BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Sunday, April 24, 2011

MITAMBO YA KUPIMIA MITA ZA MAJI


Mdau wetu akiwa ametembelea mitambo maalumu inayotumika kupima mita za maji zenye matatizo huko Mbeya.

Sunday, April 17, 2011

MANCHESTER YAKABWA KOO


Manchester united jana imefungwa bao 1-0 na mahasimu wao Manchester City,katika michuano ya FA CUP,michuano hiyo imekuwa na msisimko mkubwa kwa timu ndogo kuzitoa jasho timu kubwa.

Saturday, April 16, 2011

AJALI MBAYA YATOKEA ARUSHA

Poleni ndugu zetu wa Arusha kwa msiba uliowapata  kutokana na ajali ya iliyohusisha basi la kampuni ya ngorika na basi dogo aina ya hiace na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa.

Thursday, April 14, 2011

SHITAMBALA AISALITI CHADEMA

Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha maendeleo mkoa wa Mbeya ameamua kuhama chama chake na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM,uamuzi wake umepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi mkoani Mbeya

Monday, April 11, 2011

YANGA BINGWA


Timu ya Yanga imetwaa ubingwa wa Tanzania bara baada ya kuifunga Toto African kwa jumla ya mabao 3-0,magoli ya Yanga yalifungwa na Nurdin Bakar na Davies Mwape yote kipindi cha pili,hivyo kuifanya Yanga kufikisha pointi 49 sawa na mahasimu wao Simba lakini wanakuwa mabingwa kwa tofauti ya magoli,Simba waliifunga Majimaji ya Songea bao 4-1.

Saturday, April 09, 2011

STENDI KUU MBEYA


Ukarabati unaoendelea ndani ya kituo cha mabasi Mbeya umesababisha lango la kutokea kufungwa kwa muda na kusababisha gari zote kuingia na kutokea mlango mmoja,imekuwa ni taabu hasa asubuhi zinapoondoka gari za mikoani.

Wanafunzi wakipata elimu kwenye ukumbi wa mikutano chini ya bwana Morgan Seben.

Wanafunzi wa Swaya sekondari wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kitengo cha damu Mbeya bwana Morgan Seben walipotembelea kitengo hicho.


ZIARA YA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA SWAYA-MBEYA.


Wanafunzi wa Swaya walipotembelea benki ya damu kwa ajili ya mafunzo juu ya mfumo wa damu.

Eneo la Kabwe Mbeya.

MVUA NDANI YA MBEYA


Baadhi ya mitaa jijini Mbeya imekuwa ni kero kutokana na mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha barabara kujaa maji kutokana na mashimo kama inavyoonekana moja ya barabara eneo la Soweto.

YANGA YAKARIBIA UBINGWA


Timu ya Yanga imeamusha matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu baada ya kuwachapa African Lyon kwa jumla ya bao 3-0 na kufikisha pointi 46 na kubakiwa na mechi moja sawa na mahasimu wao Simba ambayo nayo imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Majimaji.

Wednesday, April 06, 2011

SIMBA ALMANUSRA KWA RUVU JKT


Mabingwa watetezi wa Tanzania bara Simba leo wamenusurika kichapo kutoka kwa maafande wa JKT RUVU baada ya kusawazisha bao kwa njia ya penati iliyofungwa na Emanuel Okwi,ilikuwa ni JKT RUVU iliyokuwa ya kwanza kujipatia bao la kuongoza kipindi cha kwanza lililowekwa kimiani na Hussein Bunu na kudumu hadi mapumziko,Simba ambao leo walionekana kubanwa vilivyo na wapinzani wao,mwamuzi wa mchezo huo alishindwa kuumudu mchezo huo na kuwatoa nje wachezaji wa JKT akiwemo Shabaan Dihile na George Minja,ligi hiyo itaendelea tena kesho kati ya Yanga dhidi ya African Lyon,Yanga wanahitaji ushindi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kunyakua ubingwa.

VODACOM WABADILISHA RANGI YAO.


Linaloonekana ni jengo la Vodashop Mbeya,likiwa linaendelea kupigwa rangi tofauti na ile iliyozoeleka na wengi ya bluu sijui na jina litakuwaje?umekuwepo mchezo wa kubadili majina na rangi kwa baadhi ya makampuni ya simu kama vile mobitel wakaitwa Buzy na sasa tigo na Celtel wakaitwa Zain na sasa Airtel.

Friday, March 11, 2011

EARTH QUACKE JAPAN

Japan yatikiswa na tetemeko na kimbunga na kuharibu mali kadhaa ikiwemo majengo na miundo mbinu mbali mbali.

YUKO WAPI HUYU ?

KUNA UWEZEKANO UNAMFAHAMU MTU HUYU,MI SIMFAHAMU KABISA.

DAVIES MWAPE

Davies Mwape ni moja kati ya wachezaji hatari katika ligi kuu ya msimu huu,ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufumania nyavu za adui na mbinu kuwatoka walinzi wa timu pinzani,viongozi wa Yanga mtunzeni mchezaji huyu msije mkamfanyia AMBANI

Thursday, March 10, 2011

LOLIONDO STOP

Mch.Ambilikile Mwasapile akiwawekea dawa baadhi ya watu waliofika kwa ajili ya kupatiwa huduma hiyo,lakini hata hivyo serikali imesimamisha huduma hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi na usalama wa dawa hiyo

SIMBA YAZIKALIA AZAM NA YANGA

Timu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara jana walifanikiwa kuongoza ligi kwa kuifunga Ruvu shooting ya Pwani kwa bao 1-0 dakika ya 87 likifungwa na mchezaji Ally Ahmed 'Shiboli' aliyeingia dakika ya 79 kuchukua nafasi ya Mbwana Samata aliyebanwa vilivyo na mabeki wa Ruvu,sasa Simba imefikisha pointi 41 baada kucheza michezo 18,ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 39 huku Azam ikiwa na pointi 37 

Tuesday, March 08, 2011

Mchungaji AMBILIKILE MWASAPILE (kulia) akihojiwa na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake,mchungaji huyo amekuwa akitoa dawa kikombe kimoja kwa kila mgonjwa

WATU WAFURIKA KWA MCHUNGAJI

Umati wa watu unaendelea kufurika kwa mchungaji mstaafu mzee Ambilikile Mwasapile wilayani Ngorongoro,watu wamekuwa wakitoka sehemu mbambali kwa ajili ya kufuata tiba ya magonjwa mbalimbali ambayo yamekuwa hayatibiki hospitalini

Monday, March 07, 2011

LIVERPOOL YAWACHINJA MANCHESTER UTD.

LIVERPOOL jana imeweza kuwashikisha adabu Manchester United baada ya kuwafunga mabao 3-1,magoli ya liverpool yaliwekwa kimiani na Dirk Kuyt.

SIMBA NA YANGA NGUVU SAWA

Timu  zenye upinzani wa jadi kwenye soka la bongo Simba na Yanga jana zilitoka sare ya kufungana bao 1-1

Friday, March 04, 2011

CRDB WAFUNGUA TAWI JIPYA MWANJELWA- MBEYA

Waziri wa maji,Profesa Mark Mwandosya (watatu kushoto) akikata utepe kufungua tawi jipya la benki ya CRDB eneo la Mwanjelwa jijini MBEYA,kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo bw.Martin Mmari,kulia ni mama Mwandosya,kufunguliwa kwa tawi hilo kutawasaidia wakazi wa jiji la Mbeya ambao walikuwa wakipanga foleni kwenye tawi pekee lililokuwa mjini Mbeya.

Wednesday, March 02, 2011

SOKO LA BIG BROTHER UBUNGO LAVUNJWA

Soko la big brother eneo la ubungo limevunjwa jana usiku ili ujenzi wa stend wa mabasi yaendayo kasi,hapa ni baadhi ya wafanyabiashara wakiangalia mabaki ya vibanda vyao.

GADAFFI ANG'ANG'ANIA MADARAKANI

  • Kiongozi wa Libya Muamar Gadaffi ameendelea kung'ang'ania madaraka,licha ya kuwepo kwa maandamano ya kumtaka kuachia madaraka hayo ya urais ambayo ameshikilia kwa zaidi ya miaka arobaini,amekuwa ahamini kinachotokea kwenye taifa lake kutokana na jinsi utawala wake kutowapa uhuru waandishi wa habari na redio.


WAZIRI MKUU AKIWA NA MABALOZI WA UFARANSA NA UINGEREZA

Waziri mkuu Mh.Mizengo Pinda ( kushoto) akiwa na balozi wa Ufaransa bwana Jacques Champagne De Labriolle na balozi wa Uingereza bibi Dianne Corner wakati wa mkutano wa wataalam wa uchumi leo jijini Dar es salaam.

Tuesday, March 01, 2011

Saturday, February 26, 2011


Wakazi wa Gongo la mboto wakishangaa bomu lililokita chini siku chache baada ya milipuko eneo hilo.