BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Saturday, September 20, 2014

YANGA YAANZA LIGI YA VPL KWA KUCHAPWA 2-0 NA MTIBWA

Timu ya Yanga ya Dar es salaam leo imeanza ligi kuu ya Tanzania bara kwa kufungwa goli 2-0 na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wenyeji wa mchezo huo wakicheza kwa kujiamini na kufanya mashambulizi ya kushitukiza waliduwaza Yanga dakika ya 15 ya mchezo baada ya Mussa Hassan Mgosi kupachika bao la kwanza kwa kuwazidi ujanja walinzi wa Yanga.
Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na kulisakama lango la wapinzani wao na kupata goli ambalo mwamuzi wa mchezo huo alikataa na kutoa penati kwa Yanga ambayo iliota mbawa,penati hiyo ilipigwa na Mbrazil Jaja na kumgonga miguuni golikipa Said Mohamed muda mfupi baadaye Yanga waliweza tena kupata goli lakini mwamuzi aligoma kwa madai mfungaji alikuwa ameotea.
Timu hizo zilienda mapumziko huku Mtibwa ikiwa mbele kwa goli 1-0,kipindi cha pili Yanga waliingia na kutawala mchezo huo lakini bahati haikuwa yao kwani dakika ya 83 Ame Ally aliifungia Mtibwa goli la pili hadi mwisho wa mchezo Mtibwa 2 Yanga 0
Michezo mingine iliyochezwa leo na matokeo yake:-
.Azam 3-Polisi Moro 0
.Ndanda FC 4-Stand Utd 1
.Mgambo JKT 1-Kagera 0
.Ruvu shooting 0-Prisons 2
.Mbeya City 0-JKT Ruvu 0
Ligi hiyo itaendendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Simba na Coast Union uwanja wa Taifa Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment