Yanga imeifunga AFC Leopard kutoka Kenya bao 1-0,kwenye mchezo wa kirafiki uliochechwa kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam,bao hilo lilifungwa na kiungo Kigi Makasi dakika ya 46 kwa shuti kali baada ya kumalizia pasi ya Jerry Tegete,mara baada kumalizika mchezo huo kocha mkuu wa AFC Noah Wanyama alisema mchezo utamsaidia kufanya marekebisho kadhaa kwenye kikosi chake,naye kocha wa Yanga Kosta Papic alisema mchezo huo umemsaidia kujua mapungufu kwenye kikosi chake,Yanga wanakabiliwa na michuano ya kimataifa kombb la shirikisho na imepangwa kuanza Dedebit ya Ethiopia na kama kushinda itakutana na wababe wa Simba kutoka Misri Haras el Hadood katika raundi ya pili.
Gari ya mizigo aina ya Volvo FH 12,Likiwa limeacha njia na kusababisha magari mengine kushindwa kupita hii imetokea asubuhi ya leo eneo la Songwe darajani kwenye barabara kuu ya Mbeya-Tunduma.
Nimeipenda sana hii mbinu ya kutumia matenki yaliyokuwa kwenye magari kwa ajili ya kuhifadhia maji badala ya kuuza kama vyuma chakavu,tanki moja linaweza kuchukua kama lita 21,000
Hivi ndivyo linavyoonekana soko la uhindini jijini Mbeya mara baada ya kuungua majuma kadhaa yaliyopita na kusababisha hasara kubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo.
Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa kwenye pilika pilika za maandalizi ya sikukuu ya Christmass na mwaka mpya eneo la Mwanjelwa ambalo ni maarufu jijini hapa kwa biashara za nguo za dukani na mitumba.
Madiwani wa wilaya ya Mbozi wameapishwa rasmi tarehe 17/12/10,na madiwani hao wamemchagua bwana Minga kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo,nilifanikiwa kuongea na mmoja wa madiwani hao mheshimiwa Sunday Shullah diwani wa Ichesa,alisema sasa wanaanza majukumu yao kwa nguvu kwa ajili ya kuleta mabadiliko na maendeleo ndani ya wilaya hiyo ambayo kuna matatizo ya maji,shule na vituo vya afya na mengine.
Benny signs and arts ni wataalam wa kuandika maandishi kwenye mabango,t.shirt,magari,sticker,kuta na michoro mbalimbali,wasiliana nao kwa simu 0715-539168,barua pepe bennsigns@yahoo.com
Utunzaji wa misitu ni muhimu kwa taifa lolote linalohitaji maendeleo,faida zake ni nyingi sana,lakini watanzania wengi faida wanayoelewa ni matumizi ya kuni na mkaa,kila mmoja wetu amuelimishe mwenzake juu ya umuhimu wa misitu-KATA MTI PANDA MTI.
0ne thing that children of divorce have to deal with,particularly if the divorce occurs early in their lives.....They develop emotional attachments with people who sometimes disappear from their lives.
Fred Malagi mfanyakazi wa National blood transfusion services,akiwa na meneja wa Golden city hotel,iliyopo mjini alipotembelea hotel hiyo kwa ajili ya sherehe ya family day kwa wafanyakazi wa NBTS-SOUTHERN HIGHLAND
Timu ya Zanzibar imefanikiwa kuichapa Sudan 2-0 kwenye mchezo wake dhidi Sudan,magoli ya Zanzibar yalifungwa na Allz Ahmed(shiboli) ambaye inasemekana kasajiliwa na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo.