Timu ya Coastal Union ya Jijini Tanga imelazimisha sare ya goli 2-2 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam,ikiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Simba ilikianza kipindi cha kwanza kwa kasi na kujipatia magoli mawili yaliyofungwa na Shaaban Kisiga na Amisi Tambwe,mabao yalidumu hadi mapumziko.
Coastal walirudi kipindi cha pili wakiwa na machungu na kufanikiwa kusawazisha magoli yote na hivyo kuwanyima Simba ushindi ambao tayari walikuwa na uhakika nao hadi kipenga cha mwisho timu hizo zimetoka 2-2.
Monday, September 22, 2014
COASTAL UNION YAIGOMEA SIMBA
Saturday, September 20, 2014
YANGA YAANZA LIGI YA VPL KWA KUCHAPWA 2-0 NA MTIBWA
Timu ya Yanga ya Dar es salaam leo imeanza ligi kuu ya Tanzania bara kwa kufungwa goli 2-0 na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wenyeji wa mchezo huo wakicheza kwa kujiamini na kufanya mashambulizi ya kushitukiza waliduwaza Yanga dakika ya 15 ya mchezo baada ya Mussa Hassan Mgosi kupachika bao la kwanza kwa kuwazidi ujanja walinzi wa Yanga.
Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na kulisakama lango la wapinzani wao na kupata goli ambalo mwamuzi wa mchezo huo alikataa na kutoa penati kwa Yanga ambayo iliota mbawa,penati hiyo ilipigwa na Mbrazil Jaja na kumgonga miguuni golikipa Said Mohamed muda mfupi baadaye Yanga waliweza tena kupata goli lakini mwamuzi aligoma kwa madai mfungaji alikuwa ameotea.
Timu hizo zilienda mapumziko huku Mtibwa ikiwa mbele kwa goli 1-0,kipindi cha pili Yanga waliingia na kutawala mchezo huo lakini bahati haikuwa yao kwani dakika ya 83 Ame Ally aliifungia Mtibwa goli la pili hadi mwisho wa mchezo Mtibwa 2 Yanga 0
Michezo mingine iliyochezwa leo na matokeo yake:-
.Azam 3-Polisi Moro 0
.Ndanda FC 4-Stand Utd 1
.Mgambo JKT 1-Kagera 0
.Ruvu shooting 0-Prisons 2
.Mbeya City 0-JKT Ruvu 0
Ligi hiyo itaendendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Simba na Coast Union uwanja wa Taifa Dar es salaam.
UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWA KUKATA MITI WAZIDI KUPAMBA MOTO RUKWA
Wananchi hao wamekuwa wakifanya uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na kulima mazao ya muda mfupi ambayo faida yake ni ndogo ukilinganisha na misitu hiyo,wanachohitaji ni kupewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira hususani ukataji miti ovyo,inabidi juhudi za haraka zichukuliwe ili kuinusuru hali hiyo ambayo inaweza kuli fanya eneo hilo kukosa mvua kwa miaka ya baadaye.
Hizi ni baadhi ya picha ya msitu huo unaoshambuliwa kwa kasi.
Hii ni miti ambayo imeangushwa |
Msitu ukiwa umekatwa na wananchi kwa ajili ya kilimo cha ulezi. |
Saturday, September 06, 2014
WATU ZAIDI YA 30 WAFARIKI KWENYE AJALI MUSOMA LEO
Sababu kubwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo ambayo yalikutana kwenye daraja ambalo ni jembamba na kusababisha maafa kwa abiria na wengine kujeruhiwa.
Haraka za madereva wa mabasi zimekuwa ni vyanzo vya ajali nyingi ambazo zingeweza kuepukika lakini imekuwa ni kawaida kwa madereva kujifanya kama hawajui nini kinaweza kutokea kutokana na mwendokasi wao na hii imekuwa ikichangiwa hata na baadhi ya abiria wanaojifanya wana haraka za kuwahi biashara zao na kuwakejeli madereva wanaokwenda mwendo wa taratibu.
Hii ni sehemu ya mabaki ya basi baada ya ajali |
Baadhi ya wananchi wakiangalia kwa hudhuni moja ya basi lililopata |
Saturday, August 30, 2014
YANGA YATANGAZA KAMATI YA NIDHAMU,MAADILI NA SHERIA.
Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA –(Utawala Bora) anapenda kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wana YANGA,ameunda Kamati ndogo chini ya Kamati ya Utendaji wa YANGA zifuatazo:
1) KAMATI YA MAADILI Wajumbe: 1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate) 2) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate) 3) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate) 4) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate) 5) Tenga, Cathbert (Advocate)
2) KAMATI YA NIDHAMU Wajumbe:
1) Karua, Tedy 2) Lamlembe, Roger 3) Kihanga, Pascal 4) Mahenge, Burton Yesaya 5) Mudhihir, Mudhihir (Advocate) 3)
KAMATI YA SHERIA NA KATIBA Wajumbe:
1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate) 2) Gikas, Farija (Advocate) 3) Kabisa, Jessica (Advocate) 4) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate) 5) Kambamwene, January (Advocate) 6) Lupogo, Herman (Advocate) 7) Madibi, Richard (Advocate) 8) Mahenge, Burton Yesaya 9) Mgongolwa, Alex (Advocate) 10) Mkucha, Elisha (Advocate) 11) Mudhihir, Mudhihir (Advocate) 12) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate) 13) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate) 14) Tenga, Cathbert (Advocate) 15) Tenga, Ringo Dr. (Advocate) 16) Vedasto, Audax (Advocate 4)
KAMATI YA UCHAGUZI Wajumbe:
1) Kajole, Mustafa 2) Lundenga, Hashim Ibrahim 3) Makele, Bakili 4) Mlelwa, Daniel 5) Ngongolwa, Alex (Advocate) Ifahamike kwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamati za YANGA zilizotajwa hapo juu. Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA – (Utawala Bora) atakuwa Mwenyekiti wa Kamati zilizotajwa hapo juu. Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa katika Kamati zilizotajwa hapo juu kwa dhamira njema kuwa watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka kwa wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze kutenda kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA. (YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO) (BENO NJOVU) KATIBU MKUU WA YANGA
Friday, August 29, 2014
AJALI KUBWA YATOKEA MBALIZI MBEYA
Ajali hiyo imehusisha gari ya abiria(daladala) na lori dogo aina ya TATA, na kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa Mbalizi na maeneo ya jirani.
Wananchi wa Mbalizi wakiwa wamepigwa butwaa baada ya ajali iliyosababisha vifo vya watu. |
Sunday, August 24, 2014
EL-MERREIKH MABINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI 2014
Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ilichezwa mapema na Police Rwanda wamepata nafasi hiyo kwa kuitoa KCCA ya Uganda kwa penati 4-2.
Wachezaji wa El-merreikh wakishangilia ushindi dhidi ya APR. |
Tuesday, August 19, 2014
BIOGESI KWA MAISHA BORA
FAIDA ZA BIOGESI:- .Haina moshi wala harufu mbaya
. Hupunguza madhara yanayosababishwa na moshi wa kuni au mkaa kama vile macho kuwa mekundu na kukohoa.
.Huokoa muda Hupunguza muda wa kutafuta kuni hivyo kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
Mtandao huu umekutana na mtaalamu wa kutengeneza mtambo wa biogesi maeneo ya Mbinga Kigonsela bw.Linus Komba na kuelezea jinsi mtambo huu ulivyo rafiki wa mazingira,na kuwataka wananchi wa Tanzania hususani wale wanaoishi vijijini kuwasiliana naye ili aweze kuwasaidia na kuwafanya waendelee kuyatunza mazingira kwa kutokata miti,mnaweza kuwasiliana naye kwa simu yake ya mkononi +255 762 045 808,unaweza kuwasiliana naye na yuko tayari kuwafikia sehemu yeyote kwa ajili ya ushauri na matengenezo YATUNZE MAZINGIRA ILI UWAACHIE VIZAZI VIJAVYO SEHEMU NZURI YA KUISHI
Huu ndio mtambo wa biogesi ukiendelea kujengwa |
Bw.Benjamin James akipata maelekezo kutoka kwa mafundi |
Bw.Linus Komba akitoa maelezo kuhusu mtambo wa biogesi |
Mafundi wakiendelea na kazi ya kukamilisha mtambo huo. |
Sunday, August 17, 2014
MANCHESTER UNITED YAANZA VIBAYA EPL,YAPIGWA NYUMBANI
Ligi kuu ya Uingereza imefunguliwa huku matokeo yakiiduwaza Manchester United baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 wakiwa nyumbani,matokeo ambayo hawajawahi kuyapata kwenye mechi za ufunguzi toka mwaka 1972.
Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
Man United 1-Swansea City 2 West Brom 2-Sunderland 2 Stoke City 0 -Aston Villa 1 Leicester City 2 Final Everton 2 QPR 0-Hull City 1 West Ham 0 -Tottenham 1 Arsenal 2-Crystal Palace 1 Sunday, August 17 Liverpool 3:30 PM Southampton Newcastle 6:00 PM Man City Monday, August 18 Burnley FC 10:00 PM Chelsea Saturday, August 23 Aston Villa 2:45 PM Newcastle Chelsea 5:00 PM Leicester City Swansea City 5:00 PM Burnley FC Crystal Palace 5:00 PM West Ham Southampton 5:00 PM West Brom Everton 7:30 PM Arsenal Sunday, August 24 Hull City 3:30 PM Stoke City Tottenham 3:30 PM QPR Sunderland 6:00 PM Man United Monday, August 25 Man City 10:00 PM Liverpool All times are in East Africa Time
Wednesday, August 13, 2014
REAL MADRID YATWAA EUROPEAN SUPER CUP
Ronaldo akishangilia moja ya gola lake |
Mabingwa wa kihistoria wa UEFA CHAMPION LEAGUE,Real Madrid wamefanikiwa kuongeza kikombe kingine kwenye maktaba yao baada ya kuifunga Sevilla ya Spain bao 2-0 kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Cardiff,mabao ya Real Madrid yakifungwa na mchezaji hatari Christiano Ronaldo dakika ya 30 na 49.
Sevilla walikuwa kama timu iliyokata tamaa kabla ya kuingia uwanjani kutokana na Real Madrid kuwa na washambuliaji wenye gharama kubwa na uwezo mkubwa uwanjani kama Gareth Bale,James,Kloose
Ronaldo na wenzake wakifurahia ushindi |
Sunday, August 10, 2014
MAONESHO YA KILIMO KUFANYIKA MJINI NI KUMNYIMA MKULIMA ELIMU NA MAARIFA YA KILIMO.
Pia kufanyika maonesho ya kilimo maeneo ya mjini kila mara ni kumnyima mkulima maarifa zaidi ya kilimo.
Ikiwa maonesho haya yakiwa yanafanyika vijijini yanaweza kuwafanya wakulima kubadilishana ujuzi na kujifunza mambo mengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu,kuliko kufanyika kila wakati mjini na kuyafanya kuwa ya kibiashara zaidi na kutembelewa na watu wasiokuwa walengwa na kuwaacha wakulima wakibaki vijijini kwa kunywa pombe na kucheza ngoma na kuona hiyo ndio furaha ya sikukuu ya wakulima.
Shamba la miti lililoko Vwawa Mbozi |
Ndizi zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa huko Ushirika Tukuyu |
Moja ya shamba la mpunga wilayani Kyela |
Kakao wilayani Kyela |
Shamba la mahindi Ruanda Mbozi. |
Shamba la miparachichi Itipingi Njombe. |
KAGAME CUP 2014
Friday, August 08, 2014
YANGA KUTOSHIRIKI KAGAME CUP KUTAPOTEZA WAPENZI WAPYA WA NDANI NA NJE YA TANZANIA
Kitendo cha timu hii kuwa matatizo ya maramara na shirikisho la soka la Afrika mashariki na kati(CECAFA) na kuifanya timu hii kuondolewa kushiriki michuano ya kombe la Kagame,kuna uwezekano mkubwa wa timu kupoteza wapenzi wapya kwa sababu hamna mtu anayependa kujiingiza kwenye kitu ambacho kina matatizo kila mara,na athari zake haziwezi kuonekana leo hii inaweza ikaonekana miaka ishirini ijayo au zaidi,kwa sababu wapenzi wapya ni wale ambao wana umri wa miaka mitano hadi kumi.
Wakisherekea ubingwa |
Kikosi cha Yanga |
Tuesday, January 14, 2014
KCC FC MABINGWA MAPINDUZI CUP 2014
Timu ya KCC ya Uganda leo imechukua ubingwa wa kombe la mapinduzi Zanzibar baada ya kuifunga timu ya Simba ya Dar es salaam kwa goli 1-0,kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan,mjini Zanzibar,goli pekee la KCC limefungwa na Herman Waswa dakika ya 20. Kwa matokeo hayo timu ya KCC inakuwa timu ya kwanza kutoka nje ya nchi kuchukua ubingwa huo,mashindano yalikosa msisimko baada ya timu ya Yanga kujitoa dakika za mwisho na hivyo kuwakatisha tamaa wapenzi wa soka wa Zanzibar.
KCC waliingia fainali baada ya kuwachapa Azam 3-2 na Simba waliingia fainali kwa kuwachapa URA ya Uganda 2-0.