BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Saturday, December 31, 2011

HAPPY NEW YEAR 2012


 2011 Has gone what have you done,whats your expectation in the coming year 2012 to me Latifah.I expect to be a regular blood donor and I wish to donate safe blood regularly to save peoples life.
 I wish all women to be regular blood donors in the coming new year 2012

Bi Latifa akiwa nje ya jengo la damu salama  kanda ya nyanda za juu kusini Mbeya

Mtandao huu unawatakia mwaka mpya wa 2012 wenye mafanikio mema, amani na upendo
                                        "HAPPY NEW YEAR"

Friday, December 30, 2011

HALIMA MCHUKA KUZIKWA LEO

Mh.Rais wa jamhuri ya muungano Dr.Jakaya Kikwete akiwa na baadhi ya ndugu wa marehemu Halima Mchuka kuuombea dua mwili wa marehemu
Marehemu alikuwa mfanyakazi wa TBC mpaka inamfika,alifariki jana 29| Dec 2011,MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI MEMA PEPONI.


Mh. Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima zake za mwisho na kuuaga mwili wa aliyekuwa mtangazaji maarufu wa TBC  Mchuka.Halima


THIERY HENRY KURUDI ARSENAL

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Thiery Henry anategemewa kutua kwenye klabu hiyo kwa muda wa miezi miwili akitokea Marekani ambako alienda kumalizia soka lake akitokea Hispania kwenye klabu ya Barcelona.

Thursday, December 29, 2011

SAYANSI NDIO KITU PEKEE KINACHOWEZA KULIINUA TAIFA




Fundi Fani  Mwenda akiwa kazini kwake akishughulika na kazi zake za kila siku za ufundi,kama anavyoonekana akisuka mota

Moja ya mota zinazosubiri kushughulikiwa




Mota ambazo zimeshafanyiwa kazi na mafundi hao

BAADHI YA BARABARA NI KERO KWA WATUMIAJI MBEYA



 Baadhi ya barabara jijini Mbeya zimekuwa zikipitika kwa shida kutokana na mvua inayoendelea kunyesha jijini Mbeya,maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ni kusababisha barabara kuchimbika na kujaa maji ni maeneo ya Block T na maeneo ya Soweto,tunaomba mamlaka husika kushughulikia suala hilo mapema


Hii ni bara bara inayotokea Block T kuekekea Soweto ikiwa imejaa maji

Hili ni eneo la Soweto jirani na maegesho ya taxi

Sunday, December 18, 2011

Mh.DAVID KAFULILA AFUKUZWA NCCR-MAGEUZI


Mbunge wa kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR amefukuzwa ndani ya chama hicho na halmashauri ya chama hicho.
Kufuatia hali hiyo kwa kanuni za bunge,bw.Kafulila anaweza kupoteza kiti chake cha ubunge kama jitihada za busara hazitafanywa ndani ya NCCR ili kulinusuru jimbo lao,NCCR-mageuzi ilidhoofika baada ya mgogoro mwingine uliyowahi kutokea na kumfanya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho mh.Mrema kutimkia TLP na kukiacha chama hicho kikiendelea kupoteza wanachama na mwelekeo wa kisiasa.
Chama hicho kimewahi kuwa tishio katikati ya miaka ya 90 na kuwa na wabunge wengi bungeni kuliko vyama vingine vya upinzani kwa upande wa bara.

Friday, December 16, 2011

YANGA KUJIPIMA NA RUVU SHOOTING KESHO

Mabingwa wa afrika mashariki na kati kesho watacheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.   Yanga wanaendelea na mazoezi makali kwa ajili ya michuano ya klabu bingwa Afrika na michuano ya ligi kuu ya Vodacom.

Saturday, December 10, 2011

UGANDA BINGWA


Timu ya taifa ya Uganda leo imenyakua ubingwa wa Tusker challenge cup kwa mara ya pili mfululizo,baada ya kuwachapa Rwanda kwa mikwaju ya penati.
Timu hizo zililazimika kwenye mikwaju ya penati baada ya kucheza dakika 120 na matokeo kuwa 2-2,kwenye mikwaju ya penati Uganda walipata 3 na Rwanda 2.
Kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu timu ya Sudan imefanikiwa kuishinda Kilimanjaro Stars bao 1-0

Friday, December 09, 2011

KIBAKA APEWA CHAI NA WANANCHI WENYE HASIRA.


Kibaka mmoja leo amekutana na wakati mgumu eneo la mabatini jijini Mbeya,kibaka huyo ambaye inasemekana amekuwa akiiba magunia ya mkaa mitaani,leo aliingia choo cha kike na kukutana na kichapo hicho

MIAKA 50 YA UHURU BADO ELIMU YA UCHANGIAJI DAMU HAIJAWAFIKIA WANANCHI VIZURI.


Dr.Emanuel Mbawala mwenye makazi yake jijini Mbeya,akiwa ni mmoja wa watu waliojitokeza kuchangia damu leo kwenye kituo cha damu salama nyanda za juu kusini kilichoko Mbeya,kulia kwake ni mfanyakazi wa kituo hicho akimpatia huduma nzuri Dr.Mbawala.

Thursday, December 08, 2011

KILIMANJARO STARS NJE

Timu ya Kilimanjaro stars leo imetupwa nje ya michuano ya Tusker Chalenji baada ya kufungwa bao 3-1 na Uganda Cranes,mchezo huo umechezwa kwa dakika 120,baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa zimefungana 1-1,Uganda waliweza kuzitumia vyema dk 30 za nyongeza na kujipatia mabao mawili na hadi mwisho wa Uganda 3 Kili 1

Wednesday, December 07, 2011

MOVENPICK HOTEL WABADILI JINA SASA INAITWA DAR SERENA HOTEL

Movenpick Hotel iliyopo mtaa wa ohio jijini Dar es salaam wamebadili jina na sasa hotel inajulikana kwa la Dar es salaam Serena Hotel.
 Imekuwa ni kawaida kwa wawekekezaji kubadili majina ya biashara zao kwa hapa nchini,Movenpick miaka michache iliyopita ilijulikana kama Sheraton kabla ya Movenpick,hii sasa imezoeleka kwa mfumo huu wa kubadili majina kwa makampuni makubwa kama vile ya simu na mengine.

Tuesday, December 06, 2011

MWENGE WAPANDISHWA MLIMA KILIMANJARO MIAKA 50 YA UHURU

Vijana wakiwa na mwenge wa uhuru baada ya kuagwa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro

KILIMANJARO STARS NA UGANDA CRANES ZAINGIA NUSU FAINALI

Timu ya Kilimanjaro stars na Uganda Cranes zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya kombe la Tusker chalenji 2011,Uganda wamepata nafasi hiyo kwa kuwafunga Zimbabwe bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa mchana uwanja wa taifa.
 Mchezo mwingine uliwakutanisha mabingwa watetezi Kilimanjaro Stars na timu ya taifa ya Malawi na matokeo ni Kilimanjaro Stars wameibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kiungo Nurdin Bakar kwa shuti kali na hivyo matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa mchezo.

Monday, December 05, 2011

ZANZIBAR HEROES YAFUNGASHA VIRAGO


Timu ya Zanzibar Heroes leo imeaga michuano ya kombe la chalenji baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Rwanda (Amavubi) kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,mchezo huo ulianza kwa kasi na Rwanda waliweza kutawala mchezo huo kwa vipindi vyote hasa kutokana na umahiri wa kiungo wa Rwanda Haruna Niyonzima kuwabana na kuwafunika viungo wa Zanzibar Heroes.

SUDAN YAICHAPA BURUNDI 2-0 ROBO FAINALI YA CHALENJI

Timu ya taifa ya Sudan leo imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua robo fainali kwenye michuano ya kombe tusker chalenji cup baada ya kuwafunga timu ya taifa ya Burundi kwa magoli 2-0 kwenye mchezo uliochezwa leo mchana uwanja wa taifa Dar es salaam
  Mchezo mwingine utachezwa leo jioni kati ya Rwanda (amavubi) na Zanzibar heroes ukiwa ni mchezo mwingine wa robo fainali kwenye uwanja wa taifa.

Sunday, December 04, 2011

UWANJA WA NDEGE MWANZA WAKUMBWA NA MAFURIKO


Habari zilizotufikia hivi punde,uwanja wa ndege wa Mwanza umekumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo,na hivyo kusababisha ndege kushindwa kuruka ikiwemo ya waziri mkuu aliyekuwemo mkoani humo.

Saturday, December 03, 2011

KILI STARS HOI KWA ZIMBABWE

Timu ya soka ya Tanzania bara leo imefungwa magoli 2-1 na wenzao wa Zimbabwe kwenye michuano ya kombe la CECAFA inayoshirikisha mataifa ya Afrika mashariki na kati huku timu za Malawi na Zimbabwe zikiwa zimealikwa kwenye michuano hii.
  Zimbabwe walijipatia mabao yao kipindi cha kwanza kutokana na mabeki wa Kili stars kucheza kwa kutoelewana,hatimaye Kili Stars ilipata bao la kufutia machozi kwa njia ya penati iliyopigwa na Mwinyi Kazimoto baada ya Mrisho Ngasa kufanyiwa madhambi eneo la hatari zikiwa zimesalia dakika 4 mpira kumalizika.

Thursday, December 01, 2011

TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA


leo ni siku ya maadhimisho ya ukimwi duniani,ugonjwa ambao umekuwa ukiwasumbua watu wengi duniani inakadiriwa kuwa kuna watu zaidi milioni 34 wanaishi na maambukizi ya ugonjwa huo,inonekana nchi za kusini mwa jangwa la sahara ndizo zenye wagonjwa wengi,imekuwa zikifanyika jitihada mbali mbali kuhakikisha maambukizi ya ugonjwa huu yanapungua au kuutokomeza kabisa kwa kuwaelimisha watu.

Friday, November 25, 2011

MAFURIKO YALETA MAAFA MONDULI

 Baadhi ya picha zinnazoonyesha maafa yaliyotokana na mafuriko huko Monduli na miundo mbinu kuharibika





 Mwili wa marehemu ukiwa umenaswa kwenye vichaka

 Magari nayo yalibebwa na mafuriko hayo

MVUA YANYESHA KWA MUDA MREFU MBEYA.


Jiji la Mbeya leo limekuwa na neema baada ya mvua kunyesha kwa takribani masaa 10,na kusababisha watu kushindwa kuwahi makazini.

Wednesday, November 23, 2011

CHANGIA DAMU OKOA MAISHA


Damu ni tiba inayotokana na binadamu wenyewe kwa maana hiyo sisi ndio wenye jukumu la kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wanaohitaji tiba hiyo na kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji tiba hiyo,kwa wale wale walioko Mbeya unaweza ukafika kwenye kituo cha damu salama kilichoko hospitali ya wazazi Meta,Mwanza damu salama Bugando,kwa wale walioko Dar es salaam na maeneo jirani mtafika kituo cha damu salama kilichoko Mchikichini,Moshi mkabala na hospitali KCMC,Mtwara kituo cha damu salama Mtwara na Tabora fika kwenye kituo cha damu salama Tabora-CHANGIA DAMU MARA KWA MARA ILI UOKOE MAISHA.

PAPA BENEDICT XVI KUTEMBELEA BENIN


Kiongozi wa kanisa la katoliki duniani,Papa Benedict wa 16 anatarajia kutembelea nchi ya Benin wiki hii.
Hii ni ziara ya pili kwa Papa Benedict barani Africa tangu kuteuliwa kwake,na ni mara ya tatu kwa taifa la Benin kutembelewa na uongozi wa juu wa kanisa hilo,mwaka 1982 na 1993 walitembelewa na Papa John Paul II.
Msemaji wa Vatican amesema ziara hiyo ni ya kuleta amani na maridhiano barani Afrika.

AJALI MBAYA YATOKEA UBUNGO RIVER SIDE


 Wananchi wakijaribu kuokoa maisha ya watu waliokuwa kwenye gari dogo lililoingia uvunguni mwa lori eneo la Ubungo river side mchana wa leo
Wananchi wakiangalia ajali ambayo imepoteza maisha ya watu watatu na mmoja akiwa hai ndani ya gari dogo,jitihada za kumtoa zinaendelea kufanyika


TUKUYU NI NEEMA TU

Wakina mama wa eneo la Kiwira wakiuza matunda ya aina mbalimbali kwa wageni na wenyeji wa wanaopita kwenye barabara ya Dar-Malawi.


Wakina mama wakisubiri wateja wa ndizi eneo la Kiwira

Eneo hili ndilo linlofanyiwa biashara eneo la Kiwira,licha kukaa kihatarihatari


Wakina mama wakiuza ndizi,maparachichi,mananasi nk.kwenye basi linalofanya safari kati ya Mbeya na Kyela


MACHAFUKO MENGINE CAIRO

Hali inaelekea kuwa mbaya zaidi mjini Cairo kutokana na jeshi kutumia nguvu zaidi kwa ajili ya kuwadhibiti waandamanaji wanaoshinikiza utawala wa kijeshi kuondoka madarakani,tayari mpaka sasa zaidi watu 30 wanahofiwa kupoteza maisha kwenye machafuko yanayoendelea jijini Cairo,na sasa machafuko hayo yamemeanza kwenye miji ya Alexandria,Suez,Port Said na Aswan


Mmoja wa majeruhi akipata huduma ya kwanza

Hili ni eneo la Tahrir jijini Cairo ambalo linaonekana kuwa na vurugu zaidi

Thursday, November 17, 2011

UHABA WA MAJI WATISHIA USALAMA WA AFYA ZA WANANCHI MBALIZI.


Kufuatia uhaba wa maji uliyoukumba mji mdogo wa Mbalizi na vitongoji vyake,na kusababisha wakazi wa maeneo hayo kuchota maji na kufulia kwenye kwenye mifereji na mito,kunaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kutokana na mji huo kuwa na wakazi wengi na biashara nyingi.

Tuesday, November 15, 2011

LORI LANUSURIKA NA KUZIBA BARABARA.


Lori la mizigo aina ya Scania,jioni hii limenusurika kuanguka baada ya kuacha njia na kuingia kwenye mtaro ulioko kando ya barabara na kurudi tena barabarani na kuziba barabara kwa muda na kusababisha magari makubwa kushindwa kupita,ajali imetokea leo jioni eneo la Ntokela,barabara ya Uyole-Tukuyu,hakuna mtu aliyejeruhiwa kwenye ajali hiyo.

Sunday, November 13, 2011

MAREKANI YAOMBA MSAMAHA KWA INDIA


Marekani imeiomba msamaha serikali ya India kutokana na kitendo cha maafisa wake wa uwanja wa ndege wa New York kumpekua rais wa zamani wa India,bwana Abdul Kalam mwezi Septemba.
Serikali ilitoa malalamiko yake kwa Marekani kufuatia kitendo hicho kilichoonekana kama udhalilishaji kwa mheshimiwa huyo,pia mcheza sinema maarufu wa India Shah Rukh Khan aliwahi kulalamikia kitendo kama hicho alichofanyiwa mwaka 2009.