BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Wednesday, April 22, 2015

SIMBA YAMALIZIA HASIRA ZA MBEYA CITY KWA MGAMBO JKT.

  Timu ya Simba SC ya Dar es salaam leo imewaadhibu Mgambo JKT ya Tanga kwa jumla ya magoli 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
 Magoli ya Simba yamefungwa na Emmanuel Okwi matatu na Ramadhani Singano Messi akipachika goli moja kwa mpira wa adhabu ambao ulikwenda moja kwa moja wavuni,Simba waliweza kutawala mchezo huo kwa muda wote na kama washambuliaji wake wangekuwa makini zaidi wangeweza kuondoka na kapu la magoli,Simba ambayo siku nne zilizopita ilifungwa goli 2-0 na Mbeya City leo wamerekebisha makosa yao na kucheza mpira wa hali ya juu na kuweza kuwadhibiti wapinzani wao ambao kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika Mkwakwani Tanga waliweza kuwafunga Simba goli 2-0.
 Simba sasa inafikisha alama 38,ikiwa imecheza michezo 23 wakiwa nyuma ya Azam fc wenye alama 42 na michezo 22,timu ya Yanga ndio inaongoza ligi ikiwa na alama 49 kwa michezo 22 ni dhahiri kuwa Yanga wamejihakikishia moja kati ya nafasi mbili za juu kutokana na Simba hata kama itashinda michezo yake iliyobaki itaishia alama 47 ambazo zimeshapitwa na Yanga,Simba sasa itabidi amuombee Azam matokeo mabaya ili aweze kupata nafasi ya pili ambayo itampa tiketi ya kuliwakilisha Taifa kwenye michezo ya shirikisho mwakani.
 Huu ndio msimamo wa ligi kuu baada ya mechi ya leo:
 Hali si nzuri kwa timu za Tanzania Prisons,Polisi Morogoro,Ndanda FC na JKT Ruvu zisipofanya marekebisha ya haraka zinaweza zikajikuta miongoni mwao zinashuka daraja msimu huu.

No comments:

Post a Comment