BENJAMINKAMINYOGE.BLOGSPOT.COM

Tuesday, January 14, 2014

CHRISTIAN RONALDO MCHEZAJI BORA 2014


Christian Ronaldo leo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2014/15 kwa kuwashinda wachezaji Leon Messi wa Argentina na klabu ya Barcelona na Frank Ribery wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich.
Tuzo hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Leon Mess kwa miaka minne mfululizo.

KCC FC MABINGWA MAPINDUZI CUP 2014


Timu ya KCC ya Uganda leo imechukua ubingwa wa kombe la mapinduzi Zanzibar baada ya kuifunga timu ya Simba ya Dar es salaam kwa goli 1-0,kwenye mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Amaan,mjini Zanzibar,goli pekee la KCC limefungwa na Herman Waswa dakika ya 20.
 Kwa matokeo hayo timu ya KCC inakuwa timu ya kwanza kutoka nje ya nchi kuchukua ubingwa huo,mashindano yalikosa msisimko baada ya timu ya Yanga kujitoa dakika za mwisho na hivyo kuwakatisha tamaa wapenzi wa soka wa Zanzibar.
KCC waliingia fainali baada ya kuwachapa Azam 3-2 na Simba waliingia fainali kwa kuwachapa URA ya Uganda 2-0.

Sunday, May 19, 2013

YANGA BINGWA TANZANIA BARA


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati timu ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya 24 tangu ligi ihanzishwe 1965 kwa kuwafunga watani wao wa jadi Simba kwa goli 2-0.
Magoli ya mabingwa hao yalifungwa na Didier Kavumbagu dk ya 5 huku la pili likifungwa na Hamis Kiiza dk ya 63,Yanga walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kushangiliwa kwa muda wote na mashabiki wake.
Simba walikosa penati dk ya 26 iliyopigwa na Mussa Mude lakini kwa umahiri wa kipa Ally Mustapha aliweza kuidaka penati hiyo.Sasa Yanga italikilisha Taifa kwenye michezo ya klabu bingwa Afrika na mshindi wa pili Azam atashiriki kombe la shirikisho Afrika.

Saturday, May 04, 2013

AZAM YAFA KISHUJAA MOROCCO


Wawakilishi pekee wa Tanzania waliokuwa wamebaki kwenye michuano ya kimataifa,timu ya AZAM FC leo wametolewa na AS FAR RABAAT ya Morocco kwa kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kombe la shirikisho uliochezwa nchini Morocco.
Azam walipata bao la kuongoza dakika ya 6 likifungwa na John Bocco na Far Rabaat walifanikiwa kusawazisha dakika ya 12 na kupata goli la pili dakika ya 43,dakika za mwisho wa mchezo Azam waliweza kupata penati lakini bahati haikuwa yao baada ya penati yao kugonga mwamba penati ilipigwa na John Bocco.
Mwamuzi alitoa kadi nyekundu tatu,moja kwa Far Rabaat na mbili kwa Azam, wadau wa soka wameisifu Azam kwa kuwa na maandalizi mazuri ya michuano ya kimataifa na kutegemea msimu ujao kufanya vizuri zaidi hii ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano mikubwa kama hii.

Thursday, May 02, 2013

BARCELONA ULIMI NJE KWA BAYERN MUNICH YAPIGWA GOLI 7-0 KWA WIKI MOJA.


Timu ya Barcelona jana imepokea kipigo cha goli 3-0 nyumbani kutoka Bayern Munich na kutolewa kwenye nusu fainali na wajerumani hao
Mchezo wa kwanza uliochezwa Alienz Arena wiki moja iliyopita Barcelona walifungwa goli 4-0.
Bayern Munich sasa watakutana na wajerumani wenzao wa Borussia Dortmund kwenye mchezo wa fainali utaofanyika uwanja wa Wembly nchini Uingereza.

Saturday, April 27, 2013

BARCELONA NA REAL MADRID UGONJWA MMOJA WAPIGWA NNE NNE NA WAJERUMANI.


Real Madrid chini ya special coacher Jose Maurinho jana imepata kipigo kikubwa kutoka kwa Borussia Dortmund cha goli 4-1,kwenye nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya.
Magoli ya Dortmund yote yamefungwa na Robert Lewandoski huku goli la kufutia machozi la Real Madrid likifungwa na Christian Ronaldo
Nao Barcelona juzi walikutana na kipigo kama hicho cha goli 4-0,kutoka kwa Bayern Munich,mechi za marudiano zitachezwa tarehe 30 na 31/05/2013 nchini Hispania.

Thursday, April 18, 2013

BI.KIDUDE AFARIKI DUNIA


Msanii mkongwe hapa nchini Fatma Baraka (Bi.Kidude) amefariki na atazikwa leo huko kijijini kwao Katumba Unguja.
Bi.Kidude alikuwa ni muimbaji wa nyimbo za taarab na mpiga ngoma maarufu,ambaye alikuwa maarufu ndani na nje ya nchi alikuwa kipenzi cha watu wengi kutokana na uwezo wake wa kulishambulia jukwaa pamoja na umri wake kuwa mkubwa.

Thursday, April 04, 2013

CANAAN HIGH SCHOOL-MLOWO MBOZI.


Ni moja ya shule nzuri zilizopo wilayani Mbozi,shule ipo eneo la Mlowo kilomita 1.2 toka barabara kuu iendayo Tunduma,shule ina walimu wazuri kwa masomo yote na mazingira mazuri kwa wanafunzi.
Pia ina Hosteli kwa ajili ya wavulana na wasichana,inapokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali,wahi sasa ili hupate nafasi kwenye shule hii yenye ubora mkubwa.

Thursday, March 28, 2013

EASTER CONFERENCE YAFANA MBEYA


Baadhi ya wanafunzi wa umoja wa wanafunzi wa kikristo Tanzania-Mkoani Mbeya wakimusikiliza Mhubiri toka Dar es salaam ndg.Jackson Mndeme kwenye mkutano unaofanyika kwenye ukumbi wa St.Mary's sekondari jijini Mbeya.

Monday, March 25, 2013

TAIFA STARS YAICHINJA MOROCCO 3-1


Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars jana imefanikiwa kuifunga kigogo cha soka Afrika Morocco bao 3-1 kwenye mchezo uliofanyika jijini Dar es salaam jana.
Taifa Stars walipata mabao yao kipindi cha pili yakifungwa na Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea TP Mazembe ya DRC,sasa Stars inashika nafasi ya pili kwenye kundi lake ikiwa na pointi 6 nyuma ya Ivory Coast wenye pointi 7,Morocco ya tatu ikiwa na pointi 2,huku Gambia ikiburuza mkia.

Saturday, March 16, 2013

WASABATO MBEYA WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU.


Leo ilikuwa ya matendo ya huruma duniani kwa Wasabato na kukusanyika sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu juu ya ubaya wa matumizi ya Madawa ya kulevya,tumbaku na pombe.
Mbali na yote hayo Wasabato wa Mbeya Mjini walichukua nafasi hiyo kuchangia damu kwenye viwanja maarufu vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya,mmoja wa wachangiaji damu hao bw.Leonard Msendo alionekana kufurahia huduma ya uchangiaji wa damu na kuwaomba Watanzania kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia wahitataji wa damu(wagonjwa) kwani damu ni tiba ambayo inapatikana kutoka kwa binadamu.
CHANGIA DAMU OKOA MAISHA-DAMU HAIUZWI HUTOLEWA BURE NA HOSPITALI ZOTE HAPA NCHINI,UKIUZIWA DAMU TOA TAARIFA KITUO CHA POLISI,MGANGA MKUU WA HOSPITALI HUSIKA AU KITUO CHA DAMU SALAMA KILICHO JIRANI NAWE.

Thursday, March 14, 2013

PAPA MPYA ATOKA ARGENTINA


 Hatimaye lile zoezi la kumchagua Papa limekamilika katika kanisa la St.Peters Basilica huko Vatican na Muargentina Jorge Mario Bergogli kuchaguliwa kuwa Papa mpya ambaye atajulikana kwa jina la PAPA FRANCIS WA KWANZA.

Sunday, March 10, 2013

SIMBA YAAMUKA USINGIZINI LEO KWA KUICHAPA COASTAL UNION 2-1


Mabingwa watetezi wa vodacom leo wamezinduka na kuichapa Coastal Union ya Tanga bao 2-1 kwenye uwanja wa Taifa Dsm.
Simba wamepata mabao ya mwishoni mwa kipindi cha kwanza kupitia kwa Mrisho Ngasa na Haruna Chanongo huku goli la kufutia machozi la Coast likifungwa na Razaq Khalfan kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo Simba kafikisha pointi 34 akiwa nyuma ya Azam wenye 37,huku vinara wa ligi hiyo Yanga wakiwa na pointi 45 na Coastal Union wanabaki na pointi 31 na kufanya ligi iwe ngumu kwa Azam,Simba na Coastal Union kwa mtazamo wangu Yanga hawana ugumu sana kwani wana uhakika wa nafasi moja kati ya tatu za juu,labda itokee walewe sifa na kupoteza takribani mechi nne ndio watakuwa pabaya.

YANGA YAWAADHIBU TOTO YAO


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga ya Dar es salaam imezidi kuisukumia kwenye shimo la kushuka daraja baada ya kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.
Yanga walipata goli lao kupitia kwa Nizar Khalfan dakika 78,aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete.

Wednesday, March 06, 2013

RAIS HUGO CHAVEZ WA VENEZUELA AFARIKI DUNIA

Rais Hugo Chavez wa Venezuela amefariki jana,Rais Chavez alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa  ambayo yamesababisha kifo chake.
  Rais huyo atakumbukwa kutokana msimamo wake wa kutoyumbishwa na  baadhi ya mataifa yenye nguvu duniani

Saturday, March 02, 2013

MANCHESTER UNITED YAMUONGEZEA MKATABA RYAN GIGGS


Mchezaji mkongwe katika ligi ya Uingereza ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake ya Manchester United.
Mchezaji huyo ambaye anatarajiwa kutimiza miaka 40 hivi karibuni utakuwa ni msimu wake wa 23 ndani ya Manchester united ni mmoja kati ya wachezaji waliyoipatia mafanikio klabu hiyo ya mashetani wekundu.

Monday, February 25, 2013

MZIMU WA LIBOLO WAENDELEA KUITESA SIMBA.











Mabingwa watetezi wa Tanzania Bara jana walizidi kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao baada ya kufungwa na Mtibwa ya Morogoro kwa goli 1-0 kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Mtibwa walipata bao lao dakika ya 18 likifungwa na Salvatory Ntebe akiunganisha pasi ya Vincent Barnabas,Simba imekuwa kwenye wakati mgumu toka walipomuuza nyota Emanuel Okwi na kumfukuza kocha wao Milovan Circovic na kuwafanya kuwa na matokeo yasiyoridhisha.

Tuesday, February 12, 2013

PAPA BENEDICT XVI ATANGAZA KUJIUZULU


Papa Benedict wa 16 ameushitua ulimwengu baada ya kueleza dhamira yake ya kutaka ifikapo februali 28 mwaka huu.
Kumekuwa na minong'ono mingi kutoka kwa baadhi ya watu wakidhani sasa umefika muda wa kanisa kuwa na mpasuko.

NIGERIA BINGWA KOMBE LA AFRIKA


Timu ya Taifa ya Nigeria imechukua ubingwa wa Afrika kwa kuichapa Burkina Faso goli 1-0,goli pekee la Nigeria limefungwa na Sunday Mba.

Saturday, February 02, 2013

YANGA YAPONEA KWENYE TUNDU LA SINDANO


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga leo wameponea chupuchupu kupoteza mchezo wa ligi kuu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar
Mtibwa walipata bao la kuongoza dakika ya 45 likifungwa na Shaban Kisiga,Yanga wamefanikiwa kusawazisha dakika ya 85 kupitia kwa Hamis Kiiza ambaye aliunganisha mpira wa Said Bahanuzi.

Sunday, January 27, 2013

SIMBA YAANZA VIZURI MZUNGUKO WA PILI


Mabingwa watetezi wa Tanzania bara jana wameanza vyema mzunguko wa pili wa ligi baada ya kuwachapa African Lyon goli 3-1,nao Azam FC wamepata ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Kagera Sugar,Mtibwa wameangukia pua baada ya kuchapwa goli 1-0 na Polisi Morogoro,Coastal Union wameibamiza JKT Mgambo 3-1,Toto African wamekubali kichapo toka kwa JKT Oljoro.
Ligi hii inaendelea leo kwa mchezo mmoja kati ya mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga na Tanzania Prison kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.

Saturday, January 26, 2013

CHANGIA DAMU OKOA MAISHA


Mmoja wa washiriki wa Bonanza lililoandaliwa na Life time Promotion bw.Jafar Ngalipa akichangia damu kwenye viwanja vya TIA

Wednesday, January 09, 2013

YANGA YAPIGWA 2-1 UTURUKI


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga,jana wamefungwa goli 2-1 na timu ya daraja la kwanza nchini Uturuki ya Denizlispor.
Yanga wako nchini Uturuki ambako wameweka kambi ya wiki mbili.

Tuesday, January 08, 2013

YANGA UWANJANI TENA LEO


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga ya Dar es salaam,leo wanashuka tena dimbani kucheza na timu ya Denizlspor nchini Uturuki ambako Yanga wameweka kambi.
Yanga ikiwa imesheheni vipaji iliweza kupata matokeo ya sare ya 0-0 kwenye mechi yake ya kwanza na kuzivutia timu nyingine za nchi hiyo kutaka kucheza nayo.

Friday, January 04, 2013

DEREVA WA PIKIPIKI ANUSURIKA


Dereva wa pikipiki akiwa ahamini kilichotokea baada ya kunusurika kwenye ajali eneo la Kabwe Mbeya.

Tuesday, January 01, 2013

USIKU WA MWAKA MPYA 2013 VITUKO VITUPU.


Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Willy ameonekana akiwa amevaa suti iliyoshonwa kwa kutumia mifuko ya cement na kuvinjari mitaani maeneo ya Simike jijini Mbeya.
Ilikuwa moja ya burudani kwa wakazi wa eneo hilo la Simike.

KHERI YA MWAKA MPYA 2013


Mtandao huu unawatakia kila la kheri ya Mwaka mpya wasomaji wake wote,tumshukuru Mungu kwa kuweza kuufikia mwaka huu mpya na kutuepusha na mabaya mengi yaliyokuwepo na sasa tunaanza tena mwaka kwa kujikabidhi mikononi mwake.

Sunday, December 30, 2012

TUSKER FC YAICHAPA SIMBA 3-0


Timu ya Tusker FC ya Kenya,imeendeleza ubabe wake kwa timu za Tanzania baada ya kuichapa Simba kwa goli 3-0,kwenye mechi ya kirafiki iliyofanyika uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Jumatano iliyopita waliwafunga mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga 1-0.

Sunday, December 23, 2012

TAIFA STARS YAWACHAPA MABINGWA WA AFRIKA


Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Taifa Stars imewalaza mabingwa wa soka wa Afrika Zambia(Chipolopolo) goli 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Goli pekee la Taifa Stars lilifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 45 huku Zambia wakiwatumia wachezaji wao makini kama Christopher Katongo,Felix Katongo na Nathan Sinkala lakini hawakuweza kubadili matokeo.

Saturday, December 01, 2012

WATOTO WAPATA KIPA IMARA


Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian Mlowo wamepata kipa imara,kama wanavyoonekana watoto hao katika picha Noel Ben Kaminyoge,Rehema Mbuba wakiwa na wenzao ndani ya kanisa la Moravian Mlowo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI-MBEYA.


Mamia ya wakazi wa Mbozi Mission wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh.Abbas Kandoro ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ambayo yamefanyika kimkoa wilayani Mbozi.
Mh.Kandoro amewaasa wananchi kuepukana na tabia hatarishi na kutowanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi.
Mh.Kandoro aliwaongoza wananchi katika zoezi la kuchangia damu kwa hiari,baada ya kuchangia damu siku ya leo kwenye viwanja vya Mbozi Mission.

Thursday, November 29, 2012

ZANZIBAR HEROES YAWASHANGAZA AMAVUBI YAWACHAPA 2-1.


Timu ya Zanzibar leo imeweza kufanya kile ambacho hakikutegemewa na wengi baada ya kuifunga timu ngumu ya Ruanda(Amavubi) baada ya kuifunga goli 2-1 na kuingia robo fainali ya kombe la Tusker Challenge Cup.
Katika mechi ya kwanza Malawi wameibuka kidedea kwa kuwafunga Eriterea 3-2.

Monday, November 26, 2012

UGANDA YAANZA VYEMA KOMBE LA CHALENJI.


Timu ya taifa ya Uganda imefanikiwa kuwafunga Harambee Stars 1-0 kwenye uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala.
Goli la Uganda lilifungwa na Geofrey Kizito dakika ya 74 akiunganisha krosi ya Iguma.
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo Burundi wameifunga Malawi bila huruma mabao 5-0 na Kilimanjaro Stars(Tanzania) wamewafunga Sudan 2-0

Wednesday, November 21, 2012

SERA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA BADO IPO SANA.


Wananchi wa kata ya Isyonje wilaya ya Mbeya vijijini,wakifyatua tofali kwa ajili ya kuongezea majengo ya shule ya msingi.
Mdau wetu alitembelea kata hiyo na kufurahishwa na ushirikiano huo na yeye kushiriki kama anavyoonekana pichani akiwa anafyatua tofali.
Umoja ni nguvu,utengano ni udhaifu ni maneno ya Baba ya Taifa yaliyojaa hekima na busara.

Saturday, October 13, 2012

MTOTO AZUA BALAA MBAGALA KWA KUKOJOLEA QU-RAAN


Mtoto wa kidato cha kwanza amezua balaa na kusababisha kuvunjika kwa amani kwa muda eneo la Mbagala-Kizuiani, kutokana na kitendo cha kukojolea Qu-raan wakati alipokutana na mtoto mwenzie ambaye alikuwa na kitabu hicho na kuanza ubishi uliopelekea mtoto kufanya kitendo hicho ambacho kimetokana na utoto na kusababisha watu wazima kupandwa na jazba na kuanzisha maandamano yaliyopelekea uharibifu wa vitu mbalimbali yakiwemo makanisa na magari.

Wednesday, September 19, 2012

MTIBWA YAICHAKAZA YANGA 3-0


Timu ya Mtibwa Sugar FC leo wamewafunga Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga kwa bao 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom.
Yanga ikiwa imesheheni wachezaji wake nyota,walishindwa kuwadhibiti Mtibwa ambao safu ya kiungo ilionekana kucheza vizuri chini ya Shabaan Kisiga na Shaban Nditi.
Matokeo mengine ni kama ifuatavyo:-
Toto African 2-Azam 2
Prison 1-Coastal 1
African Lyon 2-Polisi 1
JKT Oljoro 0-Kagera 0
Simba 2-JKT Ruvu 0
Ruvu Shooting 1-Mgambo 0

Tuesday, September 04, 2012

DAUD MWANGOSI AZIKWA LEO TUKUYU MBEYA.


Katibu mkuu wa taifa wa CHADEMA akiweka shada la maua kwenye kaburi la Daud Mwangosi ambaye alikuwa mwandishi wa kituo cha televisheni Chanel Ten,ambaye aliuawa juzi katika vurugu kati ya polisi na wananchi wanaosadikiwa na wanachama wa Chadema huko Nyololo wilayani Mufindi.
Marehemu Daud Mwangosi amezikwa kijijini kwao Busoka,Tukuyu,watu wengi wamehudhunishwa na kifo hicho na kulitupia lawama jeshi la polisi.

DAUD MWANGOSI AZIKWA LEO TUKUYU MBEYA.


Katibu mkuu wa taifa wa CHADEMA akiweka shada la maua kwenye kaburi la Daud Mwangosi ambaye alikuwa mwandishi wa kituo cha televisheni Chanel Ten,ambaye aliuawa juzi katika vurugu kati ya polisi na wananchi wanaosadikiwa na wanachama wa Chadema huko Nyololo wilayani Mufindi.
Marehemu Daud Mwangosi amezikwa kijijini kwao Busoka,Tukuyu,watu wengi wamehudhunishwa na kifo hicho na kulitupia lawama jeshi la polisi.

Sunday, September 02, 2012

MENAS ZENAWI AZIKWA LEO


Waziri Mkuu wa Ethiopia Menas Zenawi amezikwa leo jijini Addis Ababa.
Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nje ya Ethiopia,mmoja wa viongozi hao Rais Paul Kagame wa Ruanda alimuelezea marehemu kuwa katika uongozi wake alileta maendeleo nchini humo na bara la Afrika kwa ujumla.

MJASILIAMALI WA KATAVI


Pamoja na kuwepo kwa ushindani wa soko za bidhaa zetu kwenye masoko ya nje,bado Tanzania tuna nafasi ya kuibua vipaji vilivyo vijijini na kuviendeleza,kamera yetu ilimkuta fundi huyu wa vinu(pichani) akitengeneza vinu vidogo kwa kutumia nyenzo duni.
Bidhaa kama hizi zimekuwa zikitumika majumbani na baadhi ya watalii wakinunua kama mapambo au ukumbusho wao kutembelea Afrika,inatakiwa mipango mizuri ya kuwawekea wabunifu wetu misingi mizuri ili kuwafanya wasonge mbele

YANGA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1


Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Yanga ya Dar es salaam jana wameweza kuwafunga Coastal union ya Tanga 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa uwanja wa taifa.
Coastal walipata goli lao dakika ya 16 likifungwa na Razak Khalfan goli hilo lilidumu hadi dakika ya 84 pale beki wa Coastal Phil Kaira alipojifunga,bao la pili lilifungwa na Said Bahanuzi dakika ya 86.
Yanga iliwachezesha wachezaji wake wapya akiwemo Twite.

MBUYU TWITE APATA MAPOKEZI MAKUBWA.


Mchezaji wa Yanga raia wa DRC ameingia Nchini kwa mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo,ambao walikuwa wakimsubiri kwa muda mrefu.
Mashabiki hao walimpatia jezi namba 4 yenye jina la Rage ambaye ni mwenyekiti wa Simba kama kumdhihaki Rage ambaye alimsajili mchezaji huyo na baadaye mchezaji huyo kurudisha fedha na kusajili Yanga kwa kitita kikubwa zaidi.
Pamoja na mapokezi makubwa aliyopata mchezaji huyo,wadau wa soka wamemtaka kufanya kile kilichomleta mashabiki huwa hawachelewi kubadilika katika mchezo wa soka na kumuona si chochote.

Sunday, August 26, 2012

SENSA YAENDELEA NCHINI KWA UTULIVU MKUBWA


Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na familia yake wakishiriki zoezi la kuhesabiwa na kujibu maswali ya makarani wa sensa kwa utulivu mkubwa.
Wewe mwananchi ambaye bado hujafikiwa na makarani wa Sensa fuatilia kwa Mwenyekiti wako wa mtaa ili uhakikishe unahesabiwa kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu,kuhesabiwa kwako ndio kunalifanya taifa lielewe idadi ya watu na kupanga maendeleo na huduma za kijamii kwa eneo husika-JITOKEZE KUHESABIWA KWA MAENDELEO YETU YA BAADAYE.

Friday, August 24, 2012

YANGA NDANI YA IKULU YA RUANDA


Rais Paul Kagame akiongea na wachezaji na viongozi wa timu ya Yanga ambao ni mabingwa wa Afrika mashariki na kati walipomtembelea Ikulu ya Ruanda,jijini Kigali jana.
Pia timu hiy6 imetembelea makaburi ya watu waliouawa mwaka 1994 kwenye mauaji ya Kimbari nchini humo,mbali na hayo timu hiyo imekuwa kivutio kikubwa kwa wapenzi wa soka wa nchini humo.

Tuesday, August 21, 2012

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA MELES ZENAWI AMERIKI.


Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki dunia jana usiku nchini Belgium alikokuwa akipatiwa matibabu.
Bwana Zenawi aliingia madarakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Mengistu Hailemariam na kusababisha nchi hiyo kuingia kwenye mapigano ya kikabila na majirani zao Eriteria na baadaye akaweza kuleta amani nchini humo mpaka kifo chake hofu imetanda imetanda miongoni mwa wananchi kuwa huenda machafuko ya kikabila yakazuka tena baada ya kifo chake.
Makamu waziri mkuu wa nchi hiyo bw.Hailemariam Deselagan ndio ataongoza nchi hiyo mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2015.

Sunday, August 19, 2012

RAIS J.M.KIKWETE ASWALI SWALA YA IDD KINONDONI MUSLIM


Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akimpokea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alipofika kwenye viwanja vya Msikiti wa Kinondoni Muslim kwa ajili ya swala ya Idd-el-fitr leo.

RAIS J.M.KIKWETE ASWALI SWALA YA IDD KINONDONI MUSLIM


Mstahiki Meya wa manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akimpokea Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya muungano Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alipofika kwenye viwanja vya Msikiti wa Kinondoni Muslim kwa ajili ya swala ya Idd-el-fitr leo.

MAKAMU WA RAIS ASWALI SALA YA IDD-EL-FITR MNAZI MMOJA.


Makamu wa Rais Dr.Mohammed Gharib Bilal leo ameswali sala ya Idd kwenye viwanja vya Mnazi mmoja,jijini Dar es salaam,swala hiyo imehudhuriwa na watu wengi akiwemo Rais mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi.

EID MUBARAK


MTANDAO HUU UNAWATAKIA KHERI NA FANAKA YA SIKUKUU YA EID-EL-FITR WATANZANIA NA WAISLAMU WOTE DUNIANI,TUDUMISHE AMANI NA UPENDO-SIKUKUU NJEMA.