BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Sunday, October 05, 2014

YANGA YAICHAPA JKT RUVU 2-1

Kikosi cha timu ya Young Africans chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo leo kimeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini  JKT Ruvu mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam. Young Africans iliingia uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi  wa mabao 2-1 dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons iliyoupata mwishoni mwa wiki na ikatumia chachu hiyo hiyo kupata ushindi kama huo katika mchezo wa leo. Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Kelvin Yondani "Cotton" aliipatia timu yake bao la kwanza dakika ya 32 ya mchezo kwa shuti kali akiitumia vizuri pasi nzuri ya kiungo Haruna Niyonzima aliyewatoka walinzi wa JKT Ruvu na kumpasia Yondani ambaye pia ndiye alianzisha mashambulizi ya bao hilo toka langoni mwa Yanga na kufunga bao lake la kwanza ndani ya klabu ya Young Africans. Washambuliaji wa Young Africans wakiongozwa na Geilson Santos "Jajaj", Saimon Msuva na Andrey Coutinho walikshindwa kuzitumia nafasi walizozipata kutokana na kutokua makini na mipira kuokolewa na walinzi wa JKT.  JKT Ruvu walicharuka na kucheza kwa nguvu kwa kukamia na kukuta wachezaji wake wakipewa kadi za njano baada ya kuwachezae vibaya wachezaji wa Young Africans wakiwemo Jaja, Niyonzima na Msuva. Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Young Africans iliwaangiza Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Salum Telela waliochukua nafasi za Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima na Edward Charles aliyeumia mabadilko ambayo yalileta tija kwa kikosi cha Maximo. Dakika ya 73 ya mchezo kiungo Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao la pili kwa mpira wa adhabu kufuatia kiungo Hassan Dilunga kuchezewa madhambi nje kidogo ya eneo la hatari na Niyonzima kupiga mpira uliojaa moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda lango wa JKT Ruvu Chove akiduwaa. Young Africans iliendelea kulishabulia lango la JKT kwa mpira wa speed kupitia kwa Msuva na Ngasa lakini mipira yao ya mwisho haikuwa na madhara na kukuta harakati zao zikiishia mikononi mwa golikipa Chove wa JKT Ruvu. Dakika ya 88 ya mchezo kiungo wa Jabir Aziz aliipatia timu yake ya JKT Ruvu bao la kufutia machozi kwa shuti kali baada ya kuitumia vyema pasi ya Amos Mgisa aliyewazidi ujanja walinzi wa Young Africans na kumkuta mfungaji alipiga shuti kali na kumuacha golikipa Dida akiruka bila mafanikio. Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 1 JKT Ruvu Stars, matokeo ambayo yanaipeleka timu ya Young Africans mpaka kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.  Young Africans: 1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3.Edward Charles/Salum Telela, 4. Nadir Haroub "Cananavao" (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite 7.Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Nizar Khalfani 9.Geilson Santos "Jaja" 10.Andrey Coutinho/Mrisho Ngasa 11.Saimon Msuva
  Mchezo mwingine ulichezwa huku Manungu Turiani kati ya Mtibwa na Mgambo JKT,Mtibwa wamepata ushindi wa goli 1-0 na kufikisha pointi 9 na kuweza kuongoza ligi wakifuatiwa Azam yenye pointi 7 

No comments:

Post a Comment