BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Monday, November 10, 2014

SIMBA YAZINDUKA USINGIZINI YAWACHAPA RUVU SHOOTING 1-0

  Timu ya Simba SC imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza kwenye ligi kuu ya Vodacom kwa kuwafunga RUVU SHOOTING goli 1-0 kwenye uwanja wa Taifa,goli hilo pekee limefungwa na Emmanuel Okwi baada golikipa kuutema mpira uliopigwa na Elias Maguri.
  Simba ikiwa imeingia uwanjani kwa mara ya saba ndio ushindi wake wa kwanza baada ya kutoka sare michezo sita mfulululizo na sasa wamefikisha alama tisa,huku Mtibwa Sugar wakiwa wanaongoza ligi kwa alama 15,wakifuatiwa na Azam na Yanga zenye alama 13 kila moja.
Matokeo mengine yalikuwa kama ifuatavyo:-

.Yanga 2-Mgambo 0

.Azam 2-Coastal 1

.Stand UTD 1-Mbeya City 0

.Polisi Moro 1-Prison 0

.Mtibwa 1-Kagera 1

.JKT Ruvu  2-Ndanda 0

Ligi hiyo itaendelea tena D
esemba 26 baada kusimama kwa ajili ya michezo ya Chalenji na Uhai Cup.

Emmanuel Okwi akishangilia goli alilofunga
Kocha Patrick Phiri akimpongeza Okwi kwa kuweza kuipatia timu ushindi
Mashabiki wa Simba wakiwa na furaha ya ajabu baada ya ushindi

No comments:

Post a Comment