BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Sunday, May 20, 2012

TIMU YA STENDI KUU MBEYA YAICHAPA ITIJI RANGERS


Mashabiki wa timu ya stendi kuu Mbeya wakishangilia ushindi waliopata dhidi ya Itiji Rangers wa mabao 2-0,kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya msingi Mbata jijini Mbeya,mabao ya stendi kuu yamefungwa na Aliko Sanga na Dominick Meshack,hata hivyo mchezo uliingia dosari na mwamuzi aliamua kuvunja mchezo kutokana na Itiji kugomea mchezo.
Michuano hiyo inadhamiwa na gazeti la Raha Tele

Monday, May 14, 2012

SIMBA YATOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA PENATI


Mabingwa wa Tanzania bara,Simba ya Dar es salaam wametolewa kwenye ya kombe la shirikisho Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao ya 3-0 na timu ya Al-ahly shandy ya Sudan.
Al-ahly Shandy walipata mabao yao dakika ya 46,50 na 60 mpaka mpira unaisha Simba walikuwa nyuma kwa mabao 3-0,kwa matokeo hayo mshindi wa jumla ilibidi hapatikane kwa njia ya penati kutokana na Simba kushinda kwa idadi hiyo hiyo ya magoli kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam.
Zilipigwa penati tisa tisa huku Al-ahly wakipoteza penati ya 3 iliyokolewa na mlinda mlango Juma Kaseja.Simba walipoteza penati ya 4 iliyopigwa na Patrick Mafisango.
Simba walipoteza penati ya mwisho iliyopigwa na Juma Kaseja.

Sunday, May 13, 2012

AIR TANZANIA YAPATA NDEGE MPYA


Shirika la ndege Tanzania limepata ndege mpya aina Boeing 737-500,ndege hiyo inategemea kuanza safari zake wiki ijayo kwenye miji kati ya Dar-Kilimanjaro na Mwanza.

Monday, May 07, 2012

SIMBA YAWAHARIBIA YANGA HISTORIA


Timu ya Simba jana imewafunga mahasimu wao Yanga kwa magoli 5-0 ambayo ni idadi kubwa ya magoli kwa zaidi ya miaka 37,ambapo mwaka 1976 Simba walipata ushindi wa goli 6 na kusababisha Yanga kusambaratika.
Simba walipata bao la mapema kupitia kwa Emanuel Okwi dakika ya kwanza,bao la pili dk.54 lilifungwa na Felix Sunzu kwa penati,bao la tatu dk.61 na Okwi,goli la nne 67 Kaseja kwa penati na la tano dk.72 Patrick Mafisango dk.72 kwa penati.
Baada ya mchezo huo mwalimu msaidizi wa timu hiyo ya Yanga Fred Felix Minziro Kataraiya alisema "timu ni nzuri tatizo ni migogoro iliyoko ndani ya klabu hiyo"
Nao wapenzi wa klabu hiyo wameutupia lawama uongozi wa timu hiyo kwa kushindwa kuongoza timu hiyo na kusababisha timu kuwa katika kipindi kigumu kwa msimu huu.

CHELSEA FC BINGWA WA FA CUP


Timu ya Chelsea FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa FA jana usiku kwa kuwafunga Liverpool 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Wembly jijini London.
Chelsea walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Lamires dk.ya 10,la pili kwa Drogba dk.59 na Liverpool likifungwa na Andy Carrol aliyeingia kipindi cha pili.


MICHEZO YA UMISETA WILAYA YA MBOZI YAFUNGULIWA LEO.


Michezo ya UMISETA kwa wilaya ya Mbozi imefunguliwa leo na afisa elimu wa wilaya hiyo kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Vwawa.
Michezo hiyo itazishirikisha shule za sekondari wilayani humo.

Saturday, May 05, 2012

MTIBWA YAWAPA SIMBA UBINGWA KIRAHISI.


Timu ya Mtibwa jana imewapa ubingwa Simba baada ya kuwafunga Azam bao 2-1 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa uwanja huru kwa timu zote,uwanja wa Taifa na kwa matokeo hayo Azam hawawezi kufikisha pointi 59 ambazo Simba wanazo tayari,huku Azam wakiwa na pointi 53 na kubakiwa na mchezo mmoja kwa kila timu.

RASHID YEKINI AFARIKI DUNIA.


Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na mchezaji bora wa kwanza wa Afrika mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya utaratibu huu kuanzishwa.
Yekini amefariki akiwa na umri wa miaka 48 na ameichechezea timu yake ya taifa kwa mafanikio makubwa kabla ya kutundika daluga.

Thursday, May 03, 2012

MZEE WAWILA HERMAN NZOWA AJITOLEA KUHAMASISHA ELIMU WILAYANI MBOZI.


Mzee Wawila Hermain Nzowa(84) mkazi wa kijiji cha Igamba wilayani Mbozi,amekuwa akipita kwenye shule za sekondari na msingi wilayani Mbozi.kuhamasisha wanafunzi kujisomea na kuepukana na maambukizi ya ukimwi.
Mzee Nzowa amesema amekuwa akifanya shughuli hii kwa kutembea shule hadi shule,mzee huyu ameomba taasisi au watu binafsi kumsaidia ili kuweza kuokoa taifa la kesho.