Tuesday, June 28, 2011
BEI YA MAFUTA YAATHIRI WENGI
Picha inayoonekana ni mwili wa marehemu ukifungwa kwenye pikipiki tayari kwa safari ya kuelekea kijiji cha Isansa wilayani Mbozi kutoka wilaya Mbeya,inaonekana ni kitu cha ajabu lakini ndio halisi iliyotokea,inakadiriwa kuwa kufika kijijini kwao ni zaidi kilomita 90 kama wangetumia gari ingewagharimu kuliko uwezo wao,hii inaashiria wananchi wanavyoishi kwa taabu na kubuni njia mbadala za kutatua matatizo yao bila kujali athari zinazoweza kutokea.
Monday, June 27, 2011
Sunday, June 26, 2011
YANGA ULIMI NJE KWA EL-MEREIKH
Leo El-mereikh imewalazimisha mabingwa wa Tanzania bara timu ya Yanga sare ya bao 2-2 kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa,El-mereikh waliweza kuwatawala Yanga kipindi cha pili kwa kucheza jinsi wanavyotaka na kufanikiwa kusawazisha bao la pili,Yanga kipindi waliingia cha pili safu ya kiungo ilikuwa imezidiwa na kuwapa nafasi El-mereikh kutawala mpira.
KAGAME CUP YAANZA
Michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika mashariki na kati imeanza kwa mechi za ufunguzi,zimepigwa mechi mbili,katika mechi ya kwanza timu ya Ocean view imeilaza timu ya Eticele ya Ruanda 3-2,huku Simba ikitoka 0-0 na vitalo ya Burundi,mechi hizo zitaendelea tena kwenye viwanja vya Jamhuri Morogoro na uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Friday, June 24, 2011
Thursday, June 23, 2011
Wednesday, June 22, 2011
Tuesday, June 21, 2011
Monday, June 20, 2011
KANISA LA MORAVIAN KUHAMISHIA MAKAO MAKUU MJINI DODOMA
Kanisa la Moravian liko kwenye mipango ya kuhamishia makao makuu ya kanisa hilo mjini Dodoma hayo yameelezwa na Askofu mkuu wa kanisa ndg.Alinikisa Cheyo katika ibada ilyofanyika jana kwenye kanisa la Ruanda Mbeya,alisema tayari wameshapata ekari 225 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi na vitega uchumi mbalimbali pia alielezea kuwa wako kwenye mipango ya kufungua campus ya chuo kikuu kinachomilikiwa na kanisa hilo kwenye mikoa ya Tabora na Dar es salaam na wanategemea kuanza september mwaka huu.
Saturday, June 18, 2011
Friday, June 17, 2011
Tuesday, June 14, 2011
SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI
Leo ni siku ya wachangia damu kwa hiari duniani,maadhimisho haya hufanyika kila june 14,picha inayoonekana ni bw.Paul Haule mkazi wa Nzovwe Mbeya akichangia damu katika siku hii kwenye kitengo cha damu salama akiwa na mtaalamu wa kitengo hicho bi. Salome Magwaza.Kumbuka damu haiuzwi
Sunday, June 05, 2011
TAIFA STARS YACHAPWA TENA,U-23 YAIFUNGA NIGERIA 1-0
Timu ya Taifa ya Tanzania leo imefungwa na timu ya taifa ya Africa ya kati bao 2-1 kwenye uliofanyika uwanja wa Complex Barthelemy Bonganda mjini Bangui huko Africa ya kati,kwenye mchezo mwingine timu ya vijana ya chini ya miaka 23 leo imefanikiwa kuwafunga wenzao wa Nigeria bao 1-0,Tanzania walipata bao dakika ya 84 likiwekwa kimiani na Thomas Ulimwengu kwenye uwanja Taifa jijini Dar es salaam
Thursday, June 02, 2011
AJALI NYINGINE MBEYA
Basi la kampuni ya Abood jana lilianguka eneo la mlima nyoka na kujeruhi abiria 36,kwa bahati nzuri halikusababisha vifo kwa abiria wake,huu ni mfululizo wa ajali kutokea mkoani Mbeya,Ijumaa iliyopita basi la Sumry lilipata ajali na kupoteza maisha ya watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa,Abood ilikuwa ikitokea Dar es salaam kuja Mbeya.
Tuesday, May 31, 2011
Monday, May 30, 2011
Sunday, May 29, 2011
BARCELONA BINGWA ULAYA
Timu ya Barcelona imetwaa ubingwa wa ulaya baada kuwachapa Manchester united bao 3-1,goli la kwanza la Barca liliwekwa kimiani na Pedro na Man walisawazisha kupitia Wayne Rooney hadi mapumziko timu hizo zilikuwa nguvu sawa,kipindi cha pili Barcelona walifanikiwa kupata mabao mawili kupitia kwa Leone Messi na David Villa mechi hiyo imechezwa kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Saturday, May 28, 2011
WYDAD CANSABLANCA YAICHAPA SIMBA 3-0.
Timu ya Simba leo imefungwa jumla ya mabao 3-0 na Wydad Cansablanca ya Morroco magoli ya wamorroco hao yamefungwa dakika ya 87 na mengine mawili yakifungwa dakika za majeruhi,mchezo huo umechezwa kwenye uwanja Petrosport jijini Cairo,na hivyo kuzima ndoto za Simba kucheza hatua ya makundi klabu bingwa Africa,sasa wataingia kwenye michuano ya kombe la shirikisho na kucheza na Motema Pembe ya Congo
Wednesday, May 25, 2011
MBEYA YAINGIA FAINALI KOMBE LA TAIFA
Timu ya mkoa wa Mbeya(Mapinduzi stars) imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya kombe la taifa,baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Kagera kwa jumla ya mabao 2-1,mchezo huo umechezwa kwa dakika 120,hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1,Mbeya ndio waliofanikiwa kupata ushindi baada ya beki wa Kagera kujifunga baada ya shambulizi kutokea golini kwao,mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kucheza soka maridadi na golikipa wa Mbeya Ivo Mapunda kuonyesha uwezo mkubwa,Mbeya watakutana na Mwanza Heroes siku ya jumamosi uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha katika fainali.
Thursday, May 19, 2011
SIMBA KUVAANA NA WYDAD CANSABLANCA CAIRO
Timu ya Simba imfanikiwa kurudi kwenye michuano ya klabu bingwa Africa baada ya rufaa yao kukubaliwa na shirikisho la soka Africa(CAF) na kuitupia mbali timu ya TP Mazembe ambao ndio mabingwa wa kombe hilo baada ya kumchezesha mlinzi halali wa timu ya Esperence ya Tunisia,sasa simba watacheza na wydad cansablanca ya Morocco kwenye uwanja huru huko jijini Cairo
Sunday, May 15, 2011
Thursday, May 12, 2011
Sunday, May 08, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)