BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Wednesday, July 20, 2011

BREAKING NEEEEEWSSSS.


Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa mwandishi wetu aliyeko Morogoro ni kuwa basi lililokuwa likisafiri kati ya Mbeya na Arusha limeshika moto eneo la Mikumi na abiria kushindwa kuendelea na safari,basi hilo ni mali ya Hood transport ya Morogoro
Basi likiendelea kuwaka moto

MRISHO NGASA AKIWA MAZOEZINI MAREKANI


Mshambuliaji maarufu wa Taifa stars na Azam fc,akiwa kwenye mazoezi na wenzake kwa ajili ya kuwakabili mabingwa EPL timu ya Manchester United ya Uingereza,Ngassa aliyeonyesha uwezo mkubwa akiwa na Yanga SC misimu iliyopita na hivyo kuwavutia Azam na kumchukua kwa dau kubwa,kwa sasa anafanya majaribio kwenye klabu ya Seattle Sounders ya Marekani na anaendelea vizuri.

Tuesday, July 19, 2011

TERRY-MODRIC 'DISRESPECTFUL'


John Terry believes Luka Modric has been disrespectful to Spurs for trying to engineer a move to Stamford Bridge.

Monday, July 18, 2011

VODACOM NA MRADI WA UTUNZAJI WA MBWA MWITU SERENGETI

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania bw.Dietlof Mare akimkabidhi sanamu ya mbwa mwitu mkurugenzi wa shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA,Allan Kijazzi kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mradi wautunzaji mbwa mwitu katika hifadhi ya tafa Serengeti(Vodacom foundation's Serengeti wild dogs conservation project)
Mkurugenzi mkuu wa Vodacom Tanzania Dietlof Mare akiteta jambo na waziri wa mawasiliano na uchukuzi mh.Mahige

Sunday, July 17, 2011

MBEYA


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya ndg.Advocate Nyombi akionyesha silaha iliyotumika kwenye uporaji wa fedha NMB-tawi la Kyela mkoani Mbeya.

Tuesday, July 12, 2011

LADY JAY DEE NA YANGA KESHO NYUMBANI LOUNGE.


Mwanamuziki maarufu ukanda huu wa afrika mashariki na kati,Judith Wambura (lady jay dee) amewaandalia chakula mabingwa wa Kombe la Kagame Castle Cup,timu ya Yanga chakula cha mchana kwenye mgahawa wake maarufu wa NYUMBANI LOUNGE kwa ajili ya kuwapongeza kwa kutwaa ubingwa,inasemekana mwanamuziki ni mnazi wa wanajangwani hao

DIEGO MARADONA APATA AJALI YA GARI


Diego Amando Maradona amepata ajali ya gari akiwa na rafiki yake wa muda mrefu Veronica,ajali hiyo ilitokea kilomita chache alipokuwa akitokea nyumbani kwake kwenda uwanjani kutazama mechi za Coper America zinazoendelea nchini Argentina ambako michuano hiyo inafanyika,mara baada ya ajali alipelekwa hospital na hali yake inaendelea vizuri.

AIRTEL YAWA KAMPUNI YA KWANZA KUWAFIKIA WANANCHI WA MGAZINI-RUVUMA


Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imezindua mnara wake eneo la Mgazini mkoani Ruvuma,na hivyo kuwaondolea adha ya mawasiliano wakazi wa eneo hilo na maeneo ya Mhepai na vijiji jirani,kiongozi wa Airtel bwana Cheikh Sarr amesema ndani ya mwezi huu wanatarajia kuzindua minara 50 hapa nchini,nilifanikiwa kuongea na mmoja wa wananchi wa eneo la Mhepai bw.Morris Mapunda alionyesha kufurahia huduma hiyo na kudai walikuwa na simu kama mapambo kutokana na kutokuwepo mtandao wowote na ameishukuru sana Airtel kwa kuwaletea huduma hiyo.

Monday, July 11, 2011

YANGA BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

Hili ndilo kombe la Kagame ambalo Yanga wamelinyakua
Wachezaji wa Yanga wakiwa na furaha mara baada ya kukabidhiwa kombe hilo

Mshambuliaji wa Yanga Khamis Kiiza akijaribu kumtoka mlinzi wa Simba Said Nassor (Cholo) kwenye uwanja wa Taifa Yanga walishinda 1-0
Makocha wa Yanga na Simba wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza Sam Timbe na Moses Basena (kulia) wa Simba

Sunday, July 10, 2011

TWIGA STARS YASHIKA NAFASI YA TATU COSAFA


Timu ya taifa ya wanawake imefanikiwa kushika nafasi ya michuano ya Cosafa kwa nchi za kusini mwa Afrika licha na maandalizi mabovu,wamewalaza wenzao wa Malawi mabao 3-1

Saturday, July 09, 2011

YANGA YACHAFUA HALI YA HEWA MSIMBAZI

Mabingwa wa Tanzania bara Yanga jana walifanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kagame Cup baada kuwatoa St.George ya Ethiopia kwa mikwaju ya penati 5-4 na hivyo kukutana na Simba kwenye fainali kesho kwenye uwanja wa taifa,Simba ambayo ilionekana kucheza kandanda safi toka ilipoanza michuano hii tofauti na watani wao,watalazimika kucheza kivingine zaidi kutokana na timu kukamiana kila zinapokutana na kuharibu ladha ya mchezo

Mashabiki wa Yanga wakishangilia mara baada ya mpira kumalizika wengine hawakuamini kilichotokea baada ya penati ya mwisho ya St.George kugonga mwamba na kurudi chini jirani na mstari wa goli

MHESHIMIWA SUGU ASHIKILIWA NA POLISI MBEYA

Mh.mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbillinyi jana alishikiliwa kwa muda na jeshi la polisi kwa kufanya mkutano eneo la Nzovwe bila kibali cha jeshi hilo,Mbillinyi ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chadema.
Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya bw. Advocate Nyombi akisisitiza juu ya umuhimu wa amani na watu kufuata sheria

Friday, July 08, 2011

MIUNDO MBINU MBEYA KUBORESHWA


Wafanyakazi wa kampuni ya Sogea Sotum wakitengeneza bomba eneo la Iyunga Mbeya,kampuni hiyo ndio inatengeneza mfumo wa maji taka na safi mkoani Mbeya.

SIMBA YAINGIA FAINALI KAGAME CUP

Timu ya Simba jana imefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Kagame baada ya kuiondoa timu ya El-mereikh ya Sudan kwa mikwaju ya penati 5-4,hadi dakika 90 matokeo yalikuwa 1-1 na kuongezwa dakika 30 na matokeo kuwa hivyohivyo na mshindi kupatikana kwa njia ya penati,nusu fainali nyingine itakuwa leo jioni kati ya Yanga na St.George na mshindi wa leo ataungana na Simba kwenye mchezo wa fainali jumapili.

Tuesday, July 05, 2011

DEREVA JOHN GWAU AFANYIWA UNYAMA NA SHEMEJI YAKE SINGIDA MJINI


John Gwau akiwa wodi No.4 kwenye hospital ya mkoa Singida,baada ya kupigwa na chupa ya bia na shemeji yake Celestin Mgoo kwa tuhuma za kufuliwa nguo na dada yake aitwaye Ruth ambaye ametengana na Celestin,dada huyo ni mwalimu wa shule ya msingi Mughanga iliyoko mjini Singida,bwana Celestin aliingia chumbani kwa shemeji na kumpiga na chupa kichwani,baada ya kuzirai kama vile haitoshi alitumia vipande vya chupa kumchanja chanja usoni,mtuhumiwa leo amefikishwa mahakamani.

Monday, July 04, 2011

NOVAK DJOKOVIC ASHINDA WIMBLEDON


DAVID HAYE ALAMBA SAKAFU UJERUMANI

Bondia David Haye wa Uingereza jana alipokea kichapo kutoka kwa Vladimir Klitschko wa Ukraine kwenye pambano la kuwania wa WBC ambao ulikuwa ukishikiliwa na Haye,pambano hilo la raundi 12 liliamuliwa kwa pointi,lakini muda mwingi wa pambano Haye alionekana kuzidiwa na kuanguka mara kadhaa na kuendelea na pambano mpaka mwisho
Vladimir Klitschko akipongezwa na kaka yake Vital klitschko mara baada kupata ushindi dhidi ya David Haye na sasa anashikilia mataji matatu ya WBC,WBA na WBO

Tuesday, June 28, 2011

GODWIN FRANCIS AKIWA KAZINI GANGILONGA


Mmiliki wa mtandao wa godwinfrancis.blogspot.com akiwa juu ya jiwe la Gangilonga,katika ziara yake ya kutembelea vivutio mkoani Iringa ambavyo havijaorodheshwa mkoani Iringa.

BEI YA MAFUTA YAATHIRI WENGI


Picha inayoonekana ni mwili wa marehemu ukifungwa kwenye pikipiki tayari kwa safari ya kuelekea kijiji cha Isansa wilayani Mbozi kutoka wilaya Mbeya,inaonekana ni kitu cha ajabu lakini ndio halisi iliyotokea,inakadiriwa kuwa kufika kijijini kwao ni zaidi kilomita 90 kama wangetumia gari ingewagharimu kuliko uwezo wao,hii inaashiria wananchi wanavyoishi kwa taabu na kubuni njia mbadala za kutatua matatizo yao bila kujali athari zinazoweza kutokea.

DALADALA BALAA


Jioni hii daladala iliyokuwa ikitokea eneo la Soko Matola kuelekea Iyunga,imegonga gari ndogo aina ya Toyota Corolla eneo la Sabato ndani ya gari hiyo alikuwemo mdau wa blog hii,hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kwenye ajali hii.

Gari ndogo ambayo imegongwa na daladala

WAFANYABIASHARA SOKO LA UHINDINI MBEYA WAHAMIA ENEO JIPYA

Hili ni eneo la uwanja wa Sokoine Mbeya ambalo wafanyabiashara wa soko la uhindini wamehamia baada ya soko lao walilozoea kuungua moto mapema mwaka huu.
 Baadhi ya mafundi wakimalizia vyumba eneo la uwanja wa Sokoine Mbeya
 
Wauzaji matunda na mbogamboga kwenye soko hilo

Monday, June 27, 2011

PRESIDENT Dr.J.KIKWETE SIGNS A CONDOLENCE BOOK AT ZAMBIAN HIGH COMMISSION IN DAR ES SALAAM TO MOURN CHILUBA

President Dr.Jakaya M.Kikwete signs a condolence  book at the Zambian high commissioner's residence in  Dar es salaam this morning,following the death of former  Zambian President  Fredrick Chiluba early last week.

Sunday, June 26, 2011

YANGA ULIMI NJE KWA EL-MEREIKH


Leo El-mereikh imewalazimisha mabingwa wa Tanzania bara timu ya Yanga sare ya bao 2-2 kwenye mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa,El-mereikh waliweza kuwatawala Yanga kipindi cha pili kwa kucheza jinsi wanavyotaka na kufanikiwa kusawazisha bao la pili,Yanga kipindi waliingia cha pili safu ya kiungo ilikuwa imezidiwa na kuwapa nafasi El-mereikh kutawala mpira.

KAGAME CUP YAANZA


Michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika mashariki na kati imeanza kwa mechi za ufunguzi,zimepigwa mechi mbili,katika mechi ya kwanza timu ya Ocean view imeilaza timu ya Eticele ya Ruanda 3-2,huku Simba ikitoka 0-0 na vitalo ya Burundi,mechi hizo zitaendelea tena kwenye viwanja vya Jamhuri Morogoro na uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Friday, June 24, 2011

CHUO KIKUU CHA UFUNDI MBEYA (MIST)


Hili ni eneo la ofisi za utawala za chuo kikuu cha ufundi Mbeya,ambacho zamani kilijulikana kama Mbeya Technical College,leo ni chuo kikuu ambacho tunategemea kitatoa waandisi wa kada mbalimbali na kuliepusha taifa kuwa tegemezi kwenye upande wa wataalamu kutoka nje

Haya ni baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha ufundi (MIST) Mbeya.

Thursday, June 23, 2011

MICHELLE OBAMA AKUTANA NA NELSON MANDELA


Mke wa rais Barack Obama,bi.Michelle Obama amekutana na mzee Mandela na kufanya mazungumzo naye,Michelle yuko ziarani Afrika kusini.

Wednesday, June 22, 2011

HIKI NDIO KIKOSI CHA YANGA KILICHOTWAA UBINGWA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI MWAKA 1998



MORAVIAN KUWEKA MAKAO MAKUU DODOMA


Askofu Alenikisa Cheyo amesema kanisa la Moravian liko mbioni kuhamishia makao makuu mjini Dodoma,alikuwa akizungumza kwenye harambee iliyofanyika kanisa la Ruanda Mbeya

BAJAJ YAJERUHI ABIRIA


Mwanamke mmoja amejeruhiwa baada ya pikipiki ya tairi au Bajaj kugonga gari ndogo aina ya Carina eneo la mikocheni jijini Dar es salaam

Tuesday, June 21, 2011

UTUNZAJI WA KUMBU KUMBU NI MUHIMU

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la idara ya habari maelezo wakiangalia photo album za matukio ya uhuru wa Tanganyika,huku tukijiandaa na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru-Mungu ibariki Tanzania.

DAWA FEKI YA KUKUZA MAKALIO HII HAPA

Ofisa uhusiano wa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) Bi.G.Simwanza akionesha dawa feki ya kuongeza ukubwa wa makalio katika banda la TFDA kwenye maadhimisho ya utumishi wa umma ya umoja wa mataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya mnazi mmoja

Monday, June 20, 2011

KANISA LA MORAVIAN KUHAMISHIA MAKAO MAKUU MJINI DODOMA

                                                                  Kanisa la Moravian liko kwenye mipango ya kuhamishia makao makuu ya kanisa hilo mjini Dodoma hayo yameelezwa na Askofu mkuu wa kanisa ndg.Alinikisa Cheyo katika ibada ilyofanyika jana kwenye kanisa la Ruanda Mbeya,alisema tayari wameshapata ekari 225 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya ofisi na vitega uchumi mbalimbali pia alielezea kuwa wako kwenye mipango ya kufungua campus ya chuo kikuu kinachomilikiwa na kanisa hilo kwenye mikoa ya Tabora na Dar es salaam na wanategemea kuanza september mwaka huu.

UJENZI WA KITUO CHA DALADALA CHA MBEZI SASA WAELEKEA KUKAMILIKA

Kituo kipya cha daladala cha Mbezi sasa kipo katika hatua za mwisho mwisho kama picha hii inavyoonyesha

Saturday, June 18, 2011

CYNTHIA KIMASHA AWA MISS VODACOM CHANG'OMBE

Cynthia Kimasha (katikati) amefanikiwa kutwaa taji la vodacom miss Chang'ombe,huku mshindi wa pili akiwa Husna Twallib (kushoto) na mshindi wa tatu ni Joyce Maweda,shindano hilo limefanyika kwenye viwanja vya Tcc Chang'ombe.
Hawa ndio walifanikiwa kuingia tano bora kwenye shindano hilo