BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Monday, September 29, 2014

YANGA SASA YAANZA LIGI

  Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa na Mtibwa Sugar wiki iliyopita,Yanga wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Tanzania Prison ya Mbeya kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
  Mchezo ulianza kwa Yanga kumiliki kipindi cha kwanza idara zote na kufanikiwa kupata goli dakika ya 34 likifungwa na Mbrazil Andre Coutinho goli hilo lilidumu hadi mapumziko.
  Kipindi cha pili Prison walirudi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 62,kabla ya Simon Msuva kuipatia Yanga goli la pili dakika ya 67 kwa kichwa kufuatia pasi ya Mrisho Ngassa hadi mwisho wa mchezo Yanga 2-Prison 1.
  Katika mchezo mwingine huko Chamazi Complex timu ya Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya JKT Ruvu.

Kikosi cha Yanga
Shabiki maarufu wa Yanga na Taifa stars anayejulikana kwa jina la Ally Yanga akiwa na wenzake uwanja wa Taifa

Saturday, September 27, 2014

DAMPO JIRANI NA SHULE NI UKATILI KWA WATOTO

Eneo lililofanywa dampo
  Shule ya msingi Simike jijini Mbeya ipo katika wakati mgumu kutokana na kuwa jirani na sehemu ya kutupia takataka ambazo zinaweza kuhatarisha afya za wanafunzi hao hasa yanapotokea magonjwa ya mlipuko.
  Kumekuwa na kiasi kikubwa cha takataka ambazo zimekuwa zikitupwa bila kuondolewa kwa wakati na hivyo kufanya eneo hilo kuwa mrundikano mkubwa wa taka jirani na shule hiyo na kuwa na harufu mbaya na hewa nzito.
  Mamlaka husika zinapaswa kuangalia maeneo ya kutupia taka au kuzitoa mapema hasa maeneo ambayo yako jirani na watoto au shule ili kuwanusuru watoto na maradhi wanayoweza kuyapata,
tunaamini kwa hili linawezekana kama wahusika wakijipanga vizuri.
Lundo la taka
Huu ndio ukuta wa shule ambao uko jirani na sehemu hii ya kutupia taka.

POLISI MORO YAWABANIA SIMBA

  Timu ya Polisi ya Morogoro leo imeilazimisha timu ya Simba ya Dar es salaam sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa pili wa ligi kuu ya Vodacom, mchezo huo umechezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam ambapo Simba walikuwa wenyeji.
  Mchezo huo ulianza kwa simba kutawala kipindi cha kwanza na kuwawezesha kupata goli lililofungwa na Emmanuel Okwi na kuenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli moja,kipindi cha pili Polisi Morogoro waliingia uwanjani wakiwa wamebadilika na kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kusawazisha goli kupitia kwa Dan Mruanda aliyepokea pasi ya Salum Machaku na kumchambua golikipa wa Simba Hussein Sharrif na kuukwamisha mpira wavuni kiufundi.
Polisi walionyesha kandanda safi baada ya kuingia kwa Christopher Edward na Seleman Selembe na kukosa magoli mawili ya wazi ambayo yangeweza kupeleka majonzi mtaa wa Msimbazi.
Matokeo mengine ya ligi kuu ya Vodacom kwa leo:-
 .Azam FC 2-Ruvu Shooting 0
 .Mtibwa 3-Ndanda FC 1
 .Mgambo JKT 0-Stand UTD 1
 .Mbeya City 1-Coastal 0
  Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi mbili ambapo uwanja wa Taifa Dar es salaam Yanga watawakaribisha Tanzania Prisons ya Mbeya na JKT Ruvu watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar kwenye uwanja wa Chamazi Complex.
Mpaka sasa Didier Kavumbagu wa Azam anaongoza kwa kupachika magoli akiwa na magoli manne kwa mechi mbili .

Hiki ni kikosi cha polisi Morogoro kabla ya ligi kuu

Monday, September 22, 2014

STAND UNITED WAMILIKI WAKE NI WAPIGA DEBE NA MAKONDA KIHALALI,TUNAJIFUNZA NINI?SISI WENYE MAKAMPUNI.


Hiki ndio kikosi cha Stand United
 UKITUA katika Mkoa wa Shinyanga, hususan maeneo ya stendi ya zamani ya mabasi ya mikoani na wilayani, utakutana na shamrashamra za makonda, madereva na wapiga debe ambao wanaendelea na shughuli zao za kujipatia riziki. Lakini hao makonda, wapiga debe, mawakala na madereva, ndiyo chachu na mafanikio ya Stand United, kwani wao ndiyo waanzilishi na wamechangia kwa kiasi kikubwa kuifanya timu hiyo ifike hapo ilipo tangu ilipoanzishwa mwaka 2012.  Stand inaongozwa na viongozi wenye uchungu na mpira na uchu wa mafanikio katika soka, ndiyo maana wamefanikiwa kwa kiasi fulani. Wanaendesha timu huku wakiendelea na majukumu yao ya kila siku na kazi zao, ingawa wanahakikisha kila kitu kinakuwa kinaenda sawa kabisa bila tatizo katika mabasi wengine maduka yanayozunguka eneo hilo la stendi. Unapofika Stand, unakutana na makamu mwenyekiti wa timu hiyo, Masumbuko Charles ambaye ni mmoja wa mawakala wa basi la Loquman ambalo linafanya kazi ya kusafirisha abiria kutoka wilaya za Meatu na Bariadi hadi mkoani Dodoma. Licha ya Masumbuko kuwa na majukumu mengi, timu inapofanya mazoezi huwezi kumkosa. “Uwepo wangu katika timu hii ni furaha kwa sababu ilikuwa ndoto yetu hapa tangu muda na imefanikiwa kutimia kwa kiasi mpaka hapa tulipofika, tutapigana kwa sababu mwanzo tulikuwa tunasumbuliwa na ukata lakini tumetimiza ndoto kwa kiasi,” anaeleza Masumbuko. Rashid Daghesh ambaye ni kocha wa kwanza wa Stand kwa sasa ni mjumbe wa kamati kuu ya timu hiyo huku aliyekuwa msaidizi wake Aman Vincent akiwa ndiye mwenyekiti wa timu kwa sasa. Rashid, pamoja na majukumu ya timu aliyonayo, pia ni wakala wa mabasi ya Ruska ambayo yanafanya shughuli zake mkoani humohumo. “Kitu ambacho naweza kujivunia Stand United ni pamoja na kuifanya timu kuwa hapa ilipofika sasa, kwa sababu zamani wakati nacheza timu yangu haikuwa na bahati ya kufika ligi kuu, sasa imepiga hatua, ni jambo la kheri,” anasema Rashid.  Mohamed Ally Hemed ‘Dulla’ yeye ni mmoja wa wadau walioanza kuisapoti timu tangu inaanza, akiwa ni mfanyakazi wa hapo na anamiliki basi la Bedui Ruska ambalo ameamua kuweka jina kubwa la timu katika basi hilo. “Naipenda sana timu hii popote iendapo huwa naisapoti kwa kiasi kikubwa tangu tumeanza kuichangia Sh 500 kipindi hicho,” anaeleza. Araf Nassor akiwa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Stand United naye ni wakala wa mabasi ya Ruska lakini akiwa pia ni mmoja wa waasisi wa timu. “Timu imepiga hatua kwa kiasi kikubwa lakini napenda kuwaambia Watanzania kuwa, Stand United si timu ya wahuni, wala wafanya fujo, sisi ni watu wa malengo, ndiyo maana tumefika hapa, japo ukata kwa sana lakini tunapigana kuendesha timu,” anasema Nassor. Je, mashabiki wanaisapoti vipi timu? “Timu ilipokuwa ikienda mikoani, kipindi hicho walikuwa wanagharamiwa na timu kwa kupitisha mabakuli na kuchangisha na hawa mashabiki wetu wapo katika makundi mawili, Full Shangwe ambao muda wote wanaishangilia timu pamoja na Babu Kubwa, wote hawa ni mashabiki wa timu yetu. “Pia kwa sasa baada ya kupanda, mtashuhudia Bendi ya Stand ikitoa burudani katika michezo yake tofauti wakati ligi kuu itakapokuwa ikiendelea,” anafafanua Nassor. Hao ni baadhi ya wadau na viongozi wa Stand United ambao wamekuwa na timu tangu inaanza mpaka hapo ilipofikia, ingawa haikuwa kazi rahisi kufika hapo walipofika.

COASTAL UNION YAIGOMEA SIMBA

Timu ya Coastal Union ya Jijini Tanga imelazimisha sare ya goli 2-2 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam,ikiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania bara.
  Simba ilikianza kipindi cha kwanza kwa kasi na kujipatia magoli mawili yaliyofungwa na Shaaban Kisiga na Amisi Tambwe,mabao yalidumu hadi mapumziko.
Coastal walirudi kipindi cha pili wakiwa na machungu na kufanikiwa kusawazisha magoli yote na hivyo kuwanyima Simba ushindi ambao tayari walikuwa na uhakika nao hadi kipenga cha mwisho timu hizo zimetoka 2-2.

Saturday, September 20, 2014

YANGA YAANZA LIGI YA VPL KWA KUCHAPWA 2-0 NA MTIBWA

Timu ya Yanga ya Dar es salaam leo imeanza ligi kuu ya Tanzania bara kwa kufungwa goli 2-0 na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wenyeji wa mchezo huo wakicheza kwa kujiamini na kufanya mashambulizi ya kushitukiza waliduwaza Yanga dakika ya 15 ya mchezo baada ya Mussa Hassan Mgosi kupachika bao la kwanza kwa kuwazidi ujanja walinzi wa Yanga.
Baada ya bao hilo Yanga walikuja juu na kulisakama lango la wapinzani wao na kupata goli ambalo mwamuzi wa mchezo huo alikataa na kutoa penati kwa Yanga ambayo iliota mbawa,penati hiyo ilipigwa na Mbrazil Jaja na kumgonga miguuni golikipa Said Mohamed muda mfupi baadaye Yanga waliweza tena kupata goli lakini mwamuzi aligoma kwa madai mfungaji alikuwa ameotea.
Timu hizo zilienda mapumziko huku Mtibwa ikiwa mbele kwa goli 1-0,kipindi cha pili Yanga waliingia na kutawala mchezo huo lakini bahati haikuwa yao kwani dakika ya 83 Ame Ally aliifungia Mtibwa goli la pili hadi mwisho wa mchezo Mtibwa 2 Yanga 0
Michezo mingine iliyochezwa leo na matokeo yake:-
.Azam 3-Polisi Moro 0
.Ndanda FC 4-Stand Utd 1
.Mgambo JKT 1-Kagera 0
.Ruvu shooting 0-Prisons 2
.Mbeya City 0-JKT Ruvu 0
Ligi hiyo itaendendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Simba na Coast Union uwanja wa Taifa Dar es salaam.

UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWA KUKATA MITI WAZIDI KUPAMBA MOTO RUKWA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji cha Mtakuja njia iendayo Kapele Kasusu wilayani Sumbawanga wamekuwa wakikata misitu ili kupata maeneo ya kulima ulezi.
Wananchi hao wamekuwa wakifanya uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na kulima mazao ya muda mfupi ambayo faida yake ni ndogo ukilinganisha na misitu hiyo,wanachohitaji ni kupewa elimu juu ya utunzaji wa mazingira hususani ukataji miti ovyo,inabidi juhudi za haraka zichukuliwe ili kuinusuru hali hiyo ambayo inaweza kuli
fanya eneo hilo kukosa mvua kwa miaka ya baadaye.
Hizi ni baadhi ya picha ya msitu huo unaoshambuliwa kwa kasi.

Hii ni miti ambayo imeangushwa
Msitu ukiwa umekatwa na wananchi kwa ajili ya kilimo cha ulezi.

Saturday, September 06, 2014

WATU ZAIDI YA 30 WAFARIKI KWENYE AJALI MUSOMA LEO

 Zaidi ya watu 30 wamefariki kwenye ajali iliyohusisha magari matatu eneo la Sabasaba mjini Musoma leo,ajali hiyo imetokea leo mchana kwa kuhusisha mabasi mawili ya Mwanza Coach na J4 Express na gari ndogo aina ya Nissan Terrano baada ya J4 Express kuigonga ubavuni Nissan hiyo kuisukumia mtoni kabla ya kukutana uso kwa uso na Mwanza Coach nje kidogo ya daraja.
 Sababu kubwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo ambayo yalikutana kwenye daraja ambalo ni jembamba na kusababisha maafa kwa abiria na wengine kujeruhiwa.
  Haraka za madereva wa mabasi zimekuwa ni vyanzo vya ajali nyingi ambazo zingeweza kuepukika lakini imekuwa ni kawaida kwa madereva kujifanya kama hawajui nini kinaweza kutokea kutokana na mwendokasi wao na hii imekuwa ikichangiwa hata na baadhi ya abiria wanaojifanya wana haraka za kuwahi biashara zao na kuwakejeli madereva wanaokwenda mwendo wa taratibu.
Hii ni sehemu ya mabaki ya basi baada ya ajali
Baadhi ya wananchi wakiangalia kwa hudhuni moja ya basi lililopata 

Saturday, August 30, 2014

YANGA YATANGAZA KAMATI YA NIDHAMU,MAADILI NA SHERIA.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA –(Utawala Bora) anapenda kutoa taarifa kupitia vyombo vya habari kwa wana YANGA,ameunda Kamati ndogo chini ya Kamati ya Utendaji wa YANGA zifuatazo:
1) KAMATI YA MAADILI Wajumbe:   1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate) 2) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate)  3) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate) 4) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate) 5) Tenga, Cathbert (Advocate)
 2) KAMATI YA NIDHAMU Wajumbe:
  1) Karua, Tedy  2) Lamlembe, Roger 3) Kihanga, Pascal  4) Mahenge, Burton Yesaya 5) Mudhihir, Mudhihir (Advocate) 3)
 KAMATI YA SHERIA NA KATIBA  Wajumbe:
   1) Fimbo, Mgongo Prof. (Advocate) 2) Gikas, Farija (Advocate) 3) Kabisa, Jessica (Advocate) 4) Kabudi, Mpalamaganda Prof. (Advocate)  5) Kambamwene, January (Advocate) 6) Lupogo, Herman (Advocate) 7) Madibi, Richard (Advocate) 8) Mahenge, Burton Yesaya 9) Mgongolwa, Alex (Advocate) 10) Mkucha, Elisha (Advocate) 11) Mudhihir, Mudhihir (Advocate) 12) Njaa, Salehe Ramadhani (Advocate) 13) Rashidi, Tausi Abdallah (Advocate) 14) Tenga, Cathbert (Advocate) 15) Tenga, Ringo Dr. (Advocate) 16) Vedasto, Audax (Advocate 4)
 KAMATI YA UCHAGUZI Wajumbe:
  1)  Kajole, Mustafa  2)  Lundenga, Hashim Ibrahim  3)  Makele, Bakili  4)  Mlelwa, Daniel    5) Ngongolwa, Alex (Advocate) Ifahamike kwamba, kutakuwa na nyongeza ya uteuzi wa Wajumbe wengine wa Kamati za YANGA zilizotajwa hapo juu. Mwanasheria Sam Mapande, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya YANGA – (Utawala Bora) atakuwa Mwenyekiti wa Kamati zilizotajwa hapo juu. Kamati ya Utendaji ya YANGA, ina karibisha Wajumbe waliotajwa katika Kamati zilizotajwa hapo juu kwa dhamira njema kuwa watasaidia kujenga YANGA bora, na wanaomba ushirikiano kutoka kwa wanaYanga wote ili Wajumbe walioteuliwa waweze kutenda kazi zao vyema kwa manufaa ya YANGA. (YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO) (BENO NJOVU) KATIBU MKUU WA YANGA

Friday, August 29, 2014

AJALI KUBWA YATOKEA MBALIZI MBEYA

 Wimbi la ajali limezidi kulikumba jiji la Mbeya baada ya leo kutokea ajali eneo la Mbalizi na kugharimu maisha ya watu wasiopungua kumi na wengine zaidi ya sita wakijeruhiwa.
 Ajali hiyo imehusisha gari ya abiria(daladala) na lori dogo aina ya TATA, na kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa Mbalizi na maeneo ya jirani.
Wananchi wa Mbalizi wakiwa wamepigwa butwaa baada ya ajali iliyosababisha vifo vya watu.

Sunday, August 24, 2014

EL-MERREIKH MABINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI 2014

  Timu ya El-merreikh ya Sudan imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika mashariki na kati kwa kuwafunga APR ya Rwanda kwa bao 1-0,bao pekee la El-merreikh limefungwa na Allan Wanga dakika ya 25 ya mchezo na kuwafanya APR kushindwa kufurukuta mbele ya mashabiki wao na kunyang'anywa tonge mdomoni na wasudan hao.
  Mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ilichezwa mapema na Police Rwanda wamepata nafasi hiyo kwa kuitoa KCCA ya Uganda kwa penati 4-2.

Wachezaji wa El-merreikh wakishangilia ushindi dhidi ya APR.

Tuesday, August 19, 2014

BIOGESI KWA MAISHA BORA

 Biogesi ni nishati itokanayo na kinyesi cha wanyama ambacho huchachuka ndani ya mtambo wa biogesi na kuweza kutumika kwa kupikia na kuwasha taa.
  FAIDA ZA BIOGESI:- .Haina moshi wala harufu mbaya
. Hupunguza madhara yanayosababishwa na moshi wa kuni au mkaa kama vile macho kuwa mekundu na kukohoa.
 .Huokoa muda Hupunguza muda wa kutafuta kuni hivyo kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
 Mtandao huu umekutana na mtaalamu wa kutengeneza mtambo wa biogesi maeneo ya Mbinga Kigonsela bw.Linus Komba na kuelezea jinsi mtambo huu ulivyo rafiki wa mazingira,na kuwataka wananchi wa Tanzania hususani wale wanaoishi vijijini kuwasiliana naye ili aweze kuwasaidia na kuwafanya waendelee kuyatunza mazingira kwa kutokata miti,mnaweza kuwasiliana naye kwa simu yake ya mkononi +255 762 045 808,unaweza kuwasiliana naye na yuko tayari kuwafikia sehemu yeyote kwa ajili ya ushauri na matengenezo YATUNZE MAZINGIRA ILI UWAACHIE VIZAZI VIJAVYO SEHEMU NZURI YA KUISHI
Huu ndio mtambo wa biogesi ukiendelea kujengwa
Bw.Benjamin James akipata maelekezo kutoka kwa mafundi
Bw.Linus Komba akitoa maelezo kuhusu mtambo wa biogesi
Mafundi wakiendelea na kazi ya kukamilisha mtambo huo.

Sunday, August 17, 2014

MANCHESTER UNITED YAANZA VIBAYA EPL,YAPIGWA NYUMBANI

Ligi kuu ya Uingereza imefunguliwa huku matokeo yakiiduwaza Manchester United baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 wakiwa nyumbani,matokeo ambayo hawajawahi kuyapata kwenye mechi za ufunguzi toka mwaka 1972.
Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:-
Man United 1-Swansea City 2 West Brom 2-Sunderland 2 Stoke City 0 -Aston Villa 1 Leicester City 2 Final Everton 2 QPR 0-Hull City 1 West Ham 0 -Tottenham 1 Arsenal 2-Crystal Palace 1 Sunday, August 17 Liverpool 3:30 PM Southampton Newcastle 6:00 PM Man City Monday, August 18 Burnley FC 10:00 PM Chelsea Saturday, August 23 Aston Villa 2:45 PM Newcastle Chelsea 5:00 PM Leicester City Swansea City 5:00 PM Burnley FC Crystal Palace 5:00 PM West Ham Southampton 5:00 PM West Brom Everton 7:30 PM Arsenal Sunday, August 24 Hull City 3:30 PM Stoke City Tottenham 3:30 PM QPR Sunderland 6:00 PM Man United Monday, August 25 Man City 10:00 PM Liverpool All times are in East Africa Time

Wednesday, August 13, 2014

REAL MADRID YATWAA EUROPEAN SUPER CUP

Ronaldo akishangilia moja ya gola lake


Mabingwa wa kihistoria wa UEFA CHAMPION LEAGUE,Real Madrid wamefanikiwa kuongeza kikombe kingine kwenye maktaba yao baada ya kuifunga Sevilla ya Spain bao 2-0 kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Cardiff,mabao ya Real Madrid yakifungwa na mchezaji hatari Christiano Ronaldo dakika ya 30 na 49.
  Sevilla walikuwa kama timu iliyokata tamaa kabla ya kuingia uwanjani kutokana na Real Madrid kuwa na washambuliaji wenye gharama kubwa na uwezo mkubwa uwanjani kama Gareth Bale,James,Kloose

Ronaldo na wenzake wakifurahia ushindi

Sunday, August 10, 2014

MAONESHO YA KILIMO KUFANYIKA MJINI NI KUMNYIMA MKULIMA ELIMU NA MAARIFA YA KILIMO.

 Wakulima wa mazao mbalimbali wamekuwa hawapatiwi elimu juu ya uzalishaji wa mazao yao,na hivyo kulazimika kufanya kilimo cha mazoea na kujikuta wakiendelea kupata mavuno kidogo.
Pia kufanyika maonesho ya kilimo maeneo ya mjini kila mara ni kumnyima mkulima maarifa zaidi ya kilimo.
Ikiwa maonesho haya yakiwa yanafanyika vijijini yanaweza kuwafanya wakulima kubadilishana ujuzi na kujifunza mambo mengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu,kuliko kufanyika kila wakati mjini na kuyafanya kuwa ya kibiashara zaidi na kutembelewa na watu wasiokuwa walengwa na kuwaacha wakulima wakibaki vijijini kwa kunywa pombe na kucheza ngoma na kuona hiyo ndio furaha ya sikukuu ya wakulima.

Shamba la miti lililoko Vwawa Mbozi
Ndizi zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kusafirishwa huko Ushirika Tukuyu

Moja ya shamba la mpunga wilayani Kyela
Kakao wilayani Kyela
Shamba la mahindi Ruanda Mbozi.
Shamba la miparachichi Itipingi Njombe.