Timu ya JKT RUVU leo imefanikiwa kuwachapa mabingwa wa Tanzania bara Azam FC goli 1-0,ambao msimu uliopia walimaliza ligi bila kupoteza mchezo,kwenye uwanja wao wa Chamazi.
Na huko Shinyanga,wenyeji Stand United wamekula kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa Yanga ya Dar es salaam,Stand United waliingia uwanjani kwa kujiamini sana na hivyo kuipa Yanga wakati mgumu na kutoa mipira mingi ya kona ambazo hazikuzaa matunda.
Yanga walifanikiwa kupata goli la kwanza lililofungwa na Santos Jaja na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli hilo.
Kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Jaja,Coutinho na Niyonzima na nafasi zao kuchukuliwa na Hussein Javu,Jerison Tegete na Nizar Khalfan mabadiliko hayo yaliiwezesha Yanga kupata mabao mawili zaidi yakifungwa na Jerison Tegete dakika ya 73 na 87 hadi mwisho wa mchezo Yanga 3-Stand UTD O
Michezo mingine iliyochezwa leo na matokeo yake:-
.Azam FC 0-JKT Ruvu 1
.Prisons 1-Simba 1
.Kagera Sugar 1-Coastal 1
.Ndanda 0-Mgambo 1
Ruvu shooting 1-Polisi Moro 0
Kesho kutakuwa na mechi moja kati ya Mbeya City na Mtibwa Sugar uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kikosi cha Yanga kikiwa tayari kwa mchezo |
No comments:
Post a Comment