BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Friday, August 19, 2011

MNYAMA AITAFUNA YANGA USIKU


Timu ya Simba imefanikiwa kuwafunga mahasimu wao Yanga kwa mabao 2-0 na kuchukua ngao ya hisani,Simba wakicheza kwa ushirikiano mkubwa walifanikiwa kupata bao dakika ya 16 kupitia Haruna Moshi Boban na baadaye walipata bao kwa njia ya penati kupitia kwa Sunzu hadi mapumziko Simba walikuwa wakiongoza kwa mabao hayo mawili,kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi na kuwafanya Yanga washindwe kusawazisha kutokana na kuwazidi wapinzani wao kwenye safu ya kiungo na kuwafanya Yanga kucheza bila malengo.
Timu hizi zimekutana mara sita kwenye mechi za usiku na hivyo Simba ikiibuka na ushindi mara tano na Yanga mara moja na mechi hizo zilichezwa uwanja wa Aman Zanzibar,mechi nne zikiwa ni za ubingwa wa Afrika mashariki na kati,moja kombe la muungano na nyingine ndio hii ya ngao ya hisani ambayo imechezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam kwa matokeo hayo inaonyesha Yanga wamekuwa na udhaifu wa mechi za usiku hata za kirafiki,wiki moja tu iliyopita wamechezea kichapo mjini Khartoum Sudan kwa kufungwa mabao 3-1 na El-hilal,na katika mechi ya pili wakapokea kipigo kama hicho hicho
Mvuto zaidi ni kwa makocha wa timu hizo ambao wanatoka nchi moja kwa upande wa Simba ni Moses Basena na Yanga ni Sam Timbe ambao kila mmoja alitaka kuonyesha nani zaidi ya mwenzake kutokana na timu zote kujivunia usajili wa msimu huu.

No comments:

Post a Comment