vile.

Saturday, September 03, 2011

TAIFA STARS YALAZIMISHWA SARE NYUMBANI

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) leo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Taifa ya Algeria kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani huko Equatarial Guinea na Gabon,kwa matokeo haya ya leo yamezidi kupoteza matumaini ya kushiriki michuano hiyo kwa timu ya Taifa ambayo kwa mara ya mwisho ilishiriki michuano hiyo mwaka 1980
  Taifa stars walipata bao dakika ya 24 kupitia kwa Mbwana Samata baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Nizar Khalfan,lakini kisicho riziki hakiliki Algeria walisawazisha goli hilo na kuonyesha kandanda safi kipindi cha pili kama vile walikuwa wakisoma mchezo kipindi cha kwanza.
 Taifa Stars wakiwatumia wachezaji wengi wanaocheza nje ya nchi waliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia tatizo likiwa ni umaliziaji na makosa kadhaa ya walinzi wetu,mchezo huu umechezwa leo kwenye uwanja Taifa Dar es salaam.


Wachezaji wa Taifa stars Amir Maftah,Mbwana Samata na Dan Mruanda wakishangilia mara baada ya kujipatia bao la kuongoza dhidi ya Algeria


Tuesday, August 30, 2011

ANSWAAR SUNNA WASWALI SWALA YA IDD-EL-FITR LEO

Sheikh Juma Pori Amir wa Answaar Sunna Tanzania akiongoza ibada ya idd kwenye viwanja vya jangwani jijini leo

Baadhi ya waumini wa kiislamu wa madhehebu ya Answaar Sunna wakiwa kwenye ibada ya idd iliyofanyika kwenye viwanja vya Jangwani leo,huk u waislamu wengine wakisherekea kesho


Monday, August 29, 2011

Sir Alex Ferguson amshauri Wenger kufanya usajili makini kabla ya kesho kutwa.


Baada ya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 8-2 dhidi ya Arsenal,meneja wa Man Utd amemshauri kocha wa Arsenal kufanya usajili makini kwa masaa 48 yaliyobaki kabla ya msimu wa usajili kufungwa hapo jumatano.
Naye Wenger amesema sababu ya kipigo hicho ni uchovu wa wachezaji wake ambao jumatano iliyopita walicheza na Udinesse ya Italia kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na hivyo kusababisha majeruhi kwenye kikosi hicho na kufanya wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kutocheza.
Wenger ni kocha pekee aliyeiletea mafanikio timu ya Arsenal na kuifanya kuwa na wapenzi wengi duniani lakini mambo sasa yanataka kumuendea kombo kutokana na kipigo hicho kikubwa ambacho kwa mara ya mwisho timu hiyo ilifungwa mabao 8-0 mwaka 1896,hata hivyo Wenger amewaomba radhi wapenzi na mashabiki wa timu hiyo duniani kote.

Sunday, August 28, 2011

Manchester yaifanyia kufuru Arsenal yawachapa 8-2


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza leo wameifanyia kitu mbaya timu ya Arsenal kwa kuichapa mabao 8-2,kichapo hicho ni kikubwa kwa maisha ya mzee Arsenal Wenger ambaye ana tabia ya kujiamini sana,na sasa amekuwa na wakati mgumu kubaki kwenye timu hiyo ambayo amekuwa nayo kwa muda mrefu na inasemekana ndiye kocha pekee aliyeleta mabadiliko kwenye ligi hiyo ya Uingereza na kufuta ubaguzi wa rangi.
Lakini kutokana na kipigo cha leo kinamuweka kwenye wakati mgumu zaidi hasa baada ya kuwauza wachezaji wake nyota na kushindwa kutafuta mbadala wao,pamoja na bodi ya klabu hiyo kuruhusu fedha zitumike kwenye usajili wa msimu huu lakini alikaidi agizo hili.
Mechi hii imehudhuriwa na watazamaji 73414 kwenye dimba la Old Trafford na Man U kuibuka na ushindi mnono wa bao 8-2.

HII NDIYO KYELA BWANA


Kama kuna wilaya ambayo wanafahamu matumizi na umuhimu wa baiskeli hatuwezi kuacha kuitaja wilaya ya Kyela,kwenye picha ni baadhi ya baiskeli ambazo zimeegeshwa eneo la shule na bado ukipita mitaani wakina utawakuta wakiendesha na mtoto mgongoni,ukiuliza safari ya wapi?unajibiwa anaenda kliniki au kabeba bonge la mzigo

Tuesday, August 23, 2011

MPAKANI MWA TANZANIA NA MALAWI

Hapa ndio mpaka wa Tanzania na Malawi unaojulikana kwa jina la Border ya Kasumulu ambayo inaonekana na utulivu wa hali ya juu tofauti na mipaka mingine.

Huu ndio mto unayozitenganisha nchi hizi mbili


 <><><>Eneo la Malawi likiwa linafanyiwa ukarabati

Baadhi ya magari ya mizigo yakisubiri kupita mpakani
 

Monday, August 22, 2011

MAMBO YA KYELA

Hili ni eneo la Kyela mjini ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa mchele safi na wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuendesha baiskeli kwa umbali mrefu
Huu ni mkusanyiko wa baiskeli za wanafunzi waliopaki eneo la shule wilayani Kyela

 

wakina mama wakiwa na baiskeli zao




Sunday, August 21, 2011

MZIMU WA SIMBA WAENDELEA KUITAFUNA YANGA


Mabingwa wa Tanzania bara leo wameanza ligi ya Vodacom vibaya,baada ya kufungwa bao 1-0 na JKT Ruvu ikiwa ni siku chache baada ya kupokea kichapo kutoka kwa mahasimu wao Simba cha bao 2-0 kwenye mchezo wa ngao ya hisani,JKT Ruvu walipata bao kwa njia ya penati dakika 22 iliyofungwa na Kesy Mapande kutokana na mlinzi wa Yanga Chacha Marwa kucheza faulo eneo la hatari.
JKT Ruvu walitumia mbinu iliyotumiwa na Simba ya kuchezesha viungo wengi katikati na hivyo kuwafanya viungo wa Yanga Nurdin Bakari na Haruna Niyonzima kushindwa kuonyesha umahiri wao ipasavyo.
Na huko Arusha Simba wameanza ligi vyema baada ya kuwalaza JKT Oljoro mabao 2-0.

Saturday, August 20, 2011

SONGEA


Hapa ndio katikati ya mji wa Songea ambako kuna purukushani za hapa na pale na pikipiki za abiria nyingi

SONGEA ASUBUHI YA LEO


Mdau wetu akiwa kituo cha mabasi Songea tayari kwa safari.

Friday, August 19, 2011

USAFIRI WA LITEMBO-MBINGA


Kutokana na wilaya ya Mbinga kuwa na milima mingi wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakitumia usafiri wa Land Rover,ambazo zimepewa na kuitwa Mondolino kutokana na uwezo kupanda na kushuka milima hiyo huku zikiwa na abiria wengi na mizigo mingi.

UZALENDO KWA TAIFA LETU.


Majengo ya shule ya sekondari ya Kiamili Wilayani Mbinga,yakiwa yamepakwa rangi za bendera ya Taifa,hii ni moja ya uzalendo kwa taifa letu na kuwafanya hata wanafunzi kuelewa rangi za bendera hiyo kiurahisi zaidi.

MNYAMA AITAFUNA YANGA USIKU


Timu ya Simba imefanikiwa kuwafunga mahasimu wao Yanga kwa mabao 2-0 na kuchukua ngao ya hisani,Simba wakicheza kwa ushirikiano mkubwa walifanikiwa kupata bao dakika ya 16 kupitia Haruna Moshi Boban na baadaye walipata bao kwa njia ya penati kupitia kwa Sunzu hadi mapumziko Simba walikuwa wakiongoza kwa mabao hayo mawili,kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi na kuwafanya Yanga washindwe kusawazisha kutokana na kuwazidi wapinzani wao kwenye safu ya kiungo na kuwafanya Yanga kucheza bila malengo.
Timu hizi zimekutana mara sita kwenye mechi za usiku na hivyo Simba ikiibuka na ushindi mara tano na Yanga mara moja na mechi hizo zilichezwa uwanja wa Aman Zanzibar,mechi nne zikiwa ni za ubingwa wa Afrika mashariki na kati,moja kombe la muungano na nyingine ndio hii ya ngao ya hisani ambayo imechezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa matokeo hayo inaonyesha Yanga wamekuwa na udhaifu wa mechi za usiku hata za kirafiki,wiki moja tu iliyopita wamechezea kichapo mjini Khartoum Sudan kwa kufungwa mabao 3-1 na El-hilal,na katika mechi ya pili wakapokea kipigo kama hicho hicho
Mvuto zaidi ni kwa makocha wa timu hizo ambao wanatoka nchi moja kwa upande wa Simba ni Moses Basena na Yanga ni Sam Timbe ambao kila mmoja alitaka kuonyesha nani zaidi ya mwenzake kutokana na timu zote kujivunia usajili wa msimu huu.

Tuesday, August 16, 2011

CHANGIA DAMU OKOA MAISHA.


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Agustivo High School wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wakiwa na mfanyakazi wa kitengo cha Taifa cha damu salama kanda ya nyanda za juu kusini bw.Fred Malagi wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanyika shuleni hapo mapema leo.

Sunday, August 14, 2011

MASHINDANO YA KUHIFADHI KURAAN TUKUFU YAFANA DAR


Baadhi ya mashekhe na umati wa waislamu uliofurika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijini Dar-es-salaam,kushuhudia mashindano ya kuhifadhi Kuraan Tukufu yaliyoshirikisha wanafunzi wa madrasa toka bara na visiwani,ambayo mshindi wa kwanza alikuwa Khalid Omar Mbarouk(15) kutoka madrasa ya Madrasat An-nujum ya Temeke na kujishindia pikipiki aina ya Bajaj.

UJENZI WA BARABARA YA SONGEA-MBINGA WAENDELEA KWA KASI.


Ujenzi wa barabara ya Songea-Mbinga kwa kiwango cha lami,unaendelea kwa kasi na kuleta matumaini kwa wakazi mkoa huo kutokana na wilaya ya Mbinga kuwa na vyanzo vingi vya mapato.
Kukamilika kwa ujenzi kutawanufaisha wakazi wa mkoa wa Ruvuma na maeneo jirani waliokuwa wakitumia muda mrefu kusafiri katika maeneo hayo yenye biashara za mazao na samaki kutoka ziwa Nyasa.

MANCHESTER YAANZA VIZURI


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza (EPL) leo wameanza michuano hiyo vizuri baada ya kuwafunga timu ya West ham 2-1,Man walikuwa wa kwanza kupata bao dk 14 kupitia kwa Wayne Rooney na baadaye Long aliisawazishia Westham na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi mapumziko,kipindi cha pili Man walifanikiwa kupata bao la ushindi dk 81 kupitia kwa Ashley Young aliyepiga mpira na kuwababatiza mabeki wa Westham na kujaa wavuni

KITUO CHA MABASI NJOMBE VUMBI TUPU


Pamoja na uchumi mkubwa wa Njombe,kituo cha mabasi bado kinahitaji ukarabati wa hali juu na kufanya kiendane na hadhi ya wilaya hiyo ambayo inategemewa kupewa hadhi ya mkoa

Friday, August 12, 2011

KILIMO CHA KIANGAZI MBEYA


Kutokana na hali na hewa kuwa nzuri katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya,sehemu nyingine wanalima mahindi mara mbili kwa mwaka kama inavyoonekana eneo la Maganjo eneo la Mbeya vijijini

Thursday, August 11, 2011

UKOSEFU WA MAFUTA MBEYA WASABABISHA SHIDA YA USAFIRI


Kukosekana kwa mafuta kumesababisha watu kuchelewa maeneo yao ya kazi na wengine kulazimika kutembea kwa miguu,kutokana na baadhi ya daladala kushindwa kutoa huduma ipasavyo kutokana na vituo vya mafuta kuishiwa mafuta.

IGOMA MBEYA


Mdau wetu akiwa kwenye kijiji cha Igoma Mbeya,njia panda ya kuelekea wilaya ya Makete mkoani Iringa.

Wednesday, August 10, 2011

MACHAFUKO UINGEREZA YATIBUA MCHEZO WA TIMU YA TAIFA.


Machafuko yaliyokuwa yakiendelea nchini Uingereza yamesababisha mechi ya kirafiki kimataifa kati ya Uingereza na Uholanzi kufutwa na baadhi ya michezo ya kombe la Carling kuahirishwa.

Sunday, August 07, 2011

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI.


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini,Jenerali Davis Mwamunyange.kufuatia kifo cha Luteni Jenerali Silas Peter Mayunga kilichotokea jana katika hospital ya Apollo,mjini New Dhel,India.Mzee Mayunga amefariki akiwa na umri wa miaka 71.

Saturday, August 06, 2011

BIASHARA YA NDIZI TUKUYU.


Wafanyabiashara ya ndizi wakionekana wakisubiri usafiri kwa ajili ya kusafirisha ndizi kupeleka maeneo tofauti,biashara hiyo inaonekana kufanywa na wanawake kuliko wanaume eneo la Tukuyu na hivyo kusababisha soko lake liwe dogo,kufunguliwa kwa uwanja wa ndege wa Songwe kutaleta changamoto kwa wanaume nao kujiingiza kwenye biashara hiyo ambayo wamekuwa kama wanahidharau.

Wednesday, August 03, 2011

MAJENGO YA ILIYOKUWA HOSPITAL YA UKOMA MAKETE-KISONDELA YAMETELEKEZWA TOKA 2005

Haya ni majengo ya iliyokuwa hospital ya ukoma  Makete Kisondela,Rungwe yakiwa kwenye hali mbaya baada ya hospital hiyo kufungwa rasmi mwaka 2005 na kufanya majengo kubaki yakiwa hayatumiki mpaka leo.
   Majengo haya yangeweza kutumika kama shule au kituo cha afya kwenye kata husika lakini yameachwa yakiharibika
Sehemu ya ndani ya majengo hayo ambayo haitumiki kwa sasa

Jengo likiwa limezungukwa na nyasi pande zote


WEST TEXAS LAKE


West Texas reservoir turns blood red,Thousands of dead fish float in a feew feet of dark red water that some are saying is a sign of end times.

Monday, August 01, 2011

RAMADHAN NJEMA


Tunawatakia mfungo mwema wa mwezi wa Ramadhan waislam wote duniani,na kutenda mambo mema siku zote kama alivyoagiza mwenyezi Mungu.