BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Sunday, August 19, 2012

SIMBA B YANYAKUA UBINGWA WA ABC SUPER 8 KWA KUWACHAPA MTIBWA 4-3.


Timu ya Simba B leo imetwaa ubingwa wa Super 8 cup baada ya kuwafunga Mtibwa goli 4-3 kwenye uwanja wa Taifa,Dar es salaam.
Timu ya Simba B ambayo inaonyesha kandanda safi iliingia fainali kwa kuwatoa Azam FC kwa goli 2-1 na Mtibwa waliwatoa Jamhuri kwa 5-1,kivutio cha mchezo wa leo alikuwa Christopher Edward ambaye alifunga magoli matatu (hat trick) na kuweza kuchangia ushindi huo wa Simba B.
Nao wapenzi wa soka wamefurahishwa na kikosi cha Simba B na kuomba timu nyingine kuiga mfano huo,wengine wamedai kikosi hicho ni zaidi ya timu yao ya wakubwa na kama wakipambanishwa wanaweza kuwatia aibu kaka zao wa Msimbazi.

Wednesday, August 15, 2012

TAIFA STARS NGUVU SAWA NA BOTSWANA 3-3.


Timu ya Taifa stars leo imetoka sare na timu ya taifa ya Botswana baada ya kufungana bao 3-3 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jijini Gaborone.
Magoli ya Taifa Stars yamefungwa na Erasto Nyoni,Mwinyi Kazimoto na Mrisho Ngassa.

PATRICE MUAMBA AJIUZULU SOKA


Mchezaji wa Bolton ya Uingereza ametangaza kujiuzulu soka kutokana na ushauri wa madaktari waliomfanyia upasuaji mdogo wa moyo nchini Belgium.
Muamba ametangaza uamuzi huo leo hii na kusema kwa sasa anaangalia afya yake na pia amewashukuru madaktari wote waliohangaikia uhai wake kwa muda ambao ulikuwa ni mgumu kwake baada ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu.

SIMBA B YAILAZA AZAM FC NA KUTINGA FAINALI YA SUPER8 ABC.


Timu ya Simba B imeweza kuwaduwaza Azam leo kwa kuwafunga bao 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliofanyika uwanja wa Taifa.
Azam wakiwa na baadhi ya wachezaji wakongwe walishindwa kulimudu gwaride la watoto hao na kuambulia vumbi,magoli ya Simba yamefungwa na Rashid Idrisa na Christopher Edward wakati la Azam likifungwa na Zahor Pazi
Mechi nyingine ya nusu fainali ilipigwa saa nane mchana kati ya Mtibwa Sugar na Jamhuri ya Zanzibar,Mtibwa wamepata ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Jamhuri,kwa maana hiyo Mtibwa watacheza na Simba fainali Jumamosi.

Tuesday, August 14, 2012

MABAKI YA HELKOPTA ZA UGANDA YAPATIKANA MLIMA KENYA


Mabaki ya helkopta mbili za Uganda yamepatikana mlima Kenya,helkopta hizo ziliondoka nchini Uganda jumapili zikiwa zinaelekea nchini Somalia kuongeza nguvu kwenye jeshi la kulinda amani la Afrika.
Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.

MABAKI YA HELKOPTA ZA UGANDA YAPATIKANA MLIMA KENYA


Mabaki ya helkopta mbili za Uganda yamepatikana mlima Kenya,helkopta hizo ziliondoka nchini Uganda jumapili zikiwa zinaelekea nchini Somalia kuongeza nguvu kwenye jeshi la kulinda amani la Afrika.
Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana.

Monday, August 13, 2012

TETEMEKO IRAN LAHARIBU VIJIJI 12.


Nchi ya Iran imekumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 na 6.5 na kusababisha uharibifu wa vijiji 12 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 250 na wengine wakiwa wamefukiwa na vifusi,jitihada za kuwatafuta watu waliofukiwa na vifusi zinaendelea.

Sunday, August 05, 2012

ANDY MURRAY AMSHINDA ROGER FEDERAR NA KUTWAA DHAHABU


Mcheza tenisi wa Uingereza Andy Murray amefanikiwa kutwaa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olmpiki inayoendelea nchini Uingereza baada ya kumchapa mchezaji maarufu duniani Roger Federar kwa seti 6-1,6-0,6-4 kwenye uwanja wa Wimbledon.
Naye Serena Williams amemfunga Maria Sharapova kwa seti 6-0,6-2 na kujinyakulia medali ya Dhahabu,michezo ya leo imewakutanisha magwiji wa Tenisi duniani,furaha zaidi ni Andy Murray ambaye amekuwa na kiu ya kumufunga Federar kwa muda mrefu na hatimaye amefanikiwa

Monday, July 30, 2012

BALOZI WA VENEZUELA AUAWA KENYA


Balozi wa Venezuela nchini Kenya Bi.Olga Fonseca,ameuawa nyumbani kwake jijini Nairobi na watu wasiojulikana,jeshi la polisi linawashikilia watu sita kuhusiana na kifo hicho,Bi.Olga alianza kazi katikati ya mwezi huu nchini humo.

Sunday, July 29, 2012

JOSE CHAMELEONE AKIMBILIA UBALOZINI


Mwanamuziki maarufu Afrika mashariki Jose Chameleone na wapambe wake wakiwa nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Uganda wakiwa na mabango yanayoshinikiza kurejeshewa passport yake inayoshikiliwa na mtunzi maarufu wa vitabu bw.Shigongo kutokana na deni la US$ 3500.

Saturday, July 28, 2012

YANGA BINGWA TENA KOMBE LA KAGAME 2012


Wachezaji wa Yanga wakiwa na kombe la Kagame mara baada ya kukabidhiwa kwa kuwafunga Azam FC ya Dar es salaam kwenye mchezo wa fainali kwa goli 2-0,uwanja wa taifa.
Azam walianza mchezo huo kwa kasi na kuwatia hofu wapenzi wa Yanga,lakini Yanga walitulia na kuweza kupata bao dakika ya 44 kupitia kwa Hamis Kiiza na kuwafanya Azam kupoteana kipindi cha pili,Yanga walipata bao la pili dakika za mwisho kupitia kwa Said Bahanuzi.
Yanga wamechukua kwa mara ya pili mfululizo huku ikiwa na kocha mpya kutoka Belgium,Tom Saintfiet

Thursday, July 26, 2012

YANGA NA AZAM FC KUCHEZA FAINALI KOMBE LA KAGAME


Timu ya Yanga na Azam FC zimefanikiwa kuingia fainali ya kombe la Kagame baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali leo iliyochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Azam wamefanikiwa kuingia fainali baada ya kuwachapa Vita Club ya DRC goli 2-1,kupitia kwa John Bocco na Mrisho Ngasa kwenye mechi iliyochezwa mchana,kwenye mchezo wa pili Yanga ililazimika kucheza kwa dk.120 na hatimaye kupata bao pekee dk.99 kupitia kwa Hamis Kiiza aliyezifumania nyavu za wapinzani wao.
Kwa matokeo hayo timu hizo zitakutana kwenye fainali.

Wednesday, July 25, 2012

AZAM FC YAICHAKAZA SIMBA 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI


Simba imechezea kichapo cha aibu kutoka kwa Azam FC cha mabao 3-1,kwenye mchezo wa robo fainali kombe la Kagame.
Azam FC walipata goli la kwanza dk.17 likifungwa na John Boko ambaye alikuwa mwiba kwenye ngome ya Simba kwa kupachika mabao yote,dk ya 46 aliipatia bao la pili na Simba walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Shomari Kapombe dk.53 kwa juhudi zake binafsi,kama vile haitoshi John Boko alitupia tena kimiani bao la 3 na kuwafanya Simba wachanganyikiwe zaidi.
Mchezo mwingine uliochezwa mchana timu ya Vita Club ya DRC iliichapa Atletco ya Burundi 2-1,sasa Azam itakutana Vita Club huku Yanga wakicheza na APR ya Rwanda nusu fainali tarehe 26.

Tuesday, July 24, 2012

YANGA YAINGIA NUSU FAINALI KAGAME CUP.


Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Kagame Yanga ya Dar es salaam,wamefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuwatoa timu ngumu ya Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-3.
Hadi dakika 90 zikimalizika matokeo yalikuwa 1-1,Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 35 likifungwa na Othman Mmanga kwa njia ya kichwa na Yanga walisawazisha bao dakika ya 47 kupitia kwa Said Bahanuzi.
Katika mchezo mwingine wa nusu fainali APR ya Rwanda iliwachapa URA ya Uganda bao 2-1,michezo mingine ya nusu fainali itachezwa kati ya Azam na Simba,Atletco ya Burundi na Vita SC ya DRC.

Sunday, July 08, 2012

TENKI LA MAJI LAMWAGA MAJI MENGI SIMIKE MBEYA.


Hii inasikitisha sana kuona mamlaka husika ikiwa imekaa kimya kwa muda mrefu,kutokana na upotevu wa maelfu ya lita za maji kupotea bila kutumika huku maji hayo yakitiririka na kuingia mto Mabatini kutoka tenki la maji la mtaa wa Simike,jijini Mbeya na kusababisha baadhi ya wakazi wa eneo kukosa maji kwa muda kutokana na tatizo hilo.
Mamlaka husika inaombwa kushughulikia tatizo hili ambalo limekuwa kero kwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo kutokana na maji hayo yanayovuja kwa wingi kupita milangoni mwao.

WEWA SEPETU NA JAQUILINE WOLPER HAKUNA MBABE.


Lile pambano la ndondi la wasanii wa filamu nchini,lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki,limemalizika matokeo yakiwa sare.
Mpambano uliojulikana kama usiku wa matumaini ulionekana kama mchezo wa kuigiza kutokana na wahusika kutokuwa na fani ya mchezo huo wa ndondi,japo Wolper akionekana kumzidi ujanja mpinzani wake.

WEWA SEPETU NA JAQUILINE WOLPER HAKUNA MBABE.


Lile pambano la ndondi la wasanii wa filamu nchini,lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki,limemalizika matokeo yakiwa sare.
Mpambano uliojulikana kama usiku wa matumaini ulionekana kama mchezo wa kuigiza kutokana na wahusika kutokuwa na fani ya mchezo huo wa ndondi,japo Wolper akionekana kumzidi ujanja mpinzani wake.

Monday, July 02, 2012

HISPANIA BINGWA ULAYA 2012


Timu ya taifa ya Hispania imechukua kwa mara nyingine ubingwa wa Ulaya baada ya kuwafunga Italia bao 4-0 jijini Kiev,Ukraine.
Hispania walipata bao la kwanza kupitia kwa David Silva dakika ya 14,goli la pili dak.41 likifungwa na Jordi Alba,goli la tatu likifungwa na Fernando Torres dk.84 na la nne likifungwa na Juan Matta dk.88,Hispania sasa inakuwa timu ya kwanza kuchukua kombe hilo mfululizo toka michuano hiyo ilipoanzishwa.
Mashabiki hawakutegemea matokeo hayo ya Italia kufungwa goli nyingi kutokana na timu hiyo kuwa na ukuta imara,Hispania wenye uwezo wa kuuchezea mpira walimiliki wapinzani vilivyo na kuwafanya washindwe kufurukuta akiwemo mtukutu Mario Balotteli.

Wednesday, June 27, 2012

WAHAMIAJI HARAMU 42 WAFARIKI.


Zaidi ya watu 40 wamefariki kwa kukosa hewa wakiwa ndani ya lori lililokuwa likiwasafirisha,marehemu hao inasemekana ni raia wa Ethiopia waliokuwa wakielekea Malawi kinyume na taratibu za uhamiaji,marehemu hao wamegundulika mkoanI Dodoma baada ya kutelekezwa porini na wafanyakazi wa gari husika ambalo mpaka sasa halijajulikana.
Naibu waziri mambo ya ndani mh.Pereira Silima amethibitisha na kusema wengine waliopona tayari wanashikiliwa na jeshi la Polisi nchini.

Thursday, June 14, 2012

SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI


Hawa nia baadhi ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu siku ya leo ambayo ni siku ya wachangia damu duniani. Nilibahatika kuongea na mmoja kati ya wachangiaji hao na kuniambia kuwa amekuwa akitoa mara kwa mara hata anapokuwa nje ya nchi.
Pia bi. Jaqueline Cypirian na Jamal Abdallah walisema wanafurahia kuchangia damu na kuwataka wananchi wengine kuwa na moyo wa huruma dhidi ya wahitaji wa damu.

Tuesday, June 05, 2012

POSTA YAKABIDHI T-SHIRT KWA AJILI YA WACHANGIA DAMU.


Meneja wa tawi la Posta Mbeya,Bw.Humphrey Julius(kushoto) akimkabidhi moja ya T-shirt kiongozi wa mpango wa Taifa wa Damu salama Ndg.Kundaeli Sariah,hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za mpango wa Taifa wa Damu Salama nyanda za juu kusini,jijini Mbeya na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya posta na damu salama.
Ndg.Sariah ameishukuru Benki ya Posta na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu na kuzitaka taasisi nyingine kujitolea vitu mbalimbali kwa ajili ya wachangia damu.
Sherehe za siku ya wachangiaji damu kitaifa itafanyika mjini Moshi na kanda ya nyanda za juu kusini itafanyika mjini Songea tar.14/06/2012,
KILA MCHANGIAJI DAMU NI SHUJAA

Sunday, May 20, 2012

TIMU YA STENDI KUU MBEYA YAICHAPA ITIJI RANGERS


Mashabiki wa timu ya stendi kuu Mbeya wakishangilia ushindi waliopata dhidi ya Itiji Rangers wa mabao 2-0,kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya msingi Mbata jijini Mbeya,mabao ya stendi kuu yamefungwa na Aliko Sanga na Dominick Meshack,hata hivyo mchezo uliingia dosari na mwamuzi aliamua kuvunja mchezo kutokana na Itiji kugomea mchezo.
Michuano hiyo inadhamiwa na gazeti la Raha Tele

Monday, May 14, 2012

SIMBA YATOLEWA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA PENATI


Mabingwa wa Tanzania bara,Simba ya Dar es salaam wametolewa kwenye ya kombe la shirikisho Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao ya 3-0 na timu ya Al-ahly shandy ya Sudan.
Al-ahly Shandy walipata mabao yao dakika ya 46,50 na 60 mpaka mpira unaisha Simba walikuwa nyuma kwa mabao 3-0,kwa matokeo hayo mshindi wa jumla ilibidi hapatikane kwa njia ya penati kutokana na Simba kushinda kwa idadi hiyo hiyo ya magoli kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es salaam.
Zilipigwa penati tisa tisa huku Al-ahly wakipoteza penati ya 3 iliyokolewa na mlinda mlango Juma Kaseja.Simba walipoteza penati ya 4 iliyopigwa na Patrick Mafisango.
Simba walipoteza penati ya mwisho iliyopigwa na Juma Kaseja.

Sunday, May 13, 2012

AIR TANZANIA YAPATA NDEGE MPYA


Shirika la ndege Tanzania limepata ndege mpya aina Boeing 737-500,ndege hiyo inategemea kuanza safari zake wiki ijayo kwenye miji kati ya Dar-Kilimanjaro na Mwanza.

Monday, May 07, 2012

SIMBA YAWAHARIBIA YANGA HISTORIA


Timu ya Simba jana imewafunga mahasimu wao Yanga kwa magoli 5-0 ambayo ni idadi kubwa ya magoli kwa zaidi ya miaka 37,ambapo mwaka 1976 Simba walipata ushindi wa goli 6 na kusababisha Yanga kusambaratika.
Simba walipata bao la mapema kupitia kwa Emanuel Okwi dakika ya kwanza,bao la pili dk.54 lilifungwa na Felix Sunzu kwa penati,bao la tatu dk.61 na Okwi,goli la nne 67 Kaseja kwa penati na la tano dk.72 Patrick Mafisango dk.72 kwa penati.
Baada ya mchezo huo mwalimu msaidizi wa timu hiyo ya Yanga Fred Felix Minziro Kataraiya alisema "timu ni nzuri tatizo ni migogoro iliyoko ndani ya klabu hiyo"
Nao wapenzi wa klabu hiyo wameutupia lawama uongozi wa timu hiyo kwa kushindwa kuongoza timu hiyo na kusababisha timu kuwa katika kipindi kigumu kwa msimu huu.

CHELSEA FC BINGWA WA FA CUP


Timu ya Chelsea FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa FA jana usiku kwa kuwafunga Liverpool 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Wembly jijini London.
Chelsea walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Lamires dk.ya 10,la pili kwa Drogba dk.59 na Liverpool likifungwa na Andy Carrol aliyeingia kipindi cha pili.


MICHEZO YA UMISETA WILAYA YA MBOZI YAFUNGULIWA LEO.


Michezo ya UMISETA kwa wilaya ya Mbozi imefunguliwa leo na afisa elimu wa wilaya hiyo kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya Vwawa.
Michezo hiyo itazishirikisha shule za sekondari wilayani humo.

Saturday, May 05, 2012

MTIBWA YAWAPA SIMBA UBINGWA KIRAHISI.


Timu ya Mtibwa jana imewapa ubingwa Simba baada ya kuwafunga Azam bao 2-1 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa uwanja huru kwa timu zote,uwanja wa Taifa na kwa matokeo hayo Azam hawawezi kufikisha pointi 59 ambazo Simba wanazo tayari,huku Azam wakiwa na pointi 53 na kubakiwa na mchezo mmoja kwa kila timu.

RASHID YEKINI AFARIKI DUNIA.


Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na mchezaji bora wa kwanza wa Afrika mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya utaratibu huu kuanzishwa.
Yekini amefariki akiwa na umri wa miaka 48 na ameichechezea timu yake ya taifa kwa mafanikio makubwa kabla ya kutundika daluga.

Thursday, May 03, 2012

MZEE WAWILA HERMAN NZOWA AJITOLEA KUHAMASISHA ELIMU WILAYANI MBOZI.


Mzee Wawila Hermain Nzowa(84) mkazi wa kijiji cha Igamba wilayani Mbozi,amekuwa akipita kwenye shule za sekondari na msingi wilayani Mbozi.kuhamasisha wanafunzi kujisomea na kuepukana na maambukizi ya ukimwi.
Mzee Nzowa amesema amekuwa akifanya shughuli hii kwa kutembea shule hadi shule,mzee huyu ameomba taasisi au watu binafsi kumsaidia ili kuweza kuokoa taifa la kesho.

Sunday, April 29, 2012

SIMBA YAWATUMIA SALAMU YANGA.


Timu ya Simba ya Dar es salaam,kwa mara nyingine imeendeleza ubabe wake baada ya kuwachapa El-Ahly ya Sudan kwa mabao 3-0,kwenye mchezo wa kombe la shirikisho,uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Simba walipata mabao yao kupitia kwa Haruna Moshi dk.67,Patrick Mafisango dk.77 na Emanuel Okwi dk.84,kwa matokeo hayo yanaipa Simba asilimia kubwa ya kuingia robo fainali ya michuano hiyo na El-Ahly kuwa na deni la bao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa Sudan kati ya mei 11 au 12,baada ya kuvaana na watani wao wa jadi Yanga ambao wanaonekana kupoteana mchezo huo utachezwa mei 5 kuhitimisha ligi kuu ya Tanzania bara.

SIMBA YAWATUMIA SALAMU YANGA.


Timu ya Simba ya Dar es salaam,kwa mara nyingine imeendeleza ubabe wake baada ya kuwachapa El-Ahly ya Sudan kwa mabao 3-0,kwenye mchezo wa kombe la shirikisho,uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Simba walipata mabao yao kupitia kwa Haruna Moshi dk.67,Patrick Mafisango dk.77 na Emanuel Okwi dk.84,kwa matokeo hayo yanaipa Simba asilimia kubwa ya kuingia robo fainali ya michuano hiyo na El-Ahly kuwa na deni la bao 4-0 kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa Sudan kati ya mei 11 au 12,baada ya kuvaana na watani wao wa jadi Yanga ambao wanaonekana kupoteana mchezo huo utachezwa mei 5 kuhitimisha ligi kuu ya Tanzania bara.

MLIPUKO WATOKEA KANISANI NAIROBI


Waumini wa kanisa la God's House of Miracle leo asubuhi wamekumbwa na dhahama baada ya mlipuko kutokea kanisani wakati wa ibada na kuuwa mtu mmoja na wengine zaidi ya saba kujeruhiwa.
Kanisa hilo lipo maeneo ya mtaa wa Ngara,jijini Nairobi,mlipuko huo unasadikiwa ni wa guruneti ambalo bado halijajulikana limetegwa na nani?

MLIPUKO WATOKEA KANISANI NAIROBI


Waumini wa kanisa la God's House of Miracle leo asubuhi wamekumbwa na dhahama baada ya mlipuko kutokea kanisani wakati wa ibada na kuuwa mtu mmoja na wengine zaidi ya saba kujeruhiwa.
Kanisa hilo lipo maeneo ya mtaa wa Ngara,jijini Nairobi,mlipuko huo unasadikiwa ni wa guruneti ambalo bado halijajulikana limetegwa na nani?

Wednesday, April 25, 2012

CHELSEA YATINGA FAINALI KWA MGONGO WA BARCELONA.


Timu ya Chelsea imeingia fainali ya klabu bingwa ulaya baada ya kufungana FC Barcelona 2-2 kwenye uwanja wa Nou Camp kwenye mchezo wa nusu fainali.
Chelsea imefanikiwa kuingia fainali kwa jumla ya mabao 3-1,wiki mbili zilizopita ilipata ushindi wa goli 1-0 jijini London kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Magoli ya Barca yalifungwa na Sergio na Iniesta na Chelsea walisawazisha kupitia Lamires na Tores.

ZAO LA PARETO HATARINI KUTOWEKA


Zao la pareto ni miongoni mwa mazao ambayo wakulima wamekuwa wakiacha na kupunguza kuyalima,huenda ni kutokana na bei yake kuwa chini au soko kusumbua.
Kamera yetu ilipita maeneo ya wilaya ya Makete,kata ya Matamba na kuona zao hilo likiwa kwenye shamba la ekari moja ndani ya kijiji kizima huku kukiwa na mazao kama mahindi,ngano,maharage na alzeti kwa wingi.

Tuesday, April 24, 2012

UPONDAJI WA KOKOTO WAZIDI KUONGEZEKA MBEYA.


Kutokana na ugumu wa maisha,vijana wengi wamekuwa wakijishughulisha na kazi mbalimbali jijini Mbeya,ikiwemo kuponda kokoto pembezoni mwa barabara kuu,kamera yetu ilipita maeneo ya Ilomba jijini Mbeya na kukuta wajasiliamali wakiponda kokoto na kuuza kwa kipimo cha debe kwa sh.1500/= bila kujali jua kali lililokuwa likiwaka na kuwa kandokando ya barabara jirani na kituo cha mafuta.
Tunawaomba viongozi na taasisi mbalimbali kuweza kuwasaidia wajasiliamali hawa kuwaboreshea mazingira yao ya kazi kwa kutoa mikopo au kuwapatia vifaa vya kujikinga wanapofanya kazi zao.

Wednesday, April 18, 2012

SIMBA BINGWA KWA 92%


Timu ya Simba ya Dar es salaam leo imejiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa Tanzania bara baada ya kuwafunga JKT ruvu jumla ya mabao 3-0 kwenye uwanja wa Taifa.
Mabingwa watetezi timu ya Yanga imepoteza dira baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar,tunaweza kusema Yanga imevuliwa ubingwa kwani hata wakishinda mechi zao zilizobaki watafikisha pointi 52 ambazo Simba wameshavuka kwa sasa wana pointi 56 ambazo Yanga hawawezi kuzifikia.

MKUU WA WILAYA AFUNGUA KONGOMANO LA MADEREVA MBEYA.


Mkuu wa wilaya ya Mbeya,ndg Evance Balama akiongea na baadhi ya madereva wa mjini Mbeya kwenye ukumbi wa JM Hotel.
Bwana Balama aliwaasa madereva hao kujiendeleza kielimu na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

MARCIO MAXIMO AKUTANA NA MHESHIMIWA RAIS NCHINI BRAZIL

m

Aliyekuwa kocha mkuu wa Taifa stars mbrazil Marcio Maximo alikutana na mheshimiwa rais Jakaya Kikwete jijini Sao Paulo na kusalimiana naye,kabla ya kuongea na waandishi wa habari ambao walikuwa wakimuuliza kuhusu mpango wake wa kuja nchini tena kwa ajili ya kuifundisha Yanga au Azam lakini hata hivyo alikanusha uvumi huo.

Monday, April 16, 2012

MWENYEKITI WA VIJANA CCM MKOA WA ARUSHA AHAMIA CHADEMA

Mwenyekiti wa vijana wa CCM mkoa wa Arusha ameamua kujitoa kwenye chama hicho na kujiunga na Chadema,hii ni ishara ambayo si nzuri kwa chama cha mapinduzi baada ya vijana wengi kuanza kujiingiza kwenye siasa na kujiunga na kambi ya upinzani.

Sunday, April 08, 2012

TUNAWATAKIA PASAKA NJEMA.


Kwa niaba ya mtandao huu,tunawatakia wakristo na wananchi wote sikukuu njema ya Pasaka,tukiwakumbusha kutenda yaliyo mema siku zote za maisha za maisha yetu.

Saturday, April 07, 2012

STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA.


Kanumba enzi za uhai wake
Msanii na mwigizaji maarufu nchini Steven Kanumba amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kifo cha Kanumba kimewashitua watu wengi nchini na nchi jirani

SIMBA HAO 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO


Timu ya Simba ya Dar es salaam jana ilifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la shirikisho licha ya kufungwa bao 3-1 na Es Satif kwenye uwanja wa May 8 mjini Satif-Algeria.
Simba wakicheza pungufu baada ya mlinzi wake kucheza faulo ya kizembe na kutolewa kwa kadi nyekundu dk.8,walibanwa sana wapinzani wao na kujipatia magoli hayo matatu.
Simba walitulia dak 7 za mwisho na kuweza kupata goli dk.92 likiwekwa kimiani na Emanuel Okwi na kuwafanya Simba kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini,wiki mbili zilizopita Simba walishinda 2-0 jijini Dar es salaam.

Friday, April 06, 2012

RAIS WA MALAWI BINGU WA MUTHARIKA AFARIKA DUNIA.


Rais wa Malawi BINGU WA MUTHARIKA amefariki dunia leo hii nchini alikopelekwa kwa ajili ya matibabu baada ya kupata mshituko wa moyo akiwa ofisini kwake hapo jana.
Rais Bingu wa Mutharika alizaliwa 24/02/1934 na alionyesha nia ya kuwa kiongozi toka mwanzoni mwa miaka ya 1990 na hatimaye ndoto yake ilitimia na kuwa rais wa nchi hiyo kupitia uchaguzi uliopita.
Habari hizi ni kwa hisani ya Nyasa Times.

Thursday, April 05, 2012

MHESHIMIWA LEMA AVULIWA UBUNGE ARUSHA MJINI NA MAHAKAMA

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema amevuliwa ubunge wa jimbo la Arusha mjini baada kushindwa kesi iliyokuwa inamkabili toka alipotangazwa kuwa mbunge wa jimbo hilo.
  Kesi hiyo ilikuwa ni ya kupinga matokeo ambayo ilifunguliwa na wapinzani wake kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2010.

Wednesday, April 04, 2012

TFF YAWASHIKA YANGA PABAYA


Yanga sasa inaonekana kuchanganyikiwa baada ya kupokwa ushindi dhidi ya Coastal Union baada ya kumchezesha beki wake Nadir Haroub 'Canavaro' ambaye alikuwa ana kadi nyekundu aliyopata baada ya vurugu kwenye mchezo dhidi ya Azam na kusababisha baadhi ya wachezaji wa Yanga kufungiwa kabla ya adhabu hizo kusimamishwa na Tibaigana.

Monday, April 02, 2012

JOSHUA NASSARI MBUNGE MPYA ARUMERU KUPITIA CHADEMA.


Joshua Nassari ameibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru baada kumbwaga mpinzani wake wa karibu Sioi Sumari kwa zaidi ya kura 5000.
Uchaguzi ulifanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo mh.Jeremiah Sumari wa CCM,uchaguzi huo umefanyika jana licha ya kukumbwa na matukio madogodogo ya wanachama kulinda kura na vituo vya kuhesabia kura hizo.
Baadhi ya watu wako mitaani wakishangilia ushindi huo.