Mabingwa wa soka wa Tanzania bara wameshindwa kudhiirisha umwamba wao kwenye mechi za kimataifa baada ya kulazimishwa suluhu na wenyeji wao ELAN CLUB DE MITSOUDJE ya Comoro na hivyo kuwafanya wapinzani wao kuhitaji sare ya magoli ili waweze kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki mbili zijazo jijini Dar,nao mahasimu wao Yanga walishindwa kuutumia vyema uwanja wa taifa baada ya kulazimishwa sare ya mabao 4-4 na Dedebit ya Ethiopia na hivyo kujiweka katika mazingira magumu.
Wakina mama wa eneo la Lilondo wakifanya biashara ya ndizi kwenye mabasi yanayopita eneo hilo,mabasi yanayofanya safari kati ya Songea,Iringa,Mbeya na Dar es salaam.
Wafanyabiashara wa eneo la stendi kuu Songea,wakifanya biashara za vyakula katika eneo lisiloridhisha kwa afya za walaji na usalama kutokana na majiko kuwa jirani na mabasi.
Usafiri wa Bajaj umekuwa wa kawaida wa kawaida kwa baadhi ya sehemu hapa nchini,leo imetokea ajali ya Bajaj jijini Mbeya eneo la Meta baada ya Bajaj kuacha njia na kuingia kwenye mtaro kutokana na mwendo wa kasi na hivyo kusababisha dereva kushindwa kuimudu kwenye kona,wanaonekana wananchi wenye huruma wakiitoa bajaj hiyo,dereva na abiria wake walinusurika kwenye ajali hiyo.
Daladala inayofanya safari kati ya Mbalizi na Mwanjelwa ikiwa imeigonga gari ndogo eneo la Kadege,kwa bahati nzuri hakuna majeruhi kwenye ajali hii iliyotokea jioni hii.
Moja ya hotel za kisasa jijini Mbeya,Holiday hill hotel iko jirani na kanisa la Efatha,ina huduma za internet,chumba cha mikutana,maegesho ya magari na mambo mengi.
Dr.MATHEO KINEMO wa mpango wa taifa wa damu salama akitoa elimu juu ya kuchangia damu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Meta iliyoko jijini Mbeya,mdau wa globu hii anawapongeza na kuwashukuru wananchi wote wenye moyo wa huruma na kuchangia damu kwa ajili ya wagonjwa wenye upungufu wa damu wakiwemo wajawazito,watoto chini ya miaka mitano na waanga wa ajali mbali mbali kama vile ajali za barabarani,moto na kadhalika.
Kikosi cha zimamoto mkoani Mbeya kimefanikiwa kuinusuru hotel ya Calm inn,iliyokuwa imeshika moto,wanaonekana askari wa zimamoto wakiudhibiti moto huo.
Wauzaji wa matunda, mboga za majani na viungo wakiwa wamepanga bidhaa zao mbele ya maduka na kuzipanga chini,tunawaomba viongozi wa soko na halmashauri ya jiji kuwawekea mazingira mazuri wajasiliamali hawa kwa kuwaweka eneo zuri kwa afya za walaji na wao pia.
Wakazi wa kijiji cha Igurusi,mkoani Mbeya wakiwa kwenye pilikapilika za kila siku kwa ajili ya kujipatia riziki,kijiji hiki ni maarufu kwa biashara ya mchele.