BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Wednesday, May 25, 2011

MBEYA YAINGIA FAINALI KOMBE LA TAIFA


Timu ya mkoa wa Mbeya(Mapinduzi stars) imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya kombe la taifa,baada ya kuifunga timu ya mkoa wa Kagera kwa jumla ya mabao 2-1,mchezo huo umechezwa kwa dakika 120,hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1,Mbeya ndio waliofanikiwa kupata ushindi baada ya beki wa Kagera kujifunga baada ya shambulizi kutokea golini kwao,mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kucheza soka maridadi na golikipa wa Mbeya Ivo Mapunda kuonyesha uwezo mkubwa,Mbeya watakutana na Mwanza Heroes siku ya jumamosi uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha katika fainali.

No comments:

Post a Comment