BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Tuesday, October 07, 2014

DIKTETA WA ZAMANI HAITI JEAN CLAUDE DUVALIER AFARIKI

  Kiongozi wa zamani wa utawala wa kimabavu wa Haiti, Jean Claude 'Baby Doc' Duvalier, amefariki kutokana na mshtuko wa moyo, akiwa na umri wa miaka 63. Duvalier alitawala taifa hilo maskini la bahari ya Caribean kuanzia 1971 hadi kupinduliwa kwake na wananchi 1986. Kama babake, 'Papa Doc' Duvalier, Baby Doc alitawala kwa ukatili akitumia hasa kikosi maalum cha polisi wanamgambo maarufu kwa jina la 'Tonton Macoutes', katika kuwakandamiza wananchi. Wanamgambo hao wanatuhumiwa kwa mauwaji na kutoweka kwa mamia ya watu kisiwani humo. Baada ya kuishi miaka 25 uhamishoni Ufaransa, Baby Doc alirudi nyumbani 2011 kufuatia tetemeko kubwa kabisa la ardhi kuwahi kutokea nchini humo 2010. Aliporudi nyumbani alifunguliwa mashtaka ya ulaji rushwa, utumiaji mbaya wa utawala wake pamoja na ukatili ulotendeka chini ya utawala wake.

RAIS UHURU KENYATTA KIZIMBANI THE HAGUE

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameondoka nchini humo leo kuelekea The Hague ili kuhudhuria kikao juu ya kesi inayomkabili katika mahakama ya kimataifa –ICC
  Jumatatu Bw. Kenyatta alitoa hotuba isiyo ya kawaida kwa wabunge na maseneta iliyopeperushwa moja kwa moja kupitia vyombo vya habari na kwenye mtandao wa internet.   Katika hotuba hiyo Bw. Kenyatta alimkabidhi madaraka ya muda naibu rais William Ruto ili aweze kwenda Uholanzi bila kuacha pengo la madaraka. Alisema anakwenda kwenye mahakama hiyo kama mwananchi wa 'kawaida' na kusisitiza kuwa kamwe hana hatia. Yeye pamoja na naibu rais Ruto, wanashtakiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka wa 2007, ambapo maelfu ya wakenya waliuawa na wengine wengi kulazimika kutoroka manyumbani mwao. Katika uchaguzi huo, rais wa zamani Mwai Kibaki na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga walikuwa wanagombania urais. Bwana Kenyatta hata hivyo na mgombea mwenza William Ruto walichaguliwa na Wakenya kuongoza taifa hilo na kuapishwa mwezi Aprili mwaka 2013. Wote wawili wamekanusha kuhusika na ghasia hizo na wameshirikiana na mahakama hiyo ya ICC. Ni mara ya kwanza kwa rais anayehudumu kuwa katika mahakama hiyo ya kimataifa. Kesi ya Bw. Kenyatta itasikilizwa Jumatano.

ALIYEBADILI JINSIA ASHINDA KESI KENYA

  Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke na kutaka jina lake kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.    Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa. Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi la serikali. Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote. Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote. Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa. 'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji. Jaji alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu kuwaheshimu wengine kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo inahusu mambo mengi ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa. Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi kuwa sawa anapaswa kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu. Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.

Monday, October 06, 2014

SIERRA LEONE REPORTS RISE IN EBOLA DEATHS

  The number of deaths caused by Ebola has reached 678 in Sierra Leone, according to the country's health ministry. WHO officials are still verifying the rapid spike figures. Ebola has claimed 678 lives in Sierra Leone, officials in the West African country's capital Freetown reported on Sunday. The figure is a significant increase on the 557 deaths the health ministry reported the day before. Last week, Sierra Leone communicated to the World Health Organization (WHO) that there had been 575 Ebola deaths and 48 more cases where Ebola may have been the cause of death - a total of 632. The figures have, however, caused some confusion because the health ministry reported 557 deaths on Saturday, implying that there were 121 more cases between Saturday and Sunday. The numbers have not yet been verified by the WHO. In all, the WHO has verified 3,431 Ebola-related deaths in Liberia, Sierra Leone and Guinea. Out of these, 2,069 have died in Liberia alone because of the infection which causes severe bleeding, fever and diarrhea. West Africa needs more help Meanwhile, Liberia's ambassador to Germany, Ethel Davis, called on Monday for more contributions to stop the disease from spreading and said that "if the virus were not stopped, it would cross the borders of countries dealing with the infection." Speaking in Berlin, Davis said that West Africa needed more help or else it "would be lost" without any assistance to combat the tropical fever. German aid organization ISAR has constructed quarantine stations in the Liberian capital, Monrovia, with facilities to treat 44 patients infected with the Ebola virus. However, ISAR chief Thomas Laackmann told German news agency DPA that more needs to be done. "Even now, patients are being sent back from hospitals and people are dying on the streets every day," he said. Donations not forthcoming Donations from the German public to combat Ebola have not been easy to come by. Manuela Rossbach of the aid organization Aktion Deutschland Hilft lamented meager collections of only 90,000 euros ($113,000) compared to more generous contributions for other catastrophes. The German government is also planning to airlift supplies from Senegal to Ebola-affected countries. The aid would include medicines and supplies worth 17 million euros. German soldiers have also been asked to volunteer to help in Ebola-affected areas. Aid organization ASB has also begun a project aimed at Ebola prevention and creating awareness about the virus in Gambia, which is vulnerable to the disease because of its proximity to Senegal and because of its lack of medical supplies.

JULES BIANCHI APATA AJALI KWENYE MASHINDANO YA JAPAN GRAND PRIX

  Katika Mashindano ya mbio za magari ya langa langa ya Formula One dereva wa Ufaransa, Jules Bianchi, yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuumia vibaya kichwa chake kutokana na ajali ya kugongana na dereva mwingine katika mashindano ya Japan Grand Prix. Madaktari wa upasuaji wanaendelea kumhudumia dereva huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alipoteza fahamu wakati alipofikishwa hospitalini hapo. Bianchi alipoteza uelekeo wa gari lake kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, hata hivyo ajali hiyo iliyosababishwa na mwendo kasi mkubwa. Dereva wa Uingereza Lewis Hamilton alitangazwa mshindi katika mashindano hayo.

Sunday, October 05, 2014

YANGA YAICHAPA JKT RUVU 2-1

Kikosi cha timu ya Young Africans chini ya kocha mbrazil Marcio Maximo leo kimeendeleza wimbi la ushindi katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini  JKT Ruvu mchezo uliofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijin Dar es salaam. Young Africans iliingia uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi  wa mabao 2-1 dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons iliyoupata mwishoni mwa wiki na ikatumia chachu hiyo hiyo kupata ushindi kama huo katika mchezo wa leo. Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Kelvin Yondani "Cotton" aliipatia timu yake bao la kwanza dakika ya 32 ya mchezo kwa shuti kali akiitumia vizuri pasi nzuri ya kiungo Haruna Niyonzima aliyewatoka walinzi wa JKT Ruvu na kumpasia Yondani ambaye pia ndiye alianzisha mashambulizi ya bao hilo toka langoni mwa Yanga na kufunga bao lake la kwanza ndani ya klabu ya Young Africans. Washambuliaji wa Young Africans wakiongozwa na Geilson Santos "Jajaj", Saimon Msuva na Andrey Coutinho walikshindwa kuzitumia nafasi walizozipata kutokana na kutokua makini na mipira kuokolewa na walinzi wa JKT.  JKT Ruvu walicharuka na kucheza kwa nguvu kwa kukamia na kukuta wachezaji wake wakipewa kadi za njano baada ya kuwachezae vibaya wachezaji wa Young Africans wakiwemo Jaja, Niyonzima na Msuva. Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Young Africans iliwaangiza Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Salum Telela waliochukua nafasi za Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima na Edward Charles aliyeumia mabadilko ambayo yalileta tija kwa kikosi cha Maximo. Dakika ya 73 ya mchezo kiungo Haruna Niyonzima aliipatia Young Africans bao la pili kwa mpira wa adhabu kufuatia kiungo Hassan Dilunga kuchezewa madhambi nje kidogo ya eneo la hatari na Niyonzima kupiga mpira uliojaa moja kwa moja wavuni na kumuacha mlinda lango wa JKT Ruvu Chove akiduwaa. Young Africans iliendelea kulishabulia lango la JKT kwa mpira wa speed kupitia kwa Msuva na Ngasa lakini mipira yao ya mwisho haikuwa na madhara na kukuta harakati zao zikiishia mikononi mwa golikipa Chove wa JKT Ruvu. Dakika ya 88 ya mchezo kiungo wa Jabir Aziz aliipatia timu yake ya JKT Ruvu bao la kufutia machozi kwa shuti kali baada ya kuitumia vyema pasi ya Amos Mgisa aliyewazidi ujanja walinzi wa Young Africans na kumkuta mfungaji alipiga shuti kali na kumuacha golikipa Dida akiruka bila mafanikio. Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 1 JKT Ruvu Stars, matokeo ambayo yanaipeleka timu ya Young Africans mpaka kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015.  Young Africans: 1. Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3.Edward Charles/Salum Telela, 4. Nadir Haroub "Cananavao" (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite 7.Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Nizar Khalfani 9.Geilson Santos "Jaja" 10.Andrey Coutinho/Mrisho Ngasa 11.Saimon Msuva
  Mchezo mwingine ulichezwa huku Manungu Turiani kati ya Mtibwa na Mgambo JKT,Mtibwa wamepata ushindi wa goli 1-0 na kufikisha pointi 9 na kuweza kuongoza ligi wakifuatiwa Azam yenye pointi 7 

Saturday, October 04, 2014

SIMBA YATOKA SARE NA STAND UNITED

  Timu ya Simba ya Dar es salaam leo imelazimishwa sare na Stand United ya Shinyanga kwenye uwanja wa Taifa ambapo Simba walikuwa wenyeji kwenye mfululizo wa ligi kuu ya Vodacom.
  Simba walianza mchezo huo kwa kasi na kuwafanya Stand United kucheza mchezo huo kwa hofu kubwa na kuwafanya Simba kutawala mchezo huo kwa kipindi kirefu lakini safu ya ushambuliaji haikuwa makini na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
  Lakini hata hivyo Simba ilifanikiwa kupata goli dakika ya 35 likifungwa na Shaaban Kisiga kutokana na uzembe mkubwa wa walinzi wa Stand United,furaha ya Wanasimba hao ilikatizwa dakika ya 44 na Heri Mohamed aliposawazisha goli hilo kwa kumalizia krosi iliyochongwa kutoka kushoto na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
  Hii ni sare ya tatu mfululizo kwa Simba na kuwafanya na pointi 3 kwa michezo mitatu waliocheza,mchezo wa kwanza walitoa sare ya 2-2 na Coastal Union uwanja wa Taifa,mchezo wa pili 1-1 na Polisi Moro uwanja wa Taifa na mchezo wa tatu ndio huu wa leo hali inayoonekana sio nzuri hasa watavyotoka nje ya uwanja wa Taifa ambao wanautumia kama uwanja wa nyumbani.
  Michezo mingine iliyochezwa leo na matokeo yake ni:-
.Coastal Union 2-Ndanda FC 1
.Tz Prison 0- Azam 0
.Polisi Moro 1 Kagera 1
.Ruvu Shooting 0- Mbeya City 0
Michezo mingine miwili itaendelea kesho kati ya Yanga na JKT Ruvu uwanja wa Taifa na Mtibwa na Mgambo JKT uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Monday, September 29, 2014

YANGA SASA YAANZA LIGI

  Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa na Mtibwa Sugar wiki iliyopita,Yanga wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Tanzania Prison ya Mbeya kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
  Mchezo ulianza kwa Yanga kumiliki kipindi cha kwanza idara zote na kufanikiwa kupata goli dakika ya 34 likifungwa na Mbrazil Andre Coutinho goli hilo lilidumu hadi mapumziko.
  Kipindi cha pili Prison walirudi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 62,kabla ya Simon Msuva kuipatia Yanga goli la pili dakika ya 67 kwa kichwa kufuatia pasi ya Mrisho Ngassa hadi mwisho wa mchezo Yanga 2-Prison 1.
  Katika mchezo mwingine huko Chamazi Complex timu ya Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.

Kikosi cha Yanga
Shabiki maarufu wa Yanga na Taifa stars anayejulikana kwa jina la Ally Yanga akiwa na wenzake uwanja wa Taifa