BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Monday, December 27, 2010

YANGA YAILAZA AFC LEOPARD


Yanga imeifunga AFC Leopard kutoka Kenya bao 1-0,kwenye mchezo wa kirafiki uliochechwa kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam,bao hilo lilifungwa na kiungo Kigi Makasi dakika ya 46 kwa shuti kali baada ya kumalizia pasi ya Jerry Tegete,mara baada kumalizika mchezo huo kocha mkuu wa AFC Noah Wanyama alisema mchezo utamsaidia kufanya marekebisho kadhaa kwenye kikosi chake,naye kocha wa Yanga Kosta Papic alisema mchezo huo umemsaidia kujua mapungufu kwenye kikosi chake,Yanga wanakabiliwa na michuano ya kimataifa kombb la shirikisho na imepangwa kuanza Dedebit ya Ethiopia na kama kushinda itakutana na wababe wa Simba kutoka Misri Haras el Hadood katika raundi ya pili.

CHRISTMASS


Bw.Benjamin Kaminyoge anawapongeza wakristo na watanzania wote kwa kusherekea sikukuu ya christmass kwa amani na utulivu

MAMBO YA BARABARANI


Gari ya mizigo aina ya Volvo FH 12,Likiwa limeacha njia na kusababisha magari mengine kushindwa kupita hii imetokea asubuhi ya leo eneo la Songwe darajani kwenye barabara kuu ya Mbeya-Tunduma.

Saturday, December 25, 2010

Wednesday, December 22, 2010

Mchana mwema.


Mtoto RASMONSEN BEN KAMINYOGE akipata chakula cha mchana nyumbani kwao Mlowo Mbozi.

Consolata seminary-Mafinga


Nimeipenda sana hii mbinu ya kutumia matenki yaliyokuwa kwenye magari kwa ajili ya kuhifadhia maji badala ya kuuza kama vyuma chakavu,tanki moja linaweza kuchukua kama lita 21,000


Likizo fupi


Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Sebastian Kolowa-Lushoto Tanga,bw.FIKA-ELLY-JAMES akitafakari juu ya masomo.

MBEYA


Hivi ndivyo linavyoonekana soko la uhindini jijini Mbeya mara baada ya kuungua majuma kadhaa yaliyopita na kusababisha hasara kubwa kwa baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo.

MAANDALIZI YA SIKUKUU


Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa kwenye pilika pilika za maandalizi ya sikukuu ya Christmass na mwaka mpya eneo la Mwanjelwa ambalo ni maarufu jijini hapa kwa biashara za nguo za dukani na mitumba.


Monday, December 20, 2010

MBOZI


Madiwani wa wilaya ya Mbozi wameapishwa rasmi tarehe 17/12/10,na madiwani hao wamemchagua bwana Minga kuwa mwenyekiti wa halmashauri hiyo,nilifanikiwa kuongea na mmoja wa madiwani hao mheshimiwa Sunday Shullah diwani wa Ichesa,alisema sasa wanaanza majukumu yao kwa nguvu kwa ajili ya kuleta mabadiliko na maendeleo ndani ya wilaya hiyo ambayo kuna matatizo ya maji,shule na vituo vya afya na mengine. 


Sunday, December 19, 2010

SANAA


Benny signs and arts ni wataalam wa kuandika maandishi kwenye mabango,t.shirt,magari,sticker,kuta na michoro mbalimbali,wasiliana nao kwa simu 0715-539168,barua pepe bennsigns@yahoo.com

Saturday, December 18, 2010

MISITU NI UHAI


Utunzaji wa misitu ni muhimu kwa taifa lolote linalohitaji maendeleo,faida zake ni nyingi sana,lakini watanzania wengi faida wanayoelewa ni matumizi ya kuni na mkaa,kila mmoja wetu amuelimishe mwenzake juu ya umuhimu wa misitu-KATA MTI PANDA MTI.

Njombe


Ben James wa kushoto akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Njombe alipotembelea shule hiyo dec 11

NJOMBE SECONDARY SCHOOL


Wanafunzi wa Njombe sec kidato cha sita wanaonekana wakipendeza siku ya mahafali yao ya umoja wa kikristo yaliyofanyika lutheran centre Njombe.

Thursday, December 16, 2010

FAMILY SEPARATION


0ne thing that children of divorce have to deal with,particularly if the divorce occurs early in their lives.....They develop emotional attachments with people who sometimes disappear from their lives.

MAKAMBAKO


Hii ni sehemu ya mji wa Makambako ambayo ni njia panda ya Songea,Dar-es-salaam,Mbeya.mji huu ni wa kibiashara zaidi,wawekezaji kazi kwenu.

GOLDEN CITY HOTEL-MBEYA


Mdau wetu akiwa kwenye hotel ya Golden City iliyoko jijini Mbeya

FOREST HILL MOTEL(JM)


Forest Hill Motel ni moja kati ya sehemu tulivu kwa wageni wanaofika jijini Mbeya.

Mr.FRED MICHAEL MALAGI


Fred Malagi mfanyakazi wa National blood transfusion services,akiwa na meneja wa Golden city hotel,iliyopo mjini alipotembelea hotel hiyo kwa ajili ya sherehe ya family day kwa wafanyakazi wa NBTS-SOUTHERN HIGHLAND

Dr.Yosse Ndossy


Dr.Yosse Ndossy akiwa kazini,maabara ya kitengo cha damu salama kanda ya nyanda za juu kusini.

LATIFA BAKARI NYAKUNGA


Muamasishaji wa kitengo cha damu salama kanda ya nyanda za juu kusini,akitafakari jinsi ya kuwaelimisha wachangia damu kwa hiari.

Wednesday, December 01, 2010

Film


Ni moja ya filamu mpya inayokaribia kuingia sokoni hivi karibuni

ZANZIBAR HEROES YAIFUNGA SUDAN 2-0


Timu ya Zanzibar imefanikiwa kuichapa Sudan 2-0 kwenye mchezo wake dhidi Sudan,magoli ya Zanzibar yalifungwa na Allz Ahmed(shiboli) ambaye inasemekana kasajiliwa na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo.

Tuesday, November 30, 2010

Kilimanjaro stars yalala 1-0 kwa Chipolopolo


Nahodha wa kilimanjaro stars akimuongoza Rais wa jamhuri ya muungano mh.Jakaya Mrisho Kikwete kuwasalimia wachezaji wa kilimanjaro stars siku ya ufunguzi wa michuano inayoshirikisha mataifa ya afrika mashariki na kati na baadhi kutoka nje ya ukanda huu kualikwa kama Ivory coast,katika mchezo kili stars ilichapwa bao 1-0 na Wazambia.

Nani kama Mama


Mama mzazi wa mmiliki wa blog hii akiwa amepozi maskani kwake Mlowo Mbozi,tunakushukuru kwa malezi mema yenye maadili mema na tunaomba Mola akujalie afya njema na mafanikio mema katika maisha.