BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Monday, March 26, 2012

MASHABIKI NDIO WANAUWA SOKA LA TANZANIA.


Katika hali isiyo ya kawaida,mashabiki wa soka hapa nchini wakifanya vitu vya tofauti sana ukilinganisha na nchi nyingine.
Haya ni moja ya matatizo ya mashabiki:-
1.Kuzomea timu ya taifa inapocheza.
2.Kuzomea baadhi ya wachezaji Taifa Stars,mfano Mwaikimba na Boko.
3.Kushangilia wageni kwenye michuano mbalimbali sababu ya Usimba na Uyanga.
4.Kutolipa viingilio vilivyopangwa.
5.Hawahudhurii kwenye mechi kama vile Villa Squad v/s Polisi Dom.
6.Kuwarushia chupa na makopo wachezaji na makocha.
7.Kutumia lugha chafu badala ya kushangilia.
8.Wanahitaji ushindi tu sio kushindwa.
9.Wanataka mafanikio ya haraka bila kujiandaa
Hizi ndizo sababu zinazoua soka la Tanzania na kuwapa wakati mgumu makocha na wachezaji wa kigeni.

SIMBA YAWACHAPA ES SATIF YA ALGERIA 2-0


Timu ya Simba leo imefanikiwa kuwafunga El Satif 2-0, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,mchezo huo ulikuwa ni wa kombe la shirikisho.
Simba walipata mabao hayo kipindi cha pili yakiwekwa wavuni na Moshi Kazimoto na Haruna Moshi,Simba walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kutawala eneo la kiungo na wapinzani wao wakiwa na wakati mgumu wote wa dakika 30 za mwanzo cha kipindi cha pili.
Es Satif wakiongozwa na Yousef Satif walishindwa kuhimili muziki wa Simba kutokana na mikakati ya wachezaji wa Simba.

Tuesday, March 20, 2012

FABRICE MUAMBA SASA ANAENDELEA VIZURI


Mchezaji wa Bolton ya Uingereza Fabrice Muamba sasa anaendelea vizuri baada ya kuweza kupumua mwenyewe bila msaada wa mashine na ameweza pia kuwatambua baadhi ya watu waliomtembelea hospitali leo.
Muamba alianguka ghafla kwenye mchezo wa kombe la FA kwenye uwanja wa White hart lane,wakati timu yake ikicheza na Tottenham Hotspur,mchezo huo ilibidi huahirishwe kutokana na hali ya Muamba kuwa mbaya,huku matokeo yakiwa 1-1 na kukimbizwa hospital ya Heart attack Centre jijini London.
Muamba alijiunga na Bolton 2008 akitokea Birmingham City kwa ada ya paundi (£) milion 5.
Muamba alizaliwa DRC miaka 23 iliyopita,na alipokuwa na umri wa miaka 11 alimufuata baba yake jijini London ambako alikuwa akifanya kazi.
Tukio hili limewakumbusha wanasoka na wapenzi wa soka mchezaji wa zamani wa Cameroun Mark Vivien Foe ambaye naye alianguka uwanjani na kupoteza maisha.

KANISA KUU KATOLIKI SUMBAWANGA NI MOJA YA VIVUTIO VYA MJI HUO.


Mdau wetu akiwa nje ya kanisa kuu la katoliki Sumbawanga Mjini.
Kanisa hilo ni moja ya majengo yanayopendezesha mji huo kutokana na usafi wake.

Sunday, March 18, 2012

MAZISHI YA DIWANI WA KATA YA MYOVIZI MH.SUNDAY SHULA YAFANYIKA LEO.


Umati wa waombolezaji wakiwa kijijini Ichesa wilayani Mbozi,wakkwenye mazishi ya diwani wa kata ya Myovizi kwa tiketi ya CCM.
Mh.Shulla alifariki jana asubuhi katika hospitali ya wilaya ya Mbozi na mazishi yake ndio yanafanyika muda huu.

Saturday, March 17, 2012

UJENZI WA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI WAENDELEA KWA KASI SUMBAWANGA-TUNDUMA


Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaendelea kwa kasi eneo la Kaengesa.
Mdau wetu alipita maeneo na kukuta kazi hiyo ikiendelea licha ya mvua nayo kuendelea kunyesha.

Friday, March 16, 2012

AFRICAN RAINBOW SECONDARY YACHAPWA NA MAZWI SECONDARY KWENYE MCHEZO WA KIRAFIKI.


Timu ya netball ya Mazwi Secondary leo imewafunga wenzao wa African Rainbow mabao 46-39.
Nyota wa mchezo wa leo alikuwa Georgina Maheka wa Mazwi licha ya kukabiliana na ukuta mgumu wa African Rainbow ukiongozwa na Tamali Joseph.
Mchezo umechezwa kwenye uwanja wa Mazwi Secondary.

Thursday, March 15, 2012

LIGI YA MKOA WA RUKWA JAMAICA YAIFUNGA RUKWA UNITED 2-1


Timu ya Jamaica FC imeifunga timu ya Rukwa united bao 2-1,kwenye ligi ya mkoa huo,magoli ya Jamaica yamefungwa na Steve Mwansite dakika ya 4 na la pili likifungwa na Torres,bao la kufutia machozi la Rukwa united limefungwa kwa njia ya Penati.

Monday, February 13, 2012

ZAMBIA MABINGWA WA AFRIKA 2012


Timu ya taifa ya Zambia(Chipolopolo) imefanikiwa kutwaa kombe la mataifa ya Africa usiku baada ya kuwashinda Ivory Coast kwa mikwaju ya penati 8-7.
Timu hizo zilicheza kwa dakika 120 na matokeo kuwa 0-0 na hivyo kuingia kwenye matuta ambapo kila ilipiga penati 9,Zambia ilikosa moja na Ivory Coast ilipoteza 2.
Shukrani za pekee zimuendee golikipa wa Zambia Kenedy Mwene, ambaye alikuwa nyota wa mchezo kwa dakika zote na kuweza kuokoa penati 1 kutokana na umahiri wake.

Sunday, February 12, 2012

WHITNEY HOUSTON AFARIKI


Mwanamuziki maarufu nchini Marekani amefariki usiku wa jana,mwanadada huyo ambaye alikuwa akihusishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya lakini aligeuka na kuanza kupinga utumiaji wa madawa hayo kwa watu wengine.
Mwanadada amekuwa na sifa za uvumilivu kwenye mahusiano yake ya kimapenzi licha ya kupitia mikasa mbalimbali lakini aliweza kuvumilia pamoja na umilionea aliyokuwa nao.

Thursday, February 09, 2012

TIMU YA TAIFA YA ZAMBIA YAINGIA FAINALI MICHUANO YA AFRIKA.


Timu ya taifa ya Zambia (Chipolopolo) imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika, baada ya kuwafunga Ghana(Black Star) kwa bao 1-0,
Zambia walipata bao lao kupitia kwa kupitia kwa Emanuel Mayuka dakika ya 78 na kuwafanya Zambia kuingia fainali,katika mchezo mwingine wa nusu fainali Ivory Coast wameifunga Mali bao 1-0.
Sasa Zambia watakutana na Ivory Coast katika mchezo wa fainali utakaochezwa kesho kutwa na Ghana watawakabili Mali katika kuwania nafasi ya tatu.

Wednesday, February 08, 2012

UCHAFUZI WA MAZINGIRA


Gari ya kubeba taka likiwa limebeba takataka ambazo zinaendelea kuungua na hivyo kusababisha moshi kusambaa barabarani na kuleta athari kwa watu,mbali na hilo pia inaweza kutokea ajali ya moto iwapo taka hizo zikiendelea kupulizwa na upepo.

UCHAFUZI WA MAZINGIRA


Gari ya kubeba taka likiwa limebeba takataka ambazo zinaendelea kuungua na hivyo kusababisha moshi kusambaa barabarani na kuleta athari kwa watu,mbali na hilo pia inaweza kutokea ajali ya moto iwapo taka hizo zikiendelea kupulizwa na upepo.

UCHAFUZI WA MAZINGIRA


Gari ya kubeba taka likiwa limebeba takataka ambazo zinaendelea kuungua na hivyo kusababisha moshi kusambaa barabarani na kuleta athari kwa watu,mbali na hilo pia inaweza kutokea ajali ya moto iwapo taka hizo zikiendelea kupulizwa na upepo.

UCHAFUZI WA MAZINGIRA


Gari ya kubeba taka likiwa limebeba takataka ambazo zinaendelea kuungua na hivyo kusababisha moshi kusambaa barabarani na kuleta athari kwa watu,mbali na hilo pia inaweza kutokea ajali ya moto iwapo taka hizo zikiendelea kupulizwa na upepo.

Wednesday, February 01, 2012

MVUA NI NEEMA TATIZO SISI


Kutokana ni miundo mbinu mibovu mvua imekuwa kama kero kwa wakazi wa Soweto jijini Mbeya,wamekuwa wakipata taabu kwenye maeneo ya barabara zinazoingia na kutoka mitaa hiyo kutokana na maji kujaa na kuhathiri mpaka maeneo ya biashara.kama inavyoonekana kwenye picha.

MTI HUU UNAWEZA UKASABABISHA AJALI.


Mti huu matawi yake yameingia barabarani na kusababisha mtu unayetembea kwa miguu usiweze kuliona gari linalokuja mbele au nyuma kutokana na matawi yaliyozidi na kuingia mpaka barabarani kwenye barabara ya Uhindini kuelekea Soko matola jijini Mbeya,wahusika inabidi walishughulikie suala hili mapema kabla madhara hayajatokea.

JIJI LETU MBEYA LEO


Picha hii ni moja ya mitaa ya jiji la Mbeya.

Tuesday, January 17, 2012

WAKULIMA HAWA WANAHITAJI MSAADA WA SOKO LA BIDHAA ZAO

 Wakina mama wa kijiji cha Mshewe Mbalizi wilaya ya Mbeya vijijini wakiuza maembe kwa bei ya shilingi 500/= kwenye plastiki,ambayo ni bei isiyoendana na wingi wa bidhaa hiyo,tunawaomba wale wote wenye uwezo wa kujua soko liliko wawasaidie wakulima
 Wakina mama wakiwa na watoto wao wakisubiri wateja wa maembe kijiji hapa kama walivyokutwa na kamera yetu.

Hili ni ambalo wakina mama hawa huuzia biashara zao za matunda

Moja ya matunda yaliyopo mashambani yakisubiriwa kuvunwa matunda yanajulikana kama maparachichi au matakapela pia yanapatikana kwenye kijiji hiki.


Wednesday, January 11, 2012

Dr.WILBORD SLAA AITEKA MBEYA LEO


Dr.Slaa akiwapungia mkono wananchi wakati akiondoka kwenye viwanja vya shule ya msingi Nzovwe  jijini Mbeya


Tuesday, January 10, 2012

MESSI MCHEZAJI BORA WA DUNIA 2012






  Mchezaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Leone Messi amefanikiwa kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia kwa mara ya tatu,Messi ameiwezesha timu yake ya Barcelona kutwaa mataji ya klabu bingwa Ulaya,klabu bingwa ya Dunia na ubingwa wa Hispania,amekuwa akipachika mabao muhimu na kutengeneza magoli kwa pasi zake za uhakika.



Wachezaji wa Barcelona wakishangilia ubingwa wa UEFA champion league.

Monday, January 09, 2012

DON AND YAMAVILLA DUKA LINALOWASAIDIA WAKULIMA KWA KIASI KIKUBWA WILAYANI MBOZI

                      DON AND YAMAVILLA AGRO CHEMICAL

Duka la pembejeo na madawa ya kilimo lililopo mji mdogo wa Mlowo,linalojulikana kama DON & YAMAVILLA AGRO CHEMICAL limekuwa ni msaada mkubwa kwa wakulima wa eneo hilo na vijiji vya jirani,kutokana na kuuza mbolea,madawa ya kilimo na kutoa ushauri juu ya matumizi ya madawa kwenye mimea.

Baadhi ya madawa yaliyoko kwenye duka hilo ambalo linamilikiwa na Dominick Mwamwezi,ambaye amesema duka hilo linatoa huduma nyingi kwa wateja ikiwemo huduma ya M-Pesa  na Tigo pesa kwa ajili ya kuwasaidia wateja wake.


Thursday, January 05, 2012

SUDAN KUSINI YATANGAZA JONGLEI YAKUMBWA NA MAAFA YA KIBINADAMU

 Baraza la mawaziri Sudan kusini limetangaza janga hilo katika mkutano maalum ambapo kundi la wapiganaji 6000 la kabila Luo nuer lilishambulia baadhi ya miji ikiwemo Lukangol na Pibor wiki iliyopita,na kuchoma mahema na kusababisha maelfu kukimbia maeneo hayo
Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu bi.Valerie Amos katika mkutano na waziri wa masuala ya kijamii  wa Sudan Amira Al Fadel Mohammed huko Khartoum.

Saturday, December 31, 2011

HAPPY NEW YEAR 2012


 2011 Has gone what have you done,whats your expectation in the coming year 2012 to me Latifah.I expect to be a regular blood donor and I wish to donate safe blood regularly to save peoples life.
 I wish all women to be regular blood donors in the coming new year 2012

Bi Latifa akiwa nje ya jengo la damu salama  kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya

Mtandao huu unawatakia mwaka mpya wa 2012 wenye mafanikio mema, amani na upendo
                                        "HAPPY NEW YEAR"

Friday, December 30, 2011

HALIMA MCHUKA KUZIKWA LEO

Mh.Rais wa jamhuri ya muungano Dr.Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya ndugu wa marehemu Halima Mchuka kuuombea dua mwili wa marehemu
Marehemu alikuwa mfanyakazi wa TBC mpaka inamfika,alifariki jana 29| Dec 2011,MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI MEMA PEPONI.


Mh. Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji maarufu wa TBC  Mchuka.Halima


THIERY HENRY KURUDI ARSENAL

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Thiery Henry anategemewa kutua kwenye klabu hiyo kwa muda wa miezi miwili akitokea Marekani ambako alienda kumalizia soka lake akitokea Hispania kwenye klabu ya Barcelona.

Thursday, December 29, 2011

SAYANSI NDIO KITU PEKEE KINACHOWEZA KULIINUA TAIFA




Fundi Fani  Mwenda akiwa kazini kwake akishughulika na kazi zake za kila siku za ufundi,kama anavyoonekana akisuka mota

Moja ya mota zinazosubiri kushughulikiwa




Mota ambazo zimeshafanyiwa kazi na mafundi hao

BAADHI YA BARABARA NI KERO KWA WATUMIAJI MBEYA



 Baadhi ya barabara jijini Mbeya zimekuwa zikipitika kwa shida kutokana na mvua inayoendelea kunyesha jijini Mbeya,maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ni kusababisha barabara kuchimbika na kujaa maji ni maeneo ya Block T na maeneo ya Soweto,tunaomba mamlaka husika kushughulikia suala hilo mapema


Hii ni bara bara inayotokea Block T kuekekea Soweto ikiwa imejaa maji

Hili ni eneo la Soweto jirani na maegesho ya taxi

Sunday, December 18, 2011

Mh.DAVID KAFULILA AFUKUZWA NCCR-MAGEUZI


Mbunge wa kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR amefukuzwa ndani ya chama hicho na halmashauri ya chama hicho.
Kufuatia hali hiyo kwa kanuni za bunge,bw.Kafulila anaweza kupoteza kiti chake cha ubunge kama jitihada za busara hazitafanywa ndani ya NCCR ili kulinusuru jimbo lao,NCCR-mageuzi ilidhoofika baada ya mgogoro mwingine uliyowahi kutokea na kumfanya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mh.Mrema kutimkia TLP na kukiacha chama hicho kikiendelea kupoteza wanachama na mwelekeo wa kisiasa.
Chama hicho kimewahi kuwa tishio katikati ya miaka ya 90 na kuwa na wabunge wengi bungeni kuliko vyama vingine vya upinzani kwa upande wa bara.

Friday, December 16, 2011

YANGA KUJIPIMA NA RUVU SHOOTING KESHO

Mabingwa wa afrika mashariki na kati kesho watacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.   Yanga wanaendelea na mazoezi makali kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Afrika na michuano ya ligi kuu ya Vodacom.

Saturday, December 10, 2011

UGANDA BINGWA


Timu ya taifa ya Uganda leo imenyakua ubingwa wa Tusker challenge cup kwa mara ya pili mfululizo,baada ya kuwachapa Rwanda kwa mikwaju ya penati.
Timu hizo zililazimika kwenye mikwaju ya penati baada ya kucheza dakika 120 na matokeo kuwa 2-2,kwenye mikwaju ya penati Uganda walipata 3 na Rwanda 2.
Kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu timu ya Sudan imefanikiwa kuishinda Kilimanjaro Stars bao 1-0

Friday, December 09, 2011

KIBAKA APEWA CHAI NA WANANCHI WENYE HASIRA.


Kibaka mmoja leo amekutana na wakati mgumu eneo la mabatini jijini Mbeya,kibaka huyo ambaye inasemekana amekuwa akiiba magunia ya mkaa mitaani,leo aliingia choo cha kike na kukutana na kichapo hicho

MIAKA 50 YA UHURU BADO ELIMU YA UCHANGIAJI DAMU HAIJAWAFIKIA WANANCHI VIZURI.


Dr.Emanuel Mbawala mwenye makazi yake jijini Mbeya,akiwa ni mmoja wa watu waliojitokeza kuchangia damu leo kwenye kituo cha damu salama nyanda za juu kusini kilichoko Mbeya,kulia kwake ni mfanyakazi wa kituo hicho akimpatia huduma nzuri Dr.Mbawala.

Thursday, December 08, 2011

KILIMANJARO STARS NJE

Timu ya Kilimanjaro stars leo imetupwa nje ya michuano ya Tusker Chalenji baada ya kufungwa bao 3-1 na Uganda Cranes,mchezo huo umechezwa kwa dakika 120,baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa zimefungana 1-1,Uganda waliweza kuzitumia vyema dk 30 za nyongeza na kujipatia mabao mawili na hadi mwisho wa Uganda 3 Kili 1

Wednesday, December 07, 2011

MOVENPICK HOTEL WABADILI JINA SASA INAITWA DAR SERENA HOTEL

Movenpick Hotel iliyopo mtaa wa ohio jijini Dar es salaam wamebadili jina na sasa hotel inajulikana kwa la Dar es salaam Serena Hotel.
 Imekuwa ni kawaida kwa wawekekezaji kubadili majina ya biashara zao kwa hapa nchini,Movenpick miaka michache iliyopita ilijulikana kama Sheraton kabla ya Movenpick,hii sasa imezoeleka kwa mfumo huu wa kubadili majina kwa makampuni makubwa kama vile ya simu na mengine.

Tuesday, December 06, 2011

MWENGE WAPANDISHWA MLIMA KILIMANJARO MIAKA 50 YA UHURU

Vijana wakiwa na mwenge wa uhuru baada ya kuagwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

KILIMANJARO STARS NA UGANDA CRANES ZAINGIA NUSU FAINALI

Timu ya Kilimanjaro stars na Uganda Cranes zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la Tusker chalenji 2011,Uganda wamepata nafasi hiyo kwa kuwafunga Zimbabwe bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa mchana uwanja wa taifa.
 Mchezo mwingine uliwakutanisha mabingwa watetezi Kilimanjaro Stars na timu ya taifa ya Malawi na matokeo ni Kilimanjaro Stars wameibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Nurdin Bakar kwa shuti kali na hivyo matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.