BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Thursday, September 08, 2011

TWIGA STARS YAWAONYESHA KIWANGO BANYANA BANYANA LEO

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu (TWIGA STARS) leo imeweza kutoka sare ya magoli 2-2 na wanawake wenzao wa Afrika kusini katika mchezo mkali na kuvutia uliochezwa mchana huu jijini Maputo,mchezo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na kufanya hadi zinakwenda zikiwa nguvu sawa.  Kipindi kilianza kwa Afrika ya kusini kujipatia goli lililofungwa na Samatha Skity dakika ya 48 kwa krosi iliyojaa moja kwa moja kimiani,kufuatia bao hilo Tanzania waliongeza mashambulizi na kusawazisha dakika ya 54 kupitia kwa Sharua Omar aliyewazidi ujanja mabeki wa Banyana Banyana.
  Twiga Stars walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ester Chabruma baada ya kupata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Zena Rashid na dakika ya 72 ilimwingiza Fridian ambaye alikosa goli baada kupiga kichwa kilichotoka sentimita chache.
 Banyana Banyana walipata bao la pili kupitia kwa Chantelle Essau dakika ya 74 baada ya makosa yaliyofanywa na walinzi wa Twiga Stars na dakika moja baadaye Twiga walisawazisha kupitia kwa Zena Rashid kwa njia ya kichwa kutokana na krosi safi toka upande wa kushoto na hivyo kufanya matokeo kuwa 2-2 hadi mwisho wa mchezo

No comments:

Post a Comment