BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Friday, May 08, 2015

CHAMA CHA DAVID CAMERON CHASHINDA UINGEREZA.

                                                                                                                                                                                                                                        Waziri mkuu David Cameron amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Uingereza hiyo jana.
Chama chake cha Conservative kimejipatia 326
Chama kikuu cha upinzani Leba kimesajili jumla ya viti 217 hii ikiwa na viti 25 chini ya idadi iliyokuwa nayo katika bunge lililopita.
Wakati huohuo habari zinazotufikia ni kwamba Nick Clegg amejiuzulu kama kiongozi wa chama cha Liberal Democrat baada ya kushindwa na chama cha Conservative..
Na huku matokeo ya theluthi moja ya maaneo bunge yakiwa yametangazwa waziri mkuu David Cameron anaonekana kurejea afisini lakini bila idadi kubwa ya wabunge ikimaanisha kuwa Chama cha Conservative kitalazimika kuunda serikali ya muungano.
Cameron amesema kuwa anapania kuendelea kuiongoza Uingereza ya pamoja .
Shirika La BBC linakisia kuwa Cameron na Chama chake huenda wakasajili ushindi wa maeneo bunge 329.
Waziri huyo mkuu hata hivyo anawaomba wafuasi wake wasubiri hadi matokeo kamili yatangazwe.
Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland kutoka kwa chama cha kitaifa cha Scotland National Party SNP .

No comments:

Post a Comment