Timu ya Simba ya Dar es salaam leo imelazimishwa sare na Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Taifa ambapo Simba walikuwa wenyeji kwenye mfululizo wa ligi kuu ya Vodacom.
Simba walianza mchezo huo kwa kasi na kuwafanya Stand United kucheza mchezo huo kwa hofu kubwa na kuwafanya Simba kutawala mchezo huo kwa kipindi kirefu lakini safu ya ushambuliaji haikuwa makini na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Lakini hata hivyo Simba ilifanikiwa kupata goli dakika ya 35 likifungwa na Shaaban Kisiga kutokana na uzembe mkubwa wa walinzi wa Stand United,furaha ya Wanasimba hao ilikatizwa dakika ya 44 na Heri Mohamed aliposawazisha goli hilo kwa kumalizia krosi iliyochongwa kutoka kushoto na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
Hii ni sare ya tatu mfululizo kwa Simba na kuwafanya na pointi 3 kwa michezo mitatu waliocheza,mchezo wa kwanza walitoa sare ya 2-2 na Coastal Union uwanja wa Taifa,mchezo wa pili 1-1 na Polisi Moro uwanja wa Taifa na mchezo wa tatu ndio huu wa leo hali inayoonekana sio nzuri hasa watavyotoka nje ya uwanja wa Taifa ambao wanautumia kama uwanja wa nyumbani.
Michezo mingine iliyochezwa leo na matokeo yake ni:-
.Coastal Union 2-Ndanda FC 1
.Tz Prison 0- Azam 0
.Polisi Moro 1 Kagera 1
.Ruvu Shooting 0- Mbeya City 0
Michezo mingine miwili itaendelea kesho kati ya Yanga na JKT Ruvu uwanja wa Taifa na Mtibwa na Mgambo JKT uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Saturday, October 04, 2014
SIMBA YATOKA SARE NA STAND UNITED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment