BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Wednesday, May 20, 2015

TAIFA STARS UWANJANI TENA LEO KUPAMBANA NA MADAGASCAR

Tokeo la picha la cosafa cup 2015                                                                                                        Timu 12 kati ya 14 kutoka nchi wanachama wa COSAFA tayari zipo nchini Afrika Kusini kuchuana katika mashindano hayo. Angola na Comoro ambazo ni wanachama wa COSAFA hazikuweza kushiriki mwaka huu.
Nafasi zao zimechukuliwa na Ghana iliyofikia fainali za michuano ya Caf ya mwaka huu na Tanzania kutoka ukanda wa Afrika mashariki na kati ikiwa mwanachama wa CECAFA.
Timu nane zenye viwango vya chini kwa ubora kwa mujibu wa takwimu za FIFA kwa mwezi Februari, zimepangwa katika makundi mawili yenye timu nne kila moja, Tanzania ikiwemo katika michuano hiyo.
Kundi A lina timu za Zimbabwe, Namibia, Seychelles na Mauritius. Ambapo kundi B lina timu za Madagascar, Lesotho, Swaziland na Tanzania.
Katika kundi A Zimbabwe inaoongoza kundi hilo kwa kujikusanyia pointi sita baada ya michezo miwili ikifuatiwa na Namibia yenye pointi nne. Seychelles ni ya tatu na pointi moja. Mkiani ni Mauritius ambayo haina pointi.
Na katika kundi B, Madagascar na Swaziland zote zina pointi tatu, huku Lesotho na Tanzania zikiwa mikono mitupu.
Tanzania leo,Jumatano inarusha karata yake ya pili kwa kupambana na Madagascar baada ya kucharazwa bao 1-0 na Swaziland katika mchezo wake wa kwanza.
Timu za juu katika kila kundi zitasonga mbele hatua ya mtoano, ambapo timu sita za viwango vya juu zitaingia katika mashindano hayo yakiwa katika hatua ya robo fainali na kuendelea. Afrika Kusini kutokana na ubora wake itapambana na Botswana hatua ya robo fainali.

RAHEEM STERLING KUACHANA NA LIVERPOOL

Raheem Sterling
                   
Raheem Sterling wa Liverpool anatarajia kumuaga kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers na kuondoka Anfield msimu huu.
Mshambulizji huo katika ligi ya England tayari amekwisha saini mkataba mwingine wa kiasi cha Paund laki moja kwa wiki na kukanusha kuwa yeye hana tamaa na pesa,kama alivyohojiwa na BBC.
Mchezaji huyo anatarajiwa kukutana na Mkurugenzi wake Ian Ayre na Kocha wake Rodgers siku ya ijumaa,ambapo atakuwa tayari kuwaeleza kuwa sasa anapaswa kuiipa kisogo klabu hiyo.
Hata hivyo klabu hiyo ya Liverpool haijataka kusema lolote kwa sasa japo kuwa inaeleweka kuwa bado wanamhitaji mchezaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 20 na ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2017.
Klabu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, ikiwemo Manchester City,Arsenal pamoja na timu nyingine kubwa Ulaya zinamhitaji pia.
Hata hivyo Kaptain wa Liverpool Steven Gerrard akizungumza sikuya Ijumaa wiki iliyopita alimtaka Sterling kubakia katika timu hiyo na kusisitiza kuwa ni vizuri kuwa katika klabu ambayo kocha ana imani na wewe.



Wednesday, May 13, 2015

MRISHO NGASSA KUCHEZA AFRIKA KUSINI


Mrisho Ngassa akimiliki mpira
Sasa ni rasmi, mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa amemwaga wino kuichezea klabu ya Free State Stars ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa miaka minne .
Ngasa ameripotiwa kufurahia mkataba huo mnono na kuanza kwake kwa maisha mapya baada ya kucheza nyumbani kwa miaka kadhaa.
Ngasa ameonekana katika mitandao kadhaa akiwa na kocha wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba.
“Nataka kutumia fursa hii kuitangaza soka ya Tanzania na nitajituma ili kufanya vizuri zaidi", amesema mchezaji huyo.

TETEMEKO LA ARDHI LAJERUHI NA KUUWA NEPAL

Raia wa Nepal wakishangaa matokeo ya tetemeko jipya
Wakati kukiripotiwa mvua kubwa na tetemeko kubwa na jipya nchini Nepal, Wakuu nchini humo wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo jipya , imepanda na kufikia zaidi ya watu 60.
Wakati huo huo helikopta ya kikosi cha majini cha Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa, ndani ya helkopta hiyo kulikuwa na watu nane,miongoni mwao, sita ni askari wa kikosi cha majini cha Marekani na askari wawili wenyeji wa jeshi la Nepal.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.