Marais wa Liberia ,Sierra Leone na Guinea,mataifa matatu yalioathirika vibaya na Ebola wanataka msaada zaidi ili kuwasaidia kukabiliana na ugonjwa wa Ebola. Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ameiambia banki ya dunia katika mkutano mjini Washington kwamba jamii ya kimataifa haijachukua hatua za dharura kwa kuwa watoto wanaendelea kuwa mayatima,huku madaktari na wauguzi wakifariki. Naibu wa shirika la afya duniani Bruce Aylward ameuambia mkutano huo kwamba Ebola imesambaa katika miji yote mikuu ya mataifa hayo matatu yalioathirika pakubwa na kwamba ulikuwa unaenea kwa kasi katika kila eneo. Afisa mkuu wa matibabu nchini Marekani Thomas Frieden amesema kuwa mlipuko wa Ebola hauwezi kufananishwa na ugonjwa mwengine tangu kuzuka kwa ugonjwa wa ukimwi.
No comments:
Post a Comment